William Mshumbusi
JF-Expert Member
- Mar 27, 2012
- 1,657
- 2,252
Kitu wapinzani wanachofeli ni kuongozwa na hasira na ushindani na kupigania maslahi binafsi ya kisiasa hivyo kukosa logic na plan nzuri kufanikisha mipango yao.
Jakaya Kikwete alianzisha mchakato wa Katiba mpya Ila mchakato mzima katika mazingira hayo ulitawaliwa na wanasiasa. Bunge lilijaa wanasiasa na kwa maamuzi yao lingeleta katiba mbovu Tena iliyoegemea kuibeba CCM kwani walikuwa wengi na wenye nguvu ya maamuzi. Wangekuja na katiba mpya lkn isiyofaa. Jk alijua akaitupilia mbali mwishoni.
Sasa mnavyoomba tuimalizie mchakato mnataka tuimalizie kwa staili hiyo hiyo?!
Je, mnataka katiba mpya au katiba nzuri?
Mi nadhani kwa busara CHADEMA ombeni tume huru na chaguzi za haki. Piganieni mabadiliko hayo ya Sheria na katiba Ila swala la katiba liacheni. Waacheni watu wasio wanasiasa watuundie katiba.
*Katiba itakayowasimamia na kuwawajibisha wanasiasa pia. Katiba hiyo wanasiasa hawawezi kuiunda.
*Katiba itakayojibu kila kitu na kuondoa mizengwe kwenye kila sekta kuanzia kilimo, biashara, Viwanda, madini na Mikataba yote isiyo ya kiusalama Kama madini na manunuzi, ubia, hesabu za taasisii na mashirika ya umma kuwa wazi kwa umma wakati wote.
*Katiba itakayomlazimisha mbunge kabla ya kwenda bungeni kwenye kikao chochote akae vikao vyenye maandishi angalau vitatu na wadau wote katika Jimbo lake na kuikusanya mawazo na Kisha kuyafikisha bungeni au serikalini na sio Sasa wabunge kwenda kuzungumza mawazo binafsi na marafiki zao wachache wanaokunywa nao bia vijiweni.
Bunge jipya la katiba lisizidi 10% ya wanasiasa. Waingie wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, bunge lijae wataalamu kwa 30% mfano walimu, madaktari, wanasheria na wachumi. Na wanaoshiriki kwenye bunge Hilo wakubali kutokugombea au kuteuliwa nafasi yoyote ya kisiasa au za kiuteuzi kwa miaka kumi ili kuondoa bunge Hilo Hilo kuja kugeuka chombo Cha utawala Mara baada ya kuunda katiba.
Bunge lililopita na mchakato mzima wa Katiba ndio uliowaibua akina polepole na Kabudi. Watu watashindwa kutoa mawazo kwa Uhuru wakitarajia hisani za watawala
Na nawaomba wimbo isiwe katiba mpya Bali tunataka katiba yenye kulinda haki. Na katiba yenye kutenda haki kamwe haiwezi kuletwa na wanasiasa. Kila sehemu wanasiasa huvutana tu kutafuta msindi. Kwenye katiba lazima kila mtu awe msindi.