Jaji Mutungi: ni kweli bila shaka katiba mpya haitatekwa na wanasiasa?!

Librarian 105

JF-Expert Member
May 6, 2023
239
325
katiba-pic.jpg.jpeg

Alitoa kauli hiyo baada ya ofisi yake ya msajili wa vyama vya siasa kuelekea kukutana na baraza la vyama vya siasa nchini (bila ushiriki wa Chadema). Kujadili hatua za mwanzo za utekelezaji wa agizo la Rais la kuagiza kuanza kwa mchakato wa katiba mpya.
Rais Samia alimtaka kuitisha mkutano unaotoa fursa kwa wanasiasa kufanya tathmini ya hoja na mapendekezo ya kikosi kazi, ikiwemo suala la mchakato wa katiba mpya.
Akikabidhiwa jukumu hilo ikionekana kwamba chanzo cha mkwamo wa kuendelea mchango wa katiba mpya mwaka 2014 kupitia Bunge Maalumu la Katiba, na wananchi kubakia njiapanda. Huku Rasimu ya pili ya Warioba ndio ilipasua taifa vipande viwili kupitia mitazamo ya muundo wa serikali tatu.
(Chanzo: Mwananchi).

Hoja yangu:
  1. Jaji Mutungi anasema katiba mpya haitatekwa na wanasiasa; anauelewa wa kina wa kile kilichotokea mwaka 2014 UKAWA kuikataa Katiba Pendekezwa?
  2. Je, mchakato huu mpya, serikali ya CCM inajipambanuaje kujitoa katika kuiteka katiba mpya, na kuheshimu maoni ya wananchi waliyotoa kwenye Tume ya Jaji Warioba hadi kupatikana kwa Rasimu ya Katiba Mpya?
  3. Kinachodaiwa kugawa taifa vipande viwili, muundo wa serikali, kipengele hiki kiliongezwa na wanasiasa wa UKAWA au kilibeba maoni na mapendekezo ya wananchi?
Nawasilisha hoja jamvini.
 
Screenshot_20230602-074845.png


Kwa maneno yao wenyewe... Tayari mchakato wa Katiba Mpya ushatekwa zamani!
Nilitarajia kauli kama hiyo ipate upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi lakini sijaona chochote!
Nahisi kwamba Katiba Mpya siyo priority kwa Watanganyika (make wao ndo wanakandamizwa)
 
Back
Top Bottom