Inawezekana kauli yangu isiwaingie watu masikioni mwao kabisa, lakini nitawaeleza japo kwa kifupi.
Katika siasa kuna kitu kinaitwa siasa za jumla (general politics) na siasa za kijiografia (geography politics)
General politics inahusu mambo yanayohusu siasa za kitaifa bila kuchagua chama au itikadi na hizi mara nyingi husimamiwa kwa katiba, kanuni na sheria za nchi, hapa inahusiana pia na daftari la wapiga kura na tume ya uchaguzi,
Geography politics inahusu siasa za eneo husuka, kuna international gp, na domestic gp,
Katika hayo Chadema ime win kwenye Gp-D kwa asilimia zaidi ya 90%, hili linatokana na chama kushiriki uchaguzi kwa miaka yote huku mambo muhimu yanayopaswa kufanywa kwenye General Politics yakiwa doro kabisa, mambo hayo ni kama tume kuwa huru, daftari la wapigakura kuboreshwa, na dola kuvuruga chagizi nyingi kwa maslahi ya ccm.
Takwimu za chaguzi hizi zinatoa sura stahiki ya ubora wa domestic political ya Chadema,
Mathalani uchaguzi huu Chadema ilikuwa ikitetea kata 3, za Nyaisura, Kiborloni na Mikol.. Kigoma.
Tumepoteza Nyaisura, na Kigoma, na Tumeipoka ccm kata za Sombetini na Njombe.
Tamani ya kata ilizoshinda chadema nikubwa kuliko ccm, kubeba kata ya njombe ni turufu kubwa, vivyo hivyo kata ya sombetini. CCM hawajaongeza thamani yoyote ya kata,
Kwa lugha nyingine nikuwa CHADEMA 0-0 CCM, lakini CHADEMA wananafasi ya golden goal kwakubeba kata ya Njombe ambayo kwanza inafuta propaganda za ccm yakuwa chadema ni chama cha ukanda, sasa tunashuhudia Chadema sio chama cha ukanda tena bali chama cha kitaifa na kila pembe ya jamhuri hii.
Izingatiwe kuwa oparesheni Pamoja Daima haikuwa maalumu kwaajili ya uchsguzi huu bali sehemu ya ratiba ya chama katika kutoa elimu ya umma kudai/kuhimiza uboreshaji wa daftari la wapiga kura.
Naamini hapo mmenipata ndugu zangu mnaojenga hoja dhaifu kuwa kama dhana ni daftari la wapiga kura na polisi why kwingine chadema imeshinda?
Kuna watu kama wewe unaweza ukadhani unaisaidia sana CHADEMA katika ukuaji wake kumbe propaganda zako ndizo zinazoididimiza kabisa hasa pale unapochukua nafasi ya mmojawapo wa watu walio karibu na jiko la maamuzi ya CHADEMA (false position).
Kwanza hoja yako hii hapa juu ina matobo mengi ya kisayansi katika siasa kwa ujumla achilia mbali hali ya ksiasa nchini Tanzania bila hata kugusia maneno uliyotumia katika hoja yako.
Ukiangalia katika nchi nyingi zenye vyama vya kisiasa ambavyo ni mbadala halisi wa chama tawala kidemokrasia utaona kuwa chaguzi ndogo huwa ni mwiba kwa chama tawala kutokana sababu nyingi lakini sababu kuu huwa ni mbili.
1) Wapiga kura kuanza kukata tamaa kutokana na ahadi kupitia ilani ya uchaguzi kusua sua au kutokutimizwa na chama tawala huku muda uliobakia wakiona kama hautoshi kuzitimiza. Kwa maana nyingine, ile euphoria inayopatikana baada ya uchaguzi huwa inakumbana na political reality.
2) Chama pinzani kuwa na fursa ya consolidate uwezo wao katika human resources (human capital) and fund kutokana na uchache wa maeneo ya chaguzi yanayofanyika.
Kunapotokea hali ambayo chama mbadala hata chaguzi ndogo kinashindwa kukitikisa chama tawala lazima kutakuwa na maswali mengi sana ambayo yanataka majibu halisi ili kuweza kuondoa sababu zilizosababisha kushindwa kutoa mtazamo chanya katika chaguzi kuu ijayo.
Kwa kutumia mifano yako hiyo, Ningekuelewa kama ungesema CHADEMA kwa sasa bado haijafikia nafasi ya kuongoza nchi, kwa maana nyingine, iko kwenye mkakati wa pili wa kisiasa kwa vile haijakuwa chama cha kitaifa ndiyo maana imeanza kupata maeneo mengine ya nchi kama kwenye Kata ya Njombe. My goodness, this is 2014.
CHADEMA kwa vile kimeingia kwenye chaguzi na kinajinasibisha kama ni chama ambacho kiko tayari na kinasubiri muda kisheria kupewa nchi kuongoza, basi kilitakiwa angalau kishinde nusu ya kata zilizofanya uchaguzi au zinazofanya chaguzi ndogo bila kujali ziko pande gani ya nchi.
Kukaa hapa na kuanza kujipongeza kwa mtazamo wa chama kama ndiyo kinaanza kujijenga ni kufurahisha jukwaa lakini hakuondoi uharisia wa kuwa kilichofanyika ni total failure bila hata kuangalia nguvu iliyotumika katika kuzitafuta hizo kata.
Ukiangalia zaidi, utagundua kuwa hoja uliyojitahidi kuijenga hapa inapingana kabisa na hoja iliyoijenga kwenye thread hii,
Tatizo lako unajitahidi kutetea swala ili kufurahisha macho ya wapenda kusikia mazuri tu ya chama badala ya kuangalia mabaya yake kwa faida ukuaji wa chama ndiyo ukasahau hata ulichokiandika na kukiweka saa 10:39, yaani masaa 7 tu kupita, ukawa tayari umebadilisha mtazamo. Hata hueleweki unasimama kwenye nguzo gani kisiasa katika matokeo haya ya uchaguzi. Hapo hapo unasema chama kinayumba na hapo hapo unasema chama kimefanya vizuri sana!.
Hebu soma ulichokiandika hapa saa 10:39,
Nimeshiriki hatua zote za uchaguzi katika katika kata 27 nchini, nasema nimeshiriki kwa 100%, sijasimuliwa, wala kusikia tu,
Uchaguzi wa udiwani katika Kata 27 umemalizika kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujinyakulia ushindi.
Hata hivyo, ushindi wa chama hicho katika uchaguzi huu ulitarajiwa kwa sababu nyingi zikiwemo zile zilizozoeleka nyakati zote za uchaguzi kama, kutumia vyombo vya dola, na serikali kwa ujumla kuwadaidia wao.
Hoja ya msingi hapa ni je haya yametokea katika uchaguzi huu tu ama yalikuwepo katika chaguzi zote??
Kuna wanaoamini kuwa Chadema kuwaadhibu wanachama wake waliovunja katiba ya Chama Zitto, Killa, Mwigamba eti ni "Mgogoro" uliochangia kwa 100% kushindwa uchaguzi huu.
Nikubaliane nao wale wafikirio hivyo akini niwape shule ya falsa ya siasa kidemorasia,
Niwakumbushe kuwa, mwaka 1958 chama cha TANU kikiwa kwenye vuguvugu kali la kupigania Uhuru, kiliwafukuza kabisa uanachama Katibu Mkuu wake Mr Mtevu, na Mwenyrkiti wa Baraza la Wazee ndugu Seleiman Bin Amir aliyekuwa na nguvu ya ushawishi hasaaa, walifukizwa waliposhindwa uchaguzi mkuu uliofanyika katika ukumbi wa shule ya wavulana ya Tabora pale kanda ya Magharibi Tabora na Julius Nyerere akawa rais wa TANU, baada ya uchaguzi ule wao walianzisha uasi kwakuanzisha chama ndani ya chama, chama hicho kilikuwa cha kidini. TANU iliyumba kwa mwaka kamamoja hivi lakini mwaka 1961 ikaingia katika uchaguzi na kushinda.
Kwanza niwaambie kuwa Chama cha siasa kilichokomaa na chenye wanachama wenye nguvu ya kitaifa kinapotokea kumuwajibisha mwanachama yeyote mwenye nguvu ya kitaifa, kovu lake huwa halizibwi kwa miezi mitatu au sita tu, kisayansi itachukua mwaka kuirejesha nguvu ya chama katika mizani stahiki ya kisiasa.
Hivyo Mwanachadema yeyote na mwanamageuzi ni lazima atambue kuwa uchaguzi wa Udiwani huu kwa kata 27 nchini, sio kipimo cha kufuta pengo la akina Zitto. Labda kwa mchambuzi wa siasa asiejua sayansi ya siasa tu na mwenye agenda ya kipropaganda ndie ataamini kufukuzwa akina Zitto ni chanzo cha kushindwa uchaguzi huu.
Athari za kufukuzwa kwa Zitto na wenzie ndani ya chama zitapimwa baada ya Mwaka mmoja kutoka sasa hii ikiwa na maana uchaguzi mkuu ujao, kwa sasa yanayotokea nikuwa yalitarajiwa kwa 100% na yalipita kwenye chekecho la kimkakati kisha yakaamuliwa iwe hivyo.
Kosa kubwa kwa Chadema ni kosa la kimkakati na hili ni lazima lifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo,
Kwanza ieleweke kuwa daftari la wapiga kura ndio rungu lililoibeba ccm, ni lazima liboreshwe ikiwa ni pamoja na uingizaji wawapiga kura wapya, idadi kubwa ya wapiga kura hawakupiga kura kutokana na sababu mbalimbali kama kuuza shahada zao.
Wanamikakati tukae chini tuwafanyie utafiti wa kisayanzi viongozi wa majimbo, mikoa na kanda, nilazima tuwapime kwa nyuzi 360 kiutendaji kwakuwa hizi chaguzi ndogo za kata na serikali za mitaa zinatakiwa wao wasimamie na kuonyesha uwezo wao na sio hivyo tu bali lipo ndani ya uwezo wao kikatiba,
Ni lazima tufanye utafiti wa kimkakati usio na unafiki wala haya,
Tukiyatekeleza haya yote, uchaguzi wa serikali za mitaa utaanza kutupa majibu ya mkakati huu.
Yote kwa yote Chadema haijapoteza uchaguzi huu, kimkakati ni ccm ndio imepoteza,
Propaganda zenu ziko too much biased kiasi kwamba mnawaamisha wapiga kura wenu kuwa everything is rosy na kama kuna lawama basi wa kulaumiwa ni chama tawala.
Yetu macho na masikio.