Mkuu ukawa imepata 38% na Ccm 47% take it from me...
Hiyo 14% mnajifariji pamoja na mapingamizi na kuapisha ambao hawaja shinda na wale ambao walishinda bila kupigiwa kura hahahaha
View attachment 217817
Nimekupata Mkuu, kumbuka kwenye Fomu ya mgombea inaeleza wazi tena kwa lugha rahisi sana kuwa , taarifa za mgombea zisiwe na makosa, na endapo fomu husika ikiwa na makosa, mgombea atakuwa amekosa sifa za kugombea, Sasa hebu tueleze , Je Ulitaka wagombea walikosa sifa waruhusiwe tu kugombea hata kama wamejaza fomu kwa makosa? mfano, Fomu inamtaka ataje jina la chama chake, mgombea anaandika CCM, au CDM, au NCCR-Mageuzi, wakati hakuna vyama vinavyoitwa kwa majina hayo kwa Msajiri, Je waruhusiwe tu?, Wengine walijaza majina mwawili tu wakati fomu inataka majina kamili matatu, je waruhusiwe tu kwa vile wanatoka chama fulani?, wengine waliandika hivi kwa mfano, Ally. H. Hamis au John M.Samweli, Je waruhusiwe ili mapingamizi yasiwepo? Uchaguzi ulikuwa ukiongozwa kwa sheria, je ni halali kupinga au kuzuia viongozi kuapa kwa madai eti hawakushinda, nakuwa walioshinda wamezuiwa kuapa? Je kutumia mawe,marungu, visu,mapanga,ni njia halali ya kuwatetea viongozi ambao wamezuiwa kuapa? Je kama kweli Serikali inageuza utaratibu kwa kuwaapisha wale ambao hawakushinda na kuwaacha wale walioshinda, sasa je kwa wale viongozi wa Chadema waliotangazwa na wasimamizi kuwa wameshinda, tuamini kuwa kumbe na wenyewe nao hawakushinda ila walioshinda ni wa vyama vingine? Jamani tuwe wakweli na tujadili siasa kama watu wenye uelewa, na hoja zetu zisitawaliwe na chuki, itikadi, wivu, Mimi ningependa sana hoja zetu zitawaliwe na ukweli, takwimu, uelewa, ushahidi, na sheria. Huwa sifurahii sana mtu kuchangia kwa maneno kama haya; Chama hiki sikipendi , ukimuuliza ubaya hawezi kuuleza, hata mkifunua ukurasa kwa ukurasa aseme "Sera ya Chama hiki hasa eneo hili", siyo zuri linaturudisha nyuma. TUWE WATANZANIA BADALA YA WATAZAMIAJI.