Tathmini: Matokeo ya Uchaguzi wa Udiwani uliofanyika Februari 9, 2014

Sengeon

JF-Expert Member
Dec 29, 2011
529
112
Kumekuwa na watu wengi sana wanao hudhuria mikutano ya CHADEMA hasahasa vijana. Lakini kwa mujibu wa uchunguzi nilioufanya ni kwamba vijana wengi hawaja jiandikisha kupiga kura. Hali hiyo ndio inayosababisha ccm kushinda kata nyingi zaidi.

Lakini vile vile ushindi wa ccm sio wa kujivunia sana kwa sababu CHADEMA wamekuwa wakifuatia kwa karibu sana kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa. Nawashauri CHADEMA wahakikishe kuwa wanapambana kuhakikisha daftari la kupiga kura linaboreshwa ili vijana wengi wapate fursa ya kujiandikisha. Uboreshwaji wa daftari utakuwa na faida kubwa sana kwa upinzani na hasa hasa CHADEMA.

Hata hivyo ktk uchaguzi wa kata zote hizo inaonyesha CHADEMA ndio wenye faida zaidi kwani kata zote tatu walio chukua zilikuwa Kata za CCM. Naomba CHADEMA wazingatie Ushauri huu wa kupigania uboreshaji wa daftari la kura.

Hakika nimepata mshituko mkubwa kuona matokeo ya uchaguzi wa udiwani katika kata mbalimbali yameenda ndivyo sivyo kwa upande wa chadema. Katika kata 27 ukitoa 1 zinabaki 26.

Katika kata hizi CHADEMA imepata kata 3 tu huku NCCR ikiendelea kupata hisani ya kata 1 kwenye Jimbo la Zitto Kabwe. Zilizobakia zote CCM imechukua. Sasa hapa ndipo mshituko wangu ulipoanzia.

Lakini zipo sababu kadhaa zilizopelekea matokeo haya.CHADEMA na ujazaji wa watu kwenye mikutano yake Itakumbukwa kwamba hivi karibuni uongozi wote wa juu ulipita katika mikoa kadhaa kufanya mikutano na wananchi.

Japo agenda kuu haikuwa uchaguzi huu wa madiwani lakini walitumia nafasi hiyo pia kuwanadai wagombea udiwani wake. Kwa mahudhurio tuliyokuwa tunayaona kupitia ITV na mitandao ya kijamii tungeamini kuwa hii ilikuwa nafasi ya ushindi wa kishindo safari hii. Lakini mambo yameshtua zaidi. Nadhani tujitatmini upya.

Tubadilishe mbinu za kushambulia adui. Je wahudhuriaji wote ni wapiga kura? Nilichobaini kwa mtazamo wangu ni kuwa wale wote wanohudhuria mikutano ya CHADEMA si wapiga kura halali wanaotambulika na NEC. Wale ni wapiga kura wetu wasio rasmi.

Chukua mfano wa kata ya Nyasura huko Bunda ambayo tuliambiwa toka awali kuwa tayari CCM ipo katika hali mbaya. Lakini matokeo yamekuwa tofauti. Labda palipokuwa na ukweli ni huko Njombe mjini tu ambako CHADEMA imeshinda. Nini tatizo hapa? Kwa mtazamo wa haraka haraka unakubaliana na hoja ya CHADEMA waliyokuwa wanaililia.

Hoja ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura. Hapa ndipo CCM ilipokuwa inatumia mwanya adhimu kabisa. Ni ukweli kuwa kuna wananchi wengi hawana vitambulisho vya kupigia kura. Vijana wengi nawafahamu katika eneo langu ambao ni wakereketwa wa CHADEMA hawana vitambulisho hivi.

Kwa hiyo basi, Tume ya Uchaguzi itakapoliboresha daftari hili naamini Chadema itapata mtaji mkubwa mkononi. CCM ina wapiga kura? Ndio.Hapana. Majibu yote ni sahihi kwa sasa.

CCM ina wanachama na wapiga kura waliozeeka. Kwanini? Ukiwatazama wapiga kura wengi wa CCM ni wale wanachama wao ambao si wengi. Lakini wanafanikiwa kupata kura hizo kwa sababu CHADEMA haina wapiga kura wa kutosha ukilinganisha na idadi kamili ya wahudhuriaji wa mikutano yake.

Akina mama ndio wapiga kura namba moja kwa CCM. Idadi hii itazidiwa pindi daftari la wapiga kura litakpoboeshwa. Ni kweli CCM inanunua wapiga kura? yawezekana kweli lakini binafsi napingana na hoja hii.

Hivi tunaposema wananunua wapiga kura kwa kuchukua shahada zao, wao wenyewe wahusika wanakuwa wamejitoa ufahamu? Madai haya nayasikia kwa muda mrefu sana. Lakini mbona mimi katika eneo langu hawaji kunishawishi kununua hiyo shahada? Au wanaangalia na mtu mwenyewe wakiona unajitambua wanakuruka? Wananchi ndio wajinga kwa kukubali kuuza shahada hizo kwa bei ya kujidhalilisha.

Ushauri wangu CHADEMA tujipange upya. Tujitathmini. Kwa mwenendo ninaouona kwa sasa, chaguzi za serikali za mitaa tutapata aibu kubwa na hapo ndipo ndoto ya Ikulu itakapoyeyuka.

Nimeshauri sana kwa baadhi ya viongozi wa mkoa kujikita zaidi vijijini ambako mwamko umeanza kujitokeza kwa kuunga mkono upinzani. Sasa tusiwakatishe tamaa. Viongozi hatupendi kwenda kufanya mikutano vijijini.

Tayari mjini watu wameshaelewa umuhimu. Tusahihishe makosa yetu. Kipimo kikuuu cha CHADEMA kuingia Ikulu kitatokana na namna tutakavyojipanga kwenye serikali za mitaa. Hadi hivi sasa tunakosa wagombea wa serikali za mitaa. Hatujajipanga. Tukiendelea kulalamika tu kwa mbinu chafu wanazofanya CCM tutaishia kulia kila siku.

Kumbukeni kuwa Jeshi la Polisi hasa viongozi wake wakuu wote wapo CCM. Huwezi kupata cheo serikalini kwa sasa kama wewe si mwanachama wa CCM.

Hivyo basi, kufikiri jeshi la polisi hasa viongozi wake kuunga mkono upinzani ni ndoto kubwa ambayo hatupaswi kuota usiku wala mchana. Ni hayo tu kwa sasa. Nimesikitika sana kwa matokeo haya.

Nimeshiriki hatua zote za uchaguzi katika katika kata 27 nchini, nasema nimeshiriki kwa 100%, sijasimuliwa, wala kusikia tu,

Uchaguzi wa udiwani katika Kata 27 umemalizika kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujinyakulia ushindi.

Hata hivyo, ushindi wa chama hicho katika uchaguzi huu ulitarajiwa kwa sababu nyingi zikiwemo zile zilizozoeleka nyakati zote za uchaguzi kama, kutumia vyombo vya dola, na serikali kwa ujumla kuwadaidia wao.

Hoja ya msingi hapa ni je haya yametokea katika uchaguzi huu tu ama yalikuwepo katika chaguzi zote??

Kuna wanaoamini kuwa Chadema kuwaadhibu wanachama wake waliovunja katiba ya Chama Zitto, Killa, Mwigamba eti ni "Mgogoro" uliochangia kwa 100% kushindwa uchaguzi huu.

Nikubaliane nao wale wafikirio hivyo akini niwape shule ya falsa ya siasa kidemorasia,

Niwakumbushe kuwa, mwaka 1958 chama cha TANU kikiwa kwenye vuguvugu kali la kupigania Uhuru, kiliwafukuza kabisa uanachama Katibu Mkuu wake Mr Mtevu, na Mwenyrkiti wa Baraza la Wazee ndugu Seleiman Bin Amir aliyekuwa na nguvu ya ushawishi hasaaa, walifukizwa waliposhindwa uchaguzi mkuu uliofanyika katika ukumbi wa shule ya wavulana ya Tabora pale kanda ya Magharibi Tabora na Julius Nyerere akawa rais wa TANU, baada ya uchaguzi ule wao walianzisha uasi kwakuanzisha chama ndani ya chama, chama hicho kilikuwa cha kidini. TANU iliyumba kwa mwaka kamamoja hivi lakini mwaka 1961 ikaingia katika uchaguzi na kushinda.

Kwanza niwaambie kuwa Chama cha siasa kilichokomaa na chenye wanachama wenye nguvu ya kitaifa kinapotokea kumuwajibisha mwanachama yeyote mwenye nguvu ya kitaifa, kovu lake huwa halizibwi kwa miezi mitatu au sita tu, kisayansi itachukua mwaka kuirejesha nguvu ya chama katika mizani stahiki ya kisiasa.

Hivyo Mwanachadema yeyote na mwanamageuzi ni lazima atambue kuwa uchaguzi wa Udiwani huu kwa kata 27 nchini, sio kipimo cha kufuta pengo la akina Zitto. Labda kwa mchambuzi wa siasa asiejua sayansi ya siasa tu na mwenye agenda ya kipropaganda ndie ataamini kufukuzwa akina Zitto ni chanzo cha kushindwa uchaguzi huu.

Athari za kufukuzwa kwa Zitto na wenzie ndani ya chama zitapimwa baada ya Mwaka mmoja kutoka sasa hii ikiwa na maana uchaguzi mkuu ujao, kwa sasa yanayotokea nikuwa yalitarajiwa kwa 100% na yalipita kwenye chekecho la kimkakati kisha yakaamuliwa iwe hivyo.

Kosa kubwa kwa Chadema ni kosa la kimkakati na hili ni lazima lifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo,

Kwanza ieleweke kuwa daftari la wapiga kura ndio rungu lililoibeba ccm, ni lazima liboreshwe ikiwa ni pamoja na uingizaji wawapiga kura wapya, idadi kubwa ya wapiga kura hawakupiga kura kutokana na sababu mbalimbali kama kuuza shahada zao.

Wanamikakati tukae chini tuwafanyie utafiti wa kisayanzi viongozi wa majimbo, mikoa na kanda, nilazima tuwapime kwa nyuzi 360 kiutendaji kwakuwa hizi chaguzi ndogo za kata na serikali za mitaa zinatakiwa wao wasimamie na kuonyesha uwezo wao na sio hivyo tu bali lipo ndani ya uwezo wao kikatiba,

Ni lazima tufanye utafiti wa kimkakati usio na unafiki wala haya,

Tukiyatekeleza haya yote, uchaguzi wa serikali za mitaa utaanza kutupa majibu ya mkakati huu.

Yote kwa yote Chadema haijapoteza uchaguzi huu, kimkakati ni ccm ndio imepoteza,

Wadau, ni kama wamekata tamaa hivi.

  1. Saed Kubenea ambaye ni mshauri mkuu wa CHADEMA kwenye masuala ya kisiasa na kiusalama, amesema kuwa CHADEMA wasijidanganye kuiondoa CCM ilhali hawana mikakati ya kufanikisha hilo
  2. Kubenea amekiri kuwa mgawanyiko wa ndani ya CHADEMA umekiathiri chama ingawa ameshindwa kushauri jinsi ya kuzuia mgawanyiko huo.
  3. Kubenea ameendeleza siasa zake za uongo kwa kutoa ushahidi usiolingana na alichokieleza. Ni kama amechanganyikiwa au amerukwa na akili. Hakika kipigo hiki kimewachanganya wengi.

JISOMEE MWENYEWE ALICHOKIANDIKA JANA

HIZI NDIO SABABU ZA CHADEMA KUSHINDWA VIBAYA UCHAGUZI WA UDIWANI KATIKA KATA 27

Uchaguzi wa udiwani katika Kata 27 umemalizika kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujinyakulia ushindi mnono.

Hata hivyo, ushindi wa chama hicho katika uchaguzi huu ulitarajiwa kwa sababu mbili kubwa.

Kwanza, kama ilivyokuwa katika chaguzi zilizopita, CCM wameingia katika uchaguzi huu wakiwa na mtaji mkubwa wa kusaidiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kushinda, pamoja na jeshi la polisi.

Aidha, CCM wamengia katika uchaguzi huu huku serikali kwa ujumla wake ikiwa upande wake. Ushahidi wa hilo, ni nyaraka hii hapa ninayoibandika hapa.

Pili, washindani wakuu wa CCM – Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeingia katika uchaguzi kikiwa kimekatika vipande viwili kutokana na mgogoro wa uongozi kati ya Zitto Kabwe na wenzake kwe nye chama.

Ni mwendawazimu tu, anayeweza kusema mgogoro ndani ya CHADEMA haukukiathiri chama hicho. Hamuwezi kuingia katika uchaguzi na mkategemea kushinda, wakati hamko wamoja; hamuwezi kuingia katika uchaguzi wakati wapenzi na washabiki wenu wakiwa wamegawanyika. Haiwezekani.

Kuingia katika uchaguzi katika mazingira hayo, matokeo yake ni hayo.

Kwa msingi huo, ili CCM kiweze kung'olewa kwenye madaraka

Kwa msingi huo, ili CCM kiweze kuondolewa madarakani, sharti CHADEMA kuwe na amani. Sharti NEC isiwe tawi la CCM kama ilivyo sasa.

Vinginevyo, miaka nenda rudi, CCM kitaendelea kutawala,wakati tayari kimekubwa na mchoko.

Kumekuwa na watu wengi sana wanao hudhuria mikutano ya Cdm hasahasa vijana. Lakini kwa mujibu wa uchunguzi nilioufanya ni kwamba vijana wengi hawaja jiandikisha kupiga kura. Hali hiyo ndio inayosababisha ccm kushinda kata nyingi zaidi. Lakini vile vile ushindi wa ccm sio wa kujivunia sana kwa sababu Cdm wamekuwa wakifuatia kwa karibu sana kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa. Nawashauri Cdm wahakikishe kuwa wanapambana kuhakikisha daftari la kupiga kura linaboreshwa ili vijana wengi wapate fursa ya kujiandikisha. Uboreshwaji wa daftari utakuwa na faida kubwa sana kwa upinzani na hasa hasa Cdm. Hata hivyo ktk uchaguzi wa kata zote hizo inaonyesha Cdm ndio wenye faida zaidi kwani kata zote tatu walio chukua zilikuwa Kata za Ccm. Naomba chadema wazingatie Ushauri huu wa kupigania uboreshaji wa daftari la kura.

miaka yote CHADEMA wanakuwa wanafuatia kwa karibu hivyo hivyo wala wasifikiri kuna improvement yoyote.
 
Vipi na hizo kata chadema walizoshinda daftafi la wapiga kura zilirekebishwa? ?
 
Hilo neno ila kwa asiye jua siasa atakupinga kwa sababu ni shabiki wa siasa
 
CCM wanajua siku watathubutu tu kuboresha daftari la wapiga kura - KITANZI. Cha msingi waendelee kugomea
 
"Performance yetu kwenye chaguzi ndogo nayo ni ishara kwamba mabadiliko yanahitajika. Tanguuongozi huu uingie madarakani, kumefanyika chaguzi ndogo 8 za wawakilishi kwenye chombo kikuu, kati ya hizo tumeshinda 2 tu sawa na asilimia 25.

Aidha baada ya mwaka 2010 kumefanyika chaguzi kadhaa za wawakilishi kwenyehalmashauri. Mwezi Oktoba 2011, mwezi wa 4 2012, mwezi Septemba 2012 na mwezi Juni2013. Kote performance yetu imekuwa poor kupindukia. Mfano mwezi wa Juni 2013 tumepata viti 6 kati ya 22 (27%) na mwezi Septemba 2012 tulipata viti 7 kati ya29 (24%).

Ni dhahiri mabadiliko yanahitajika kwa kuwa wakuu waliopo wanatumia mbinu zile zile na kupata matokeo yale yale. Tunahitaji mbinu mpya. Kwa kifupi, ushindi ambao tumekuwa tukiupata katika chaguzi ndogo haulingani na ukubwa wa hamasa kwa taasisi yetu iliyopo mitaani. Hii ni kwa sababu tumekuwa tukitumia mbinu hizohizo katika kila chaguzi. Aidha, tu wepesi mno wa kuridhika na kujisifu kwa mafanikio madogo badala ya kukaa chini na kutafakari kwa kina mahala tunapojikwaa".

Dr.Kitila Mkumbo & Mr. Samson Mwigamba, Mkakati wa Mabadiliko, Dar es salaam, 2013.
 
Hakika nimepata mshituko mkubwa kuona matokeo ya uchaguzi wa udiwani katika kata mbalimbali yameenda ndivyo sivyo kwa upande wa chadema. Katika kata 27 ukitoa 1 zinabaki 26.

Katika kata hizi CHADEMA imepata kata 3 tu huku NCCR ikiendelea kupata hisani ya kata 1 kwenye Jimbo la Zitto Kabwe. Zilizobakia zote CCM imechukua. Sasa hapa ndipo mshituko wangu ulipoanzia.

Lakini zipo sababu kadhaa zilizopelekea matokeo haya.CHADEMA na ujazaji wa watu kwenye mikutano yake Itakumbukwa kwamba hivi karibuni uongozi wote wa juu ulipita katika mikoa kadhaa kufanya mikutano na wananchi.

Japo agenda kuu haikuwa uchaguzi huu wa madiwani lakini walitumia nafasi hiyo pia kuwanadai wagombea udiwani wake. Kwa mahudhurio tuliyokuwa tunayaona kupitia ITV na mitandao ya kijamii tungeamini kuwa hii ilikuwa nafasi ya ushindi wa kishindo safari hii. Lakini mambo yameshtua zaidi. Nadhani tujitatmini upya.

Tubadilishe mbinu za kushambulia adui. Je wahudhuriaji wote ni wapiga kura? Nilichobaini kwa mtazamo wangu ni kuwa wale wote wanohudhuria mikutano ya CHADEMA si wapiga kura halali wanaotambulika na NEC. Wale ni wapiga kura wetu wasio rasmi.

Chukua mfano wa kata ya Nyasura huko Bunda ambayo tuliambiwa toka awali kuwa tayari CCM ipo katika hali mbaya. Lakini matokeo yamekuwa tofauti. Labda palipokuwa na ukweli ni huko Njombe mjini tu ambako CHADEMA imeshinda. Nini tatizo hapa? Kwa mtazamo wa haraka haraka unakubaliana na hoja ya CHADEMA waliyokuwa wanaililia.

Hoja ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura. Hapa ndipo CCM ilipokuwa inatumia mwanya adhimu kabisa. Ni ukweli kuwa kuna wananchi wengi hawana vitambulisho vya kupigia kura. Vijana wengi nawafahamu katika eneo langu ambao ni wakereketwa wa CHADEMA hawana vitambulisho hivi.

Kwa hiyo basi, Tume ya Uchaguzi itakapoliboresha daftari hili naamini Chadema itapata mtaji mkubwa mkononi. CCM ina wapiga kura? Ndio.Hapana. Majibu yote ni sahihi kwa sasa.

CCM ina wanachama na wapiga kura waliozeeka. Kwanini? Ukiwatazama wapiga kura wengi wa CCM ni wale wanachama wao ambao si wengi. Lakini wanafanikiwa kupata kura hizo kwa sababu CHADEMA haina wapiga kura wa kutosha ukilinganisha na idadi kamili ya wahudhuriaji wa mikutano yake.

Akina mama ndio wapiga kura namba moja kwa CCM. Idadi hii itazidiwa pindi daftari la wapiga kura litakpoboeshwa. Ni kweli CCM inanunua wapiga kura? yawezekana kweli lakini binafsi napingana na hoja hii.

Hivi tunaposema wananunua wapiga kura kwa kuchukua shahada zao, wao wenyewe wahusika wanakuwa wamejitoa ufahamu? Madai haya nayasikia kwa muda mrefu sana. Lakini mbona mimi katika eneo langu hawaji kunishawishi kununua hiyo shahada? Au wanaangalia na mtu mwenyewe wakiona unajitambua wanakuruka? Wananchi ndio wajinga kwa kukubali kuuza shahada hizo kwa bei ya kujidhalilisha.

Ushauri wangu CHADEMA tujipange upya. Tujitathmini. Kwa mwenendo ninaouona kwa sasa, chaguzi za serikali za mitaa tutapata aibu kubwa na hapo ndipo ndoto ya Ikulu itakapoyeyuka.

Nimeshauri sana kwa baadhi ya viongozi wa mkoa kujikita zaidi vijijini ambako mwamko umeanza kujitokeza kwa kuunga mkono upinzani. Sasa tusiwakatishe tamaa. Viongozi hatupendi kwenda kufanya mikutano vijijini.

Tayari mjini watu wameshaelewa umuhimu. Tusahihishe makosa yetu. Kipimo kikuuu cha CHADEMA kuingia Ikulu kitatokana na namna tutakavyojipanga kwenye serikali za mitaa. Hadi hivi sasa tunakosa wagombea wa serikali za mitaa. Hatujajipanga. Tukiendelea kulalamika tu kwa mbinu chafu wanazofanya CCM tutaishia kulia kila siku.

Kumbukeni kuwa Jeshi la Polisi hasa viongozi wake wakuu wote wapo CCM. Huwezi kupata cheo serikalini kwa sasa kama wewe si mwanachama wa CCM.

Hivyo basi, kufikiri jeshi la polisi hasa viongozi wake kuunga mkono upinzani ni ndoto kubwa ambayo hatupaswi kuota usiku wala mchana. Ni hayo tu kwa sasa. Nimesikitika sana kwa matokeo haya.
 
Nchi hii ina kila kitu isipokuwa WATANZANIA tu!

Hivi kwa matatizo yote haya ambayo CCM imetusababishia,unaweza kupoteza muda wako kwenda kwenye kituo cha kupigia kura kuipigia CCM kura kweli?
 
Nimeshiriki hatua zote za uchaguzi katika katika kata 27 nchini, nasema nimeshiriki kwa 100%, sijasimuliwa, wala kusikia tu,

Uchaguzi wa udiwani katika Kata 27 umemalizika kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujinyakulia ushindi.

Hata hivyo, ushindi wa chama hicho katika uchaguzi huu ulitarajiwa kwa sababu nyingi zikiwemo zile zilizozoeleka nyakati zote za uchaguzi kama, kutumia vyombo vya dola, na serikali kwa ujumla kuwadaidia wao.

Hoja ya msingi hapa ni je haya yametokea katika uchaguzi huu tu ama yalikuwepo katika chaguzi zote??

Kuna wanaoamini kuwa Chadema kuwaadhibu wanachama wake waliovunja katiba ya Chama Zitto, Killa, Mwigamba eti ni "Mgogoro" uliochangia kwa 100% kushindwa uchaguzi huu.

Nikubaliane nao wale wafikirio hivyo akini niwape shule ya falsa ya siasa kidemorasia,

Niwakumbushe kuwa, mwaka 1958 chama cha TANU kikiwa kwenye vuguvugu kali la kupigania Uhuru, kiliwafukuza kabisa uanachama Katibu Mkuu wake Mr Mtevu, na Mwenyrkiti wa Baraza la Wazee ndugu Seleiman Bin Amir aliyekuwa na nguvu ya ushawishi hasaaa, walifukizwa waliposhindwa uchaguzi mkuu uliofanyika katika ukumbi wa shule ya wavulana ya Tabora pale kanda ya Magharibi Tabora na Julius Nyerere akawa rais wa TANU, baada ya uchaguzi ule wao walianzisha uasi kwakuanzisha chama ndani ya chama, chama hicho kilikuwa cha kidini. TANU iliyumba kwa mwaka kamamoja hivi lakini mwaka 1961 ikaingia katika uchaguzi na kushinda.

Kwanza niwaambie kuwa Chama cha siasa kilichokomaa na chenye wanachama wenye nguvu ya kitaifa kinapotokea kumuwajibisha mwanachama yeyote mwenye nguvu ya kitaifa, kovu lake huwa halizibwi kwa miezi mitatu au sita tu, kisayansi itachukua mwaka kuirejesha nguvu ya chama katika mizani stahiki ya kisiasa.

Hivyo Mwanachadema yeyote na mwanamageuzi ni lazima atambue kuwa uchaguzi wa Udiwani huu kwa kata 27 nchini, sio kipimo cha kufuta pengo la akina Zitto. Labda kwa mchambuzi wa siasa asiejua sayansi ya siasa tu na mwenye agenda ya kipropaganda ndie ataamini kufukuzwa akina Zitto ni chanzo cha kushindwa uchaguzi huu.

Athari za kufukuzwa kwa Zitto na wenzie ndani ya chama zitapimwa baada ya Mwaka mmoja kutoka sasa hii ikiwa na maana uchaguzi mkuu ujao, kwa sasa yanayotokea nikuwa yalitarajiwa kwa 100% na yalipita kwenye chekecho la kimkakati kisha yakaamuliwa iwe hivyo.

Kosa kubwa kwa Chadema ni kosa la kimkakati na hili ni lazima lifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo,

Kwanza ieleweke kuwa daftari la wapiga kura ndio rungu lililoibeba ccm, ni lazima liboreshwe ikiwa ni pamoja na uingizaji wawapiga kura wapya, idadi kubwa ya wapiga kura hawakupiga kura kutokana na sababu mbalimbali kama kuuza shahada zao.

Wanamikakati tukae chini tuwafanyie utafiti wa kisayanzi viongozi wa majimbo, mikoa na kanda, nilazima tuwapime kwa nyuzi 360 kiutendaji kwakuwa hizi chaguzi ndogo za kata na serikali za mitaa zinatakiwa wao wasimamie na kuonyesha uwezo wao na sio hivyo tu bali lipo ndani ya uwezo wao kikatiba,

Ni lazima tufanye utafiti wa kimkakati usio na unafiki wala haya,

Tukiyatekeleza haya yote, uchaguzi wa serikali za mitaa utaanza kutupa majibu ya mkakati huu.

Yote kwa yote Chadema haijapoteza uchaguzi huu, kimkakati ni ccm ndio imepoteza,
 
Kinachotakiwa ni kufanyia kazi chambuzi za kisomi na sio, kuitana ''wahaini'' , ''wasaliti''...........ila hili linaendeea kuwavua nguo misukule na vifaranga kwani waliumia muda mwingi kuongopa na kuwachafua wenzao........zamu yao imefika!
 
Hata hivyo, ushindi wa chama hicho katika uchaguzi huu ulitarajiwa kwa sababu nyingi zikiwemo zile zilizozoeleka nyakati zote za uchaguzi kama, kutumia vyombo vya dola, na serikali kwa ujumla kuwadaidia wao.

Kama ndivyo hakuna haja ya kumtafuta mchawi zaidi ni kujipanga kukabiliana na hizo changamoto kwenye Chaguzi zijazo.
 
Chadema tuliyoijua sisi,ilisheheni wapanga mikakati,wajuzi wa sayansi ya siasa,chadema ya sasa imegeuka kuwa kijiwe cha wajuaji,wapanga matukio ili wapate umaarufu wa kubebwa na kushangiliwa,sioni future njema ya siasa za chadema mikononi mwa lema,msigwa na wajuaji wenzio ambao ndo wamegeuka wajua chama,wapanga mikakati kwa mwenyekiti,ukweli huu waweza pingwa sana,lakini tutarajie mavuno ya mabua zaidi katika chaguzi zijazo.
 
Insanity: doing the same thing over and over again expecting different results. - Einstein

Hapa nafikiri tunashuhudia vichaa wa siasa za Tanzania.
 
Nakubaliana na wewe rungu la kuiadhibu hawa wakolon weusi.ni kuboresha daftari la wapiga kura tu.
 
Uliyosema ni sahihi kabisa ila swala la maboresho ya daftari la wapiga kura lita chukua muda kwa sababu CCM na Serilali wana jua kuwa kama wataruhusu daftari kuboreshwa vijana wengi wataingia na huo ndio utakuwa ushindi wa vyama vya upinzan.
 
Wewe unayejiita Yericko Nyerere ni miongoni mwa wafuasi wa Lema ambao mmekuwa mkimdanganya sana Mwenyekiti wenu taifa kwa siasa za majitaka kwa kumwita mhaini kila anayetaka kuleta mabadiliko ndani ya chama.

Endeleeni kujidanganya tutaona chama kitakakoishia. Kama unajua CCM wana uwezo wa kunyang'anya ushindi, kwa nini unawadanganya watu kwamba mkifukuza mnaoita wahaini basi chama kinaingia madarakani 2015. Au mwaka huo CCM haitakuwepo?

Bila kufanya mabadiliko ya uongozi mtakesha!!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ngalikivembu pole sana, kwani wewe unaishi wapi???? Mbona chadema imeendelea kuongeza viti kwa kuvinyang'anya toka ccm??? Ok laskini pia hebu chunguza na uone kote tulikoshinda chadema ni kwa maumivu na vipigo tulivyopata kwa kulind kura zetu na sio vinginevyo, uchaguzi wote huu na kama kila mahali kungelindwa kwa vipigo na maumivu kama hayo hakika matokeo yangekuwa ccm 3, nccr 1 na chadema 23 bali ni sehemu chache zenye wabunge na watu jasiri kama kamanda lemma tu ndio tunapata ushindi na hakuna mahali ulinzi wa kura ulipoimarishwa na tukashindwaaaaaaa.

Ukweli ni kwamba kule tumeshindwa ni kwa nguvu za policcm, serikali, na tume yao ya uchaguzi, lakini ndani ya mioyo ya umma wa watanzania tumeshinda na tutashinda..................twende kazi mkuu tuko vyema.
 
Last edited by a moderator:
Chadema tafakarini sana!Mna kazi nzito sana kuing'oa sisiemu,acheni maneno ya kujifariji mbivu na mbichi zimeonekana katika uchaguzi huu mdogo.Why ushindi ni Kilimanjaro na Arusha tuu kwa asilimia kubwa?
 
Back
Top Bottom