CHADEMA imeng'ara kwenye Uchaguzi na Itashinda 2015

CHADEMA imeng'ara kwenye Uchaguzi na Itashinda 2015

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,026
Reaction score
20,511
Inawezekana kauli yangu isiwaingie watu masikioni mwao kabisa, lakini nitawaeleza japo kwa kifupi.

Katika siasa kuna kitu kinaitwa siasa za jumla (general politics) na siasa za kijiografia (geography politics)

General politics inahusu mambo yanayohusu siasa za kitaifa bila kuchagua chama au itikadi na hizi mara nyingi husimamiwa kwa katiba, kanuni na sheria za nchi, hapa inahusiana pia na daftari la wapiga kura na tume ya uchaguzi,

Geography politics inahusu siasa za eneo husuka, kuna international gp, na domestic gp,

Katika hayo Chadema ime win kwenye Gp-D kwa asilimia zaidi ya 90%, hili linatokana na chama kushiriki uchaguzi kwa miaka yote huku mambo muhimu yanayopaswa kufanywa kwenye General Politics yakiwa doro kabisa, mambo hayo ni kama tume kuwa huru, daftari la wapigakura kuboreshwa, na dola kuvuruga chagizi nyingi kwa maslahi ya ccm.

Takwimu za chaguzi hizi zinatoa sura stahiki ya ubora wa domestic political ya Chadema,

Mathalani uchaguzi huu Chadema ilikuwa ikitetea kata 3, za Nyaisura, Kiborloni na Mikol.. Kigoma.

Tumepoteza Nyaisura, na Kigoma, na Tumeipoka ccm kata za Sombetini na Njombe.

Thamani ya kata ilizoshinda chadema nikubwa kuliko ccm, kubeba kata ya njombe ni turufu kubwa, vivyo hivyo kata ya sombetini Arusha ambapo sasa rasmi ccm inakuwa chama cha upinzani Arusha, CCM hawajaongeza thamani yoyote ya kata,

Kwa lugha nyingine nikuwa CHADEMA 0-0 CCM, lakini CHADEMA wananafasi ya golden goal kwakubeba kata ya Njombe ambayo kwanza inafuta propaganda za ccm yakuwa chadema ni chama cha ukanda, sasa tunashuhudia Chadema sio chama cha ukanda tena bali chama cha kitaifa na kila pembe ya jamhuri hii kipo.

Izingatiwe kuwa oparesheni M4C Pamoja Daima haikuwa maalumu kwaajili ya uchaguzi huu bali sehemu ya ratiba ya chama katika kutoa elimu ya umma kudai/kuhimiza uboreshaji wa daftari la wapiga kura.

Kuna wanaoamini kuwa Chadema kuwaadhibu wanachama wake waliovunja katiba ya Chama akina Zitto, Killa, Mwigamba eti ni "Mgogoro" uliochangia kwa 100% kutopata kata nyingi zaidi katika uchaguzi huu.

Nikubaliane nao wale wafikirio hivyo lakini tupeane shule ya falsa ya siasa kidemorasia kwa ufupi ambayo ndio hutawala siasa za uwanda wa chama kinachojiandaa kushika dola.

Niseme kuwa Chama cha siasa kilichokomaa na chenye wanachama wenye nguvu ya kitaifa kinapoamua kumuwajibisha mwanachama yeyote mwenye nguvu ya kitaifa aliyevunja katiba,itikadi,itifaki na falsafa ya chama hicho, kovu lake huwa halizibwi kwa miezi mitatu au sita tu, kisayansi itachukua hata mwaka kuirejesha nguvu ya chama katika mizani stahiki ya kisiasa.

Hivyo Mwanachadema yeyote na mwanamageuzi ni lazima atambue kuwa uchaguzi wa Udiwani huu kwa kata 27 nchini, sio kipimo stahiki cha kufuta pengo la akina Zitto. Labda kwa mchambuzi wa siasa asiejua sayansi ya siasa tu na mwenye agenda ya kipropaganda ndie ataamini kufukuzwa akina Zitto ni chanzo cha kupata kushindwa kupata kura nyingi zaidi katika uchaguzi huu.

Athari za kufukuzwa kwa Zitto na wenzie ndani ya chama zitapimwa baada ya miezi sita hadi mwaka mmoja kutoka sasa hii ikiwa na maana uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao ndivyo vitakuwa vipimo vyake, kwa sasa yanayotokea yalitarajiwa kwa 100% na yalipita kwenye chekecho la kimkakati la chama na kisha yakaamuliwa iwe hivyo.

Kosa kubwa kwa Chadema ni kosa la kimkakati na hili ni lazima lifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo,

Kwanza ieleweke kuwa daftari la wapiga kura ndio rungu lililoibeba ccm, ni lazima liboreshwe ikiwa ni pamoja na uingizaji wawapiga kura wapya ambao utafiti unaonyesha ni kundi kubwa la vijana wenye umri kati ya miaka 18-26 ambao hawakuwa na sifa ya kupiga kura 2010. Lakini hata hawa waliojiandikisha yaani wenye kupiga kura sasa, idadi kubwa ya wapiga kura hao hawakupiga kura kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuuza shahada zao.

Pili Tume ya Uchaguzi, hii ni lazima juhudi za msksudi zitumike kuitoa mikononi mwa chama tawala, ni hatari kuiacha iendelee kuwa wakala wa ccm badala yakuwa tume huru.

Tatu Vyombo vya dola, hapa ndipo panahitaji mkakati mkuu wa kisiasa, jeshi la polisi ni lazima tukabiliane nalo na ieleweke vema kuwa ccm haitakoma kulitumia jeshi la polisi ama vyombo vya dola kwa ujumla mpaka siku inakata roho kabisa, hivyo njia mbadala ni muhimu sana tunapoelekea kushika dola hili la Tanzania mnamo octobar 25, 2015.

Kwanza uundwe mkakati wa uhusiano mwema na vyombo vyote vya dola nchini, hili linaweza kuwa gumu kidogo na linaweza kuifanya serikali ianze kupata mafua ya msimu na kujikuta tunaingia kwenye mgogoro unaoweza kutumiwa na wakware wa akili wa ccm kama akina Mwigulu na kufikiria uhaini, jambo la muhimu ni kuziangalia sheria za nchi hasa zinazoratibu vyama vya siasa na mienendo yake,

Mathalani kiongozi wa kisiasa kuzuru makao makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania na kusikiliza changamoto zinazowakabilli, hili halina zuio kisheria, ilimradi haendi kugawa kadi za chama hapo,

Ni lazima tuitazame upya sheria inayosema mtumishi wa umma asijihusihe na siasa, hii ni nzuru lakini iboreshwe ili iwe na tafsiri ya maslahi kwa nchi na hatimae taifa kuzaa siasa za kisasa na za kimaendeleo.

Wanamikakati warejee chini wawafanyie utafiti wa kisayansi viongozi wa majimbo, mikoa na kanda, nilazima tuwapime kwa nyuzi 360 kiutendaji kwakuwa hizi chaguzi ndogo za kata na serikali za mitaa zinatakiwa wao wasimamie na kuonyesha uwezo wao na sio hivyo tu bali lipo ndani ya uwezo wao kikatiba, Chama lazima sasa kijikite kwa nguvu zote kwenye msingi (chadema ni msingi).

Ni lazima tufanye utafiti wa kimkakati usio na unafiki wala haya,

Tukiyatekeleza haya yote, uchaguzi wa serikali za mitaa utaanza kutupa majibu ya mkakati huu na uchaguzi mkuu ujao tutashinda!

Yote kwa yote Chadema haijapoteza uchaguzi huu bali imeng'ara, kimkakati ni ccm ndio imepoteza.
 
Wajinga wenzio watakasupoti. Hakuna justfication yeyote itakayofuta kichapo kikali mlichopata. Tutaheshimiana tu.
 
Hiyo ni sawa na kuisifia status quo.
Status quo
ni okay kwa chama tawala na siyo pinzani. Ila kama mnaona mmefanya vizuri, poa.
Yaani mnajisifia kuacha mambo vilevile.
 
Nyerere,
Wawekee historia tangu vyama vingi vimeanza hadi leo, waone jinsi Raia wameelewa haki zao. sasa waboreshe daftari la wapiga kura waone utamu wao.
 
asante sana YERICKO nimekuelewa sana , thamani ya kata ya NJOMBE MJINI ni kubwa mno! Labda niongeze tu kwamba OPD ndiyo iliyoitikisa TUME YA UCHAGUZI , hatimaye sasa daftari kuboreshwa hivi karibuni .
 
Hiyo ni sawa na kuisifia status quo.
Status quo
ni okay kwa chama tawala na siyo pinzani. Ila kama mnaona mmefanya vizuri, poa.
Yaani mnajisifia kuacha mambo vilevile.

Variable factors katika aspect mbalimbali za uchaguzi

1😀aftari la wapiga kura lililotumika ni lile la mwaka 2010 kwa hiyo CHADEMA kimefanya kazi kutoka pale kilipokua mwaka 2010

2: Kuna vijana wengi ambao hawajandikishwa kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura

3:Kuna maeneo ambayo CHADEMA hakikuweka mgombea mwaka 2010 lakini leo kimevuna maelfu ya kura

4:CHADEMA kilifanya operesheni kuzungumzia katiba Mpya,Kuboresha daftari la wapiga kura nchi nzima

5:Kata zilizochukuliwa CCM zimechukuliwa kwa wapiga kura wale wale wa Mwaka 2010

6:Maeneo yote ya kata hizo tuonyeshe uwiano wa kura za mwaka 2010 na kura za sasa tuweke kwenye analytical graph ili kujua pamoja na changamoto nilizotaja hapo juu kati ya CCM na CHADEMA ni kipi kimekua/kimekubalika kwa kasi tangu 2010
 
Inawezekana kauli yangu isiwaingie watu masikioni mwao kabisa, lakini nitawaeleza japo kwa kifupi.

Katika siasa kuna kitu kinaitwa siasa za jumla (general political) na siasa za kijiografia (geography political)

General political
inahusu mambo yanayohusu siasa za kitaifa bila kuchagua chama au itikadi na hizi mara nyingi husimamiwa kwa katiba, kanuni na sheria za nchi, hapa inahusiana pia na daftari la wapiga kura na tume ya uchaguzi,

Geography political inahusu siasa za eneo husuka, kuna international gp, na domestic gp,

Katika hayo Chadema ime win kwenye Gp-D kwa asilimia zaidi ya 90%, hili linatokana na chama kushiriki uchaguzi kwa miaka yote huku mambo muhimu yanayopaswa kufanywa kwenye General Political yakiwa doro kabisa, mambo hayo ni kama tume kuwa huru, daftari la wapigakura kuboreshwa, na dola kuvuruga chagizi nyingi kwa maslahi ya ccm.

Takwimu za chaguzi hizi zinatoa sura stahiki ya ubora wa domestic political ya Chadema,

Soma kaka, soma vitabu ,journals, online articles ... etc

Simaanishi darasani, jisomee tu kama hobby. Inasaidia hata kwa maisha ya kawaida.
 
Inawezekana kauli yangu isiwaingie watu masikioni mwao kabisa, lakini nitawaeleza japo kwa kifupi.

Katika siasa kuna kitu kinaitwa siasa za jumla (general political) na siasa za kijiografia (geography political)

General political inahusu mambo yanayohusu siasa za kitaifa bila kuchagua chama au itikadi na hizi mara nyingi husimamiwa kwa katiba, kanuni na sheria za nchi, hapa inahusiana pia na daftari la wapiga kura na tume ya uchaguzi,

Geography political inahusu siasa za eneo husuka, kuna international gp, na domestic gp,

Katika hayo Chadema ime win kwenye Gp-D kwa asilimia zaidi ya 90%, hili linatokana na chama kushiriki uchaguzi kwa miaka yote huku mambo muhimu yanayopaswa kufanywa kwenye General Political yakiwa doro kabisa, mambo hayo ni kama tume kuwa huru, daftari la wapigakura kuboreshwa, na dola kuvuruga chagizi nyingi kwa maslahi ya ccm.

Takwimu za chaguzi hizi zinatoa sura stahiki ya ubora wa domestic political ya Chadema,

Mathalani uchaguzi huu Chadema ilikuwa ikitetea kata 3, za Nyaisura, Kiborloni na Mikol.. Kigoma.

Tumepoteza Nyaisura, na Kigoma, na Tumeipoka ccm kata za Sombetini na Njombe.

Tamani ya kata ilizoshinda chadema nikubwa kuliko ccm, kubeba kata ya njombe ni turufu kubwa, vivyo hivyo kata ya sombetini. CCM hawajaongeza thamani yoyote ya kata,

Kwa lugha nyingine nikuwa CHADEMA 0-0 CCM, lakini CHADEMA wananafasi ya golden goal kwakubeba kata ya Njombe ambayo kwanza inafuta propaganda za ccm yakuwa chadema ni chama cha ukanda, sasa tunashuhudia Chadema sio chama cha ukanda tena bali chama cha kitaifa na kila pembe ya jamhuri hii.

Izingatiwe kuwa oparesheni Pamoja Daima haikuwa maalumu kwaajili ya uchsguzi huu bali sehemu ya ratiba ya chama katika kutoa elimu ya umma kudai/kuhimiza uboreshaji wa daftari la wapiga kura.

Naamini hapo mmenipata ndugu zangu mnaojenga hoja dhaifu kuwa kama dhana ni daftari la wapiga kura na polisi why kwingine chadema imeshinda?

Kaka usisahau kuwaambia sisi hatukutumia polisi kama wao wabunge wetu waliwekwa ndani upigaji kura ukiwa unaendelea mimi kuchukuwa sombetini kwangu ni kama kuchukuwa nchi

USHAURI WANGU
Jografia imeonyesha wazi propaganda ya udini ndio nguzo yao tuwashe chopa zote tuzunguke nchi nzima tuelimishe wananchi kuhusu hii sumu ya ccm iliyo na madhara kwa taifa letu.HONGERA cdm tutamaliza na mungu tu!
 
Kwa mtazamo wangu, wengi wanaohudhuria mikutano ya CHADEMA, ni wapenzi haswa wa CHADEMA. Lakini kutokana na kuhamahama kutafuta maisha, wengi wa hao wapenzi wa CHADEMA utagundua walijiandikisha katika kata, jimbo au mkoa mwingine, na hawana sifa ya kupiga kura pamoja na kwamba wangependa wapige. CCM ina advantage kwamba wanachama wake ni walewale wasiohangaika huku na kule kutafuta maisha bora, ni wakazi wa hapo hapo wanaoletewa mahitaji yao na watoto wao waliopo mikoani, kwa hiyo ukifika wakati wa uchaguzi wapiga kura halisi wa CCM wanakuwapo tayari, huku vijana wahangaikaji wa CHADEMA wanakuwa wamefuata biashara mbalimbali huku na huku, na hata waliopo eneo hilo wanakuwa walijiandikisha sehemu nyingine. Tatizo hili lingekwisha kwa kuboresha daftari la wapiga kura, lakini CCM wanajua kuwa daftari likiboreshwa tu watashindwa. Ndio maana usishangae kauli za serikali kwamba hakuna fedha za kuboresha daftari la wapiga kura! Uongo mtupu, wanajua likiboreshwa wananchi walliopo kata husika wakati huo watapata fursa ya kuwa na sifa za kuwa wapiga kura halali. Jaribu kufanya tathmini ndogo tu, hivi katika eneo lako, ni watu wangapi na wa aina gani waliokuwapo mwaka 2010 ambao sasa either hawapo au wanakuja na kuondoka? Jiulize kuna wakazi wangapi ambao hawakuwepo eneo lako lakini sasa wapo? Solution ni kuboresha daftari, jambo ambalo serikali ya CCM inaliogopa!
 
Nyerere,
Wawekee historia tangu vyama vingi vimeanza hadi leo, waone jinsi Raia wameelewa haki zao. sasa waboreshe daftari la wapiga kura waone utamu wao.

vijana mil 5 unusu wanasubiri kujiandikisha , katiba mpya ikija na MUUNDO MPYA WA TUME YA UCHAGUZI , huo ndiyo UTAKUWA mwisho wa ccm mkuu ,HAWA POLISI wengi sana ni wanaCDM , hata CCM wenyewe wanajua , wanamtUMIKIA KAFIRI TU ILI MKATE WAO WAUPATE .
 
Wajinga wenzio watakasupoti. Hakuna justfication yeyote itakayofuta kichapo kikali mlichopata. Tutaheshimiana tu.

Kichapo kikali ni CCM kupoteza Kata ya Sombetini-Arusha.

Inawauma sana maana tamaa yenu ni mapato ya Jiji la Arusha Mmezoea kuiba mpaka mnahamisha watu waaminifu kama akina MkurugenziLiana.
 
Variable factors katika aspect mbalimbali za uchaguzi

1😀aftari la wapiga kura lililotumika ni lile la mwaka 2010 kwa hiyo CHADEMA kimefanya kazi kutoka pale kilipokua mwaka 2010

2: Kuna vijana wengi ambao hawajandikishwa kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura

3:Kuna maeneo ambayo CHADEMA hakikuweka mgombea mwaka 2010 lakini leo kimevuna maelfu ya kura

4:CHADEMA kilifanya operesheni kuzungumzia katiba Mpya,Kuboresha daftari la wapiga kura nchi nzima

5:Kata zilizochukuliwa CCM zimechukuliwa kwa wapiga kura wale wale wa Mwaka 2010

6:Maeneo yote ya kata hizo tuonyeshe uwiano wa kura za mwaka 2010 na kura za sasa tuweke kwenye analytical graph ili kujua pamoja na changamoto nilizotaja hapo juu kati ya CCM na CHADEMA ni kipi kimekua/kimekubalika kwa kasi tangu 2010
Politics is a game of numbers.

Miaka minne iliyopita kulikuwa na wagombea tofauti, marehemu mzee Sumari alimshinda Nasari. Hii haimaanishi mtu yeyote kutoka CCM angemshinda Nasari.

Tatizo siyo daftari la wapiga kura, tatizo ni kumsimamisha mgombea anaependwa na wengi. Ile process ya primary voting ikiingiliwa, basi kuna uwezekano wa kupoteza kiti. Na primaries za CDM zipo too centralized.

Kilichofanya CCM ni decentralization of primary voting .... matokeo ni wagombea wanaokubalika.

Hayo mambo ya madaftari is nonsense, acheni.
 
ccm hawajui ubaya wa kuhubiri udini anagalieni afrika ya kati?waafrika wenzetu wana uana kisa chuki na siasa za kijinga?viongozi wao na familia zao wapo ulaya wametulia,sasa wale wanao mpinga yeriko waje na data,maana hata waziri wa nishati na madini huwa anapenda sana kuwajibu watu kwa data nawao wanaobisha waje na data zao ili tujue nani ni mpotoshaji?ok hila za ccm za kugawa watu kikabila na kikanda lazima ziandikie kifungu kwenye katiba mpya mtu aweze kupelekwa mahakamani kushitakiwa kwa kutumia lugha ya uchochezi kwenye majukwaa ya siasa
anayeongoza kuchochea ni WASSIRA na NAPE ndio wanaoongoza kuchochea na kuhubiri udini na ukanda
mshindwe na mlegee
 
Variable factors katika aspect mbalimbali za uchaguzi

1😀aftari la wapiga kura lililotumika ni lile la mwaka 2010 kwa hiyo CHADEMA kimefanya kazi kutoka pale kilipokua mwaka 2010

2: Kuna vijana wengi ambao hawajandikishwa kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura

3:Kuna maeneo ambayo CHADEMA hakikuweka mgombea mwaka 2010 lakini leo kimevuna maelfu ya kura

4:CHADEMA kilifanya operesheni kuzungumzia katiba Mpya,Kuboresha daftari la wapiga kura nchi nzima

5:Kata zilizochukuliwa CCM zimechukuliwa kwa wapiga kura wale wale wa Mwaka 2010

6:Maeneo yote ya kata hizo tuonyeshe uwiano wa kura za mwaka 2010 na kura za sasa tuweke kwenye analytical graph ili kujua pamoja na changamoto nilizotaja hapo juu kati ya CCM na CHADEMA ni kipi kimekua/kimekubalika kwa kasi tangu 2010

NAKUSHUKURU SANA , umefafanua Taratibu MNO , HATA YULE WA KIWANGO CHA CHINI KABISA ATAKUELEWA .
 
Soma kaka, soma vitabu ,journals, online articles ... etc

Simaanishi darasani, jisomee tu kama hobby. Inasaidia hata kwa maisha ya kawaida.

Haya niliyokwambia ndio msingi na nguvu ya chadema, sijui nisome nini ndugu,

Au inakuchang'anya miundo ya siasa hapo?
 
Haya niliyokwambia ndio msingi na nguvu ya chadema, sijui nisome nini ndugu,

Au inakuchang'anya miundo ya siasa hapo?
Kwanza English .... umekosea.

Halafu Geography na General politics sijawahi kusikia categorization hii (according to who?) na explanation yako haitoshelezi, ni kama umechanganya zaidi.

Mwisho kabisa, hiyo 90% ni lazima uelezee umeipataje otherwise anybody can come up with a number. Usitumike, utadharaulika.
 
Back
Top Bottom