CHADEMA imeng'ara kwenye Uchaguzi na Itashinda 2015

CHADEMA imeng'ara kwenye Uchaguzi na Itashinda 2015

mbona hao ambao tayari wanaexist katika daftari la kudumu mmeshindwa kuwaconvince wawapigieni kura?-
Kama juhudi zenu za toka 2010 mpaka leo hii 2014 mmeshindwa kuwabadiri mtizamo wale ambao wameshajiandikisha katika daftari la kudumu, basi juhudi zenu hazina atahri kubwa kisiasa!

Kwao wameleweshwa na drugs za uccm. Sumu yake hamuondoki mtu hadi afe. Vijana hawajanywa hii sumu. Ndio wataleta mabadiliko tz. Mao ktk wiaka ya 70 aliwambia vijana kuwa mapinduzi ya uchumi yatatokea China pindi wazee watakapokuwa wamekufa. Angalia China inavyotisha kiuchumi duniani.
 
Uongo mwingine bana ! eti na wewe unataka sisi tuamini kwamba wewe ni mmoja wa viongozi wa CDM ! Duh !

Bwana nyerere akili yake naifananisha na gazeti ya tanzania daima kwani limetuwaminisha kuwa cdm kimeshinda kata nane tena kwa wino mkubwa kurasa za mbele sasa namini nyerere nae anakuja na mambo ya kipumbafu anasema cdm kilienda kwenye opd kwajili ya kuwamasisha uwandikishaji wa daftari ya kupigia kura uongo mtupu bado jamjawambia wana cdm ukweli ile ilikuwa njia ya kupitia tu na chakusemea lengo la opd ilikuwa ni majungu na fitina kwa watu fulani nikupe mfano kwa yale ninayo juwa nilikuwepo kwenye kikao cha viongozi cha ndani kbla ya mkutano wa public uwanjani mbowe baada ya kulitaja jina la kabwe nakuonesha waraka unaomkshfu zito aliambiwa hawtaki kusikia kashfa yoyote kuhusu zito utubia usimkashfu na maneno yalimfanya mbowe kutokwenda kigoma akawatuma lema mnyika na mpemba kwenda kigoma swla hilo waliambiwa mikowa ya katavi na sumbawanga yeye akanyweya hapo wewe utaniambia nini ilnikuwelewe? Kaka najuwa umependa sana viongozi ndio mana ujajuwa mapungufu yao cdm leo kimehathirika kwa uchaguzi huu bado utaki kutambuwa jipangeni upya mje na maneno ya kutuweleza sio kwa kisa ya kuboresha daftari wala kuibiwa kura tatizo la cdm lipo ndni ya viongozi
 
Kama mnashindwq kupokea ushauri unaotolewa humu JF, mtapokea wa individuals? Mwigamba na Kitila wametufumbua macho

Kama unategemea kila uandikacho hapa jf basi chama kikusikilize basi umepotea, chadema sio KIlabu cha walevu
 
tutafanya vizuri 2015 kabisa hili liko wazi,
madamu tume sasa wamekubali kuboresha daftari la wa piga kula
vijana ambao hawana vipande hivi waende wajiandishe.

nilikuwa naongea na mwanaccm mmoja pamoja na hizi kata walizo shinda amekili wana kazi ya ziada,

ameongelea pia kitendo cha wanakalenge kumupitisha mtoto wa mugimwa , akasema
huenda kikawangusha kukomboa jibo hilo.

chadema tumeshinda kwa mazingira ya kuonewa na selikari hii ,
there is nothing to fear at all, God is tremendous ' at the end he will be on our side!
 
Hebu kosoa kwa tathimini mkuu sio hisia tu, rejea nyuma uone nilivyoeleza
Yericko nimezisoma hoja zako. CHADEMA kwa sasa siyo chama cha kujitangaza na hasa katika kipindi cha uchaguzi, you are supposed to have gone beyond that. Wote tunajua mazingira tuliyomo, lakini si sababu tosha kwa matokeo mliyopata katika uchaguzi huu na hasa ukichukulia matumaini mliyokuwa mnawapa watu. Kumbuka uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu uko usoni kabisa.

Kumbuka mnaposema uboreshaji wa daftari la wapiga kura ni hawahawa watanzania. Wamo watakaowasupport na wamo watakuwa kwa washindani wenu. Hii hoja pekee haiwezi kuwapa ushindi, nafikiri mnapaswa kuangalia zaidi ya hapo...
 
Hiyo ni sawa na kuisifia status quo.
Status quo
ni okay kwa chama tawala na siyo pinzani. Ila kama mnaona mmefanya vizuri, poa.
Yaani mnajisifia kuacha mambo vilevile.

dah!!! mkuu nimekosa kitufe cha like yani huu ujinga wa kujisifia kubaki pale pale ulipo cjui hawa jamaa wameuiga kutoka wapi maana mi ninivyojua uhai wa chama ni kujiongezea uwakilishi kstika nafasi za uwakilishi na c kubaki pale pale ulipo!
 
Inawezekana kauli yangu isiwaingie watu masikioni mwao kabisa, lakini nitawaeleza japo kwa kifupi.

Katika siasa kuna kitu kinaitwa siasa za jumla (general politics) na siasa za kijiografia (geography politics)

General politics inahusu mambo yanayohusu siasa za kitaifa bila kuchagua chama au itikadi na hizi mara nyingi husimamiwa kwa katiba, kanuni na sheria za nchi, hapa inahusiana pia na daftari la wapiga kura na tume ya uchaguzi,

Geography politics inahusu siasa za eneo husuka, kuna international gp, na domestic gp,

Katika hayo Chadema ime win kwenye Gp-D kwa asilimia zaidi ya 90%, hili linatokana na chama kushiriki uchaguzi kwa miaka yote huku mambo muhimu yanayopaswa kufanywa kwenye General Politics yakiwa doro kabisa, mambo hayo ni kama tume kuwa huru, daftari la wapigakura kuboreshwa, na dola kuvuruga chagizi nyingi kwa maslahi ya ccm.

Takwimu za chaguzi hizi zinatoa sura stahiki ya ubora wa domestic political ya Chadema,

Mathalani uchaguzi huu Chadema ilikuwa ikitetea kata 3, za Nyaisura, Kiborloni na Mikol.. Kigoma.

Tumepoteza Nyaisura, na Kigoma, na Tumeipoka ccm kata za Sombetini na Njombe.

Tamani ya kata ilizoshinda chadema nikubwa kuliko ccm, kubeba kata ya njombe ni turufu kubwa, vivyo hivyo kata ya sombetini. CCM hawajaongeza thamani yoyote ya kata,

Kwa lugha nyingine nikuwa CHADEMA 0-0 CCM, lakini CHADEMA wananafasi ya golden goal kwakubeba kata ya Njombe ambayo kwanza inafuta propaganda za ccm yakuwa chadema ni chama cha ukanda, sasa tunashuhudia Chadema sio chama cha ukanda tena bali chama cha kitaifa na kila pembe ya jamhuri hii.

Izingatiwe kuwa oparesheni Pamoja Daima haikuwa maalumu kwaajili ya uchsguzi huu bali sehemu ya ratiba ya chama katika kutoa elimu ya umma kudai/kuhimiza uboreshaji wa daftari la wapiga kura.

Naamini hapo mmenipata ndugu zangu mnaojenga hoja dhaifu kuwa kama dhana ni daftari la wapiga kura na polisi why kwingine chadema imeshinda?

Unakwenda hatua 2 mbele, unarudi nyuma hatua 3, halafu unajifariji.
 
malalamiko na maneno mengi ambayo mnayaweka hapa leo mtayaongea au kuyaandika tena mwaka 2015 october
 
Naunga mkono hoja!!

Kwa wasioelewa watabaki kutukuna!!!
 
Laiti kama hizi fedha nyingi zinazotumika kukodi chopa zingepelekwa vijijini kuimarisha chama huko walau tungeshuhudia mabadiriko chanya.

Hizi operations binafsi nahesabu ni ulaji sawasawa na ulaji mwingine ndani ya CCM. Hii inadhihirisha kwamba, kwenye suala la ulaji wa bila kunawa, CDM na CCM wote ngoma droo.

Badilisheni mipango ya ushindi, ondokaneni na haya maoperations yasiyo na tija. Haya masingizio ya daftari la mpiga kura hayana mashiko.
 
Variable factors katika aspect mbalimbali za uchaguzi

1😀aftari la wapiga kura lililotumika ni lile la mwaka 2010 kwa hiyo CHADEMA kimefanya kazi kutoka pale kilipokua mwaka 2010

2: Kuna vijana wengi ambao hawajandikishwa kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura

3:Kuna maeneo ambayo CHADEMA hakikuweka mgombea mwaka 2010 lakini leo kimevuna maelfu ya kura

4:CHADEMA kilifanya operesheni kuzungumzia katiba Mpya,Kuboresha daftari la wapiga kura nchi nzima

5:Kata zilizochukuliwa CCM zimechukuliwa kwa wapiga kura wale wale wa Mwaka 2010

6:Maeneo yote ya kata hizo tuonyeshe uwiano wa kura za mwaka 2010 na kura za sasa tuweke kwenye analytical graph ili kujua pamoja na changamoto nilizotaja hapo juu kati ya CCM na CHADEMA ni kipi kimekua/kimekubalika kwa kasi tangu 2010

Sasa kama mmeshindwa kuwabadilisha baadhi tu wale waliokuwa na mawazo mgando mwaka 2010 mtawezaje kuwabadilisha watanzania wote mwaka 2015?!

Am not Ccm member but hata ukiangalia katika hizi kata ki asilimia (c kiidadi) CCM imepanda kwa zaid ya 20% ukilinganisha na mwaka 2010.

Matokeo haya Chadema inaonekana imepata kura nyingi kwa sababu mwaka 2010 kuna baadhi ya kata haikusimamisha wagombea lakn pia kuzidi kuporomoka kwa cuf kumeinufaidha chadema!

Lakini jambo la msingi n nature ya uchaguzi wetu n mwenye nyingi apewe (First Past the Post system) so chama cha siasa kinatakiwa kifight ili kipate kura nyingi zaid ya wengne ili kiweze kuwaongoza na c kupata kura nyingi tu za kuweka record za kujitetea tetea kitoto!!!
 
Kwanza English .... umekosea.

Halafu Geography na General politics sijawahi kusikia categorization hii (according to who?) na explanation yako haitoshelezi, ni kama umechanganya zaidi.

Mwisho kabisa, hiyo 90% ni lazima uelezee umeipataje otherwise anybody can come up with a number. Usitumike, utadharaulika.

kama unaandika kingereza basi hutasomeka maana nu kibovu mno.
 
domestic political ya CDM! haya bhana waziri wa mambo ya ndani!
 
Usitukane watu maana hata wewe mwenyewe unaweza kuwa na damu ya mchaga.Huwezi jua maana wachaga wametapakaa nchi nzima na huenda ''mangi'' ni baba au babu yako:Kama ndivyo,nawe ni chadema?
 
Ushindi wa CHADEMA ni nguvu ya Umma. CCM ni kama timu za Uarabuni. Wao kushinda kwa mabavu, hila na fitina ni kawaida sana kwao!
Tume ya Uchaguzi inawabeba; Polisi inawabeba. Lakini yote yana mwisho. Na mwisho wa hila ni adhabu ya kusambaratika vipande vipande!
 
Wajinga wenzio watakasupoti. Hakuna justfication yeyote itakayofuta kichapo kikali mlichopata. Tutaheshimiana tu.

Ha ha ha kumbe kweli ccm mnajua CHADEMA Kiboko ndo maana mnashangilia kurejesha kata 24 mlizokuwa nazo kabla
 
Back
Top Bottom