CCM Zanzibar impe heshima yake John Gideon Okello

CCM Zanzibar impe heshima yake John Gideon Okello

Kama nimekuelewa vizuri ni kwa nini ASP walipinga ushindi ambao upo kikatiba?

Hili ukiunganisha na hali iliyopo Sasa Tanzania utawaelewa CHADEMA kugomea uchaguzi wa 2025.

Katiba ni ramani ya nchi, kama Katiba haipo sawa nchi pia haiwezi kuwa sawa.
Sidhani kama hata kwa katiba hii kama ilivyo leo kama kusingekuwa na wizi wa kura mambo yangeharibika kama yalivyoharibika sasa. Tatizo linaweza kuwa katiba ila tatizo kubwa zaidi ni jinsi katiba hiyo inavyofatwa.

Pamoja na hayo hakukuwa na malalamiko ya katiba kutoka kwa ASP kabla ya mapinduzi, ASP hawasemi kama walishinda uchaguzi halafu wakanyang'anywa viti vya ubunge au walizuiwa kushiriki uchaguzi. Masuala yao hayafanani na ya CHADEMA ya sasa.
 
Sio Okello pekee bali kuna Wamakonde waliokuwa shamba la mkonge Sakura, Tanga walivuka maji usiku wa kuamkia mapinduzi na kutia nguvu kubwa ambazo Waunguja hawakuwa nao.
Doa kubwa hawa ndio walitekeleza mauaji ya kimbari kwa Waarabu bila kujali nani ni nani.
Wamakonde kutoka Tanga mambo ya Zanzibar yalikuwa yanawahusu vipi??
 
..Wazanzibari wanazidi kuchangamana na Watanganyika hivyo utafika muda Uarabu utapotea kabisa Zanzibar.

..Upo uwezekano ndani ya miongo michache, idadi ya Wazanzibari waliohamia Tanganyika kuzidi idadi ya Wazanzibari waliobaki Unguja na Pemba.

..Sasa hali hiyo ikitokea SIASA za Zanzibar nazo zitabadilika kwa kiwango kikubwa. Je, ni chama gani kati ya CCM na ACT kinalipa umuhimu suala ya DEMOGRAFIA ya Zanzibar miaka 10, 20, 30, mbele?
 
Je, ni chama gani kati ya CCM na ACT kinalipa umuhimu suala ya DEMOGRAFIA ya Zanzibar miaka 10, 20, 30, mbele?
Wanasiasa wa Tanzania wana chuki binafsi na matumizi ya takwimu, hivyo hili swali lako ni gumu kujibiwa.
 
Inajulikana kuwa aliyeongoza mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 ni mganda aliyejulikana kwa jina la John Gideon Okello, lakini CCM Zanzibar haitaki kumtambua wala kumpa heshima yake.

CCM tunawajua ni wabinafsi lakini hili la kutokumpa heshima yake aliyeongoza mapinduzi ya Zanzibar litawagharimu.

Kila siku mnayaita ni mapinduzi matukufu wakati aliyeyaongoza hamtaki kumpa heshima yake inayostahili.

Lazima Zanzibar kuwe na mtaa, jengo, uwanja wa michezo, chuo kikuu au alama yoyote kama kumbukumbu kwa ajili ya Okello.

Mtu aliyefanya yale mapinduzi huku kina Karume na wenzake wakiwa wamejificha anawezaje kudharauliwa kiasi hiki?
John Okello, hakuyapanga Mapinduzi wala hakuyaongoza yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, aliyepanga Mapinduzi na kiongozi wa Mapinduzi ni Abedi Amani Karume, akishirikiana na ma comredi,wakiongozwa na Abrahman Mohammed Babu, baada ya kuweka mipango yote sawa, yeye alikimbilia Bara kujificha, kwasababu hakuwa na uhakika kama Mapinduzi yangefanikiwa 'Karume Hakuyakimbia Mapinduzi ya ZnZ'- Karume Jnr

Kufuatia Okello kuwa na a sharp commanding voice, alipewa kazi ya kutangaza Mapinduzi hayo kwenye redio, Sauti ya Zanzibar, akavunja kituo cha polisi cha Malindi, akaiba uniforms za polisi akavaa, akaiba silaha na kuwapa kikundi cha vijana wa kitaa, yeye ns pistol mkononi, akatinga studio kutangaza Mapinduzi, akajiita Field Marshall John Okello, na baada ya tangazo hilo, akawapindua waliopindua, akajitangaza yeye ndie boss!

Akawa anatoa amri za ajabu ajabu, akawaogopesha wote!.
Akazungumza na foreign media na kujinasibu yeye ndie kiongozi wa Mapinduzi na cheo chake ni field Marshall kweli wakati yote ni uongo mtupu!Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

Ndipo Karume akaomba msaada Okello aondoshwe, akaondoshwa!

Hata hivyo, japo hakuwa field marshall kweli na hakuongoza mapinduzi yale,lakini bado anastahili kuenziwa for the role he played kwenye mapinduzi yale!

Hizi sintofahamu za mara kwa mara za mapinduzi ya Zanzibar zinafuatia kutokuwepo kwa narrative iliyonyooka

P
 
Kufuatia Okello kuwa na a sharp commanding voice, alipewa kazi ya kutangaza Mapinduzi hayo kwenye redio, Sauti ya Zanzibar, akavunja kituo cha polisi cha Malindi, akaiba uniforms za polisi akavaa, akaiba silaha na kuwapa kikundi cha vijana wa kitaa, yeye ns pistol mkononi, akatinga studio kutangaza Mapinduzi, akajiita Field Marshall John Okello, na baada ya tangazo hilo, akawapindua waliopindua, akajitangaza yeye ndie boss!

Akawa anatoa amri za ajabu ajabu, akawaogopesha wote!.
Akazungumza na foreign media na kujinasibu yeye ndie kiongozi wa Mapinduzi na cheo chake ni field Marshall kweli wakati yote ni uongo mtupu!
Haya 👆🏾 yalikuwa ni maelezo ya Karume na timu yake baada ya kumsaliti Okello japo si kwamba ndiyo uhalisia wa mambo ulivyokuwa.
 
Wamakonde kutoka Tanga mambo ya Zanzibar yalikuwa yanawahusu vipi??
Hili jeshi lilikusanywa na Mwenyekiti wa Umma Party hayati Abdurahman Babu na kufadhiliwa kwa siri na serikali ya Tanganyika
Babu alijua pekee Wazanzibari wenyewe hawataweza maana Sultani alikuwa na support ya Waingereza
Mohamed Said vijana wengi hawalijui hili.
 
Nimekuja kufuatilia historia ya hayo mapinduzi nimejua kuna mambo mengi sana ya uongo na propaganda yaligeuzwa kuwa historia.
 
Hili jeshi lilikusanywa na Mwenyekiti wa Umma Party hayati Abdurahman Babu na kufadhiliwa kwa siri na serikali ya Tanganyika
Babu alijua pekee Wazanzibari wenyewe hawataweza maana Sultani alikuwa na support ya Waingereza
Mohamed Said vijana wengi hawalijui hili.
Sijui kama umesoma mabandiko mengine... Hakuna ushahidi wowote ule wa kihistoria unaoonesha kama Karume na Okello kama walikuwa wanafahamiana au walishawahi kuwa kwenye kikao chochote kile cha kupanga mapinduzi ya Zanzibar.
 
1784477382658.jpeg

Hii picha inaongea maneno mengi sana kuliko propaganda zilizopo.

Ukiangalia nguo alizokuwa kavaa Okello na walizokuwa wamevaa wenzake na eneo alilokaa yeye kwenye hiyo picha... Ujumbe wake ni mkubwa sana.
 
..Upo uwezekano ndani ya miongo michache, idadi ya Wazanzibari waliohamia Tanganyika kuzidi idadi ya Wazanzibari waliobaki Unguja na Pemba.
Mambo yakiendelea kama yanavyokwenda sasa, ndani ya hiyo miongo michache upo uwezekano wa huu muungano kubaki historia.

Ikitokea, kila mtu atalazimika kurudi kwao.
 
Nimekisoma... Kile kitabu ukikiangalia kwa makini ni kitabu kilichoandikwa na watu wanaoamini kuwa "walipinduliwa. Zipo Zanzibar mbili zinazoyaangalia yale mapinduzi Kwa mitazamo miwili tofauti kabisa.
Sio waliopinduliwa....

Ila ni waliovamiwa na nchi jirani na kumezwa kimabavu kupitia muungano.
 
Sio Okello pekee bali kuna Wamakonde waliokuwa shamba la mkonge Sakura, Tanga walivuka maji usiku wa kuamkia mapinduzi na kutia nguvu kubwa ambazo Waunguja hawakuwa nao.
Doa kubwa hawa ndio walitekeleza mauaji ya kimbari kwa Waarabu bila kujali nani ni nani.
Uwepo wa hao wamakonde kutoka Tanganyika ni kiashiria huo ulikuwa uvamizi kutoka Tanganyika kwa kushirikiana na wazanzibari wachache.
 
Sio waliopinduliwa....

Ila ni waliovamiwa na nchi jirani na kumezwa kimabavu kupitia muungano.
Bado maudhui ndiyo hayo hayo. Wazanzibari wanaoamini kuwa zazibar "ilivamiwa" ndiyo wale wanaoamini kuwa iliyokuwa serikali "halali" ya wazanzibari ilipinduliwa.

Lakini ukisikia mtu anasema "mapinduzi daima" ujue huyo anaamini Zanzibar ilikombolewa toka kwenye mikono ya usultani na kukabidhiwa kizazi cha mvuvi na mkwezi.
 
Kiufupi Zanzibar kulikuwa na siasa za uhasama kabla hata ya mapinduzi na muungano..
 
Jinsi Okello historia yake ilivyopindishwa ni mtindo ule ule waliutumia kupindisha historia na mawazo ya Kambona na kumgeuza kama msaliti.

Kitendo cha Kambona kumnusuru Nyerere kwenye mapinduzi ya kwanza ilikua ni kiashiria kwamba alikua na ushawishi kuliko Nyerere japo wanaficha, ukija kupinga sera mbovu za ujamaa ndio akaonekana hafai kabisa .
images - 2026-07-19T134206.181.jpeg
 
Back
Top Bottom