CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

Hii mada imebadilishwa heading yake zaidi ya mara mbili, yote heri kwani CCM ndio kijogoo!
 
Last edited:
Lazima tujiulize ni kwa nini CCm inapendeka sana vijijini zaidi ya mjini?
Hili ni fumbo kubwa sana na linatakiwa lipatiwe jib na ikibidi tuingie mtaani kuwaelimisha wananchi vijijini,sababu ni uelewa mdogo wa walio wengi vijijini na si vinginevyo ndugu zanguni.
 
Nashukuru kwa mchango wako FELISTER kwani kukua kwa chama kingine zaidi ya ccm kutaleta check and balance na hii itasaidia chama kilicho madarakani kifanye kazi kwa uadilifu mkubwa .CCM kimevua ile nadharia ya kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi sasa ni chama cha watu wachache `````` wafadhili`` na wako tayari kutumia mbinu zote halali na zisizo halali kushinda.Kwa faida yao ni bora wakatengeneza haki na usawa kwani hawatatawa milele.
 
CHADEMA, "You can helicopter it if you want to. But it's no substitute for knocking on doors or setting up town hall meetings" (Hazel Blears).

Please go back to basics of grassroot politics.
 
Ushindi wa CCM huko vijijini ni jibu kwetu tupendao kuona CCM ina lala ngoma kwamba bado tuna kazi ya kufanya ili kubadili nyoyo za watu.

Mabadili ni hatua, hatua ni mikakati. Hii ina maana kwamba katika mikakati yetu kuna kitu muhimu sana kinakosekana. Ni lazima tujiulize ni kitu gani kinakosekana katika mikakati yetu cha kuwafanya wananchi wote wa mijini na vijijini kubadili mwelekeo wao kwa moyo mmoja????

Kushindwa kunauma lakini kushinda bila kuwa na mkakati uliokamilika kunauma zaidi.

Najua CCM wametumia fedha nyingi sana kupata ushindi huu. Zaidi ya fedha wametumia nguvu nyingi sana za kijeshi na za kiserikali kuihakikisha kwamba wanashinda.
Pia Viongozi wa ngazi ya juu kabisa kitaifa wametumia masaa yao mengi sana katika uchaguzi huu.

Hili ni jambo linipalo matumaini makubwa sana kuhusu uchaguzi wa 2010.

Kila kiongozi wa kuchaguliwa wa CCM atakuwa buze kwenye jimbo lake kutetea unga wake. Maana yake umoja wao wa kishetani utanyumbulika kiasi cha kuwaacha hoi.

Hawatakuwa na polisi wengi wa kuwasambaza kwa fujo kila mahali. Hii itafanya wapinzani wote wenye ujkali wa hoja na nguvu ya ushawishi wa kuongea kuwazidi kete CCM.

Kushindwa Busanda ni pigo kubwa sana kwa kambi ya upinzani, lakini ni shule ya kutosha kabisa. Naamini chochote kilichojitokeza Busanda NI STEPING STONE YA 2010.

Shoka limevunjika mpini, hiyo haina maana ni mwisho wa kazi.
 
Duh, watanzania jamani? Sielewi kabisa. Matatizo yote haya bado CCM inapewa ushindi?
Watanzania hawana matatizo,kama kweli unataka kuangalia katika angle hiyo.

Kabla ya kuja conclusion yako, jaribu kujiangalia wewe mwenyewe una tatizo gani na una matatizo gani ambayo yanahitaji ushirikishwaji wa wanasiasa!
 
Kuna mambo ambayo CHADEMA wanapaswa kuzingatia katika kampeni zao zinazofuata.

1. Matumizi ya Helikopta yawe kwa nia ya kuwafikisha sehemu zisizofikika kwa urahisi/haraka.
Ila, kwa style yao (Ya sasa) ya kufanya vikao vingi kwa siku moja na kukimbia bila kuvifanyia tathmini, wakidhani kuwaeleza tu wapiga kura kuwa CCM haifai inatosha kuwahakikishia ushindi, ni kujidanganya, na kupoteza pesa zao bure.
Inabidi wafahamu kuwa, wananchi huwa wanakusanyika hata kama kuna janga (mfano ni milipuko ya mabomu, ajali n.k.).
Waangalie maana ya mikusanyiko wanayofanikiwa kuipata, wawe na mipango ya jinsi ya kuitumia mikusanyiko hiyo, na walinde kura wanazoahidiwa.
Wajue, kura nyingi nchini ni floating votes (nadhani zaidi ya 70%). Watumie wanachama wapya (kupitia operation zao - Sangara n.k.) kuongeza idadi ya wanachama, nao waelimishwe kupiga kura na kukisaidia chama kwa mambo mbalimbali.

2. Kwa maoni yangu, CCM itaamka kwa kishindo zaidi kuelekea uchaguzi ujao (Biharamulo, serikali za mitaa na 2010). Baada ya kazi kubwa iliyoipata Tarime na Busanda, ni dhahiri kuwa CCM imejifunza.

Nashauri CHADEMA (ambao inaelekea kuanza kukubalika) kuwekeza zaidi katika chaguzi za Serikali za Mitaa. Na kuachana kabisa na Biharamulo (afterall Mbunge huyo wa mwaka mmoja hawezi kuisaida sana).
Baada ya kuanguka Busanda, sidhani kuwa kuweka nguvu zao Biharamulo kutasaidia CHADEMA kushinda. Ni dhahiri kuwa watashindwa tena (kwa anaebisha "lets bet"). CCM wataendelea kutumia uwezo wake wote (kumbuka wako tayari kwa chaguzi hizi -kifedha na resources nyingine). Hivyo CHADEMA kujiingiza Biharamulo kutawapunguzia nguvu za kushinda Serikali za Mitaa (Mwaka huu).
Serikali za mitaa huongeza nguvu kwa chama kuweza kushinda udiwani, na ubunge katika uchaguzi mkuu (endapo itatumika vizuri). Inabidi wao wawe wakifanya kampeni za serikali za mitaa wakati wenzao wakitafuta ubunge Biharamulo. CHADEMA waamue kusaidia chama wanachotaka kishinde. iyo itawapa presence kidogo kwa wananchi Biharamulo ambayo itasaidia kuwapa nguvu kwenye uchaguzi Mkuu ujao.


Huu ni ushauri ama ulaghai? Jamani uchambuzi wa siasa ni proffesion sio biashara ya kuuza njugu.........Ishhhhhhh

omarilyas
 
CCM yanguruma Busanda: Wapinzani chali

It is very sad that power hungry CCM may precipitate the abortion of democracy in Tz. And it is shame that of all people, a female Minister, Mwantumu Mahiza, has been caught with voter identity cards; which obviously render the valid owners, presumably fellow women, unable to exercise their constitutional right to vote for the person they want to be their M.P. Shame on you for this disreputable infringement of this women emancipation!
Chadema and the other opposition parties must refuse to accept these results. Mr Finias Magessa must go to court. the grounds for nullifying this poll are too obvious: 1. A CCM Diwani was caught red-handed buying shahada za kupigia kura and was arrested by the Polisi. This diwani confessed he was carrying out orders from his seniors, presumably the leaders of the ccm campaign. ??TINGATINGA??? Wow! 2. The Honourable Deputy Minister (honourable indeed!!!) similarly was caught with shahadas. 3. Magodoro and other requisites for the household were being distributed by ccm cadres during the election campaign period. 4. The CCM government ordered TANESCO to deliver nguzo for the transmission of electricity in Busanda. All these are breaches of the Election Act and even the National Electoral Commission confirmed this irregularity.
The result of the purchase of Shahadas fron prospective voters made only about 40 percent of the registered voters turn up at the polling stations. This gross abuse of money power. It is worse when it is probable that this money originated from the Bank of Tanzania (EPA).
It is a sad turn of history that people who have held senior positions of trust in Tanzania like Prime Ministership and Speaker of the National Assembly led the CCM campaign in Busanda and probably approved this flagrant abuse of the democratic principles Tz. wants to nurture.
The High Court should be prevailed upon to reverse this trend Magessa must go to court

kilasara
 
CCM wadai mtandao umewapa ushindi mnono Busanda

Frederick Katulanda na Elias Msuya, Busanda (mwananchi)
WAKATI Chadema ilipopeleka helikopta kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa kiti cha ubunge cha Busanda, makamu mwenyekiti wa zamani wa CCM, John Malecela aliipuuza na kusema kuwa chombo hicho kilikuwa kinatimua vumbi tu na kwamba askari wa ardhini ndio watakaofanya kazi.

Ndivyo ilivyodhihirika jana wakati msimamizi wa uchaguzi huo, Dani Mollel alipomtangaza Lolensia Bukwimba kuwa mshindi wa kiti hicho kwa tofauti ya zaidi ya kura 5,000 dhidi ya mgombea wa Chadema, ambayo ilikuwa ikikusanya mamia ya watu kwenye mikutano yake ya kampeni.

Bukwimba, ambaye kampeni zake za mwanzo zilitawaliwa na zomeazomea, aliibuka kidedea kwa kupata kura 29,242 na kufuatiwa na mgombea wa Chadema, Finias Magesa aliyepata kura 22,799 huku wagombea wa CUF Oscar Ndallawah na Beatrice Lubambe wa UDP wakigawana kura 1,248 zilizosalia.

"CCM ilijipanga vizuri kwa kuwa ina mtandao kuanzia ngazi ya shina, matawi, wilaya hadi mkoa," alisema mwanasiasa mkongwe na muasisi wa chama hicho alipozungumza na Mwananchi jijini Dar es salaam jana.

"Mara nyingi, vyama vya upinzani vimekuwa vikienda kwa pupa na hata kuonekana vinaungwa mkono na umati mkubwa wa watu, lakini havina kiungo cha kuwaunganisha watu hao kwenye ngazi za chini.

"Kampeni zao huwa zenye hamasa nyingi, lakini wakishaondoka wananchi hurudi kwenye maeneo yao na kujikuta wako kwenye mtandao wa CCM," alisema mkongwe huyo ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na ambaye amefanya kazi kwenye serikali za awamu zote nne.

Kingunge alisema kwa mtandao huo mzuri wa CCM, wana uhakika wa kuendelea kunyakua zaidi ya asilimia 80 ya viti vyote vya ubunge katika uchaguzi ujao wa mwaka 2010 kwa sababu wapinzani hawajajijenga.

Pamoja na ushindi huo mkubwa, kulikuwa na matukio mengi ya utata yaliyosababisha baadhi ya viongozi wa Chadema na mgombea wake kupinga matokeo hayo kwa madai kuwa msimamizi alishinikiza ayatangaze, huku mgombea wa Chadema akieleza kuwa atajaza fomu za kutokubali matokeo na kusubiri uamuzi wa chama chake kuhusu kufungua kesi.

Viongozi hao wa Chadema walifika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita na kumuomba msimamizi kuwapatia fursa ya kuwasikiliza na kuwasomea matokeo kabla ya kusaini, lakini wakajibiwa kuwa hawakuwepo wakati fursa hiyo ilipotolewa.
Matokeo hayo hayakutangazwa asubuhi kama ilivyopangwa awali kutokana na msimamizi wa uchaguzi kueleza kuwa alikuwa akiwangojea wawakilishi wa vyama kwa ajili ya kushuhudia ujumlishaji wa kura hizo kabla ya kuzitangaza.
Msimamizi huyo, Molleli alieleza alijaribu kuwatafuta kwa simu lakini hawakupatikana na ndipo alipowasiliana na mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ambaye alimshauri kuwaandikia barua kuvikumbusha vyama kutuma wawakilishi hao.
Kiliwaandikia barua tarehe 23 mwezi huu kuwaeleza kuwa Mei 24 usiku wanatakiwa kuwa na mawakala katika kujumulisha kura. Mwakilishi wa Chadema alikuwa (Habibu) Mnyaa pekee hadi usiku alipoamua kuondoka," alisema Mollel.

"Nilipomuuliza alisema tuendelee. Asubuhi tena nikampigia Mnyaa aje akanijibu endeleeni, lakini tukaandika barua kwa vyama tena kuwaomba wawakilishi.?p>
Ilipofika saa 4: 45 mgombea wa Chadema, Magesa alifika akiwa ameambatana na kamanda wa uchaguzi wa chama chake, Benson Kigaila na baadaye akaingia mgombea wa CCM, Lolesia Bukwimba na viongozi wa chama chake.
Mara baada ya kuingia msimamizi wa uchaguzi aliwaeleza alikuwa akiwasubiria kwa ajili ya kutoa matokeo, lakini alikwama kutokana na kuwepo kwa mwakilishi wa CCM pekee na kwamba wakati huo angeweza kutangaza kwa sababu idadi imetimia.
Chadema walitaka kupatiwa fursa ya kupitia upya kura zote kabla ya kujumlisha kwa madai kuwa walikuwa na mashaka nayo, lakini msimamizi alipinga akieleza kuwa muda huo ulishapita na hivyo kuwaomba wananchi kusubiria nje kwa muda wa dk 45 ili akamilishe kujumlisha matokeo katika baadhi ya kata kabla ya kusoma matokeo yote lakini muda huo ulipitiliza hadi majira ya saa 9:35.
Wakati msimamizi akifanya majumuisho hayo, wafuasi wa CCM walikuwa wakipiga kelele nje kutaka kutangazwa kwa matokeo huku ndani ya ukumbi akizongwa na wafuasi wengine wa chama hicho tawala waliokuwa wakishinikiza kutangazwa kwa matokeo.
Kamanda wa polisi wilayani Geita, Shaaban Kimea alilazimika kuwaondoa nje baadhi ya wafuasi hao wa CCM na kubakia viongozi wachache wa chama hicho na Chadema.

Pamoja na Chadema kushinikiza matokeo hayo yasitangazwe, msimamizi wa uchaguzi alishikilia msimamo wake.
Hilo halina nafasi naomba wagombea waje kusaini matokeo?hatuna muda wa kuanza hayo tena,?alieleza Mollel akiwa amezungukwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, Clement Mabina, Anthony Diallo na Esau Barnabas ambao walikuwa wakitaka matokeo yatangazwe.
Baada ya mgombea wa CCM kusaini, ndipo matokeo yalipotangazwa.
Mara baada ya kutangaza matokeo hayo, mgombea wa Chadema, Magessa aliongea na waandishi wa habari kueleza sababu za kukataa kuyatambua.
Tuliitaarifu tume ya uchaguzi kuwa CCM wanagawa chumvi, chupi, magodoro kwa mgongo wa kanisa na kutandaza nguzo za umeme na kujenga barabara wakati wa kampeni, lakini hawakuchukua hatua yoyote. Nitawezaje kuyakubali matokeo,?alihoji Magessa.
Magesa pia alilalamikia ukiukwaji wa taratibu siku ya kupiga kura,
siku ya kupiga kura tulimkamata mratibu wa elimu Kata ya Katoro akigawa posho za wasimamizi wakati wa kupiga kura kitu ambacho ni kosa kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi wa wilaya. Lakini tunashangaa kumwona mratibu huyo akiendelea na kazi yake ya kuhesabu kura,?alisema.
Aidha Magessa pia alilalamikia kitendo cha Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha kutembelea vituo vya kupigia kura na hata kuwaruhusu askari polisi kuingia kwenye vyumba vya kupigia kura. Alidai Waziri Masha aliwatishia wanachama wa Chadema na kushindwa kuwakamata wafuasi wa CCM kila walipotuhumiwa kufanya makosa.

Naye Robert Kakwesi kutoka Uyui anaripoti kuwa CCM wilayani Uyui imeibuka mshindi katika uchaguzi mdogo wa kata ya Ibiri uliofanyika juzi Jumapili.

Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi huo, Dorothy Rwiza CCM iliibuka mshindi kwa kupata kura 1,059 dhidi ya mahasimu wao wakubwa, CUF ambayo ilipata kura 317. Kutokana na matokeo hayo, diwani mpya anakuwa Juma Athumani (CCM) aliyemshinda Mbaraka Kapulilo (CUF) katika uchaguzi ulioshirikisha vyama viwili.
 
Kuishinda ccm kwenye by election kunahitajika nguvu kama za wanatarime.... kwani tra, polisi, walimu wote huitwa na wakuu wa kampeni kupewa maelekezo, usipotimiza uhamisho unakufuata. Mahita alifukuza kazi polisi saba kwenye uchaguzi mdogo kisa walinukuliwa wakisema... kama kigoma wanampenda kaburu walid hakuna haja yakutumia nguvu.... wakakosa kazi.... mzee mmoja kule tarime amelimwa uhamisho kwenda sumbawanga kisa hakutoa ushirikiano kwa chama dume....
nguvu za giza ni nyingi mno na hawa jamaa wanabadili mbinu za giza kila uchaguzi

mwezi wa tatu wamekutana kupeana semina ya kututawala kwa miaka mingine 50... kiakao kilikuwa zanzibar... usalama wa tuifaaa walikuwako.. wasemaji walikuwa wakina RA (igunga), LW (monduli), BWM(Lushoto), Mbeki na wengine zimbabwe na Anc vilikuwa na wawakilishi.......
Miaka mingine 10 ya sisiem ...nchi itakwisha na itakuwa masikini kupindukia
tutabaki na upumbavu wetu.......

Tanzania wil never ever develop under ccm... it is a carrot and stick story
 
Leo hii hata wakija Umoja wa Matafifa, EU, AU, SADC na wengine wasimamie uchaguzi, bado CCM itaondoka kidedea.

Swali la msingi ni kwa nini basi CCM inaendelea kupiga tobo wapinzani?

Si suala la kuwepo Polisi, Mwantumu Mahiza na kura za ziada au sababu nyingine nyingi kuonyesha kuwa CCM inatumia faulo, bado hatupati jibu kwa nini katika Mkoa kama Dar Es Salaam, viti vyote vya Ubunge 2005 vilikwenda CCM.

Sasa ikiwa Dar mji mkubwa na chimbuko la mageuzi, Wapinzani bado wako chali mithili ya kifo cha Mende, itakuwaje tutegemee kule Nkenge, Manyoni na Njombe kuwa Upinzani utapata kura?

Hata ukiangalia uwiano wa Wapinzani katika Serikali (TAMISEMI na Bunge) bado ni mwakilishi mmoja wa Upinzani katika kila watu 15!

Sasa sijui kama leo ukifanyika chaguzi pale Dar ni kwa kiasi gani Upinzani utavuna viti iwe ni TAMISEMI au Ubunge?

Kumkamata Mchawi kutafanikiwa pindi Wapinzani wakibaini mbinu za kisasa na kisiasa kuiangusha CCM kila kona ya nchi na si kubahatisha kuokota jimbo moja hapa au pale.
 
Leo hii hata wakija Umoja wa Matafifa, EU, AU, SADC na wengine wasimamie uchaguzi, bado CCM itaondoka kidedea.

Swali la msingi ni kwa nini basi CCM inaendelea kupiga tobo wapinzani?

Si suala la kuwepo Polisi, Mwantumu Mahiza na kura za ziada au sababu nyingine nyingi kuonyesha kuwa CCM inatumia faulo, bado hatupati jibu kwa nini katika Mkoa kama Dar Es Salaam, viti vyote vya Ubunge 2005 vilikwenda CCM.

Sasa ikiwa Dar mji mkubwa na chimbuko la mageuzi, Wapinzani bado wako chali mithili ya kifo cha Mende, itakuwaje tutegemee kule Nkenge, Manyoni na Njombe kuwa Upinzani utapata kura?

Hata ukiangalia uwiano wa Wapinzani katika Serikali (TAMISEMI na Bunge) bado ni mwakilishi mmoja wa Upinzani katika kila watu 15!

Sasa sijui kama leo ukifanyika chaguzi pale Dar ni kwa kiasi gani Upinzani utavuna viti iwe ni TAMISEMI au Ubunge?

Kumkamata Mchawi kutafanikiwa pindi Wapinzani wakibaini mbinu za kisasa na kisiasa kuiangusha CCM kila kona ya nchi na si kubahatisha kuokota jimbo moja hapa au pale.

- Tupo pamoja sana hapa mkuu, saafi sana hakuna cha kuongeza!

FMES!
 
hizi takwimu zinatuambia nini jamani? kwanini zaidi ya nusu ya waliojiandikisha hawakupiga kura? kulikoni?

WoS swali zuri sana hilo. Kwa maoni yangu hizi ni dalili kwamba baadhi ya wapiga kura wameshaona chaguzi zetu zimejaa USANII MTUPU!! na hawana imani nazo tena. Asilimia ya wapiga kura ni 39% tu ya wale waliojiandikisha kwa maana nyingine waliomua kukaa majumbani kwao ni 61%!! Hii inatisha. Anapatikana mbunge ambaye hakuchaguliwa na 61% ya wananchi katika jimbo lake!!!
 
WoS swali zuri sana hilo. Kwa maoni yangu hizi ni dalili kwamba baadhi ya wapiga kura wameshaona chaguzi zetu zimejaa USANII MTUPU!! na hawana imani nazo tena. Asilimia ya wapiga kura ni 39% tu ya wale waliojiandikisha kwa maana nyingine waliomua kukaa majumbani kwao ni 61%!! Hii inatisha. Anapatikana mbunge ambaye hakuchaguliwa na 61% ya wananchi katika jimbo lake!!!


Lakini pia kumbuka hapo huenda kuna asilimia zaidi ya 30% wameuza shahada za kupigia kura ili wapate mlo wa mchana na beer moja!! Hili swala la kununua shahada ndiyo njia kubwa sana hutumiwa na CCM kwa kuwatumia wajumbe wa serikali za mitaa, kwani hao huwa wanawajua vizuri wafuasi wa upinzani, hivyo huwafuata na kuwarubuni na kwa kuwa wameshawafanya masikini hawana uwezo wa kupata hata mlo, basi hawana jinsi zaidi ya kukubaliana. Hizo shahada zikishanunuliwa huchomwa moto, kwa hiyo wanakuwa wameshapunguza wapiga kura upande wa upinzani. Hao waliokamatwa nazo ni vijisehemu tu vidogo na huenda walijisahahu wakati zinachomwa wakatia mfukoni!!!

Na ndiyo maana siku zote utakuta zaidi ya nusu hawajapiga kura.
 
Lakini pia kumbuka hapo huenda kuna asilimia zaidi ya 30% wameuza shahada za kupigia kura ili wapate mlo wa mchana na beer moja!! Hili swala la kununua shahada ndiyo njia kubwa sana hutumiwa na CCM kwa kuwatumia wajumbe wa serikali za mitaa, kwani hao huwa wanawajua vizuri wafuasi wa upinzani, hivyo huwafuata na kuwarubuni na kwa kuwa wameshawafanya masikini hawana uwezo wa kupata hata mlo, basi hawana jinsi zaidi ya kukubaliana. Hizo shahada zikishanunuliwa huchomwa moto, kwa hiyo wanakuwa wameshapunguza wapiga kura upande wa upinzani. Hao waliokamatwa nazo ni vijisehemu tu vidogo na huenda walijisahahu wakati zinachomwa wakatia mfukoni!!!

Na ndiyo maana siku zote utakuta zaidi ya nusu hawajapiga kura.

Hmmmm! Ama kweli chama cha mafisadi ni nambari one!!!! Kigumu Chama Cha Mafisadi...Kigumu!!!!
 
Ndio matokeo ya siasa za keyboard hayo na kupeana false hope.
Wananchi wa Busanda wameongea, tena wameongea loud and clear! hii tabia ya akina Pasco na genge lake kututukania wazee wetu ikome hao hao anao waita wasio na elimu ndio waliomfikisha hapo alipo na leo na elimu yake kubwa ya uhandisi habari, inanikumbusha hadithi ya wimbo wa marehem Marijan wa Chakubanga kujiita John Smith.

Huu ni wakati muafaka kwa Chadema kurudi kwenye drawing board ba kuanza upya. Hawa pundit wa JF watawadanganya hawa ni arm-chair generals wanapigana kwenye keyboards tu.
Asante Masatu, nayaheshimu mawazo yako. Kama ilipitia ile thread yangu ya 'Masaa 48 Muhimu Busanda' utaona nimesimamia wapi.

Naomba kukuhakikishia, sina genge, sina chama, sio mshabiki wa Chadema wala sina chuki na CCM, bali ni pro-democracy wa kweli mwenye kutaka kuona Tanzania tunapata heathy opposition ndani ya Bunge for checks and Balance.

Sikutoa false hopes bali nilikisema kile nilichokiona Busanda. Nilihudhuria kampeni ya mwisho ya CCM na Chadema mji mkuu wa Busanda uitwao Katoro. Mjini hapo CCM ilikuwa hoi kweli na Chadema ilikuwa juu. Hicho ndicho kilichotokea, false hope zipi.

Baada ya matokeo kutoka, Chadema imeshinda mijini
na CCM imeshinda vijijini, hivi bado kuna ubishi hapo?.

Wapenda demokrasia ya kweli wangependa kuona ushindi kwa wapinzani ili kutanua uwigo wa demokrasia ndani ya Bunge ambalo linahodhiwa na chama kimoja cha CCM.

Naomba utofautishe wapenda demokrasia ya kweli na washabiki wa upinzani.

Nakuthibitishia na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere (RIP), ni shahidi yangu, akifufuka, hatafurahia kuiona demokrasia legelege ndani ya Bunge. Hatafurahia kuona utitiri wa vyama.

Nimeipongeza CCM kwa ushindi mnono na kutafakari kile nilichokiona na matokeo ya kilichotokea.
 
Back
Top Bottom