Masatu,
Unajua mkuu wangu mimi hutazama mbali sana ktk maswala kama haya na nimejaribu sana hapa kijiweni kuwaamsha wana Chadema na Wapinzani wote lakini tamaa zao za ruzuku na Ubwana.. kuitwa Mheshimiwa kumewalegeza zaidi..
Ukweli ni kwamba uchaguzi wa mwaka 2005 nili ufanyia uchunguzi wangu binafsi na kugundua kwamba CCM imeshinda sana sehemu zote kutokana na utengano wa Wapinzani.
CCM sehemu nyingi ilishinda kwa asilimia 50 hadi 60 ktk kura za Wabunge na Madiwani karibu nusu ya mikoa yote.. Na nikasema ikiwa wapinzani wanataka kuleta ushindani wa haki ni bora kabisa wamsimamishe mgombea mmoja ktk kila jimbo..
CCM mara nyingi inashindwa kwa sababu ya migogoro kati ya Wapinzani..CCM wakitumia mbinu ya udini na Ukabila ktk kujenga hoja zao kuvishutumu vyama vya CUF na Chadema mbavyo kwa nyakati tofauti vilipata umaarufu..
Lakini kama siku itatokea CUF na Chadema wakiungana wataondoa hizo dosari ambazo kila siku huwaumiza na CCM wanafahamu wapi pa kubonyeza..Nina hakika kabisa wakiungana hawa wengine watafuata na wananchi watavitazama vyama hivi kama vyama pinzani badala ya kupachikwa majina ya chama cha Walalahoi, Wapemba, Waislaam, Wakristu na Wachagga!..
Hakuna mtu wala kiongozi anayeweza kuondoa dosari hizi kwa sababu zimeisha pandikizwa siku nyingi sana na vyombo vya habari..
Ni kweli kabisa CCM ina madiwani wengi mijini na vijijini lakini yote haya yanatokana na vyama pinzani kugawana kura..Dar hawana kwa sababu hiyo hiyo wapinzani waligawana kura CCM akaondoka mshindi tena sehemu nyingine kwa asilimia 40 tu..
Kuna Washikaji wangu kibao ambao walipigia kura chama cha CUF mwaka 2000 wakiwa wakristu, lakini hofu za udini na Upemba zilipoingia tu baadhi walihamia Chadema na wengine kurudi CCM na hawa mwaka 2005 nina hakika walipiga kura against CUF chama ambacho wanaamini mrengo na sera zake kuwa ni bora..Na bila kuficha hata mimi nimeshaulizwa kuwepo kwangu Chadema kama naelewa kinachoenelea ndani ya chama hiki..
Majibu yangu siku zote yamekuwa mimi ni Conservative, siwezi kuondoka chama kwa sababu ya mambo yao binafsi nikaacha imani yangu ktk mrengo unaoweza kuiendeleza nchi yangu..Kesho ukinambia CCM ni Conservative nitahamia huko na kuondoka Chadema kama wao watageuka kuwa Progressive bila kujali akina nani ndio viongozi.. Huu ndio mtazamo wangu wa siasa na ndio maana sintaweza kuingia siasa za Bongo..
Na bahati mbaya hakuna demokrasia Tanzania na haitapatikana tusidanganyane!.. haiwezi kuwepo demokrasia kwa sababu tupo wachache sana wanaotazama Siasa za Tanzania kwa jicho la mrengo..Hivyo mategemeo yangu hayawezi hata siku moja kuzaa matunda kwani watu wote Tanzania wanakichagua chama kutokana na sura za watu, ahadi pamoja na kuendekeza imani za kidini kwamba ukizaliwa Muislaam au Mkristu huwezi kubadilisha dini..Sisi sote tumezaliwa Wana CCM na tunapojiunga na vyama vingine ni sawa na kubadilisha dini.. hivyo tunaonekana kuwa waasi na mara zote waasi hawana sifa nzuri ktk jamii ya Kidanganyika...
Nakushukuru Mkuu kulisemea hili, kwa mtazamo wangu, nimewagawanya wanasiasa katika makundi makuu matatu.
Kundi la Kwanza:Ni wanasiasa wanaipenda siasa kwa dhati, na wenye uwezo wa uongozi, hawa sio wapiga domo wazuri, ni makini kwenye mambo yao na wengi wao ama lazima washawishiwe na watu, ama wateuliwe. Wengi wa kundi hili wanashughuli zao hivyo hawawi mstari wa mbele kugombea nafasi za uongozi kutokana na uchafu katika mchezo wa siasa.
Kundi la Pili:Ni la wanasiasa oportunists ambao wanaingia kwenye siasa kutafuta madaraka kutokana na njaa zao. Kwao siasa ni ajira, wengine wana uwezo wa uongozi na wengine hawana ila lengo lao ni moja, kuchumia tuu na kutaka kuula. Wengi wao hata baada ya kuukwaa ubunge, huwa wanasikitika kuukosa ulaji wa uwaziri. Hawa huwa tayari kufanya lolote ili kupata wanachokitaka. Hili ndilo kundi kubwa la wanasiasa wetu wakiwemo wengi walio kwenye upinzani.
Kundi la Tatu:Ni la wanasisa walioshiba wanaoingia kwenye siasa kutafuta power. Hawa wanafedha zao ambazo huweza kuzitumia kupata uongozi wanaoutaka na mara nyingi, hawana uwezo wa uongozi na wala siasa hawazijui, wao kila kitu itaongea pesa tuu.
NB, Hii tathmini yangu haihusiani na Natural Born Leaders, Self Made Leaders na Opportunists.
Lengo la kutanguliza tathmini hiyo ni ili kukuongoza kujua kwa nini wapinzani hawataki kuungana na kamwe hawataungana kutokana na wengi wa viongozi wake kuangukia kwenye kundi la pili ambao ni wanasiasa njaa wenye uchoyo na ubinafsi wa umimi hali inayopelekea kila chama kung'ang'ania kusimamisha wagombea wake na kushindwa kusimamisha mgombea mmoja.
Mimi naamini wale waliosusia uchaguzi Busanda, ni wafuasi wa CUF na UDP ambao walishakatishwa tamaa na uwezekano wa kushinda wagombea wao, wakaona kuliko kupoteza muda kwenda kupiga kura, bora wajipumzie na kujilia raha zao na muda wao.
Kama wapinzani wangesimamisha mgombea mmoja, Busanda wangeiteka kwa ulaini kama kumsukuma mlevi.
Ubinafsi na umimi ndio unawaponza wapinzani, mathalan, baada ya Chadema kuenguliwa Mbeya vijijini, walikuwa hawana sababu ya kususa, bali kuunganisha nguvu kumuunga mkono mgombea anayekubalika zaidi, kwa kususa kwao, CCM wamepeta, na Busanda hali ni hiyo hiyo.
Swali ni lini wapinzani watafungua macho na kuukubali ukweli halisi kuhusu siasa za Tanzania.