CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

Nimejaribu sana kuweka hesabu sawa naona sipati majibu na ninaomba yeyote ambaye ana-data au ujuzi wa kuvumbua hili fumbo anieleze.

Kwanza ningeomba tabia ya watu wa busanda kujiandikisha na kupiga kura miaka ya nyuma. je niwangapi huwa wanajiandikisha na wangapi huwa hawatokei kwenye booth kupiga KURA.

Halafu ningependa kujua nini hasa kilitokea kwa zaidi ya 77,000 kutokupiga kura au kutokea kwenye vituo vya kura.

Je wanangu Chadema nini kiliwasibu kutokulijua hilo au CCM ilinunua shahada zote na wapiga kura wakaingia mitini.

Naomba kujua kura zilivyopigwa kila kituo ili kujua athari za Chadema zililetwa na kura za vijijini au vyote au rafu. Uwiano wa vijijini na mjini ulikuwajE wakati wa kupiga kura bahati mbaya hapa nyumbani huwa hatuweki ankara za umri wa wapiga kura, kazi, elimu nk.

Nawapa Hongera Chadema kwani wameonyesha mapinduzi ni matumaini yangu 2010 hawawezi kwenda nchi nzima kila mtu atakuwa kwake. Ni kuongeza nguvu kwenye majimbo yao kwani kama hawataiba fedha nyingi wengi watakwenda na maji.

KUKATA TAMAA NI DHAMBI YA MAUTI. MOTO KWA KWENDA MBELE
Habari kuu ndio hiyo.
 
nipo chali kabisa hata mimi sielewi
labda baada ya kupewa magodoro mapya wakalala wakajisahau kupiga kura
unajua mambo ya godoro jipya tena
 
nipo chali kabisa hata mimi sielewi
labda baada ya kupewa magodoro mapya wakalala wakajisahau kupiga kura
unajua mambo ya godoro jipya tena

Wanachofanya ccm kura zote zinapigwa kama wanavyotaka wao ushindi uwe vp, then zile kura wanazopiga wananchi hazihesabiwi!!!! ni mchezo wa kubadilisha masanduku ya kura, tume ya uchaguzi wanajua hii dili!!

Dawa ni tume huru ya uchaguzi itakayokuwa na wajumbe toka pande zote!!!

Mara nyingi baada ya zoezi la kura kwisha, huwa kuna muda wa kwenda kula au kupumzika kdg, hapo ndo mchezo huu wa kubadilisha masanduku hufanywa, polisi wanajua!!!

Bila tume huru ushindi kwa wapinzani ni ndoto!!!madai ya tume huru ya uchaguzi yapewe kipaumbele sasa kabla ya 2010.
 
mzee-mwanakijiji-albums-news-worthy-picture478-toleola40.jpg


Kuna taarifa ambayo tumekuwa tukifuatilia wiki mbili zilizopita ambayo itakuwa na matokeo makubwa kisiasa nchini. Na kutokana na hilo tumeamua kufanya mabadiliko kadhaa; kubwa ni kuwa kijarida kitakuwa kinatoka Ijumaa.

Na twende na tuendelea kuwa "Cheche"..

Mhariri
 

Attachments

mzee-mwanakijiji-albums-news-worthy-picture478-toleola40.jpg


Kuna taarifa ambayo tumekuwa tukifuatilia wiki mbili zilizopita ambayo itakuwa na matokeo makubwa kisiasa nchini. Na kutokana na hilo tumeamua kufanya mabadiliko kadhaa; kubwa ni kuwa kijarida kitakuwa kinatoka Ijumaa.

Na twende na tuendelea kuwa "Cheche"..

Mhariri


Asante Mkuu, doc haifunguki inasema iko damaged and cannot be repaired. Pengine post tena.
 
Jamani mna uhakika Adobe zenu ni updated? Kama unatumia Adobe chini ya 8.1 nadhani utapata shida kuifungua. Je kuna mtu yeyote ameweza kuifungua?
 
Mimi nimejaribu kufungua ikafunguka. Muda mwingine ukiona docu inakataa kufunguka, jaribu kuisave (kwenye temp folder) kisha uifungue.

Asante

shukrani.. na kwa wale ambao inakuwa vigumu, fuata maelekezo ya kumuandikia mhariri na kuomba utumiwe kijarida kila wiki kwenye email yako.
 
Mh. Zitto, Benson Kigaila, Dr. Slaa, Mbowe. Na nani vile... Dada Asha Abdallah.
Nawaomba sana msijekuwakatisha tamaa wapenzi waliowapigia kura! Waambie kura mlizopata hazijatosha tu 2010 zitatosha. Naomba msirudi Dar Kabla ya kuwashukuru wananchi wa Busanda.
There is a STRONG mesg kwa CC0
Kasheshe,
Kasheshe na Wana JF, kwanza naomba radhi kuwa sikuwa hewani muda wote. Sikuwa nimeenda na Laptop, na hivyo sikuwa na mtandao. Mnavyojua Internet ni accessible Geita na siyo Katoro. Hivyo kama hatukupatikana kwenye mtandao ni kwa sababu hiyo siyo kwa vile mambo yalikuwa magumu. Katika kushindana daima mshindani wa kweli lazima afahamu hilo.

Kasheshe nakushukuru sana kwa ushauri kuhusu kuwashukuru Wana Bussanda. Tulipanga hivyo kwa bahati mbaya tulinyimwa "kibali" na polisi kwa maelezo kuwa "polisi wamechoka". Hata hivyo, tunapanga kuwa na mikutano kadhaa kabla ya kwenda Biharamulo kuwashukuru wananchi. Kura tulizopata zaidi ya 22,000 siyo haba na tunaziona kuwa mwanzo mzuri kwa 2010.
 
wakuu hapa si swala la nadharia bali najaribu kutoa changamoto kwa jinsi ninavyoyaona mambo haya. Mtu asome Sera,Ilani ya vyama vyetu vyote,nawahakikishia sijaona bora kuliko CCM, tatizo ni watekelezaji wa mipango hiyo, ndo mara nyingi hutusaliti japo nao sio wote.
Usaliti wao kwa makubaliano na dhamana tuliyowapa ndio msingi wa malalamiko yote haya, ndo maana naamini yakifanyka mabadiliko katika utendaji,mambo si mabaya kiasi hicho.
Nauye,
Kwanza nakusalimu. Lakini nadhani kusoma na kuona kuwa hujaona sera bora kuliko ya CCM is very relative. Inategemea ulikuwa unasoma kwa jicho gani. Kama unasoma kwa jicho la "Farasi" basi utakuwa unaona siku zote "uni directional". Nadhani ni tatizo. Ndiyo maana daima objectivity ni tatizo kwa watu wengi. Sitaki kusema Sera za Chadema zote ni bora, lakini nadhani kwa independent analysists wanakiri kuwa kuna mambo mazuri katika Sera za Chadema. La pili, objectivity daima inapingana na "ushabiki" usio na vigezo. May be we need more objective analysis before we make conclusions.
 
Nauye,
Kwanza nakusalimu. Lakini nadhani kusoma na kuona kuwa hujaona sera bora kuliko ya CCM is very relative. Inategemea ulikuwa unasoma kwa jicho gani. Kama unasoma kwa jicho la "Farasi" basi utakuwa unaona siku zote "uni directional". Nadhani ni tatizo. Ndiyo maana daima objectivity ni tatizo kwa watu wengi. Sitaki kusema Sera za Chadema zote ni bora, lakini nadhani kwa independent analysists wanakiri kuwa kuna mambo mazuri katika Sera za Chadema. La pili, objectivity daima inapingana na "ushabiki" usio na vigezo. May be we need more objective analysis before we make conclusions.

Dokta...nafuu umekuja mwenyewe. Unaweza kutuambia kwa maoni yako, ni kitu kimewafanya mshindwe kutoka kidedea Busanda? Na kuna marekebisho yoyote mfanyayo katika kampeni kutokana na haya matokeo?
 
Dokta...nafuu umekuja mwenyewe. Unaweza kutuambia kwa maoni yako, ni kitu kimewafanya mshindwe kutoka kidedea Busanda? Na kuna marekebisho yoyote mfanyayo katika kampeni kutokana na haya matokeo?
Mtoto,

Thanks. Kwa maoni yangu kuna mambo kadhaa yaliyotufanya tushindwe. Facts ziko clear kwa sababu ni cases ambazo zimeripotiwa na polisi lakini kwa vile Polisi wamekuwa partisan hakuna hatua iliyochukuliwa.

1) Pamoja na kuwa ni kweli kuwa mtandao wa Chadema siyo mpana hadi kwenye vijiji kama ilivyo kwa CCM, mtandao sio muhimu sana kwa uchaguzi kwani Watanzania wengi wanaonyesha dhahiri kuwa "wamechoka" na wako hoi. Hivyo wanahitaji mabadiliko japo hawajui mabadiliko hayo yaje vipi, na wengi kutokana na level ya elimu yao, wanashindwa kuoanisha uhusiano kati ya kura yao na maendeleo. Hili ni tatizo la msingi kabisa, na siku 28 za Kampeni hazitoshi kabisa kupeleka elimu hii kila mahali( ukizingatia kwa mfano Bussanda inayo vijiji 75).

2) System yote ya Serikali, kuanzia Mkuu wa Wilaya, Tarafa, Kata hadi mtendaji wa Kijiji wanafanyia kazi chama Tawala, na hasa kwa kuwatumia Watendaji wa Vijiji na wa Kata (WEO na VEO) ambao kimsingi wanatumia sana vitisho. Kwa maeneo mengi hawa bado ni "Miungu watu" na wanaogopwa sana. Hawa ndio waliotumika kushusha bendera zetu, ndio waliotumika kupasua mabango yetu, na kusimamia zoezi la kuandikisha namba za Shahada na hatimaye kuzinunua.

Tunao ushahidi kamili na kesi kadhaa zilipelekwa polisi lakini hakuna kilichoendelea. Hata kesi mmoja ingelisimamishwa mahakamani wengine wangeliogopa kufanya hivyo. Lakini kwa vile ni syndicate, hakuna hatua iliyochukuliwa, hata waliokamatwa waliachiwa wakati yeyote aliyedhaniwa wa upande wetu alikamatwa na kukaa ndani, hata kwa flimsy charges kwa mfano Waitara Mwikwabe alikamatwa na tuhuma zilizoandikishwani kusemekana kutamka " Busanda ni zaidi ya Tarime" ambayo ni slogans za kawaida kisiasa. Lakini amelala lock up siku 5 na kesi yake iko mahakamani wakati aliyekamatwa kununua shahada ya kupigia kura waliachiwa na hadi leo hakuna mwelekeo kuwa watafikishwa mahakamani.

Afisa wetu Basil Lema na Sabula walivamiwa kwenye Guest house saa 6 Usiku, mlango kuvunjwa na makada wa CCM wakiongozwa na Mtendaji wa Kijiji na Diwani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Geita. Maofisa wetu walipigwa sana na Basil alichomwa kisu, kwenye eneo la nyumba ya Diwani huyo ambako walipelekwa kwa kuongozwa na Mtendaji wa Kijiji. Walifungwa pingu ( hata polisi hawaelewei wakereketwa wa CCM walipata wapi Pingu), na hatimaye kuwafunga pia kamba mikono na miguu, mateso ya ajabu. Waliwaita polisi, lakini cha ajabu polisi walipofika walikamatwa wao (waliovamiwa) na polisi hawakutaka kusikia chochote mpaka tulipoingilia sisi kwa nguvu kubwa. Hadi leo wahusika hawakukamatwa na kupelekwa mahakamani. Ni dhahiri kuwa kuna jambo hapa.

3) Zoezi la kuandika namba za shahada na hatimaye kuzinunua imechangia kwa kiwango kikubwa katika kupunguza idadi ya wapiga kura hadi chini ya 40%.Utafiti wetu wa kina unaonyesha kuwa kwanza wanaandika namba za shahada kwa kupita nyumba hadi nyumba, kwa kutumia gear kubwa ya watendaji na maofisa VEO na WEO ikiandamana na vitisho. Baada ya kuwaandikisha wote huchambua wale ambao hawatawapigia kura, na hapo huanza kununua shahada, na kwa wanaoghairi hutumia mabavu, mathalan kata ya Nyakagomba alitumika mratibu wa Elimu kutoa vitisho vya kila aina ikiwa ni pamoja na kuwatishia kuwanyang'anya leseni za biashara, kunyang'anywa nyumba za biashara zilizopangishwa na kadhalika. Hivyo wengi wa watu wanaoondolewa katika upigaji wa kura ni wale ambao wana uhakika hawataipigia kura CCM kwa mujibu wa utambuzi wa viongozi na mtandao wao.

4) Rushwa kubwa iliyokuwa inatembea mchana kweupe, na hasa rushwa ya kitu kama Chumvi na "chupi", na matumizi ya fedha taslimu ambayo imeanzishwa safari hii, ni sababu kubwa sana vijijini kutokana na wananchi wengi wa vijijini kujali mahitaji ya "leo" badala ya mahitaji mapana (macro) yatokanayo na mchakato wa uchaguzi. Mathalan kijiji cha Nyachiluluma, tuliwakamata na kutoa taarifa polisi lakini polisi wakakataa kata kata kuwa " wanamaelekezo kuwa hawana ruksa ya kumkamata yeyote wakati wa uchaguzi mpaka maelekezo yatoke ngazi ya juu. OCD alipojulishwa naye akang"angania kuwa hiyo ni kazi ya PCB na PCB nayo haikuwa tayari. Katoro alikamatwa Mratibu wa Elimu aliyekuwa anagawa fedha wakati kura zinaendelea kupigwa na Returning Officer alipoulizwa alisema ni kosa kufanya hivyo. Polisi bado wakakataa kumkamata hadi tulipoamua kutumia nguvu na kumkamata kwa kutumia vijana wetu wenyewe. Wananchi nao walitaka kumpiga na katika hatua hiyo polisi waliingilia kumnusuru na kumpakia kwenye gari lao na kumchukua. Wakati polisi walipokataa kumkamata, alifika hapo Bwana Kiravu, Mkurugenzi wa Uchaguzi (T) akitaka akabadhiwe yeye, kwa kujua kuwa yeye hana mamlaka hayo alikataliwa. Lakini yeye ndiye aliyeenda kumtoa polisi. Mwenye kuelewa atajua hapo nako kuna nini? Hakuna kesi iliyoendelea. Mawaziri wamekutwa wakishiriki katika kugawa hizo rushwa.

5) Tunaushahidi wa dhahiri, tangu Airport Dar, hadi walipotua Geita, watuhumiwa wa Ufisadi ndio waliopeleka fedha Geita ili zitumike Busanda. Katika hali hii ni dhahiri vita haikuwa kati ya Vyama na CCM bali ufisadi na vyama kwa kutumia nguvu ya dola.

Ni kweli kuwa kazi ya kuandikisha namba za Shahada Biharamulo ilifanyika hata kabla ya kifo cha Kabuya. Ndiyo kusema kulikuwa na mawasiliano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na CCM kwa vile wakati huo, rufaa ya Kabuye ilikuwa haijaamuliwa. Lakini CCM waliisha kufahamu kuwa uchaguzi utafanyika. Tunao ushahidi wa hilo pia. Ni dhahiri Tume ya Uchaguzi (T) inafanya kazi ya CCM badala ya kuwa chombo huru kinachojitegemea kama inavyotaka ieleweke kila mara.

Kuna mengine mengi ambayo sikuyasema hapa yatajitokeza wakati tutakapotoa taarifa yetu kamili ya mchakato mzima wa Uchaguzi wa Busanda. Hatua kadhaa zimeisha kuchukuliwa na nisingelipenda kuelezea hatua hizi kwani ni mikakati ya ndani ambayo kwa hatua hii si vizuri kuitangaza hadharani. Niwajulishe tu wapenzi wetu kuwa kwa Biharamulo tumezingatia changamoto hizo zote, na tunajipanga kwa uangalifu zaidi ikiwa ni pamoja na kuzipigia kelele sana hujuma hizo za wenzetu kwenye ngazi zote.

Tusaidiane kwa wapenzi wetu wote, na ushauri wenu unakaribishwa sana.
 
Asante Dr, nilikuwa nataka kukuuliza juu ya 'low turnout' lakini maelezo yako yamenitosheleza nilikuwa najiuliza kwa nini zaidi ya 50% ya watu waliojiandikisha hawakupiga kura?
 
Back
Top Bottom