CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

- Zitto usiende huko Biharamulo na bajaji, tafuta helikopta usije ukaachwa kwenye mataa ndugu yangu, Bwa! ha! ah! mmeangukia pua sasa njooni hapa mtafute ushauri kuliko kujifanya kujua na maneno mengi empty ,

- Humble yourself njoo hapa mpate ushauri, Biharamulo bado njoo hapa utupe tathmini ya yaliyojiri Busanda ili tukupe elimu kwanza kabla ya kwenda Biharamulo!

FMES

wewe ni nani mpaka utoe ushauri?....hahahaha!
 
Natumai CH. kitashida mambo yatakwenda sawa watupigie mahesabu hela wamepata wapi? kwani watu wanakufa na njaa Mbagala wao wanamwaga Mamilioni BUSANDA sasa. SAfi mzee endelea kuleta DATA
 
FMES,

Bwa bwa bwa ha ha ha ha..Ijumaa zittoo alikuwa anajitapa sana mambo yameshakwisha na jimbo watalikamata!

Mwanakijiji uko wapi uje utuambie hiyo asilimia 50 uliyoisema imeishia wapi?zitto hajatoa sababu na keshampongeza mzee Mkuchika na wewe una sababu zipi?

Biharamuro ndiyo watapoteza kabisa!

Gembe,

Mwacheni Mwanakijiji, alisema ule ulikuwa utabiri na utabiri wowote unaweza usiende sawa.

Ila hawa CHADEMA wa JF walinifunga kamba mimi, niliamini kabisa wameshinda huko Busanda, kumbe tofauti ya kura nyingi hivyo?
 
Gembe,

Mwachie Mwanakijiji, alisema ule ulikuwa utabiri na utabiri wowote unaweza usiende sawa.

Ila hawa CHADEMA wa JF walinifunga kamba mimi, niliamini kabisa wameshinda huko Busanda, kumbe tofauti ya kura nyingi hivyo?

Hao ndio CHADEMA wanaishi kwenye kidunia chao wenyewe. Kama wanaamini kuwa wanaweza kukifuta cheo cha u-Urais wa Zanzibar hata kama hawana mbunge visiwani unadhani wanashindwa kuamini kuwa kila anayekuja kuangalia helikopta atawapigia kura!!! Wale wanaokuja kuangalia helikopta kwanza wengi ni below 18!
 
Natumai CH. kitashida mambo yatakwenda sawa watupigie mahesabu hela wamepata wapi? kwani watu wanakufa na njaa Mbagala wao wanamwaga Mamilioni BUSANDA sasa. SAfi mzee endelea kuleta DATA

Urenga,

mbona hauongelei mambo ya helikopta?pesa iliyomwagwa huko na CHADEMA kwanini isingepelekwa Mbagala?
 
wewe ni nani mpaka utoe ushauri?....hahahaha!

- Hakuna cha nani hapa mmeangukia pua huko Busanda puh! chini, maneno mengi matusi mengi kuzomea kwingi, matokeo mmepigwa chini, sasa mje hapa mpewe elimu ya bure namna ya kushinda kama tulivyowashauri kabla hamjaenda Tarime.

Respect.

FMEs!
 
nasikia pombe iliyoandaliwa kwa ajili ya ngoma ya ushindi, uliotarajiwa na CHADEMA, imetiwa kiroba cha chumvi. hainyweki tena!!!
 
😱
Sababu kama hizi huwa tunazipata pindi timu zetu za mpira zikienda kucheza nje na kufungwa, watanzania hatujambo kwa kutafuta maelezo ya kuhalalisha failure. Jamani tukubali ushindi huu na mwingine wowote wa CCM unapangwa na hao wapinzani, tena wananchi wanapoonesha nia ya kuin'goa CCM wao wanatafuta njia zote za kuibakisha (ushahidi tumeuona Busanda).

Nimehalalisha failure kivipi? Kwani mi chadema?
 
We got results from our own tally since midnight and confirmed that we have lost the Busanda election. It was a tough battle which we poised to win. I have called Mkuchika to congratulate him for the victory.

CHADEMA has increased its share of votes from 4% to 44%. To us the people have spoken though we will not seat an MP in Dodoma for Busanda. The votes give us courage to go to Biharamulo strengthened and with high spirit. There are minor mistakes we shall correct, internal and external.

Thanks all for your support. Vijana wamepigana sana. Ni bahati mbaya tu tumeshindwa.
We have a country to run. Tutakutana Biharamulo

Zitto

Zitto kumbuka kuwa mwaka 2005 cuf walipata kura 26,000 na mwaka huu chadema mmepata kura 21,000....Wananchi walishaanza kupoteza imani na mwelekeo wa Lipumba,na ikaonekana kuwa wakahamia chadema,baadaye na wewe ukafuatana na Lipumba kwenye misimamo yenu mnayoiita "Binafsi" kwa kusapoti RA na Dowans.Baadhi wakaona ujinga hawakupiga kura na wengine labda wakaipigia ccm kwa kuona hakuna jipya....Kwa hiyo sijui kama hayo ndo manaconsider "Minor Mistakes" na sijui kama hiyo ni "external" ama "internal" ila kwa maoni yangu sidhani kama mnaziendesha siasa zenu inavyotakiwa,ama pengine mnafahamu mnachofanya ila mmeamua kuwa typical politicians,inasikitisha...Kwa kifupi upinzani wenyewe kwa wenyewe mmejiangusha,na hizo hatua mlizopiga ni dhidi ya wenyewe kwa wenyewe kama tukifuata data zilizopo,hilo linapelekea mimi kujiuliza vita hii ya ufisadi inaelekea wapi,kwasababu kwa uelewa mdogo wa wananchi huwezi kuwaambia hawa watu ni mafisadi wamewaletea matatizo haya na haya lakini nawasapoti kwenye suala hili la umeme wa Dowans licha ya kwamba lina ufisadi,kwamba unasapoti dili za kifisadi kwasababu zinaleta umeme,sasa unashangazwa nini na mafisadi kushinda kwa kuleta nguzo za umeme?
I hate politics kama wanasiasa ndo nyie!
 
We got results from our own tally since midnight and confirmed that we have lost the Busanda election. It was a tough battle which we poised to win. I have called Mkuchika to congratulate him for the victory.

CHADEMA has increased its share of votes from 4% to 44%. To us the people have spoken though we will not seat an MP in Dodoma for Busanda. The votes give us courage to go to Biharamulo strengthened and with high spirit. There are minor mistakes we shall correct, internal and external.

Thanks all for your support. Vijana wamepigana sana. Ni bahati mbaya tu tumeshindwa.
We have a country to run. Tutakutana Biharamulo

Zitto

Nadhani mnastahili pongezi kubwa sana. Ikumbukwe kwamba hili lilikuwa ni jimbo linaloshikiliwa na CCM kabla hii by-election. So, kupata asilimia 44% sio kazi ndogo hata kidogo. Its a strong message to the rulling party. Mwisho wa siku sio lazima upinzani kushinda kila jimbo la uchaguzi, lakini kuwa kama watch dogs ni jambo muhimu sana. Kwa hii message ya wananchi wa Busanda, tunaamini kabisa CCM itatekeleza ilani yake ya uchaguzi kwa wananchi hawa maana 2010 sio mbali sana. Na nia ya kila mtanzania ni kuona maisha yetu yanaboreka bila kujali itikadi za kisiasa.

So, well done again. Nikiwa na imani kwamba maisha ya wananchi wa Busanda yataboreshwa kutokana na jitihada zenu za kupambana bila kuchoka. Viongozi mbalimbali wa CCM waliofika kwenye kampeni za uchaguzi huu ni ishara tosha kwamba maji yalikuwa yamewafika shingoni. Keep on pushing them, na tutafika siku nchi hii itakuwa ya maziwa na asali.
 
Kuna mambo ambayo CHADEMA wanapaswa kuzingatia katika kampeni zao zinazofuata.

1. Matumizi ya Helikopta yawe kwa nia ya kuwafikisha sehemu zisizofikika kwa urahisi/haraka.
Ila, kwa style yao (Ya sasa) ya kufanya vikao vingi kwa siku moja na kukimbia bila kuvifanyia tathmini, wakidhani kuwaeleza tu wapiga kura kuwa CCM haifai inatosha kuwahakikishia ushindi, ni kujidanganya, na kupoteza pesa zao bure.
Inabidi wafahamu kuwa, wananchi huwa wanakusanyika hata kama kuna janga (mfano ni milipuko ya mabomu, ajali n.k.).
Waangalie maana ya mikusanyiko wanayofanikiwa kuipata, wawe na mipango ya jinsi ya kuitumia mikusanyiko hiyo, na walinde kura wanazoahidiwa.
Wajue, kura nyingi nchini ni floating votes (nadhani zaidi ya 70%). Watumie wanachama wapya (kupitia operation zao - Sangara n.k.) kuongeza idadi ya wanachama, nao waelimishwe kupiga kura na kukisaidia chama kwa mambo mbalimbali.

2. Kwa maoni yangu, CCM itaamka kwa kishindo zaidi kuelekea uchaguzi ujao (Biharamulo, serikali za mitaa na 2010). Baada ya kazi kubwa iliyoipata Tarime na Busanda, ni dhahiri kuwa CCM imejifunza.

Nashauri CHADEMA (ambao inaelekea kuanza kukubalika) kuwekeza zaidi katika chaguzi za Serikali za Mitaa. Na kuachana kabisa na Biharamulo (afterall Mbunge huyo wa mwaka mmoja hawezi kuisaida sana).
Baada ya kuanguka Busanda, sidhani kuwa kuweka nguvu zao Biharamulo kutasaidia CHADEMA kushinda. Ni dhahiri kuwa watashindwa tena (kwa anaebisha "lets bet"). CCM wataendelea kutumia uwezo wake wote (kumbuka wako tayari kwa chaguzi hizi -kifedha na resources nyingine). Hivyo CHADEMA kujiingiza Biharamulo kutawapunguzia nguvu za kushinda Serikali za Mitaa (Mwaka huu).
Serikali za mitaa huongeza nguvu kwa chama kuweza kushinda udiwani, na ubunge katika uchaguzi mkuu (endapo itatumika vizuri). Inabidi wao wawe wakifanya kampeni za serikali za mitaa wakati wenzao wakitafuta ubunge Biharamulo. CHADEMA waamue kusaidia chama wanachotaka kishinde. iyo itawapa presence kidogo kwa wananchi Biharamulo ambayo itasaidia kuwapa nguvu kwenye uchaguzi Mkuu ujao.
 
FMES said:
Zitto usiende huko Biharamulo na bajaji, tafuta helikopta usije ukaachwa kwenye mataa ndugu yangu, Bwa! ha! ah! mmeangukia pua sasa njooni hapa mtafute ushauri kuliko kujifanya kujua na maneno mengi empty

FMES,

..kama una nia njema na unataka kuwasaidia kiushauri kina Zitto basi usiwa-approch kwa lugha ya kejeli kama uliyotumia.
 
Naomba Kuuliza

Je inaruhusiwa Mawaziri walioajiriwa na Serikali, wanaolipwa mishahara kwa kodi zetu Kuacha shughuli na Kwenda kwenye KAmpeni za Kisiasa BUSANDA??

MH. LAWrence Masha, MH William Ngeleja, MH George Mkuchika, Mh, Sofia Simba, MH Mwantumu Mahiza, jameni ongeezeeni list yao hapa

Sheria za tume ya uchaguzi zinasemaje?

Na Je wale waliotuhumiwa kununua Shahada je?

Naombeni ufafanuzi wa kisheria hapa...
 
FMES,

..kama una nia njema na unataka kuwasaidia kiushauri kina Zitto basi usiwa-approch kwa lugha ya kejeli kama uliyotumia.

Joka kuu,hiyo ni Lugha ya siasa na haya maneno ndiyo yankoleza siasa,Politiki mzee!
 
Back
Top Bottom