Malunde-Malundi
JF-Expert Member
- Jan 10, 2008
- 1,288
- 131
Tathmini ya Mchungaji kuhusu uchaguzi wa Busanda:
Hili ni somo jingine kwa Upinzani, na sijui ni nini kinahitajika kifanyike kuwasaida wabadilike. Inasikitisha kuwa Dr. Slaa, Zitto na Mnyika ambao tunajua wako humu ndani, wanashindwa kujifunza kutoka hili Darasa la bure la namna gani wanaweza kufanikiwa.
- Operesheni Sangara haijasaidia kitu. Ukizingatia kuwa Operesheni hii ilianzia kanda ya Ziwa Magharibi, ungetarajia iwe ni msukumo fulani ambao ungeleta mabadiliko. Lakini mpaka sasa ni wazi ama Maudhui ya Operesheni Sangara ni dhaifu au Operesheni nzima ni dhaifu na haina mantiki ya kisayansi.
- Hotuba ya Zitto na Vita vya Ufisadi. Pamoja na kuwa hotuba hiyo ilikuwa ni murwa, lakini ilitolewa kwenye wakati mbovu. Kauli nyingi za Upinzani na hata humu ndani hazileti mvuto wa mtu kufikiria kwa makini kuwa akichagua kingine, kuna ubora na ataona unafuu wa kuboresha maisha yake. Upinzani umeegemea nguvu zake kuulaani Ufisadi kama ndiyo njia pekee ya kuing'oa CCM na si kuonyesha Mtanzania ni vipianaweza jitegemea kuondokana na CCM au kutegemea chama cha Siasa. Hotuba ya Zitto ilipaswa iwe ndiyo mhimili wa kuhubiriwa kila siku kuonyesha kwa kunyu,bulisha jinsi gani Wananchi wanavyokosa mapato ya rasilimali zao na kupungua kwa maendeleo kutokana na uongozi dhaifu wa CCM, na si kegemea nguvu zote kuwa CHADEMA ndio waliovumbua Ufisadi wa EPA na Kagoda!
- Umoja ni Nguvu; Upinzani unaendelea kushindwa kujifunza kuwa kuna umuhimu wa kuwa na umoja. Hebu fikirieni, Mama Killango pamoja na kuchoshwa na Ufisadi na Udhaifu ndani ya CCM, bado alisimama kidete kwenda kuiuza CCM Busanda. Aliacha tofauti zake na Rostam na kufanyia kazi na kuhakikisha Ushindi CCM. Je upinzani uko tayari kuachana na migogoro na mivutano kila siku na kuunda umoja wa kweli na wenye nguvu?
- Nguzo na Mizizi iko vijijini: Nilipoandika Chadema must Reform na Focus 2010, nilitoa ushauri kwa Upinzani kujiandaa kwa kujijenga kupitia Serikali za Mitaa na kuachana na pilika za majukwaa makubwa. Nafahamu hizi chaguzi za Kiteto, Mbeya Vijijini, Tarime, Busanda na Magogoni ni namna ya kujipatia Ruzuku, lakini ukweli ni kuwa Upinzani umepoteza nguvu, muda na fedha kujiingiza kwenye Chaguzi ambazo ilikuwa wazi kwamba CCM ingeshinda. Badala ya kuekeza kwenye Ubunge na Uraisi, ka nini Upinzani usiwekeze kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu? Hivi hawaoni CCM ilivyo mahiri mpaka kumfanya Katibu Mwenezi wake Aggrey Mwnri kuwa Waziri Mdogo TAMISEMI ni mbinu ya kuhakikisha mizizi na nguzo za CCM zinaimarika huku vijijini ambako ndiko kuna 80%?
- Upinzani hauna Sera: Mpaka leo hii, sijui CHADEMA, CUF, TLP na hata NCCR wana sera za namna gani! Nilimuuliza Mnyika miezo kadhaa akaniambia niende kwenye webusaiti yao nikasome Ilani na Mwongozo wa CHADEMA. Mpaka kesho CCM inajulikana ni Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea hata kama imefanya mabadiliko, lakini ile imani ya Ujamaa na Kujitegemea haijafutika kwa wananchi. Je Upinzani mna Sera gani za kujiuza zaidi ya vilio vya Ufisadi?
- Watanzania si Tatizo. Ingawa majuzi nilihoji iweje 60% y Watanzania wanaridhika na shida na hivyo kuihakikishia CCM ushindi wa 60%, tatizo la kuleta madadiliko si Watanzania na hata kuwaita Wajiinga au Ndivyo Walivyo. Kosa si Watanzania ni wajinga, bali ni sisi ambao ambao tumeshindwa kuwafundisha namna gani wanaweza kuwa jamii huru yenye kujitegemea!
Inaelekea Darasa tunalotoa, anayeelimika na kufaidika ni yule tusiyemtaka; CCM!
Well presentes; wenye macho waone na kujifunza haya sasa kuelekea 2010