CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

FMES,

..kama una nia njema na unataka kuwasaidia kiushauri kina Zitto basi usiwa-approch kwa lugha ya kejeli kama uliyotumia.

- Mkulu Joka kumbe na wewe unaifahamu lugha ya kejeli na huipendi? Mbona makubwa sana haya madogo yana nafuu, eti toka lini hiyo mkulu hupendi lugha za kejeli? au toka Ijumaa mchana? Bwa! ha! ha! .......Hillarious!

- Yaani kumuomba awe careful na kibajaji ni kejeli?

Respect.

FMES!
 
Naomba Kuuliza

Je inaruhusiwa Mawaziri walioajiriwa na Serikali, wanaolipwa mishahara kwa kodi zetu Kuacha shughuli na Kwenda kwenye KAmpeni za Kisiasa BUSANDA??

MH. LAWrence Masha, MH William Ngeleja, MH George Mkuchika, Mh, Sofia Simba, MH Mwantumu Mahiza, jameni ongeezeeni list yao hapa

Sheria za tume ya uchaguzi zinasemaje?

Na Je wale waliotuhumiwa kununua Shahada je?

Naombeni ufafanuzi wa kisheria hapa...

- Kwenye hilo hakuna sheria, wanaruhusiwa sana wote uliowataja ni wabunge kama Zitto, DK. Slaa na Ndesamburo ambao wote walikuwepo huko Busanda, labda useme lingine mkuu!

FMEs!
 
Naomba Kuuliza

Je inaruhusiwa Mawaziri walioajiriwa na Serikali, wanaolipwa mishahara kwa kodi zetu Kuacha shughuli na Kwenda kwenye KAmpeni za Kisiasa BUSANDA??

MH. LAWrence Masha, MH William Ngeleja, MH George Mkuchika, Mh, Sofia Simba, MH Mwantumu Mahiza, jameni ongeezeeni list yao hapa

Sheria za tume ya uchaguzi zinasemaje?

Na Je wale waliotuhumiwa kununua Shahada je?

Naombeni ufafanuzi wa kisheria hapa...

Usisumbuke sana,hao wapinzani "Chadema" wameshakubali matokeo,ni miujiza tu kwenye siasa zetu,shangaa kuna wanaompinga RA na Dowans na wako ccm na wanaomsapoti wako upinzani,mwananchi mwenye uelewa mdogo si unamchanganya tu? Hawakumpeleka RA kusaidia kampeni huko lakini upinzani ulimpeleka mwenye kumsapoti,matokeo yake ni "Mkorogo"
 
Next attempt (2010) at Busanda it will be 90%. kwa hiyo uwezekano wa wapinzani kupata majombo mengi 2010 ni mkubwa. Tupambane kwa hali na mali kwani 'TANZANIA BILA YA SISIEMU INAWEZEKANA'

Mataokeo unayoya predict yanategemea kama Umeme hautafika Busanda kabla ya 2010. Bahati mbaya ni kwamba TANESCO imetenga ku spend $33.4 million on a 134 km (83 mile) high voltage line to add 25,000 new customers to its network, usiulize why now? Mikakati ya Uchaguzi mzee.
 
Field MArshall ES na Jmushi Asanteni.

Cha maana hapo ni kuwa somo limepatikana kwa wapinzani na kwa ccm.

ccm wamejifunza kuwa wananchi wanahitaji kutimiziwa ahadi zao na pia maendeleo yapatikane kwa kutumia rasilimali zilizopo. Ahadi hewa hazisaidiii.

Pia wabunge kama Anne Kilango na Magufuli ni wabunge wachapakazi,watetezi wa wanyonge na wasiokumbatia ufisadi na hao wamekubalika na wananchi wa busanda.

KWa wapinzani wamefanya kazi yao ya kuwaelimisha wananchi kujua na kudai haki zao.
Wapinzani wamejifunza kuwa wanahitajika kuingia zaidi vijijini na kueleza sera zao na kuwaeleza wananchi madhara ya ufisadi.

Wapinzani penye uwezekano wa kuungane mfanye hivyo, angalia kama Prof Lipumba hakuona upepo ukoje na angeamua kujitoa kuliko kupoteza muda na kupata kura 827???

Cha maana kwetu sisi ni kusubiri mechi ya MAN UTD dhidi ya BARCA ....

MAN UTD ITASHINDA, I BET!!!!
 
CCm inashinda chaguzi hizi ndogo ndogo sio kwa kupendwa na watu bali on technicalities ambazo TUME YA Uchaguzi haizirekebishi kwa makusudi ili kuipa ushindi CCM!! Mtakumbuka kwenye uchaguzi mdogo wa Mbeya vijijini, msimamizi wa uchaguzi alingoja mpaka siku ya mwisho ndio akamdisqualify CHADEMA candidate kwa kutokupeleka form yake kuhakikiwa kwa resident Magistrate kitu ambacho wangeweza kumtaalifu na yeye kurekebisha kabla ya dealine. Huko Busanda wananchi wengi waliokuwa na haki ya kupiga kura wamenyimwa haki hiyo eti kwa sababu majina yao hayakuonekana kwenye daftari; ikumbukwe kuwa watu wengi wakazi wa Geita huja huko migodini kutoka sehemu nyingi ambako walikuwa wamejiandikisha kwa hiyo Tume ya Uchaguzi ina wajibu wa kuhakikisha kuwa watu waliohamia kutoka sehemu nyingine wanaelimishswa ili wajiorodheshe kwenye madaftari ya kupiga kura huko walikohamia; bahati mbaya kwa kuisaidia CCm Tume ya Uchaguzi hukaa kimya mpaka siku ya siku ndio wanawakatalia wananchi kupiga kura na hili limetokea huko Busanda!! CCm Haishindi kwa kupendwa bali kwa kutumia mbinu chafu wanazosaidiwa na tume ya Uchaguzi!! Bila kubadili katiba ya nchi hii CCM itashinda Daima!!
 
nimekaa na kutafakari kwa kina sana juu ya hili la busanda lakini pia kwa nchi nzima.
ninachokiona ni tatizo la uelewa na uwezo wa kuchambua mambo kwa watz ni mdogo sana hasa wale wa vijijini!! kwa madudu ambayo ccm imefanya(ufisadi), ni dhahiri shairi walipaswa kuanguka huko busanda, lkn ndo hivyo wameshinda! KWA NINI?
sasa nikiangalia kwa jumla ndani ya ccm kuna mpasuko mkubwa tu, naamini next time kutakuwa na ushinda mkubwa maana watagawanyika sana,
juhudi za makusud lazima zifanyike kuhakikisha kwamba huko vijijini ambako wezi hawa wana mizizi ili wapate kuelewa.
kwa mbali naona moshi mweupe unatoka, siku moja litatokea anguko kubwa sana kwa ccm maana tayari joto linazid kupanda taratiiibu. wao bado wana ile dhana ya maisha ni ''riheso'' anyway one day tutafika, ccm hawana title deed ya nchi hii
 
Tathmini ya Mchungaji kuhusu uchaguzi wa Busanda:

  1. Operesheni Sangara haijasaidia kitu. Ukizingatia kuwa Operesheni hii ilianzia kanda ya Ziwa Magharibi, ungetarajia iwe ni msukumo fulani ambao ungeleta mabadiliko. Lakini mpaka sasa ni wazi ama Maudhui ya Operesheni Sangara ni dhaifu au Operesheni nzima ni dhaifu na haina mantiki ya kisayansi.
  2. Hotuba ya Zitto na Vita vya Ufisadi. Pamoja na kuwa hotuba hiyo ilikuwa ni murwa, lakini ilitolewa kwenye wakati mbovu. Kauli nyingi za Upinzani na hata humu ndani hazileti mvuto wa mtu kufikiria kwa makini kuwa akichagua kingine, kuna ubora na ataona unafuu wa kuboresha maisha yake. Upinzani umeegemea nguvu zake kuulaani Ufisadi kama ndiyo njia pekee ya kuing'oa CCM na si kuonyesha Mtanzania ni vipianaweza jitegemea kuondokana na CCM au kutegemea chama cha Siasa. Hotuba ya Zitto ilipaswa iwe ndiyo mhimili wa kuhubiriwa kila siku kuonyesha kwa kunyu,bulisha jinsi gani Wananchi wanavyokosa mapato ya rasilimali zao na kupungua kwa maendeleo kutokana na uongozi dhaifu wa CCM, na si kegemea nguvu zote kuwa CHADEMA ndio waliovumbua Ufisadi wa EPA na Kagoda!
  3. Umoja ni Nguvu; Upinzani unaendelea kushindwa kujifunza kuwa kuna umuhimu wa kuwa na umoja. Hebu fikirieni, Mama Killango pamoja na kuchoshwa na Ufisadi na Udhaifu ndani ya CCM, bado alisimama kidete kwenda kuiuza CCM Busanda. Aliacha tofauti zake na Rostam na kufanyia kazi na kuhakikisha Ushindi CCM. Je upinzani uko tayari kuachana na migogoro na mivutano kila siku na kuunda umoja wa kweli na wenye nguvu?
  4. Nguzo na Mizizi iko vijijini: Nilipoandika Chadema must Reform na Focus 2010, nilitoa ushauri kwa Upinzani kujiandaa kwa kujijenga kupitia Serikali za Mitaa na kuachana na pilika za majukwaa makubwa. Nafahamu hizi chaguzi za Kiteto, Mbeya Vijijini, Tarime, Busanda na Magogoni ni namna ya kujipatia Ruzuku, lakini ukweli ni kuwa Upinzani umepoteza nguvu, muda na fedha kujiingiza kwenye Chaguzi ambazo ilikuwa wazi kwamba CCM ingeshinda. Badala ya kuekeza kwenye Ubunge na Uraisi, ka nini Upinzani usiwekeze kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu? Hivi hawaoni CCM ilivyo mahiri mpaka kumfanya Katibu Mwenezi wake Aggrey Mwnri kuwa Waziri Mdogo TAMISEMI ni mbinu ya kuhakikisha mizizi na nguzo za CCM zinaimarika huku vijijini ambako ndiko kuna 80%?
  5. Upinzani hauna Sera: Mpaka leo hii, sijui CHADEMA, CUF, TLP na hata NCCR wana sera za namna gani! Nilimuuliza Mnyika miezo kadhaa akaniambia niende kwenye webusaiti yao nikasome Ilani na Mwongozo wa CHADEMA. Mpaka kesho CCM inajulikana ni Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea hata kama imefanya mabadiliko, lakini ile imani ya Ujamaa na Kujitegemea haijafutika kwa wananchi. Je Upinzani mna Sera gani za kujiuza zaidi ya vilio vya Ufisadi?
  6. Watanzania si Tatizo. Ingawa majuzi nilihoji iweje 60% y Watanzania wanaridhika na shida na hivyo kuihakikishia CCM ushindi wa 60%, tatizo la kuleta madadiliko si Watanzania na hata kuwaita Wajiinga au Ndivyo Walivyo. Kosa si Watanzania ni wajinga, bali ni sisi ambao ambao tumeshindwa kuwafundisha namna gani wanaweza kuwa jamii huru yenye kujitegemea!
Hili ni somo jingine kwa Upinzani, na sijui ni nini kinahitajika kifanyike kuwasaida wabadilike. Inasikitisha kuwa Dr. Slaa, Zitto na Mnyika ambao tunajua wako humu ndani, wanashindwa kujifunza kutoka hili Darasa la bure la namna gani wanaweza kufanikiwa.

Inaelekea Darasa tunalotoa, anayeelimika na kufaidika ni yule tusiyemtaka; CCM!
 
Inawezekana baadhi ya wachangiaji hapa wakadhani kuwa kura za CCM Busanda zimepungua ikilinganishwa na 2005. Inawezekana pia wengine wakashangaa kuwa zimeongezeka kuliko mwaka 2005, na zilizopungua ni za upinzani.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi huu, baadhi ya kura zilizokuwa za CUF zimechukuliwa na CHADEMA na baadhi zimechukuliwa na CCM. Vile vile, inaelekea kura nyingi zaidi badala ya kubaki kwa upinzani zimehamia CCM. Kwahiyo ukiangalia jumla ya kura zilizokuwa za upinzani mwaka 2005 zimepungua katika uchaguzi huu. Hii inaashiria kuwa CCM imefanikiwa zaidi katika uchaguzi huu kuliko ilivyofanikiwa mwaka 2005.
 
Zitto alisema licha ya kugubikwa na wingu la ufisadi, bado aliwasapoti Dowans ili wananchi wasiendelee kupata shida na badala yake waweze kupata umeme,sasa ccm wamemwaga nguzo za umeme lakini ni mafisadi,kwa kutumia vigezo vile vile vya Zitto kuhusu kuwasaidia wananchi,kwanini ccm wasichaguliwe?
Principle ile ile iliyotumika na msomi kama Zitto kusapoti mafisadi ndo hiyo hiyo waliyoitumia wana Busanda na kwahivyo pesa za wananchi zinazidi kufujwa kwa hivi vyama vingi wakati kiukweli kwa asilimia kubwa lao moja wanasiasa.
 
Inawezekana baadhi ya wachangiaji hapa wakadhani kuwa kura za CCM Busanda zimepungua ikilinganishwa na 2005. Inawezekana pia wengine wakashangaa kuwa zimeongezeka kuliko mwaka 2005, na zilizopungua ni za upinzani.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi huu, baadhi ya kura zilizokuwa za CUF zimechukuliwa na CHADEMA na baadhi zimechukuliwa na CCM. Vile vile, inaelekea kura nyingi zaidi badala ya kubaki kwa upinzani zimehamia CCM. Kwahiyo ukiangalia jumla ya kura zilizokuwa za upinzani mwaka 2005 zimepungua katika uchaguzi huu. Hii inaashiria kuwa CCM imefanikiwa zaidi katika uchaguzi huu kuliko ilivyofanikiwa mwaka 2005.

Ulichokisema hapo juu ndo nimekuwa niwaambia hawa wanachadema toka matokeo rasmi ya ushindi wa ccm yalipoanza kutolewa....Niliwaambia vurugu ni kati yao wapinzani na ccm ndo imenufaika zaidi,cha msingi walichotakiwa kufanya ni wapiga kura wapya ambao hata hivyo wanaweza wakawa walikatishwa tamaa na siasa za Zitto na Lipumba.
Inasikitisha lakini ndo ukweli.
 
Ndio matokeo ya siasa za keyboard hayo na kupeana false hope. Kilichobali sasa ni mtuletee vile visingizio vyenu vya kawaida wizi, ubabe, mkono wa serikali nk.

Ukweli utabaki kuwa wapinzania hususan Chadema hawana mikakati, kuna wapiga genge la wazomeaji tu na sikumbuki ni lini mara ya mwisho kuzomea kumeleta mafanikio kwa chama chochote cha kisiasa.

Wananchi wa Busanda wameongea, tena wameongea loud and clear! hii tabia ya akina Pasco na genge lake kututukania wazee wetu ikome hao hao anao waita wasio na elimu ndio waliomfikisha hapo alipo na leo na elimu yake kubwa ya uhandisi habari, inanikumbusha hadithi ya wimbo wa marehem Marijan wa Chakubanga kujiita John Smith.

Zipo wapi zile tambo na majigambo? zimesaidia nini sera za kuchoma moto bendera? kejeli na matusi kuwaita watu wa makamo vibajaji zimewafikisha wapi?

Huu ni wakati muafaka kwa Chadema kurudi kwenye drawing board ba kuanza upya. Hawa pundit wa JF watawadanganya hawa ni arm-chair generals wanapigana kwenye kkeyboards tu kaeni chini muanze upya siasa si tu kungurumisha chopa na kukusanya watoto kwenye mikutano, kunahitajika mikakati endelevu ya muda mrefu na mfupi.
 
....nadhani bado wapinzani wana kazi nzito...kuna swali nataka ..tulijibu??

kwa nini turn out number ya wapiga kura imekuwa ndogo sana busanda pamoja na muamko walioonesha???

nashangaa waliojiandikisha ni karibu 120,000...waliopiga kura ni 50,000[refer alasiri na dar leo online]...that is almost 50% turn out of voters.. ,ni turn out ndogo sana ..je inatokana na ...

vitisho vya dola ..wengine wanaogopa polisi wenye mabunduki na maji washa...

je ni shahada zimenunuliwa....[za akina nani??]

kumbukeni uchaguzi wa mbeya turn out ilikuwa asilimia 30 ...ccm wakashinda..[tulijiuliza hao asilimia 70% ambao hawakujitokeza walimtaka nani?]

na je tumejiuliza hiyo asilimia ...50 % ambao hawakuweza kupiga kura busanda ..walimtaka nani???

nadhani tusiwalaumu sana wapinzani....nimeangalia datas nimeona hata madhara ya CUF na UDP kuweka mgombea hayakuwa makubwa kama unprecedented low voters turn out[serious problem-kuna kitu hapo!].....

kumbukeni Tarime voters turn out ilikuwa nzuri na CHADEMA walishinda asilimia 62%[correct me].......

nina sababu ya kuamini kuwa kama watu wote wangepiga kura busanda mshindi angeweza kuwa CHADEMA kwa asilimia 60% au CCM angeshinda kwa margin kubwa zaidi....

tatizo lipo wapi...demokrasia yetu inakuwa ya kuchonga!!
 
Poleni sana wana-Chadema wa JF, mmepigana na kushindwa kiume.

Kubalini matokeo, kumbuka; 'He Who Surrenders, Lives Longer to Fight Another Battle'
 
Poleni sana wana-Chadema wa JF, mmepigana na kushindwa kiume.

Kubalini matokeo, kumbuka; 'He Who Surrenders, Lives Longer to Fight Another Battle'

Acha upotoshaji, si "He who surrenders" Bali ni "He who fights and run away,lives to fight another day" Na hiyo ni principle ya Guerilla warfare.
 
Ndio matokeo ya siasa za keyboard hayo na kupeana false hope. Kilichobali sasa ni mtuletee vile visingizio vyenu vya kawaida wizi, ubabe, mkono wa serikali nk.

Ukweli utabaki kuwa wapinzania hususan Chadema hawana mikakati, kuna wapiga genge la wazomeaji tu na sikumbuki ni lini mara ya mwisho kuzomea kumeleta mafanikio kwa chama chochote cha kisiasa.

Wananchi wa Busanda wameongea, tena wameongea loud and clear! hii tabia ya akina Pasco na genge lake kututukania wazee wetu ikome hao hao anao waita wasio na elimu ndio waliomfikisha hapo alipo na leo na elimu yake kubwa ya uhandisi habari, inanikumbusha hadithi ya wimbo wa marehem Marijan wa Chakubanga kujiita John Smith.

Zipo wapi zile tambo na majigambo? zimesaidia nini sera za kuchoma moto bendera? kejeli na matusi kuwaita watu wa makamo vibajaji zimewafikisha wapi?

Huu ni wakati muafaka kwa Chadema kurudi kwenye drawing board ba kuanza upya. Hawa pundit wa JF watawadanganya hawa ni arm-chair generals wanapigana kwenye kkeyboards tu kaeni chini muanze upya siasa si tu kungurumisha chopa na kukusanya watoto kwenye mikutano, kunahitajika mikakati endelevu ya muda mrefu na mfupi.

Masatu;
Watu tuunatofautiana sana kimtazamo; hata hapa JF;
1. Wengine kazi kulaumu tu;for anything
2. Wengine palipo ukweli wanakubali na hawalaumu
3. Wengine kazi yao kukubali tu for anything
Mie ninachoona hata hapa JF; kuna wengine wapo ktk JF kwa sababu kuna mtandao; happened accidentaly akakuta JF; akaungana nao basi anasema useful and useless tone; wengine wana vision and when on JF they aim;provided time is allowed; they present;
Chadema ni chama kichanga; kilipata asilimia 3%; sasa kina almost 40% (for 500% perfomance kwa wana mahesabu ya trend) kwa Busanda tu; CCM ilifikia wakawa wanadefence wakati actually ni jimbo lao;wameleta kila aina y a cadre pale;kila pesa ( sijui kama pia zitakuwa audited); wamepeleka umeme wa uongo; wametisha wananchi kwa polisi na maneno ya akina ngeleja/mkuchika/masha alitenda kupitia polisi; wamegawa nguo na vitenge; wametoa hela; wamekamatwa na wakiandika namba za wapiga kura bila kukamatwa (waliokamatwa niwa pale mjini tu; kule kijijini walitumia udhaifu wa mtandao wa chadema kufanya hayo yote) na mengine chungu mzima;
La ukweli nawapongeza Chadema; naona wameshinda Busanda; ingawa hawakukabidhiwa Jimbo; ila wameshinda; wamedhihirisha ndio namba mbili Tz bara (maneno ya nyerere yanakaribia kutimia); CCM wakiingia sasa ktk uchaguzi hawana lelemama kwa chadema maana kosa moja goli; na pamoja niko ktk keynorad lakini naona mwanga mbele ya safari; upo; tusiwalaumu; hawana TRA; hawana kitega uchumi chochote; its real a spirit; Angalia radio/TV za dialo zilivyowahadaa wana Busanda kwa matangazo ( a shame in democracy)
Masatu mie naona huenda wana matatizo yao; yes; lakini tuwape moyo; tyuwaunge mkono; baadhi ya wanaJF tuwachangie ( nashauri accout yao iwe wazi pia watu wenye mapenzi mema wawasaidie kwa hali na mali); watoe tamko kuwa sasa chadema ni movemnet ya watu sio movement ya viongozi; ningependa siku moja TZ tukiwa na Republican na Democrat huku amani ikiwepo; ili kujenga TZ yenye mshiko; mijadala yao ibase ktk utafiti wao na wa watu wengine uliopo ili kupiga hatua mbele; naamini TZ can

Nawasilisha yangu hayo
 
....nadhani bado wapinzani wana kazi nzito...kuna swali nataka ..tulijibu??

kwa nini turn out number ya wapiga kura imekuwa ndogo sana busanda pamoja na muamko walioonesha???

nashangaa waliojiandikisha ni karibu 120,000...waliopiga kura ni 50,000[refer alasiri na dar leo online]...that is almost 50% turn out of voters.. ,ni turn out ndogo sana ..je inatokana na ...
Inashangaza sana Mkuu. Inawezekana hawakuwa na muda wa kwenda kupiga kura, ama walipata tabu kujua vituo vyao vya kupigia kura, au kuyaona majina yao au sababu nyingine yoyote. Ila ni idadi inayosikitisha sana.

vitisho vya dola ..wengine wanaogopa polisi wenye mabunduki na maji washa...
je ni shahada zimenunuliwa....[za akina nani??]

Siamini kuwa idadi ambayo haikupiga kura inaweza kuwa ilishawishiwa kufanya hivyo kwa kununuliwa kwa shahada zao za kupigia kura. NI watu wengi sana. Fikiria, kama ukinunua kila moja kwa kulipia shilingi elfu moja (1000/=), itagharimu zaidi ya shilingi million 60. Sasa sijui unaweza kutumia kiasi gani cha fedha kuzinunua zote hizo na wao wakaridhika. Pia upinzani ulikuwa macho sana kiasi kwamba isingewezekana kununua shahada nyingi kiasi hicho bila kujulikana.

Sababu ya kuogopa vitisho vya dola nalo sioni kama inawezekana kwa baadhi tu ya watu. Maana hata waliojitokeza nao pia waliona kama kulikuwa na vitisho hivyo, nao pia wangeogopa kujitokeza.

kumbukeni Tarime voters turn out ilikuwa nzuri na CHADEMA walishinda asilimia 62%[correct me].......

Bila kujali takwimu za Tarime, inajulikana kuwa CHADEMA wako imara zaidi kule. Wana uwakilishi mkubwa hata kwenye Halmashauri ya wilaya ya Tarime. Nguvu hiyo ni kubwa na inabidi waitunze. Ila pia kushinda kama walishinda kwa 62% inaelekea ushindani ulikuwa mkubwa sana kwa kuzingatia vigezo vya hapo juu.

nina sababu ya kuamini kuwa kama watu wote wangepiga kura busanda mshindi angeweza kuwa CHADEMA kwa asilimia 60% au CCM angeshinda kwa margin kubwa zaidi....
tatizo lipo wapi...demokrasia yetu inakuwa ya kuchonga!!
Nadhani tatizo lililopo ni nia ya wananchi kusimama kwenye foleni na kupiga kura. Bado watu wanatakiwa kuonyeshwa umuhimu wa kura zao moja moja. Kuna ambao hudhani kuwa wengine wanaweza kupiga kura na kumchagua wanaomtaka wao. Wengine hudhani kuwa, hata wakipiga kura, hakuna tofauti yoyote kwani kura yake ni moja tu kati ya nyingi. Kwa kifupi elimu inahitajika ili kuleta matokeo yanayotakiwa kwa wananchi kushiriki uchaguzi kila wanapopata fursa ya kufanya hivyo.
 
- Mkulu Joka kumbe na wewe unaifahamu lugha ya kejeli na huipendi? Mbona makubwa sana haya madogo yana nafuu, eti toka lini hiyo mkulu hupendi lugha za kejeli? au toka Ijumaa mchana? Bwa! ha! ha! .......Hillarious!

- Yaani kumuomba awe careful na kibajaji ni kejeli?

Respect.

FMES!

Kuna mtu aliniambia siku moja hapendi kwenda JF maana kuna Mashetani; huenda kweli wapo; maana shetani hujifanya ndiye mfalme kumbe anatekeleza malengo yake; wenye nia na mioyo safi hukimbia mashetani; kuna vigezo vingi kujua nani shetani nani si shetani; ila wataalam waliobobea huweza kubaini nawasilisha hili kama angalizo; unaweza kukaa ktk keyboard kumbe unatekeleza mambo yake mwovu; angalia ndg
 
FMES,

Bwa bwa bwa ha ha ha ha..Ijumaa zittoo alikuwa anajitapa sana mambo yameshakwisha na jimbo watalikamata!

Mwanakijiji uko wapi uje utuambie hiyo asilimia 50 uliyoisema imeishia wapi?zitto hajatoa sababu na keshampongeza mzee Mkuchika na wewe una sababu zipi?

Biharamuro ndiyo watapoteza kabisa!

nilishatoa observation yangu tangu jana kabla wewe hujaamka. Soma threads za mwanzoni.
 
Back
Top Bottom