Nakushukuru Mkuu kulisemea hili, kwa mtazamo wangu, nimewagawanya wanasiasa katika makundi makuu matatu.
Kundi la Kwanza:Ni wanasiasa wanaipenda siasa kwa dhati, na wenye uwezo wa uongozi, hawa sio wapiga domo wazuri, ni makini kwenye mambo yao na wengi wao ama lazima washawishiwe na watu, ama wateuliwe. Wengi wa kundi hili wanashughuli zao hivyo hawawi mstari wa mbele kugombea nafasi za uongozi kutokana na uchafu katika mchezo wa siasa.
Kundi la Pili:Ni la wanasiasa oportunists ambao wanaingia kwenye siasa kutafuta madaraka kutokana na njaa zao. Kwao siasa ni ajira, wengine wana uwezo wa uongozi na wengine hawana ila lengo lao ni moja, kuchumia tuu na kutaka kuula. Wengi wao hata baada ya kuukwaa ubunge, huwa wanasikitika kuukosa ulaji wa uwaziri. Hawa huwa tayari kufanya lolote ili kupata wanachokitaka. Hili ndilo kundi kubwa la wanasiasa wetu wakiwemo wengi walio kwenye upinzani.
Kundi la Tatu:Ni la wanasisa walioshiba wanaoingia kwenye siasa kutafuta power. Hawa wanafedha zao ambazo huweza kuzitumia kupata uongozi wanaoutaka na mara nyingi, hawana uwezo wa uongozi na wala siasa hawazijui, wao kila kitu itaongea pesa tuu.
NB, Hii tathmini yangu haihusiani na Natural Born Leaders, Self Made Leaders na Opportunists.
Lengo la kutanguliza tathmini hiyo ni ili kukuongoza kujua kwa nini wapinzani hawataki kuungana na kamwe hawataungana kutokana na wengi wa viongozi wake kuangukia kwenye kundi la pili ambao ni wanasiasa njaa wenye uchoyo na ubinafsi wa umimi hali inayopelekea kila chama kung'ang'ania kusimamisha wagombea wake na kushindwa kusimamisha mgombea mmoja.
Mimi naamini wale waliosusia uchaguzi Busanda, ni wafuasi wa CUF na UDP ambao walishakatishwa tamaa na uwezekano wa kushinda wagombea wao, wakaona kuliko kupoteza muda kwenda kupiga kura, bora wajipumzie na kujilia raha zao na muda wao.
Kama wapinzani wangesimamisha mgombea mmoja, Busanda wangeiteka kwa ulaini kama kumsukuma mlevi.
Ubinafsi na umimi ndio unawaponza wapinzani, mathalan, baada ya Chadema kuenguliwa Mbeya vijijini, walikuwa hawana sababu ya kususa, bali kuunganisha nguvu kumuunga mkono mgombea anayekubalika zaidi, kwa kususa kwao, CCM wamepeta, na Busanda hali ni hiyo hiyo.
Swali ni lini wapinzani watafungua macho na kuukubali ukweli halisi kuhusu siasa za Tanzania.