CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

Dr Slaa,
Kwa waliosikia kauli ya rais juzi akiwa Misungwi kuhusu ushindi wao Busanda, haishangazi kwa nini wahalifu waliachiwa na Polisi pamoja na uhalifu wote walioufanya. Ni bahati mbaya sana kuwa viongozi wengi wa Afrika wamekuwa na dharau sana kwa wananchi wao na kugeuka watumishi wa hao wanaoitwa nchi wahisani/wafadhili.

Halitakuwa jambo baya kama uovu wa watawala wetu, sambamba na kuwajulisha wananchi, pia mtawajulisha na mabalozi wa hizo nchi za hao wafadhili wao.
 
mzee-mwanakijiji-albums-news-worthy-picture478-toleola40.jpg


Kuna taarifa ambayo tumekuwa tukifuatilia wiki mbili zilizopita ambayo itakuwa na matokeo makubwa kisiasa nchini. Na kutokana na hilo tumeamua kufanya mabadiliko kadhaa; kubwa ni kuwa kijarida kitakuwa kinatoka Ijumaa.

Na twende na tuendelea kuwa "Cheche"..

Mhariri

Mzee MKJJ, nimesoma kijarida cha cheche lakina nimeshindwa ku connect dots na bolded info. yako hapo juu.
 
Mtoto,

Thanks. Kwa maoni yangu kuna mambo kadhaa yaliyotufanya tushindwe. Facts ziko clear kwa sababu ni cases ambazo zimeripotiwa na polisi lakini kwa vile Polisi wamekuwa partisan hakuna hatua iliyochukuliwa.

1) Pamoja na kuwa ni kweli kuwa mtandao wa Chadema siyo mpana hadi kwenye vijiji kama ilivyo kwa CCM, mtandao sio muhimu sana kwa uchaguzi kwani Watanzania wengi wanaonyesha dhahiri kuwa "wamechoka" na wako hoi. Hivyo wanahitaji mabadiliko japo hawajui mabadiliko hayo yaje vipi, na wengi kutokana na level ya elimu yao, wanashindwa kuoanisha uhusiano kati ya kura yao na maendeleo. Hili ni tatizo la msingi kabisa, na siku 28 za Kampeni hazitoshi kabisa kupeleka elimu hii kila mahali( ukizingatia kwa mfano Bussanda inayo vijiji 75).

2) System yote ya Serikali, kuanzia Mkuu wa Wilaya, Tarafa, Kata hadi mtendaji wa Kijiji wanafanyia kazi chama Tawala, na hasa kwa kuwatumia Watendaji wa Vijiji na wa Kata (WEO na VEO) ambao kimsingi wanatumia sana vitisho. Kwa maeneo mengi hawa bado ni "Miungu watu" na wanaogopwa sana. Hawa ndio waliotumika kushusha bendera zetu, ndio waliotumika kupasua mabango yetu, na kusimamia zoezi la kuandikisha namba za Shahada na hatimaye kuzinunua.

Tunao ushahidi kamili na kesi kadhaa zilipelekwa polisi lakini hakuna kilichoendelea. Hata kesi mmoja ingelisimamishwa mahakamani wengine wangeliogopa kufanya hivyo. Lakini kwa vile ni syndicate, hakuna hatua iliyochukuliwa, hata waliokamatwa waliachiwa wakati yeyote aliyedhaniwa wa upande wetu alikamatwa na kukaa ndani, hata kwa flimsy charges kwa mfano Waitara Mwikwabe alikamatwa na tuhuma zilizoandikishwani kusemekana kutamka " Busanda ni zaidi ya Tarime" ambayo ni slogans za kawaida kisiasa. Lakini amelala lock up siku 5 na kesi yake iko mahakamani wakati aliyekamatwa kununua shahada ya kupigia kura waliachiwa na hadi leo hakuna mwelekeo kuwa watafikishwa mahakamani.

Afisa wetu Basil Lema na Sabula walivamiwa kwenye Guest house saa 6 Usiku, mlango kuvunjwa na makada wa CCM wakiongozwa na Mtendaji wa Kijiji na Diwani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Geita. Maofisa wetu walipigwa sana na Basil alichomwa kisu, kwenye eneo la nyumba ya Diwani huyo ambako walipelekwa kwa kuongozwa na Mtendaji wa Kijiji. Walifungwa pingu ( hata polisi hawaelewei wakereketwa wa CCM walipata wapi Pingu), na hatimaye kuwafunga pia kamba mikono na miguu, mateso ya ajabu. Waliwaita polisi, lakini cha ajabu polisi walipofika walikamatwa wao (waliovamiwa) na polisi hawakutaka kusikia chochote mpaka tulipoingilia sisi kwa nguvu kubwa. Hadi leo wahusika hawakukamatwa na kupelekwa mahakamani. Ni dhahiri kuwa kuna jambo hapa.

3) Zoezi la kuandika namba za shahada na hatimaye kuzinunua imechangia kwa kiwango kikubwa katika kupunguza idadi ya wapiga kura hadi chini ya 40%.Utafiti wetu wa kina unaonyesha kuwa kwanza wanaandika namba za shahada kwa kupita nyumba hadi nyumba, kwa kutumia gear kubwa ya watendaji na maofisa VEO na WEO ikiandamana na vitisho. Baada ya kuwaandikisha wote huchambua wale ambao hawatawapigia kura, na hapo huanza kununua shahada, na kwa wanaoghairi hutumia mabavu, mathalan kata ya Nyakagomba alitumika mratibu wa Elimu kutoa vitisho vya kila aina ikiwa ni pamoja na kuwatishia kuwanyang'anya leseni za biashara, kunyang'anywa nyumba za biashara zilizopangishwa na kadhalika. Hivyo wengi wa watu wanaoondolewa katika upigaji wa kura ni wale ambao wana uhakika hawataipigia kura CCM kwa mujibu wa utambuzi wa viongozi na mtandao wao.

4) Rushwa kubwa iliyokuwa inatembea mchana kweupe, na hasa rushwa ya kitu kama Chumvi na "chupi", na matumizi ya fedha taslimu ambayo imeanzishwa safari hii, ni sababu kubwa sana vijijini kutokana na wananchi wengi wa vijijini kujali mahitaji ya "leo" badala ya mahitaji mapana (macro) yatokanayo na mchakato wa uchaguzi. Mathalan kijiji cha Nyachiluluma, tuliwakamata na kutoa taarifa polisi lakini polisi wakakataa kata kata kuwa " wanamaelekezo kuwa hawana ruksa ya kumkamata yeyote wakati wa uchaguzi mpaka maelekezo yatoke ngazi ya juu. OCD alipojulishwa naye akang"angania kuwa hiyo ni kazi ya PCB na PCB nayo haikuwa tayari. Katoro alikamatwa Mratibu wa Elimu aliyekuwa anagawa fedha wakati kura zinaendelea kupigwa na Returning Officer alipoulizwa alisema ni kosa kufanya hivyo. Polisi bado wakakataa kumkamata hadi tulipoamua kutumia nguvu na kumkamata kwa kutumia vijana wetu wenyewe. Wananchi nao walitaka kumpiga na katika hatua hiyo polisi waliingilia kumnusuru na kumpakia kwenye gari lao na kumchukua. Wakati polisi walipokataa kumkamata, alifika hapo Bwana Kiravu, Mkurugenzi wa Uchaguzi (T) akitaka akabadhiwe yeye, kwa kujua kuwa yeye hana mamlaka hayo alikataliwa. Lakini yeye ndiye aliyeenda kumtoa polisi. Mwenye kuelewa atajua hapo nako kuna nini? Hakuna kesi iliyoendelea. Mawaziri wamekutwa wakishiriki katika kugawa hizo rushwa.

5) Tunaushahidi wa dhahiri, tangu Airport Dar, hadi walipotua Geita, watuhumiwa wa Ufisadi ndio waliopeleka fedha Geita ili zitumike Busanda. Katika hali hii ni dhahiri vita haikuwa kati ya Vyama na CCM bali ufisadi na vyama kwa kutumia nguvu ya dola.

Ni kweli kuwa kazi ya kuandikisha namba za Shahada Biharamulo ilifanyika hata kabla ya kifo cha Kabuya. Ndiyo kusema kulikuwa na mawasiliano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na CCM kwa vile wakati huo, rufaa ya Kabuye ilikuwa haijaamuliwa. Lakini CCM waliisha kufahamu kuwa uchaguzi utafanyika. Tunao ushahidi wa hilo pia. Ni dhahiri Tume ya Uchaguzi (T) inafanya kazi ya CCM badala ya kuwa chombo huru kinachojitegemea kama inavyotaka ieleweke kila mara.

Kuna mengine mengi ambayo sikuyasema hapa yatajitokeza wakati tutakapotoa taarifa yetu kamili ya mchakato mzima wa Uchaguzi wa Busanda. Hatua kadhaa zimeisha kuchukuliwa na nisingelipenda kuelezea hatua hizi kwani ni mikakati ya ndani ambayo kwa hatua hii si vizuri kuitangaza hadharani. Niwajulishe tu wapenzi wetu kuwa kwa Biharamulo tumezingatia changamoto hizo zote, na tunajipanga kwa uangalifu zaidi ikiwa ni pamoja na kuzipigia kelele sana hujuma hizo za wenzetu kwenye ngazi zote.

Tusaidiane kwa wapenzi wetu wote, na ushauri wenu unakaribishwa sana.

Heshima kwako Dokta,
Maelezo yako yameelemea sana katika matendo CCM waliyofanya kuhakikisha ushindi. Na nadhani wengi tutakubali ni matendo yanayoweka doa kubwa katika chaguzi za kidemokrasia na yapaswa kukemewa kwa hali na mali.
Lakini, mimi binafsi ningependa pia kuona Chadema inachacharika zaidi katika msakato mzima wa uchaguzi. Sina uhakika wa ukubwa wa base yenu hapa nchini. Lakini nadhani kama Chadema ingeweka kundi la watu ambao inahakikisha ndio wako targeted katika sera, ingesaidia sana katika kuimarisha nguvu ya chama. Nadhani mnatumia sana slogan ya vijana katika kampeni zenu. Lakini katika wapiga kura wote, vijana wanachukua asilimia ngapi? Waliojiandikisha ni wangapi? Na wanaotoka kupiga kura ni wangapi? Sina uhakika wa data mnazokuwa nazo katika uchaguzi, na nisingependa kuwaeleza ni jinsi gani ya ku-run kampeni yenu, lakini nadhani ingesaidia kuweka angalau asilimia kadhaa ya kura mfukoni mwenu tayari, kama mtakuwa na a 'target' group. Swala hili unalionaje mheshimiwa?
 
Dr. Slaa kama haya yote uliyoyasema yametokea na mna ushahidi (kama ilivyokuwa Kiteto) kwanini mnataka kushiriki uchaguzi mdogo wa Biharamulo? Mnatarajia kutakuwa na tofauti?
 
CCM imewaliza tena Watanzania. Ili kuwe na maisha bora, ni lazima kuanza upya. Bila CCM.

As Obama says, you cannot do things the same way over and over again and expect a different result. As long as the same “wenzetu” continue to steal elections and to rule us, and in the same way, we shall continue to be one of the five poorest countries in the world.

Watanzania wameelemewa na CCM, na CCM imeelemewa na corruption. Ili Watanzania waweze kudhibiti corruption, itabidi kwanza waondokane na CCM. Hilo linakuwa gumu kwani CCM inaiba kura, tena kwa kutumia vyombo vya uma!

Nchi inayotawaliwa na wezi itaendeleaje?
 
CCM imewaliza tena Watanzania. Ili kuwe na maisha bora, ni lazima kuanza upya. Bila CCM.

As Obama says, you cannot do things the same way over and over again and expect a different result. As long as the same “wenzetu” continue to steal elections and to rule us, and in the same way, we shall continue to be one of the five poorest countries in the world.

Watanzania wameelemewa na CCM, na CCM imeelemewa na corruption. Ili Watanzania waweze kudhibiti corruption, itabidi kwanza waondokane na CCM. Hilo linakuwa gumu kwani CCM inaiba kura, tena kwa kutumia vyombo vya uma!

Nchi inayotawaliwa na wezi itaendeleaje?

Sawa, Hilo linajulikana, swali ni 'what to do'?
 
Bila shaka wanatupeleka kule tusikotaka kuwa. Watafurahi tukitumia nguvu kuwanyang'anya dola na hapo watapata nafasi ya kusema upinzani ni vita. Lakini uonevu huwa na mwisho ndugu zangu, na ukifika mwisho mnabashiri nini? Subirini hawa vijana wanaomaliza shule na vyuo sasa ambao kwao wakikosa uvumilivu ugoma na kutumia nguvu kutafuta haki watakapofikia umri wetu, sisiemu watajua nini nasema!
 
Sawa, Hilo linajulikana, swali ni 'what to do'?

Ni swala zuri, Mtoto; Nini cha kufanya!

  1. Wakati Dr. Lamwai alipogombea na kuchukua Jimbo la Ubungo, wapiga kura wake waliweza kuthibiti wizi wa CCM. Itabidi wananchi wajitolee kulinda haki yao. Nadhani hilo lilifanyika Musoma vile vile.
  2. Uongozi wa Chadema umefanya vizuri kukusanya ushahidi na mashahidi wa ujangili uliofanywa na CCM. Dr. Slaa anajua wanavyofanya hawa CCM. Tunatarajia atumie mahakama sasa kufichua angalau sehemu ya ufisadi uliofanyika. Tuko wengi sana ambao tunasema TUMAINI LETU NI SLAA.
  3. Tunatawaliwa na watu hatari sana. Inapofikia Mzee Mzima kama Malechela anaongoza kundi la watu wanaowapiga wapinzani visu, basi ujue hawa wanazungumzia amani, lakini wenyewe hawaijali hata kidogo. Polisi wakikataa kulinda usalama wa wapinzani, basi itabidi wapinzani wajilinde kwa njia zao wenyewe.
  4. CCM ni kizazi cha nyoka. Tufikishe huo ukweli kwa wananchi. Njia mbali mabali zinaweza kutumika. Hata hapa JF ni mahali pazuri pa kuanzia. Wako wanahabari wengi wanaosoma hapa.
 
Ni swala zuri, Mtoto; Nini cha kufanya!

  1. Wakati Dr. Lamwai alipogombea na kuchukua Jimbo la Ubungo, wapiga kura wake waliweza kuthibiti wizi wa CCM. Itabidi wananchi wajitolee kulinda haki yao. Nadhani hilo lilifanyika Musoma vile vile.
  2. Uongozi wa Chadema umefanya vizuri kukusanya ushahidi na mashahidi wa ujangili uliofanywa na CCM. Dr. Slaa anajua wanavyofanya hawa CCM. Tunatarajia atumie mahakama sasa kufichua angalau sehemu ya ufisadi uliofanyika. Tuko wengi sana ambao tunasema TUMAINI LETU NI SLAA.
  3. Tunatawaliwa na watu hatari sana. Inapofikia Mzee Mzima kama Malechela anaongoza kundi la watu wanaowapiga wapinzani visu, basi ujue hawa wanazungumzia amani, lakini wenyewe hawaijali hata kidogo. Polisi wakikataa kulinda usalama wa wapinzani, basi itabidi wapinzani wajilinde kwa njia zao wenyewe.
  4. CCM ni kizazi cha nyoka. Tufikishe huo ukweli kwa wananchi. Njia mbali mabali zinaweza kutumika. Hata hapa JF ni mahali pazuri pa kuanzia. Wako wanahabari wengi wanaosoma hapa.

- Mkuu Moshi habari za siku nyingi umepotea sana vipi mkuu? Huku Busanda uchaguzi ulishaisha na CCM ilishinda tena hata Chadema wamekubali kwamba ulikuwa ni uchaguzi wa haki bin halali, sasa tunajitayarisha kuelekea Biharamulo, cha msingi ni wapinzani kusimamisha mgombea mmoja tu, ama sivyo yatakuwa ni yale yale tu,

Otherwise ujumbe wako ni mzito sana.

Respect.

FMEs!
 
- Huku Busanda uchaguzi ulishaisha na CCM ilishinda tena hata Chadema wamekubali kwamba ulikuwa ni uchaguzi wa haki bin halali, sasa tunajitayarisha kuelekea Biharamulo, cha msingi ni wapinzani kusimamisha mgombea mmoja tu, ama sivyo yatakuwa ni yale yale tu,
Wapinzani kuungana peke yake hakutoshi japo ni mwanzo mzuri. Funzo la Busanda ni somo tosha, hata ukijumlisha kura zote za wapinzani, CCM bado ni kidedea.
Nasisitiza, CCM imeshinda Busanda sio kwasababu inapendwa sana, bali wanaBusanda bado wako kwenye mfumo wa chama kimoja, hivyo Biharamulo wanaweza kusema hapana.
2010 tutashuhudia majimbo walokwenda shule, upinzani angalau angalau. Kule kwa wenzangu na mimi, ni CCM tuu!.
 
FMES,

Heshima mbele mkuu! Mie nipo, ila nazidi kuumia zaidi ninavyoona wananchi wenzangu wanavyoonewa. Iweje watu wa CCM wamkamate mtendaji wa CHADEMA, wamfunge kamba na kumchoma kisu, na Polisi wasiwakamte wahalifu? Kumbe mikutano aliyoongoza Mzee Malechela ilikuwa ya kupanga namna ya kufanikisha uhalifu kama huu?

I am completely convinced now that the greatest and most debilitating corruption in Tanzania is that of CCM. This group of evil doers sign secret deals with people who rape us, embezzle funds from the national coffers, and rig elections! There is no limit on what this den of vipers could do!
 
- Ingekuwa ni kweli basi upinzani wasingepata hata kura moja, sasa unasema hao 44% walioipigia Chadema ni wakimbizi huko Busanda au?

Respect.

FMEs!

Haya ni mambo ya mind set. Niliposema Busanda bado wako kwenye usingizi wa mfumo wa chama kimoja kama yalivyo maeneo mengi Tanzania, ndio maana CCM imeshinda na itaendelea kushinda as long as usingizi unaendelea.
Kazi kubwa sasa iwe ni kuwaamsha waliolala (civic education), wa mijini wameanza kuamka, 2010 hilo litathibiki, kwa vijijini, kazi ni kubwa labda maeneo ya waliokwenda shule.
Busanda Walipomuona Mzee wakamkumbuka Nyerere, Wasukuma huwaambii lolote kuhusu Nyerere, ilipita kampeni ya kikabila kuchagua chama cha Nyerere.

Busanda wa mijini wameamka, wa vijijini wanaamka, 2010 Mzee atakuwa bize na msalaba wake, tegemeo la Mama kurudi Busanda, ni kama atabebeka baada ya Ma-mdogo kumshika mkono na kumnadi pale Katoro huku akiahidi atambeba Bungeni, hivyo akibebwa, abebeke, vinginevyo Busanda ni majimbo ya uhakika ya Chadema kama Tarime.
 
Nakushukuru Mkuu kulisemea hili, kwa mtazamo wangu, nimewagawanya wanasiasa katika makundi makuu matatu.
Kundi la Kwanza:Ni wanasiasa wanaipenda siasa kwa dhati, na wenye uwezo wa uongozi, hawa sio wapiga domo wazuri, ni makini kwenye mambo yao na wengi wao ama lazima washawishiwe na watu, ama wateuliwe. Wengi wa kundi hili wanashughuli zao hivyo hawawi mstari wa mbele kugombea nafasi za uongozi kutokana na uchafu katika mchezo wa siasa.
Kundi la Pili:Ni la wanasiasa oportunists ambao wanaingia kwenye siasa kutafuta madaraka kutokana na njaa zao. Kwao siasa ni ajira, wengine wana uwezo wa uongozi na wengine hawana ila lengo lao ni moja, kuchumia tuu na kutaka kuula. Wengi wao hata baada ya kuukwaa ubunge, huwa wanasikitika kuukosa ulaji wa uwaziri. Hawa huwa tayari kufanya lolote ili kupata wanachokitaka. Hili ndilo kundi kubwa la wanasiasa wetu wakiwemo wengi walio kwenye upinzani.
Kundi la Tatu:Ni la wanasisa walioshiba wanaoingia kwenye siasa kutafuta power. Hawa wanafedha zao ambazo huweza kuzitumia kupata uongozi wanaoutaka na mara nyingi, hawana uwezo wa uongozi na wala siasa hawazijui, wao kila kitu itaongea pesa tuu.
NB, Hii tathmini yangu haihusiani na Natural Born Leaders, Self Made Leaders na Opportunists.
Lengo la kutanguliza tathmini hiyo ni ili kukuongoza kujua kwa nini wapinzani hawataki kuungana na kamwe hawataungana kutokana na wengi wa viongozi wake kuangukia kwenye kundi la pili ambao ni wanasiasa njaa wenye uchoyo na ubinafsi wa umimi hali inayopelekea kila chama kung'ang'ania kusimamisha wagombea wake na kushindwa kusimamisha mgombea mmoja.
Mimi naamini wale waliosusia uchaguzi Busanda, ni wafuasi wa CUF na UDP ambao walishakatishwa tamaa na uwezekano wa kushinda wagombea wao, wakaona kuliko kupoteza muda kwenda kupiga kura, bora wajipumzie na kujilia raha zao na muda wao.
Kama wapinzani wangesimamisha mgombea mmoja, Busanda wangeiteka kwa ulaini kama kumsukuma mlevi.
Ubinafsi na umimi ndio unawaponza wapinzani, mathalan, baada ya Chadema kuenguliwa Mbeya vijijini, walikuwa hawana sababu ya kususa, bali kuunganisha nguvu kumuunga mkono mgombea anayekubalika zaidi, kwa kususa kwao, CCM wamepeta, na Busanda hali ni hiyo hiyo.
Swali ni lini wapinzani watafungua macho na kuukubali ukweli halisi kuhusu siasa za Tanzania.
Hapa najifanyia tathmini nilisema nini kuhusu Wapinzani ile 2009 na kulinganisha hiki kinachoendelea UKAWA.

Pasco
 
Ushindi ni ushindi tuu, 'The Winner Takes it All, the looser standing small' ni wimbo wa ABBA.
Lazima tuipongeze CCM kwa ushindi wa kishindo.
Nimehudhuria kampeni na kushuhudia upigaji kura. aminini msiamini, CCM imeshinda sio kwasababu inapendwa sana, bali CCM imeshinda kwa sababu vijijini bado wamelala!, mimi ni Msukuma niliyezaliwa, kukulia na kusomea mjini. Kitendo na kurudi vijijini na kushuhudia jinsi low literacy level ilivyo kubwa, kimenistua, kimenisikitisha na kunihuzunisha!. Asilimia kubwa ya ndugu zangu hawajui kusoma wala kuandika! na hizo kura imebidi wapigiwe!.

Hii high ignorance level ya Watanzania, CCM wameitumia to their advantage. Siwatukani ndugu zangu Wasukumu, ila nimethibitisha CCM inaendelea kupendwa Kanda ya Ziwa kwa sababu za ujinga tuu!, sisi Wasukuma, sio watu wa fujo ila sio siri Wasukuma wa vijijini, wamelala mno!.

Inahitajika civic education ya ukweli kuwaelimisha mamilioni ya Watanzania wanaoichagua CCM bila kujua wanachagua nini au waendelee kuchagua CCM kwa sababu, au waipige chini CCM kwa sababu!. Pia kuna akina sisi tunaoichagua CCM kwa sababu so far, bado hakuna mbadala muafaka!. Baada ya kuhudhuria kampeni za Chadema jana pale Katoro, nikasema kama CCM itashinda, basi wanaKatoro ni vichaa au wamelogwa!.

Chadema imethibitisha inaweza kuwa chama mbadala, Watanzania waliolala wanazidi kuamka na wale wajinga wanazidi kuelimika. Naamini uchaguzi wa 2010 will never be the same, japo bado sioni anguko kuu la CCM, but as the going gets tough, the tough will get going, hivyo mabadiliko yanakuja.

Kwa wenzetu ilio mbali na Geita, Geita isikieni hivyo hivyo tuu mnavyoisikia!, Geita ndio wilaya yenye utajiri mkubwa wa dhahabu kuliko wilaya zote!. Kwa kifupi ndio wilaya tajiri zaidi Tanzania mzima kuliko wilaya nyingine zozote kwa utajiri wa madini ya dhahabu!, lakini watu wake ni masikini wakutupwa!.

Geita ina nyumba nyingi za udogo na nyasi kuliko nyumba za bati!. Watoto wa Geita, wanasura za kutilisha huruma!, Wakinamama wa Geita wasura za kukatisha tamaa, wakinababa wa Geita wana sura za mashaka, dada poa Geita ni buku!, buku mbili!, ukitoa dala unang'ang'aniwa! mdada anataka kuhamia, ile unagusa tuu, kwisha hata hujasema!, kama ni kwenu mtu unaweza kulia!.

Hiyo ndiyo Geita iliyozungukwa na mgodi mkubwa wa Geita Gold Mine, (wenyewe wanauita JIJIEMU kwa kukazia maneno Kisukuma!, upande mwingine kuna mgodi wa Bulyanhulu, upande mwingine kuna mgodi wa Buzwagi, upande mwingine mgodi wa Kahama Gold Mine, kitongoji cha Nyarugusu ndiko wanakohemea dhahabu wale wachimbani wadogo ambao kiukweli hali zao ni destitute!, yaani Geita ni dhahabu na dhahabu na dhahabu kila upande!, hivi kuna sababu kweli ya Geita kuzama kwenye lindi la Umasikini?. Yote hayo Wasukuma hawayajui, hawayaoni, wameambiwa hiyo dhahabu ni ya wazungu, na sasa inachimbwa kwa kazi nzuri iliyofanywa na CCM kuleta wawekezaji!, hivyo CCM is just so good na ndio maana bado mnawachagua kuyaendeleza mazuri haya kisa Wasukuma ni masikini by nature!, ila ni masikini jeuri, umasikini ni jadi yetu, utajiri hatuujui and you can never miss something you have never had!.
Wasukuma bado wamelala, wakiamka, walioamka watalala 2010!.
Naomba nikatishie hapa nisije ishia kulia bure...
Kidumu Chama Cha Mapinduzi ....
John Pombe Magufuli aliyepiga kampeni kwa Kisukuma lugha ambayo wanaielewa .
Baada ya John Pombe Magufuli kupitishwa kuwa mgombea wa CCM, nimeukumbuka huu uzi, nimemkumbuka John Pombe Magufuli alivyokuwa akipiga kampeni kwa lugha ya Kisukuma!.

Ndugu zangu wapinzani, wakati mnatafakari mtamleta nani wa kushindana na Magufuli kwenye urais, pia jiandaeni kuangalia mtakavyo yaokoa majimbo yanayoshikiliwa na upinzani kwenye kanda hii ya Ziwa, kwa nilichokishuhudia kwenye kampeni hizi za kanda hii, uchaguzi wa mwaka huu, Magufuli atayarudisha CCM, majimbo yote yanayoshikiliwa na wapinzani!.

Ila pia Tanzania tujiandae kushuhudia ukabila wa ajabu Magufuli akiishaingia Ikulu yetu. Kama kwenye kampeni NEC imepiga marufuku kuhutubia kwa kutumia lugha za makabila, lakini Magufuli amehutubia kwa Kisukuma, ni uthibitisho tosha huyu jamaa ni mkabila, hivyo subirieni tutakuja kukumbushana


Pasco
 


Baada ya John Pombe Magufuli kupitishwa kuwa mgombea wa CCM, nimeukumbuka huu uzi, nimemkumbuka John Pombe Magufuli alivyokuwa akipiga kampeni kwa lugha ya Kisukuma!.

Ndugu zangu wapinzani, wakati mnatafakari mtamleta nani wa kushindana na Magufuli kwenye urais, pia jiandaeni kuangalia mtakavyo yaokoa majimbo yanayoshikiliwa na upinzani kwenye kanda hii ya Ziwa, kwa nilichokishuhudia kwenye kampeni hizi za kanda hii, uchaguzi wa mwaka huu, Magufuli atayarudisha CCM, majimbo yote yanayoshikiliwa na wapinzani!.

Pasco

Kwa ujumla ccm zaid ya kupoteza majimbo mengi kwa upinzani hakuna wanachoweza kufanya
 


Baada ya John Pombe Magufuli kupitishwa kuwa mgombea wa CCM, nimeukumbuka huu uzi, nimemkumbuka John Pombe Magufuli alivyokuwa akipiga kampeni kwa lugha ya Kisukuma!.

Ndugu zangu wapinzani, wakati mnatafakari mtamleta nani wa kushindana na Magufuli kwenye urais, pia jiandaeni kuangalia mtakavyo yaokoa majimbo yanayoshikiliwa na upinzani kwenye kanda hii ya Ziwa, kwa nilichokishuhudia kwenye kampeni hizi za kanda hii, uchaguzi wa mwaka huu, Magufuli atayarudisha CCM, majimbo yote yanayoshikiliwa na wapinzani!.

Pasco

Mkuu Pasco mbona unazidi kujidhalilisha sana?.Kwa muda mrefu humu ulituaminisha eti ccm lazima impe Lowasa urais.Leo tena uko kuzusha uongo kuhusu majimbo ya ziwa.Ni hivi Chadema itayatetea yote na kuongeza mengine!!
 


Baada ya John Pombe Magufuli kupitishwa kuwa mgombea wa CCM, nimeukumbuka huu uzi, nimemkumbuka John Pombe Magufuli alivyokuwa akipiga kampeni kwa lugha ya Kisukuma!.

Ndugu zangu wapinzani, wakati mnatafakari mtamleta nani wa kushindana na Magufuli kwenye urais, pia jiandaeni kuangalia mtakavyo yaokoa majimbo yanayoshikiliwa na upinzani kwenye kanda hii ya Ziwa, kwa nilichokishuhudia kwenye kampeni hizi za kanda hii, uchaguzi wa mwaka huu, Magufuli atayarudisha CCM, majimbo yote yanayoshikiliwa na wapinzani!.

Pasco
Pasco nazidi kukuzarau usiwe mwepesi kubadilika kama kinyonga. Juzi hadi kamati kuu inaendelea wewe ulikuwa upande wa mh lowassa... Kama wewe aupo kimaslahi ni bora muda mwingine ukanyamaza kwa sababu sio lazima kila kinachokujia ubongoni mwako ukiandike hapa ... Nyani Ngabu message yake inasema miafrika ndivyo tulivyo na ihii ni kweli akuna watu wabaya duniani kama waafrika wanacheka,wanakula,wanakunywa na wewe lakini dakika moja inatosha kukusaliti tatizo ni ufukara wa akili na mali za dunia ihii.... Najua sasa hivi unajipendekeza kwa mh magufuli kusaka ukuu wa wilaya au mkoa hongera sana ...ila unajizalilisha kwa ukigeugeu kama kinyonga hata wiki bado ushakuwa na mahaba na magufuli na kumsahau mzee el kabisa .... Haya maisha haya rafiki wa kweli ni ndugu yako wengine akuna kitu zaidi ya unahaaaaaaa
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Pasco mbona unazidi kujidhalilisha sana?.Kwa muda mrefu humu ulituaminisha eti ccm lazima impe Lowasa urais.Leo tena uko kuzusha uongo kuhusu majimbo ya ziwa.Ni hivi Chadema itayatetea yote na kuongeza mengine!!
Mkuu , wengi wa wachangiaji humu are theoretical, not practical!, idadi kubwa ni wishful thinkers tuu kuwa 2015 wapinzani wataingia ikulu, ukiuliza how?, hawana majibu!. Mimi ni realist, kazi yangu ni kuwaletea ukweli nilioushuhudia kwenye ground, nikawatolea mfano wa jimbo la Busanda, na kueleza CCM ilishindaje!. Vitu vingine ni kuelezana tuu humu ndani, yakitimia tujakuja kukumbushana tuu!.

Pasco
 
Pasco nazidi kukuzarau usiwe mwepesi kubadilika kama kinyonga. Juzi hadi kamati kuu inaendelea wewe ulikuwa upande wa mh lowassa.. Najua sasa hivi unajipendekeza kwa mh magufuli kusaka ukuu wa wilaya au mkoa hongera sana ...ila unajizalilisha kwa ukigeugeu kama kinyonga hata wiki bado ushakuwa na mahaba na magufuli na kumsahau mzee el kabisa .... Haya maisha haya rafiki wa kweli ni ndugu yako wengine akuna kitu zaidi ya unahaaaaaaa
Mkuu kwanza naomba nikuhakikishie kuwa Pasco wa jf, huwa hajipendekezi kwa yoyote!. Kama unadhani Magufuli ndio nimeanza kumzungumzia baada ya kupitishwa juzi, nenda kanisome hapa, uangalie huu uzi ulipandishwa lini humu!. Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" .

Hili la ukuu wa wilaya nalo neno!. Kaangalie mshahara wa DC shilingi ngapi kwa mwezi, kisha nenda Brella kaangalie mmiliki wa kampuni inaitwa PPR ni nani, hapo Brella pia utaona hiyo PPR iko jengo gani!. Baada ya hapo nenda NHC kaangalie kodi ya pango ambayo PPR inalipa NHC, kisha ulinganishe na mshahara wa DC!, na baada ya hapo malizia kwa kwenda TRA ukaangalie hiyo PPR inalipa kodi kiasi gani!, baada ya kuyajua yote hayo, ujiulize huyo jamaa wa PPR anajipendekeza ili awe DC akapate nini?!. Kwa taarifa yako huyo DC naweza kumuajiri na kumlipa mshahara mkubwa kuliko anaolipwa!.

Pasco
 
Back
Top Bottom