CCM yaibwaga CHADEMA katika Umeya jiji la Mwanza

CCM yaibwaga CHADEMA katika Umeya jiji la Mwanza

wengine wanaulaumu uongozi wa juu wa cdm lakini kwa wale wanaokiangalia chama kwa miaka 15 na 30 ijayo ni bora walivyowafukuza watu ambao kwa uwazi wameonyesha usaliti.
Kuendelea kuwang'ang'ania isingekuwa na tofauti yoyote kama ccm wanavyowang'ng'ania mapacha wawili waliosalia na mafisadi wengine ili 'kulinda chama kisimomonyoke'. Let them go but cdm stick on its vision!




Kweli, kwani bado kuna siasa za kuganga njaa hatujafika kwenye siasa za kusimamia issues. Ni vema maamuzi kama hayo iwe ndo chachu ya kutuvusha kuelekea huko.
 
Wasukuma saizi hawataki kabisa mchezo wanataka kuongozwa na msukuma mwenzao (Wagwise) si hunajua Wenje sio msukuma ni mtu wa Kenya.
Wenje mwache achezee wasukuma kama hatukumpeleka pale nyamagana na kumchoma moto, mwanza ya leo sio ya zamani.
 
safi sana kiongozi kwa ufafanuzi wako nimekupata na hapo imejidhiilisha wazi kuwa ccm na cuf ni mtu na mpenz wake

Hapo kwenye red umekosea, CCM + CUF ni moto wa kuotea mbali. Subiri 2015, wakishirikiana kuunda serikali ya mseto (iwapo katiba mpya itaelekeza hivyo), na iwapo itakuwa ni lazima kutegemea matokeo, CDM wataendelea kuiona Magogoni kwa mbaaali kwa miaka mingine 100.
 
Mkuu unashangaa kitu gani hapo au umesahau sifa za uongozi kwenye chama chetu siku ni zipi? Ujiulizi anakatwa jina Deo Fulikunjombe halafu Lowasa na Chenge wanapeta? kama ulikuwa unadhani Duniani kuna maajabu 7 peke yake basi ujuwe Tanzania ni ajabu la 8.

Ndio maana mimi mpaka leo nimegoma kuupigia kura Mlima Kilimanjaro kwenye New 7 world wonders kwa sababu Tanzania yenyewe ni ajabu tosha kwahiyo hakuna sababu ya kupigia kura Mlima anayetaka kuprove aje ajionee mwenyewe.


Filikunjombe amewajibishwa kwa kosa la kutaka kumuengua waziri mkuu kinyume na taratibu za chama siyo yeye hata wenzake waliosaini ile karatasi ya ZK nao wameingia kwenye mkumbo huo huo. Hakuna chama kinachoweza kuvumilia kitu kama hicho. Wakati Chagulani na mwenzake wanafukuzwa uanachama tuliaambiwa kuwa walimuangusha meya wa jiji kinyume na taratibu za chama. Yaliyomkuta chagulani ndo hayo yamemkuta Deo.
 
Mtu na Mkewe na kuwadi wake=10, ushindi ni dhahiri. Poleni sana wana mwanza.
 
The main looser wa huu uchaguzi ni CUF. Meya anapatikana kutokana na kura za madiwani, na madiwani wanapiga kura along paety lines. Hatuwezi kusema CCM sasa inakubalika Mwanza kwa kuangalia kura za madiwani kwa sababu statistically chama kikiwa na madiwani wengi bais nafasi ya Meya inakuwa yao (unless kuna mamluki).

Kwa upande wa CUF uchaguzi huu ulikuwa ni nafasi muhimu kuutangazia umma kama wao wanasimama upande upi? Huko nyuma walidai wanasingiziwa kuwa wao ni CCM B, lakini baada ya huu uchaguzi wa Meya Mwanza mambo yote yamewekwa hadharani- CCM na CUF ni wamoja. Hiki ndicho kimefanyika Mwanza kwamba sasa wananchi wanajua hakuna vuguvugu tena.

Kwa upande wa CHADEMA walijua gharama ya kuwaondoa madiwani. Na hapa wameonesha wako tayari kusimamia principles za chama kwa gharama yoyote ile. Hawafugi toxic za siku 90 kwa hofu ya kupoteza nafasi za uongozi.

Imekuwa ni afadhali CHADEMA wamewatema madiwani vuguvugu mapema even kwa gharama ya kiti cha umeya na sasa wanaweza kuelekea 2015 bila mamluki. CCM wanaweza kujipongeza leo kwa ushindi wa uchaguzi wa mezani uanofanywa na watu wachache, lakini je wana ubavu kwenye uchaguzi wa uraiani?

Demokrasia ina gharama zake na ndio kama hii ya leo. Pamoja na kwamba imekuwa chungu lakini lazima tuimeze hivyo hivyo kisha tusonge mbele.
Lazima tukubali kwamba nafasi ya kuchukua umeya wa jiji la mwanza ilikuwa inaamuliwa na madiwani wa cuf na kwahiyo wameamua kuupeleka umeya ccm labda kwa sababu ni mshirika mwenzao.

Kwa upande mwingine mimi siwezi kusikitika kwa kupoteza kiti cha umeya kwakuwa Chadema tumelipa gharama ya demokrasia yetu ndani ya chama kwa kuwatimua madiwani "waasi" ambao kimsingi hata kama wangeachwa hatukuwa na uhakika wa kupata kura zao.

Wakati ccm na cuf wakishangilia ushindi huu mzuri kwao, ni muda muafaka kwetu kufanya tathmini ya kina na kutambua chimbuko la uasi wa baadhi ya madiwani wetu na kisha kuchukua hatua madhubuti kudhibiti hali hiyo isitokee tena. Muhimu zaidi ni kuendelea na M4C ili tuweze kujiimarisha zaidi kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao wa 2015, lakini pia kwa namna ya pekee kuweka mkazo katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 ili kutengeneza mtandao wa kutosha huku ngazi za chini.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kuna kipindi nilikuwa nikikosa kurog in JF nilikuwa naona kama nimepoteza kitu cha thamani kubwa ni bora nikose hata chakula, na nina declare JF ilinisaidia hata kupunguza vile vikao vya ulevi, lakini siku zinavyosonga mbele naona mabadiliko ya ghafla.

Thread hii tangu imeanza viewers ni wengi kwelikweli, lakini wachangiaji hawazidi 10, na wengi wao ni mahoka tupu, ukiisoma thread hii kwa makini unaweza ukapick some critical comment kutoka kwa Member wasiozidi 4. hii ni aibu kubwa sana kwa JF.

Nadhani sasa ni wakati muhafaka wa Reputation Power zianze kutumika ili hata mimi Matola nikiongoza kwa Pumba humu niwe nakosa Prevalege za kushiriki baadhi ya thread, hakuna tena ile taste iliyokuwa inapatikana hapa JF. Kwa maoni yangu hii ndio njia pekee ya kurudisha heshima ya mtandao huu.

New Series from Matola today Episode 1.
 
Hizi ni habari njema sana kwangu na natumia fursa hii kumpongeza naibu katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe kwa kazi nzuri anayoifanya kukimaarisha chama cha Chadema.

Hongera CCM kwa ushindi huu, na mjiandae kwa ushindi zaidi mpaka adui wenu atakapojitambuwa ni nini tatizo lake basi Lowasa atakuwa ndani ya mjengo wa Ikulu tayari.

Na hapo ndipo mtakapomsikia Rais wetu wakufikirika Zitto Kabwe anaachana na siasa na anakwenda kufanya PHD yake Ujerumani na kutangaza sasa anataka kufanya kazi alizosomea. wajinga ndio waliwao.

Ama hakika Zitto kambwe unakazi ya ziada ndani ya CDM
Hii ni laana ya kutamani nafasi za uongozi za wenye chama chao..........
Nauhakika uchaguzi ujao ikitokea CDM imeshindwa zigo zima atabebeshwa Zitto
 
Hahaaaa! Mkuu GeniusBrain nitaomba msaada wako nikishindwa ya Arusha. Tarehe 2.10 Chalii yetu Lema anarudi mjengoni, mtindo ni ule ule!


Mkuu usijali haki itatendeka na tuko pamoja kwani siasa si uadui bali kuwaletea wananchi maendeleo yao
 
Wewe kama unaona vipi unaweza ukakitoa, wakati haupo hakuna kilicho pungua na sasa umerudi hakuna kilicho zidi.unakua kama hujui uhuru wa maoni.
Mkuu achana na makapi yule, mfua nguo za magwanda.
Siku zote hana point, na ukimpakia kisawasawa, si dictionary ya matusi hiyo aliyokariri.
 
Wewe kama unaona vipi unaweza ukakitoa, wakati haupo hakuna kilicho pungua na sasa umerudi hakuna kilicho zidi.unakua kama hujui uhuru wa maoni.
Mimi sasa nashiriki JF kwa vitendo kwa kuzitumia button zote zilizopo, kwa kuanza tu nime deduct you're Reputation Power. ur not a Great Thinker but a Great Sinker.
 
Bi mdogo kaongeza majeshi kwa Mume wake kushinda Umeya. Lakini kama matokeo yalipangwa, ambao ni uvunjaji wa sheria
 
Kuna kipindi nilikuwa nikikosa kurog in JF nilikuwa naona kama nimepoteza kitu cha thamani kubwa ni bora nikose hata chakula, na nina declare JF ilinisaidia hata kupunguza vile vikao vya ulevi, lakini siku zinavyosonga mbele naona mabadiliko ya ghafla.

Thread hii tangu imeanza viewers ni wengi kwelikweli, lakini wachangiaji hawazidi 10, na wengi wao ni mahoka tupu, ukiisoma thread hii kwa makini unaweza ukapick some critical comment kutoka kwa Member wasiozidi 4. hii ni aibu kubwa sana kwa JF.

Nadhani sasa ni wakati muhafaka wa Reputation Power zianze kutumika ili hata mimi Matola nikiongoza kwa Pumba humu niwe nakosa Prevalege za kushiriki baadhi ya thread, hakuna tena ile taste iliyokuwa inapatikana hapa JF. Kwa maoni yangu hii ndio njia pekee ya kurudisha heshima ya mtandao huu.

ni swala la msingi umeshauri. ila ushauri wako ungekuwa kwenye jukwaa la complains lingewafikia wahusika kwa uharaka zaidi
 
Hapo kwenye red umekosea, CCM + CUF ni moto wa kuotea mbali. Subiri 2015, wakishirikiana kuunda serikali ya mseto (iwapo katiba mpya itaelekeza hivyo), na iwapo itakuwa ni lazima kutegemea matokeo, CDM wataendelea kuiona Magogoni kwa mbaaali kwa miaka mingine 100.

CUF hana dira kwa bara kwa sasa wabunge wawili watasaidia nini na 2015 watakuwa chini.Kule zanzibar mzee Moyo anasema zanzibar huru inakuja kwa hiyo cuf maumivu.
 
Wasukuma saizi hawataki kabisa mchezo wanataka kuongozwa na msukuma mwenzao (Wagwise) si hunajua Wenje sio msukuma ni mtu wa Kenya.


Hii akili ya kuku kwamba Wenje si mtanzania alijaribu kuitumia Masha akiwa waziri wa mambo ya ndani lakini akagonga mwamba. Sasa ccm mnapofikia hatua ya kuanza kuhubiri siasa za ukabila waziwazi kiasi hiki ni dhahiri kwamba mmeishiwa kabisa. Na kesho utakuja hapa kuhubiri ukabila wa Chadema wakati unakiri na unajua kwamba ninyi ccm ndio wakabila.
 
Mimi sasa nashiriki JF kwa vitendo kwa kuzitumia button zote zilizopo, kwa kuanza tu nime deduct you're Reputation Power. ur not a Great Thinker but a Great Sinker.
Tumia na ile ya logout.
 
Matola katikati ya ushabiki kama huu unaweza kweli kujenga hoja yenye mantiki? Kuna tatizo kubwa sana humu JF siku hizi kwani badala ya watu kujadilio hoja wamegeukia kujadili haiba za watu. Kuna thread mmoja nimeona watu jinsi walivyomjadili Maggid Mjengwa kama vile yeye si binadamu anayestahili kuheshimiwa utu wake.

Kama hatutabadili hulka yetu ya kutumia hisia badala ya akili kwenye mijadala basi JF inatumbukia shimoni. Siku hizi cha msingi si hoja bali ni wewe kama ni CCM au CHADEMA na watu wamejigawa katika misingi hiyo. Mtu wa CCM atabishana mpaka povu limkauke mdomoni na wa CHADEMA naye ndiyo hivyo hivyo.

Haya makundi mawili ndiyo yameweka tabia ya kuonesha kwamba wote wanaopingana nao hawana akili. Matola kuna hoja mbili hivi zimejirudia rudia kwenye mjadala huu na hoja zenyewe ni ile ya njia nzuri zaidi ya kuchagua Meya na nini nafasi ya nidhamu ya chama kwenye demokrasia yetu.

Tukianzia na hili ya kuchagua Meya kiukweli tatizo kubwa si mfumo wenyewe bali wanaohusika na kuutumia mfumo huo yaani madiwani. Aina hii ya kutumia wawakilishi kuchagua viongozi kwenye jamii si ngeni na inatumiwa na sehemu kubwa ya dunia. Hata Spika wa Bunge la JMT anachaguliwa na wabunge na si wananchi wote.

Kwa hiyo kuchagua Meya kwa kura za moja kwa moja si kwamba ndiyo kutaleta ufanisi kwani hata Rais wa nchi yetu tunamchagua kwa kura za moja kwa moja na bado watu huona aliyepo madarakani hafai. Ufanisi wa Halmashauri unategemea na aina ya watu wanaoshika nafasi za uwakilishi wa wananchi na si aina ya mtindo wa kuchaguliwa kwao.

Kwanza niwapongeze CHADEMA kwa kuonyesha kwamba wanaweza kufanya maamuzi ya kuwafukuza Madiwani wao kwa kukiuka maadili ya chama chao. Kwa hili la Chagulani ni wakati wa CHADEMA kuweka utaratibu wa kuwapa na kuwajua kwa undani wagombea wao ili baadaye wasipishane njia.

lakini ukiliangalia suala hili kwa undani unapata utata kidogo. Hivi kati ya Chagulani na Shibuda nani hasa mtovu zaidi wa nidhamu za kichama? Mimi nafikiri maamuzi "magumu" huwagusa wale tu wenye urahisi wa kugusika. Hivi ni kwa nini mpaka leo Shibuda hajatiwa Adabu kama alivyofanyiwa Chagulani? Hapa kuna jambo la kujifunza.

Huko zamani njia ya kumchagua Meya kwa kura za moja kwa moja ilishawahi kutumika kwenye Halmashauri Tano na Halmashauri ya Mji Mkongwe (?) ikiwa mojawapo. Nini majaribio ya kutumia mfumo huo hayakuhalalisha matumizi yake kwa nchi nzima badala yake tukarudi kwenye huu mfumo tulionao ni suala ya kujadili.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom