Nurdin Juma (Shetta) apitishwa na CCM kugombea Umeya DAR

Nurdin Juma (Shetta) apitishwa na CCM kugombea Umeya DAR

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,152
Mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wa kumpata mgombea wa Umeya wa Jiji la Dar es Salaam umeingia katika sura mpya baada ya matokeo kumuibua Nurdin Juma (Shetta) kuwa mshindi.

Katika uchaguzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa CCM Wilaya ya Ilala, Diwani wa Mchikichini, Shetta ameibuka mshindi baada ya kupata kura 25, akimshinda Diwani wa Kata ya Segerea, Robert Manangwa, aliyepata kura 21.

Ushindi huo umefikiwa baada ya mchakato wa kura kurudiwa kwa mara ya pili kufuatia duru ya awali kufutwa kutokana na mgombea aliyekuwa anaongoza kushindwa kufikisha nusu ya kura halali 52 zilizopigwa.

Hatua hiyo iliyowashangaza wengi, kwani aliyekuwa anatetea nafasi hiyo na ambaye alionekana kuwa na nafasi kubwa ya kushinda, Omary Kumbilamoto, kuondolewa mapema baada ya kupata kura nne tu katika duru ya kwanza.

Ili kumpata mshindi katika duru ya pili, Kumbilamoto na Saad Khimji waliondolewa kwenye mbio hizo, na nafasi kupewa Shetta na Manangwa ambao kura zao zilikuwa zimekaribiana zaidi.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchakato huo, Msimamizi wa uchaguzi huo, Haji Kilimo ambaye ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM, amethibitisha kuwa mshindi amepatikana kwa mujibu wa taratibu baada ya mchakato wa kura kurudiwa.
1764597653120.jpeg
 
Shetta Shetani.

Kamtoa mtoto wake kama kafara kwa shetani, kaanza kuonja faida za kafara lake.
 
Siku hizi udalali Kila kona.... Haya kapasuane mshiko na aliyekupitisha hapo.
 
Huyu sijui kama hata ya hapa na pale au Mbalimbali kama anayo
 
Back
Top Bottom