CCM yaibwaga CHADEMA katika Umeya jiji la Mwanza

CCM yaibwaga CHADEMA katika Umeya jiji la Mwanza

Matola katikati ya ushabiki kama huu unaweza kweli kujenga hoja yenye mantiki? Kuna tatizo kubwa sana humu JF siku hizi kwani badala ya watu kujadilio hoja wamegeukia kujadili haiba za watu. Kuna thread mmoja nimeona watu jinsi walivyomjadili Maggid Mjengwa kama vile yeye si binadamu anayestahili kuheshimiwa utu wake.

Kama hatutabadili hulka yetu ya kutumia hisia badala ya akili kwenye mijadala basi JF inatumbukia shimoni. Siku hizi cha msingi si hoja bali ni wewe kama ni CCM au CHADEMA na watu wamejigawa katika misingi hiyo. Mtu wa CCM atabishana mpaka povu limkauke mdomoni na wa CHADEMA naye ndiyo hivyo hivyo.

Haya makundi mawili ndiyo yameweka tabia ya kuonesha kwamba wote wanaopingana nao hawana akili. Matola kuna hoja mbili hivi zimejirudia rudia kwenye mjadala huu na hoja zenyewe ni ile ya njia nzuri zaidi ya kuchagua Meya na nini nafasi ya nidhamu ya chama kwenye demokrasia yetu.

Tukianzia na hili ya kuchagua Meya kiukweli tatizo kubwa si mfumo wenyewe bali wanaohusika na kuutumia mfumo huo yaani madiwani. Aina hii ya kutumia wawakilishi kuchagua viongozi kwenye jamii si ngeni na inatumiwa na sehemu kubwa ya dunia. Hata Spika wa Bunge la JMT anachaguliwa na wabunge na si wananchi wote.

Kwa hiyo kuchagua Meya kwa kura za moja kwa moja si kwamba ndiyo kutaleta ufanisi kwani hata Rais wa nchi yetu tunamchagua kwa kura za moja kwa moja na bado watu huona aliyepo madarakani hafai. Ufanisi wa Halmashauri unategemea na aina ya watu wanaoshika nafasi za uwakilishi wa wananchi na si aina ya mtindo wa kuchaguliwa kwao.

Kwanza niwapongeze CHADEMA kwa kuonyesha kwamba wanaweza kufanya maamuzi ya kuwafukuza Madiwani wao kwa kukiuka maadili ya chama chao. Kwa hili la Chagulani ni wakati wa CHADEMA kuweka utaratibu wa kuwapa na kuwajua kwa undani wagombea wao ili baadaye wasipishane njia.

lakini ukiliangalia suala hili kwa undani unapata utata kidogo. Hivi kati ya Chagulani na Shibuda nani hasa mtovu zaidi wa nidhamu za kichama? Mimi nafikiri maamuzi "magumu" huwagusa wale tu wenye urahisi wa kugusika. Hivi ni kwa nini mpaka leo Shibuda hajatiwa Adabu kama alivyofanyiwa Chagulani? Hapa kuna jambo la kujifunza.

Huko zamani njia ya kumchagua Meya kwa kura za moja kwa moja ilishawahi kutumika kwenye Halmashauri Tano na Halmashauri ya Mji Mkongwe (?) ikiwa mojawapo. Nini majaribio ya kutumia mfumo huo hayakuhalalisha matumizi yake kwa nchi nzima badala yake tukarudi kwenye huu mfumo tulionao ni suala ya kujadili.

Nimekuelewa uchambuzi wako kwamba CDM wasijutie kukosa meya lakini waangalie investment wanayojaribu kuweka kwa kuingiza utawala bora yaani transparency, responsibility and accountability, viongozi lazima wawajibike kwa makosa wanayofanya ya kukiingiza chama katika gharama ya uzembe, chagulani the case to site.

utaratibu wa kumpata meya siyo rafiki kwani ukiweza kupata 1/3 ya voters wakapendelea mlungura basi mmekwisha, lakini pia wale si wawakilishi halisi wa idadi ya wanamwanza, kwa hiyo ccm au chadema wanaposhangilia matokeo ya meya bila kuangalia kukubalika kwao sehemu husika unaweza kujidanganya.
Haiwezekani leo ccm wakatoka kifua mbele kwamba sasa wamewapata wana mwanza kumbe ushindi wao umetokana na ushawishi wa pesa.
Kinachojitokeza ni kwamba uamuzi wa cc ya cdm umekiponza chama kumbe yaliyofanya na cc ndiyo future KPIs tuendelee kutathmini lakini yote kwa yote maamuzi ya cdm-cc ni uwekezaji ktk good governance, lazima wafanye mambo kwa mbinu tofauti na ccm kuepuka kukopi na kupaste ya JOTI
 
Nimetumiwa Inbox eti kuna mtu hapa ananiuliza swali kwenye hii thread lakini sijamjibu, ningependa kila Member aelewe na hasa akijijuwa kabisa kwamba akili yake ni ya viwango vya kb au mb basi ajuwe ni lazima nitakuwa nimemuweka kwenye orodha yangu ya Ignore list, kwahiyo siwezi kuona post zake ila yeye atakuwa anaziona za kwangu. sina muda wa porojo miye.
 
Kwa hili ililolifanya Ritz la kutaka kutuonyesha kwenye jamii sisi wasukuma wa Mwanza mjini ni wajinga na akili zetu zimefungwa kwenye ubaguzi wa kikabila ni dharau na matusi makubwa sana kwetu.

Siwezi kuacha likapita hivi hivi.

Wacha mkwala wewe ndio mwenye hati miliki ya wasukuma Tanzania hata mie msukuma wa Nyanguge...kwani Wenje ni mtu wa wapi.
 

Maneno yakujifariji ndio haya, Slaa amefanya mazuri ndani ya cdm yes, ila haya mabaya yana cost chama sana kuliko hata hayo mazuri, kukoa u-meya mwanza sio kitu cha mchezo, tuache kupepesa pepesa macho hapa kwa slaa kiukweli ametuingiza mkenge maamuzi yake

Unavyodramatise hii issue na kufukia chanzo cha kwa nini uchaguzi ulirudiwa unatufanya sisi wote hatuna kumbukumbu unadhani unaweza kumsiliba Dr Slaa kwa matope kwa maamuzi halali ya kikao cha chama ,Jakaya kakaa juzi dodoma kampitisha Mohamedi Salma,Ridhiwani,Mwanaasha Kikwetes bila kupingwa kawafyeka akina Deo bila sababu lakini hapa umekaa unataka kutusokomeza maneno as if kuna muujiza wakati ni madiwani wa CCM kwa nyongeza ya Cuf 2 waliompa ushindi huyo meya sasa jipya lipi unalo link na Dr Slaa
CUF wamejiuliza kwa kitendo cha kumpa umeya mgombea wa CCM kwa wana Mwanza watakuwa salama ,maswali ni mengi sana katika siasa za aina hii
 
Wacha mkwala wewe ndio mwenye hati miliki ya wasukuma Tanzania hata mie msukuma wa Nyanguge...kwani Wenje ni mtu wa wapi.
Basi we mtoto haramu juzi hapa ulisema wewe mgogo ukaja mara mwera mara mzaramo inaelekea humjui babayo weye kabila gani embu tuambiye ukweli
 
Ni vizuri ukaisoma vizuri post yako kabla hujaipost humu JF ili kuepusha matatizo.

Ni hatari sana kuingiza mambo ya Ubaguzi wa kikabila kwenye mambo ya kisiasa tena kwa kuwasemea wengine.

Unataka kuwaaminisha watu kuwa sisi wasukuma ni wabaguzi sana hivyo tunachagua mtu kwa kufuata kabila lake?

Unataka kusema Laurence Masha tulimchagua 2005 kwa sababu ni msukuma na 2010 hatukumchagua kwa sababu hakuwa msukuma?

Please Ritz kama wewe ni muungwana naomba uifute post yako na kutuomba radhi sisi wasukuma ama sivyo nitamwomba MODS wakuchulie hatua.
Hebu nenda Msukuma ukagombee udiwani Moshi. Watakuvurumisha utajuta.
 
Tumia Report Abuse button kuwaeleza moderators na watachukuwa hatuwa ndani ya dakika 10 watakavyoona wao inafaa either wataifuta post au Ritz mwenyewe atapunguzwa makeke kidogo akae pembeni kwa muda ili ajifunze ustaarabu.

Option zote hapa JF ila Members hatuzitumii

Naona baada kipigo cha Mwanza mnakimbilia kwa mods kulia lia bahati nzuri kanuni na sheria za JF nazitambua.
 
ccm
oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
kuna siku mtavua chupi muvae vichwan kwa aibu. nakushangaa sana kwa umbea wako na kuzid kujizeesha kwa kuishabikia ccm
 
Wacha mkwala wewe ndio mwenye hati miliki ya wasukuma Tanzania hata mie msukuma wa Nyanguge...kwani Wenje ni mtu wa wapi.

tABIA YAKO MBAYA waSUKUMA HAWANA TABIA YA UBAGUZI NDIYO MAANA WAMETAPAKAA KILA KONA YA tANZANIA NA SASA WAMEINGIA ZAO MSUMBIJI WAKITAFUTA GRRENER PASTURE.STOP TRIBAL DISCRIMINATION WEWE
 
Yasemekana dokta hayupo tena mwanza, baada aya matokeo kutangazwa alitoka nje fasta na kutokomea kusiko julikana, ilikuwa ni aibu kubwa sana kwa dokta

Katika kuonyesha jinsi Nape anavyowapeleka puta CDM kwasasa nchini kaingia Mwanza siku tatu baada ya Dr. Slaa,kaongoza kikosi kazi cha ccm mpaka wamechukua jiji la Mwanza baada ya kuwagaragaza cdm kwa kura 11 kwa 8 za cdm!


Nimefuatilia. Vikao vya mikakati hapa jiji Mza vikiongozwa na Nape na DR. Slaa kila moja kwa style yake! Jana usiku saa mbili nikashuhudia DR. Slaa aliyekuwa kaambatana na Mpendazoe wakiondoka Mwanza kwa ndege ya precion kurudi Dar, nikajua Nape kawazidi akili nao wamejua!
Hongera Nape, pole sana Dr. Slaa!

Uchaguzi umefanyika leo, sasa nyie wenyewe magamba tuambieni Dr Slaa aliondoka jana (baada ya "kujua kazidiwa akili na nape") au kaondoka leo ("kwa aibu baada ya matokeo kutangazwa")?

Uongo mwingine bwana!
 
Kweli kuna ma great humu,unaweza soma post kama ishirini alakini moja tu,itakata kiu yako yote na kupata jibu lenye matumaini.
 
Hii akili ya kuku kwamba Wenje si mtanzania alijaribu kuitumia Masha akiwa waziri wa mambo ya ndani lakini akagonga mwamba. Sasa ccm mnapofikia hatua ya kuanza kuhubiri siasa za ukabila waziwazi kiasi hiki ni dhahiri kwamba mmeishiwa kabisa. Na kesho utakuja hapa kuhubiri ukabila wa Chadema wakati unakiri na unajua kwamba ninyi ccm ndio wakabila.

Mwita Maranya,nilifatilia mchakato wa uchaguzi wa umeya wa mwanza kwa karibu sana.Bila kuficha wala kuuma maneno kete ya ukabila ilipandikizwa na wengi hawakuitafakari waliichukua kama ilivyo na kuifanyia kazi bila kujali maslahi mapana ya jamii zetu.
Tatizo hapa watu wako tayari kupata ushindi kwa gharama yoyote ile bila kujali athari zake kwa jamii zetu.
 
Basi we mtoto haramu juzi hapa ulisema wewe mgogo ukaja mara mwera mara mzaramo inaelekea humjui babayo weye kabila gani embu tuambiye ukweli

Achana naye huyo hajui siri ya ubora wa wasukuma anafikiri umekuja hivi hivi, wasukuma hawana makuu leo akija mtanzania yeyote atapewa uongozi ili mradi ahifadhi interest zao na kuziheshimu na ndiyo maana wao pia wanakaribishwa morogoro, rukwa, mbeya lindi na mtwara.achunge sana asichezee sukuma waaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Basi we mtoto haramu juzi hapa ulisema wewe mgogo ukaja mara mwera mara mzaramo inaelekea humjui babayo weye kabila gani embu tuambiye ukweli

Wewe utakavyoniita kwangu sawa, naona umerukia kujibu kwa taarifa zaidi kesho takuwa mtu wa Kigoma kwa Zitto Kabwe, una lingine?
 
Wacha mkwala wewe ndio mwenye hati miliki ya wasukuma Tanzania hata mie msukuma wa Nyanguge...kwani Wenje ni mtu wa wapi.
Ritz, nakuaminia kwa siasa za kuhubiri ukabila na udini ila siku moja utalipwa. R.I.P
 
Naona baada kipigo cha Mwanza mnakimbilia kwa mods kulia lia bahati nzuri kanuni na sheria za JF nazitambua.
Unazitambuwa kwamba zinaruhusu Religion & tribe hatred!? unashangaza sana, sasa unavyopigwagwa ban anakuwa ni Ritz yupi huyo? subili unyolewe, Moderator watakutendea haki yako kama mlalamikaji amerepoti, mimi nilichofanya ni kumuelekeza, Member wengine hawajui namna ya kuwasiliana na moderators immediately.
 
Lu-ma-ga kuna wakati nilitoa ushauri kwa CHADEMA kupitia upya Katiba yake kwani naamini matatizo yake yamelalia hapo watu hawakunielewa. Kwa nini Slaa alikwenda Mwanza? Hii ni hoja ya kikatiba na wala si suala la Slaa kutaka kuonyesha kwamba yeye ana uwezo wa kufanya kila kitu kwenye CHADEMA.

Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA mambo yakiamuliwa ngazi ya Jimbo au Wilaya (yenye Jimbo moja) ngazi inayofuatia ni Makao Makuu. Kwa maana nyingine Mgogoro wa Chagulani hauwezi kujadiliwa na Uongozi wa Mkoa wa Mwanza kwa sababu katiba haitambui hivyo, badala yake baada ya Chagulani kushindana na Kamati tendaji ya Wilaya ngazi iliyofuatia ilikuwa ni Makao Makuu.

Kama Katiba ingeelekeza mambo ya udiwani na madiwani kuishia au kupitia kwanza kwenye ngazi ya Mkoa kabla ya kwenda Makao makuu, basi bila shaka Slaa angekuwa ni mtu wa mwisho kwenda Mwanza kwenye uchaguzi wa Meya. Lakini kwa sababu watu wa wilaya ya Mwanza hawaelewani basi ngazi inayofuatia kimadaraka (siyo kiprotokali) ni Makao Makuu na hapo ndipo Katibu Mkuu anapoingia, Lakini kwa nini iwe hivyo? Hivi haya si mambo madogomadogo kwa Katibu Mkuu kuyashughulikia!!?
 
Last edited by a moderator:
Tunahangaika weeeeeeeeee, but the truth ni kwamba adui wa chadema mwanza ni chadema wenyewe

wameshindwa kuelewa mazingira ya mwanza wakapeleka imla mwanza

mwanza ni mwanza na sio kwingine............... viongozi wa chadema taifa lazima wabadilike na kuelewa kwamba tofauti zipo tu, hata kama wote wanapenda mabadiliko

i take this loss kama changamoto kuliko chanzo cha mporomoko mwanza:dizzy:
 
Mwita Maranya,nilifatilia mchakato wa uchaguzi wa umeya wa mwanza kwa karibu sana.Bila kuficha wala kuuma maneno kete ya ukabila ilipandikizwa na wengi hawakuitafakari waliichukua kama ilivyo na kuifanyia kazi bila kujali maslahi mapana ya jamii zetu.
Tatizo hapa watu wako tayari kupata ushindi kwa gharama yoyote ile bila kujali athari zake kwa jamii zetu.

Nakubaliana na wewe kwa sasa ccm wanatumia sana ukabila na hilo alilisema DIALLO kwa chaguzi za ccm, kwa sasa mwanza wanatumika kupandikiziwa ukabila, diallo msukuma lakini wa kutoka maswa-nguliguli, lakini kuna chuki imeanzakuoteshwa kwa wasukuma wa mwanza na wa shinyanga wengine wanaitwa wa kuja.Wana mwanza lazima wawe makini sana na ccm, ccm wako ladhi yatokee ya Rwanda na burundi kuliko kuachia utawala.na tusipokuwa macho huenda taifa hili litasambaratika iwapo ccm watashindwa, yaweza kupaNDIKIZWA YA CHUKI KAMA ZA KENYA
 
Back
Top Bottom