Wanabodi,
Leo tarehe 28 2012 unafanyika Uchaguzi wa Meya pamoja ni Naibu Meya wa Halamashauri ya Jiji la Mwanza.
Kamati ya utendaji ya Chadema Nyamagana, kushirikiana na kamati za madiwa wa Chadema zimekamilisha mchakato wa kupata wagombea nafasi ya Umeya na Naibu Meya. Diwani wa Kata ya Maina, Charles Chibara, amepitishwa kuwa mgombea Umeya wa Halamashauri ya Jiji la Mwanza, Chadema wamefanya makubaliano na chama cha CUF ili wapate wingi wa kura na kumpitisha Diwani wa CUF Kata ya Mirongo Daudi Mkama, kuwa mgombea wa nafasi ya Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Siasa aina adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu Chadema wanawaita CUF ni CCM B sababu wameshirikiana na CCM Zanzibar sasa Chadema sijui wataitwaje huko Mwanza.