CCM wamekosea kutumia M4C kumnadi Magufuli


Duh! MTASHITAKI WENGI!
Na wengine hawa hapa:
M4C.png


M4C-logo-523x523-369x369.png

M4C.gif


M4C_logo.JPG
 
Nyie mnajisumbua tu, naona kipigo kimewazidi na mnaanza kukimbilia mahakamani, kesi yenu itasikilizwa baada ya uchaguzi. Mnalialia kuhusu nembo wakati sie tumewapa mgombea, mbona nyie binadamu hamna heri.
 
Hivi CCM mmeishiwa kiasi hicho? hamuoni aibu kutumia slogan ya mwenzanko tena mshindani wako mkuu? Hii si ni kuconcede defeat? CCM hapa wanaonekana wameshakubali wamezidiwa!
Yaani hiyo slogan ya Movement for Change (M4C) imeanzishwa na CHADEMA? Mkapa hakukosea.
 
Sioni hoja hapo , hiyo nembo , inatoa maana tofaut na chadema kwanini ulalamike acheni kukurupuka
Abbreviation ndio hutoa tofaut na sio nembo

BARO ELIMU YAKO ,NI KIASI GANI?
UNAFAHAMU KITU KINAITWA
1. Interectualproperty and material transfer right?
2. BRANDING AND COPY RIGHT?
KUNA WATU WANAZANI HIZI NEMBO NA MAANDISHI PAMOJA NA RANGI NA STYLE ZAKE NI SAWA NA MABANGO YANAYOBANDIKWA KWENYE BAJAJI NA BODABODA UKIVUTIWA UKAIGA TUUU UNAFUNGWA KIJANA
UMESIKIA BAROOO????
 
BARO ELIMU YAKO ,NI KIASI GANI?
UNAFAHAMU KITU KINAITWA
1. Interectualproperty and material transfer right?
2. BRANDING AND COPY RIGHT?
KUNA WATU WANAZANI HIZI NEMBO NA MAANDISHI PAMOJA NA RANGI NA STYLE ZAKE NI SAWA NA MABANGO YANAYOBANDIKWA KWENYE BAJAJI NA BODABODA UKIVUTIWA UKAIGA TUUU UNAFUNGWA KIJANA
UMESIKIA BAROOO????
Nenda mahakamani. Acha kupiga porojo zisizo na mashiko kwenye mitandao. Eti Interecualproperty, loh.
 
CCM imefilisika vibaya mpaka naogopa,sasa wameamua kutembelea nyota ya chadema,its a big gamble,it could backfire badly.

You cant allow yourself to dog think like that,as a party you can't show that level of incompitence!

Moreover,you can't allow that kind of cheap thinking to raise its voice in the party!

CCM wanatembelea nyota ya CHADEMA au Chadema ndo wanatembelea nyota ya CCM kupitia Lowasa?
 
Sioni hoja hapo , hiyo nembo , inatoa maana tofaut na chadema kwanini ulalamike acheni kukurupuka
Abbreviation ndio hutoa tofaut na sio nembo
Kama hujui kitu ni heri ukakaa kimya ueleweshwe unadhani inawezekana mtu kuanzisha chama akakiita CCM na ikakubalika kisheria?
 
Hivi inawezekana kweli CCM ikawa imeishiwa mbinu kiasi cha kukopi na ku-paste M4C?!
Kwa hili na mengine mengi ikiwemo ufisadi hamhitaji kurudishwa madarakani tena, mkubali tu akili mpya, ya kiubunifu, ya kutaka mabadiliko ifanyie mabadiliko ya kifikra, kiuchumi, kijamii, kisiasa katika nchi yetu.

WAKATI WA MABADILIKO NI SASA!

Wakianza kukosea mapema hivi wakichaguliwa si ndio wataboronga sana na kupoteza hela za walipa kodi ?!
 
Nyie wanasheria angalieni maneno yalotumika ni tofauti kabisa. Mie ni artist Magufuli for Change ni kitu tofauti kabisa na Movement for Change mnajihangaisha kwenda mahakamani mtashindwa tu.
 
Yaani hiyo slogan ya Movement for Change (M4C) imeanzishwa na CHADEMA? Mkapa hakukosea.

Mkubwa Huyo siku zote hoja hana. Tunangojea atujibu kuhusu Viwanda alivyouza, majengo TTCL, Kagoda/Kiwira, TANESCO/Net Group Solutions. Anadhani ataweza kujihami kwa matusi/ukali.
 
UVCCM mko wap mbona mnaaibisha kuweni wabunifu jaman.Mbona kwenye kutangaza nia niliona mmetengeneza logo kama 4U MOVEMENT au wale vijana walihama na lowasa.daaaa
 
jamani mbona mnakuwa wagumu wa kuelewa. M4C ni logo ya CHADEMA. kama wanatamani kutumia neno la Magufuli 4 Change waandike logo tofauti na hiyo mfano: MA4C, MFC, MAFC, etc. umeelewa?

pili, neno hilo la ----4 CHANGE ni mali ya CHADEMA. kwa hiyo hairuhusiwi KUIGA, KUNAKILI, KUTAFSIRI wala kuanzisha brand nyingine ya namna hiyo pasipo idhini ya kimaandishi kutoka CHADEMA. ingekuwa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia Magufuli angeenda jela kabla ya tarehe 25, Oktoba. umeelewa?

M can stand for anything. Let them go. Hata Lowassa walimlalamikia na kumtukana sasa wanamuabudu kushinda Mungu
 
M can stand for anything. Let them go. Hata Lowassa walimlalamikia na kumtukana sasa wanamuabudu kushinda Mungu
Hawa jamaa inaonekana hawafahamu maana ya psychological warfare. Maccm yamewashika pabaya sana kwa hili. Yaani sasa itabidi hizo kapelo zao zenye M4C wazitupilie mbali. Manaake kuanzia sasa, wakivaa hizo kapelo, wapiga kura tutaona kama wanampigia kampeni Magufuli, yaani Magufuli4Change. Imekula kwao.
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom