Nilipata wasaa wa kutazama taarifa ya habari ya AZAM TV leo usiku, nikamuona mwanasheria wa Chadema ameshika vipeperushi viwili vinavyofanana michoro ya nembo ya M4C.
ya Chadema imenogeshwa na rangi nyekundu, buluu (blue), na nyeupe. Wakati ya CCM imenogeshwa kwa rangi ya manjano na kijani.
Tukirejea kwenye suala umiliki wa logo ( namaaanisha "M4C" ) chadema wanaweza kutuonesha hadharani kuwa wao ndio wamiliki halali? Pili watueleze kinaga ubaga pasipo na shaka kuwa wao ndio wamiliki wa logo hiyo kwa kuleta hati miliki toka mamlaka husika ikiwamo basata na msajili wa vyama vya siasa kudhihirisha kuwa herufi hizo ni sehemu ya nembo yao ya usajili.Vinginevyo zitabaki kuwa sehemu ya vifupisho vya kawaida na kila mtu ana haki ya kutumia
Halafu tukirejea kwenye hiyo sheria ya umiliki na ubunifu. Nadhani inaeleza wazi uhalali wa kumiliki nembo utakamilika pale utakapopata cheti cha umiliki toka mamlaka husika, vinginevyo ikitokea CCM wanaiwahi Chadema kusajili basata na kwa msajili wa vyama vya siasa itakuwa yao. Udhaifu hapo ni mazoea ambayo unataka kutuaminisha kuwa ni mali ya chadema.
Hivi umejiuliza swali aliyebuni mchoro huo akisema yeye ndiye mmiliki halali wa hiyo logo , na kisha akatoa hati miliki yake hiyo nguvu ya kuongea mitandaoni itatoka wapi? Na akisema kwa hiyari yake kawauzia CCM mtaanzaje kujenga hoja yenu juu ya umiliki?
msimamo wangu upo pale pale kwenye tafsiri hivyo vifupisho, kama havisemi neno moja basi hiyo ndio tofauti.Vingine vinabaki kuwa mazoea kwenye maisha