Kwanza weka wazi hatimiliki ya nembo ya M4C, Kuwa ni mali ya CHADEMA vinginevyo mwacheni Magufuli atumie kwa sababu sheria uliyoorodhesha ingekuwa na nguvu kama mtaweka hadhari hatimiliki ya M4C.
Elewa kwenye siasa unaruhusiwa kutumia mbinu zozote zitakazo mdoofisha mpinzani wako , vinginevyo naona kuna tofauti ya matamshi ambayo CCM na CHADEMA wanamaanisha wakitumia M4C.Nadhani ni mbinu ya kupotosha umma wa watu wasiojua ukweli wa nani ni wa kwanza kutumia, na endapo itapata kiki basi CHADEMA itakula kwao.
M4C= MOVEMENT FOR CHANGE (CHADEMA)
M4C= MAGUFULI FOR CHANGE (CCM)
Mimi naona bado CCM wana haki kwa sababu haijadurufu uhalisia wa kifupi M4C, kirefu cha kifupisho hicho kinatoa tafsiri mbili tofauti. Litabaki suala la rangi peke yake ambalo kama CCM watatumia rangi zao basi ni wazi itakuwa mali yao ila kama wataiga na rangi ambalo hakuna mwenye hatimiliki na rangi zipi za nani kwa sababu target ya CCM ni kupotosha umma bado wanabaki pale pale kwenye kitu kinaitwa propaganda, huenda ikafanikiwa kuwatoa CDM kuacha kujadili masuala ya msingi na kuanza kulalamikia nembo.
391