CCM wamekosea kutumia M4C kumnadi Magufuli

CCM wamekosea kutumia M4C kumnadi Magufuli

Azamcola = Cocacola..... M4C = movement for change (chadema). M4C = magufuli for change (ccm). Kimbieni tu huko mahakamani mkishindwa muanze kuitukana mahakama
 
Tangu jana kumekuwepo na mijadala sehemu mbalimbali kuhusiana na matumizi ya logo ya M4C kwa chama cha Mzpinduzi (CCM). Wengine wakisema ni sawa lakini wengine wakisema si sawa.

Sikutaka kulizungumzia hili lakini naona kuna upotoshaji (wa makusudi) unaoendelea, hivyo nimeona nitumie uzoefu wangu ktk taaluma ya Mahusiano (Public Relations) na uelewa mdogo wa Sheria nilionao kutoa ufafanuzi juu ya jambo hili.

Lakini kabla sijaendelea nimpongeze sana mwanasheria wa CHADEMA John Mallya kwa kutoa msimamo wa Chama kuwa wataifikisha CCM mahakamani kwa kitendo cha kurudufu nembo yao.

Kwa uelewa wangu kinacholalamikiwa si logo tu, kinacholalamikiwa ni kitendo cha CCM kutumia nembo ya utambulisho ya chama kingine (Corporate Identity) ya CHADEMA, while are two oponent parties.

Muaasisi wa Taaluma ya Public Relations, Arthur Page alisema ili kutengeneza utambulisho wako kwa jamii (Corporate Identity) unahitaji kuwa alama zitakazokutambulisha.

Alama hizo ni pamoja na Nembo (Logo), Jina (brand name), Rangi (corporate colour), Mundo wa maandishi (designing) kama ilivyo Cocacola, etc.

Vyote hivi ndio vinatengeneza kinachoitwa utambulisho wa kampuni/shirika/asasi/chama etc.

Nembo ya M4C ni Corporate Identity ya Chama cha Demokrasia na maendeleo na imesajiliwa hivyo. Kwa hiyo CCM au chama kingine kutumia nembo hiyo bila ridhaa au makubaliano maalumu na CHADEMA ni kosa kisheria (Criminal Fraud).

KWANINI CCM WAMEKOSEA.

Sheria zinazolinda haki miliki Tanzania (The copyright and neighbouring Act, ya mwaka 1999 na The Trade and Service marks Act, ya mwaka 1986) pamoja na Sheria za kimataifa zinazolinda haki miliki zinataka kuwe na utouti wa utambulisho kati ya asasi moja na nyingine, bidhaa moja na nyingine, shirika moja na jingine etc.

Utofauti huo unakuwa kwenye maeneo mengi lakini kwa uchache ni kama ifuatavyo;

1. Jina/Brand name.
Jina moja haliwezi kutumiwa na asasi mbili tofauti zinazofanya kazi za kufanana. Kwa mfano Kampuni ya bia ya TBL ikizindua kinywaji kiitwacho "Burudani" kampuni ya Serengeti haipaswi kuanzisha kinywaji chenye jina kama hilo. Sheria inazuia ili kutowachanganya wateja na kulinda haki ya mwanzilishi wa hiyo "brand name".

Kwa hiyo kitendo cha CHADEMA kusajili nembo ya M4C kama "operation brand name" yake kinazuia chama kingine cha siasa kutumia jina hilo. Kwa hiyo CCM kutumia M4C ni kosa kisheria.

2. Muundo/Designing.
Muundo wa maandishi una hati miliki kisheria. Kwa mfano muundo wa neno Cocacola ulivyo ni tofauti na muundo wa neno Pepsi. Cocacola wanaandika kwa kucharaza. Hiyo ni designing yao. Pepsi hawaruhusiwi kuiga muundo huo unless kuwe na makubaliano maalumu na Cocacola.

Sasa CCM kwa ujinga wa kiwango cha "PhD" wameiga muundo wa neno M4C. Bora hata wangeandika kwa muundo mwingine, kwa mfano M-FOR-C, au m4c au namna nyingine itakayotofautisha brand name yao na ya CHADEMA. Lakini wamecopy na kupaste. Hapa haihitaji degree ya sheria kujua kuwa CCM wamekosea.

3. Rangi/Corporate colour.
Unaposajili bidhaa yako au kampuni yako ni vizuri kusajili na rangi yako ya utambulisho.

Kwa mfano hati ya usajili ya Chama cha mapinduzi inatambua rangi za kijani na njano kama rangi zao za utambulisho (corporate colour). Chadema rangi zao ni Blue, nyekundu, nyeupe na nyeusi.

Ukisajili rangi yako ya utambulisho ni kosa kisheria kutumia rangi ya mshindani wako hasa kwenye ulimwengu wa leo wa ushindani wa kimasoko wa "Oligopoly Marketing"

Simba hawaruhusiwi kuvaa jezi za Njano kwa sababu sio rangi yao ya utambulisho, vivyo hivyo Yanga kuvaa nyekundu.

Japo Sheria inatoa ruhusa kubadili rangi ikiwa unaona kuna haja ya kufanya hivyo. Yani ukiona "clients" wako au "audience" wako hawaridhiki na rangi yako unaweza kubadili kwa kufuata taratibu za kisheria. Na si rangi tu bali hata logo au muundo (design).

Ndio maana Vodacom ilianza na rangi ya Blue na nyeupe, lakini wakachange na sasa wanatumia nyekundu na nyeupe. Sheria inaruhusu kubadilisha.

Lakini CCM hawakufanya hivyo. Bado hati yao ya usajili inaonesha rangi zao za utambulisho ni Kijani na Njano, lakini leo wamekurupuka kutengeneza logo ya M4C kwa rangi ambazo si zao. CCM hawana utambulisho wa rangi nyekundu, blue, nyeupe wala nyeusi. Wamezitoa wapi?

Haihitaji elimu ya sheria kujua hawa watu wamekurupuka. Yani baba Njano, mama Kijani halafu mnazaa mtoto mwekundu au mweupe.. haya ni maajabu ya 8 ya dunia.

Haiwezekani baba awe Punda, mama awe Nyumbu halafu mnazaa mtoto Twiga?? Hakuna "cross genetics" ya aina hiyo. CCM u have proved failure.

Nisiwachoshe sana lakini kwa kifupi CCM wamekurupuka mno. Ni kukosa umakini kwa kiwango kikubwa. CCM ina wataalamu wa Sheria, ina wataalamu wa PR and Marketing, ina wataalamu wa Communication, kwanini wanafanya "Technical Mistake" ya kitoto namna hii? Hizi ndio akili za kushauriwa na kina Lusinde (standard seven) na kupuuza wataalamu. Poor u.!

Malisa GJ.
Makamanda acheni kupoteza muda. Haisaidii.
Sahizi tunatakiwa tupige ilani zetunza uchaguzi watu watuelewe.
Sahizi tunatakiwa tukae chini na ku solve conflicts kwenye majimbo ambayo ukawa tumegongana.
Sahizi tunatakiwa tutatue tatizo la kupika demokrasia kutoka kwa wanachama na kuwaelewesha au kujirekebisha.
Sahizi tunatakiwa tujitafakari namna gani ilani za vyama vyote zitatumika badala ya chama kimoja tuu.
Tuangalie sana tusije viua vyama vingine kwa kila chama kina umuhimu wake kwa sababu kina wanachama wake
 
Kwa iyo magufuli for change maana yake ni M4C ya chadema?

jamani mbona mnakuwa wagumu wa kuelewa. M4C ni logo ya CHADEMA. kama wanatamani kutumia neno la Magufuli 4 Change waandike logo tofauti na hiyo mfano: MA4C, MFC, MAFC, etc. umeelewa?

pili, neno hilo la ----4 CHANGE ni mali ya CHADEMA. kwa hiyo hairuhusiwi KUIGA, KUNAKILI, KUTAFSIRI wala kuanzisha brand nyingine ya namna hiyo pasipo idhini ya kimaandishi kutoka CHADEMA. ingekuwa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia Magufuli angeenda jela kabla ya tarehe 25, Oktoba. umeelewa?
 
ccm wameratibu mienendo ya nccr, na sasa chadema, tusiwasubiri chini tuwapandie juu kwa kutumia mianya ya chama chao vinginevyo tutaishia kulalama. binafsi simpigii fisadi hata akiwa ukawa!
magufuli ni dhaifu kama alivyo lowasa ila tofauti ni makandokando ya lowasa.
kwa kukubali mabadiliko magufuli amekiacha kifua cha ccm wazi kushambuliwa na watu wenye nia nZuri ya maendeleo ya umma wa watanganyika.
 
Kwanza hao CHADEMA hiyo M4C nao wameiiba kwa wengine. Huo sio ubunifu wao. Mkapa hakukosea. Mwaka huu itabidi waitupy
ilie mbali hiyo "nembo" ya M4C manaake tayari imeshakuwa kaa la moto. Maccm yamewazidi kete.

Kama ni hivyo basi kampakeni Magufuli chokaa kichwani awe kama Lowasa. Hovyo kabisa manyani wa Lumumba.
 
Kwa iyo magufuli for change maana yake ni M4C ya chadema?

mkuu, ni hivi: kwa mfano kikianzishwa chama kipya kikaamua kujiita Chama Cha Mageuzi hawawezi kutumia ufupisho wa CCM kwa kuwa tayari Chama Cha Mapinduzi wanatumia kifupisho hicho. wewe huoni kwamba wataleta mkanganyiko? nadhani sasa umenielewa. kama una swali la ziada unaruhusiwa kuuliza.
 
Sioni hoja hapo , hiyo nembo , inatoa maana tofaut na chadema kwanini ulalamike acheni kukurupuka
Abbreviation ndio hutoa tofaut na sio nembo

CCM mmeishiwa mpaka mnatia huruma, hivi slogan zenu "Mbele kwa Mbele" au Hapa Kazi Tu" mmeona hazifai mpaka mnaiba za watu

Ila siwashangai kwakuwa mmezoea kuiba kila kitu, japo kura mwaka huu hamtaweza kuiba, hahahahahaha daaaaa kwishney
 
aiseee...!!vijana wangu mbn mnakosa maarifa...
hiyo logo kwani ccm wameitumia officially...?
isitoshe hiyo ni abbreviation it can be used and Interpreted in different ways...!!

wewe unajiona maarifa sana eti? ni hivi: mfano, kama kikianzishwa chama kipya kikaamua kujiita Chama Cha Majuha hakiwezi kutumia ufupisho wa CCM kwa kuwa tayari ufupisho huo unatumiwa na Chama Cha Mapinduzi. wewe unadhani kukiwa na vyama viwili vinavyotumia ufupisho wa CCM haiwezi kuleta mkanganyiko wowote?
 
Uki google M4C utapata mashirika, bidhaa na makampuni yanatumia neno hilo! Kama M4C imesajiliwa Brela na Chadema wana Hati miliki, hilo litakuwa kosa kwa CCM. Vinginevyo ni kukubali yaishe!
 
Kabla hujaandika habar kama hii ni vema ungejiridhisha na upande wa pili(CCM) kujua kama kweli matumizi ya logo hiyo yameidhinishwa na chama au la? Otherwise kinachoendelea ni ushabiki wa mitandaoni na ccm haiwez kuwazuia watu kufanya wanachojiaikia kiushabiki..

Sheria itasema; tulia
 
Aliye na ushahidi kuwa mkono wa magufuli ndio ulioandika maneno hayo aende Mahakamani.!
 
Nimakosa kisheria, ndio maana kuna pepsi na cocacola.. Atherwise Coca-Cola angetumia jina la pepsi na kutoumiza kichwa kutafta nemdo yake na bland name.. Yake. Hivo sheria ichukue mkondo wake, lakini pia ijulikane kuwa, kwa ccm ya leo ambayo imejaa mapapa wa ufisadi pia ni watalaamu wa kusoma saikolojia ya watanzania.. Wanajua kuwa upepo ni mgumu, leo kesho na hata kufikia uchaguzi mkuu.. So wamefanya kwa makusudi mazima ili kuathiri speed ya ukawa.. Ili waanze kuwaza M4C na kulunguza nguvu ya ukawa ktk campaign.. Maana wanajua kesi ikifunguliwa leo haiishi kesho hasi baadae saana na uchaguzi utakuwa umepita..
 
chadema kusema watamshitaki mahakamani eti anatumia logo yao kivipi.wao ni MOVEMANT FOR CHANGE.
MAGUFURI FOR CHANGE.
ni tofauti na kusema jamii forum na mwanahalisi forum au cocacola na pepsi cola au azam cola au mo cola.
muwe makini msije mkaingia kichwa kichwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom