CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

kwa ufupi CCM ndo imepoteza kabisa hivyo viti vya udiwani.

Inaonekana huwajui wahaya wewe!ni wanafiki balaa.Wataendelea na CCM yao tu.We hujui ndio wamejaa serikalini na wameifaidi sana serikali tangu uhuru wa nchi hii.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Ina maana utumwa wa fikra bado upo huko, haiwezekani mumchague mtu wakati hayupo hata kama ni Ruhangisa

Tehe!
Ni mzaliwa wa ukoo wa kifalme hvyo kwa kutukuza uasili huwa ni vigumu mtu yeyote kumshinda Ruhangisa kweny uchaguzi
 
CCM yatimua madiwani wanane Bukoba Mjini

Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kagera kimewafukuza uanachama wa chama hicho, madiwani wake wanane kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kukaidi maelekezo mbalimbali ya chama hicho, pia kushirikiana na upinzani kukihujumu.

Madiwani waliotimuliwa ni wale Manispaa ya Bukoba ambao wamekuwa wakitajwa kumuunga mkono Mbunge wa Bukoba Mjini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki ambaye amekuwa akivutana vikali na Meya wa Manispaa hiyo, Anatory Amani.

Miongoni mwa waliotimuliwa ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba na Diwani wa Kashai, Yusuph Ngaiza, aliyepata kuwa mbunge wa muda mrefu wa Bukoba Mjini na baadaye Meya wa Manispaa hiyo, Samuel Ruhangisa ambaye ni Diwani wa Kitendagulo na Diwani wa Buhembe, Alexander Ngalinda ambaye pia alikuwa Naibu Meya.

Katibu wa CCM wa Mkoa wa Kagera, Averin Mushi alisema uamuzi wa kuwatimua madiwani hao umefikiwa jana na halmashauri ya CCM ya Mkoa kwa kile alichosema ni kwa ajili ya "kulinda masilahi ya chama na wananchi wa Bukoba".

Ibara ya 93 (15) ya Katiba ya CCM inataja moja ya kazi za halmashauri ya chama hicho ngazi ya mkoa kuwa ni: "Kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Halmashauri ya CCM ya Mkoa".

Hata hivyo kipengele cha 14 cha ibara hiyo ya 93 kinasema hatua kumwachisha au kumfukuza mtu uanachama itachukuliwa endapo halmashauri itaridhika kwamba tabia na mwenendo wake vinamwondolea sifa za uanachama.

Hatua ya kuwafukuza uanachama madiwani hao ambao pia watakuwa wamepoteza nafasi zao za udiwani, imekuja siku chache tangu Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipozitaka pande zinazohusika katika mgogoro huo kumaliza kwa njia ya mazungumzo.

"Madiwani wote wa CCM walioendelea na mgomo hata baada ya maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwa kusaini barua ya kutaka Mkurugenzi aitishe kikao cha kumwondoa Meya tumefikia uamuzi mgumu wa kuwafukuza uanachama kwa masilahi ya chama na wananchi wa Bukoba,'' alisema Mushi.

Mushi aliwataja madiwani wengine waliofukuzwa ni Robert Katunzi (Hamugembe), Deus Mutakyahwa (Nyanga), Richard Gasper (Miembeni), Mulungi Kichwabuta (Viti Maalumu) na Dauda Kalumuna aliyekuwa Diwani wa Ijuganyondo.

Katibu huyo alisema Balozi Kagasheki na Meya Amani ambao mamlaka yao ya uteuzi ni ya kitaifa na wanatakiwa kumaliza tofauti zao kama walivyoelekezwa na Rais.

Mgogoro uliosababisha madiwani hao kutimuliwa uliibuka baada ya Kagasheki kumtuhumu Meya Amani kwamba ameingiza Manispaa katika miradi ya ufisadi hali ilioibua makundi na kukwamisha kufanyika hata vikao vya Baraza la Madiwani.

CHANZO: CCM yatimua madiwani wanane Bukoba Mjini - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Inaonekana huwajui wahaya wewe!ni wanafiki balaa.Wataendelea na CCM yao tu.We hujui ndio wamejaa serikalini na wameifaidi sana serikali tangu uhuru wa nchi hii.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
hao madiwani wanne wa CHADEMA na CUF walichaguliwa na wahutu?
 
vipi tena, ule umoja na mshikamano ndani ya chama umeanza kumongonyoka?
 
It is very very interesting kwamba kwa CCM wanaopinga ufisadi ndio hufukuzwa katika chama lakini yale mafisadi, majambazi, majangili, na mauza unga yaliyokubuhu ndio kwanza yanaachwa na hata kupewa nafasi za juu za uongozi katika chama, serikalini, na bungeni.

Hili linashangaza sana! Hivi CCM wanaweza kuwaeleza wananchi sababu ya msingi na inayoingia akili ya kuwafukuza hao madiwani zaidi ya bla bla za kisiasa za akina Nape?

Well said Mkuu dudus, hakika hii ni vita dhidi ya ufisadi. Nijuavyo mimi, huyu Meya wa Manispaa ni mtu wa ndani ya kambi ya PM aliyejiuzulu na sitashangaa vikao vya juu vya ccm wakabariki maamuzi haya.

Siasa za Bukoba zimejaa unafiki nakumbuka mwaka 2000, kwa unafiki huu wa Meya Anatoli Amani, ccm walikorogana na Lwakatare akashinda kiulaini. Naona hali inavyoendelea hakuna suluhu na hili jimbo liko wazi kwa wapiganaji ifikapo 2015 tunamkabidhi Lwakatare hata kama bado amelala hospitali huko India.
 
Last edited by a moderator:
CCM yatimua madiwani wanane Bukoba Mjini

Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kagera kimewafukuza uanachama wa chama hicho, madiwani wake wanane kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kukaidi maelekezo mbalimbali ya chama hicho, pia kushirikiana na upinzani kukihujumu.

Madiwani waliotimuliwa ni wale Manispaa ya Bukoba ambao wamekuwa wakitajwa kumuunga mkono Mbunge wa Bukoba Mjini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki ambaye amekuwa akivutana vikali na Meya wa Manispaa hiyo, Anatory Amani.

Miongoni mwa waliotimuliwa ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba na Diwani wa Kashai, Yusuph Ngaiza, aliyepata kuwa mbunge wa muda mrefu wa Bukoba Mjini na baadaye Meya wa Manispaa hiyo, Samuel Ruhangisa ambaye ni Diwani wa Kitendagulo na Diwani wa Buhembe, Alexander Ngalinda ambaye pia alikuwa Naibu Meya.

Katibu wa CCM wa Mkoa wa Kagera, Averin Mushi alisema uamuzi wa kuwatimua madiwani hao umefikiwa jana na halmashauri ya CCM ya Mkoa kwa kile alichosema ni kwa ajili ya "kulinda masilahi ya chama na wananchi wa Bukoba".

Ibara ya 93 (15) ya Katiba ya CCM inataja moja ya kazi za halmashauri ya chama hicho ngazi ya mkoa kuwa ni: "Kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Halmashauri ya CCM ya Mkoa".

Hata hivyo kipengele cha 14 cha ibara hiyo ya 93 kinasema hatua kumwachisha au kumfukuza mtu uanachama itachukuliwa endapo halmashauri itaridhika kwamba tabia na mwenendo wake vinamwondolea sifa za uanachama.

Hatua ya kuwafukuza uanachama madiwani hao ambao pia watakuwa wamepoteza nafasi zao za udiwani, imekuja siku chache tangu Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipozitaka pande zinazohusika katika mgogoro huo kumaliza kwa njia ya mazungumzo.

"Madiwani wote wa CCM walioendelea na mgomo hata baada ya maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwa kusaini barua ya kutaka Mkurugenzi aitishe kikao cha kumwondoa Meya tumefikia uamuzi mgumu wa kuwafukuza uanachama kwa masilahi ya chama na wananchi wa Bukoba,'' alisema Mushi.

Mushi aliwataja madiwani wengine waliofukuzwa ni Robert Katunzi (Hamugembe), Deus Mutakyahwa (Nyanga), Richard Gasper (Miembeni), Mulungi Kichwabuta (Viti Maalumu) na Dauda Kalumuna aliyekuwa Diwani wa Ijuganyondo.

Katibu huyo alisema Balozi Kagasheki na Meya Amani ambao mamlaka yao ya uteuzi ni ya kitaifa na wanatakiwa kumaliza tofauti zao kama walivyoelekezwa na Rais.

Mgogoro uliosababisha madiwani hao kutimuliwa uliibuka baada ya Kagasheki kumtuhumu Meya Amani kwamba ameingiza Manispaa katika miradi ya ufisadi hali ilioibua makundi na kukwamisha kufanyika hata vikao vya Baraza la Madiwani.

CHANZO: CCM yatimua madiwani wanane Bukoba Mjini - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Hivi Kikwete alipowaambia wamalize tofauti zao kwa mazungumzo aliwaambia kama Rais au kama Mwenyekiti wa Chama?
Naona kuna mkanganyiko mahali
 
wakati ni ukuta kweli. Muda wa mabadiliko ya kweli huu umefika sasa hii ni msg nyingine kwa watawala maamuzi haya ni magumu ila je yanatija kwa maendeleo au ni kutaka kuficha mafisadi
 
Hivi Kikwete alipowaambia wamalize tofauti zao kwa mazungumzo aliwaambia kama Rais au kama Mwenyekiti wa Chama?
Naona kuna mkanganyiko mahali

aliwaambia kama mwenyekiti ili kulinda maslai ya chama si unaona ndugu yangu kinachoendele
 
Hii habari nimeisikia BBC jioni ya leo.CCM wamewaiga CDM.Mtoa taarifa anasema kama CDM wameweza Arusha,hata wao watatetea kata zao hizo kama uchaguzi mdogo utaitishwa. Chaguzi ndogo tena:Mwanza(meya wa kichina),Arusha na Kagera kwa uchache.Katiba mpya itupatie majibu...diwani akifukuzwa kwenye chama,aendelee na nafasi yake.

Aendelee je wakati chama ndo kimemdhamini?
 
Inaonekana huwajui wahaya wewe!ni wanafiki balaa.Wataendelea na CCM yao tu.We hujui ndio wamejaa serikalini na wameifaidi sana serikali tangu uhuru wa nchi hii.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Waliofukuzwa wao hawakuwahi kufaidi... na waliowachagua hao waliofukuzwa nao hawakuwahi kufaidi....
 
Mbona magamba makubwa yaliwashinda Kuyavua sasa mnakimbilia kufukuza dagaa,mapapa na sangara je? Kweli ccm hamna jipya ila ni kujichora tu.

Wanatafuta cha kuongea uchaguzi ujao
 
Wale hawakuwa na chochote cha maana zaidi ya kutumiwa na upinzani kuivuruga ccm wao ndiyo wachafu na mafisadi wakubwa leo wanasema walikuwa wanazuia wizi,wizi gani huo kama siyo wehu tu wanasiasa wa namna hii hawana msaada kwa watu.

unakazi kubwa sana ya kutetea kinyesi ccm.
 
aliwaambia kama mwenyekiti ili kulinda maslai ya chama si unaona ndugu yangu kinachoendele

Kwa hiyo ni sawa kutumia resources za Taifa kwa shughuli za kichama?
Hapa ndipo kunapotokea a thin line between CCM na ufisadi.
 
Back
Top Bottom