CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

Halafu wanafukuza vidagaa wanaacha Lisangala Kagasheki ndo Kiongozi wao wasipomfukuza huyo watakuwa wanacheza makida
 
Wakati nikiwa mwangalizi wa Uchaguzi jimboni mwaka 2010, kata za Kashai, Ijuganyondo, Hamugembe, na Buhembe CCM walipita kwa mbinde!
Lakini kumfumuza Ruhangisa ni kujiua zaidi mkoani Kagera maana yeye ni mzee wa kuchaguliwa bila kuwepo!

Ina maana utumwa wa fikra bado upo huko, haiwezekani mumchague mtu wakati hayupo hata kama ni Ruhangisa
 
Kupitia ITV Nimesikia taarifa ya kisaliti juu ya CCM kuwafukuza madiwani wake.Nimepitia kwa kina taarifa zinazohusiana na msimamo wa madiwani hawa na kile wanachokipigania.

Nawapongeza madiwani hao 8 wa Kagera kwa msimamo thabiti walioonyesha kukabiliana na ufisadi ndani ya chama chao,halmashauri na mkoa wa Kagera kama wawakilishi wa wananchi wanaouchukia ufisadi.Kwa kuwa wamegutuka na kugundua ufisadi ni nguzo kuu ya kiitikadi ndani ya chama chao na kwa kuwa dhamira iliwasuta na kuamua kusimama ili kuirudisha CCM katika misingi iliyoasisiwa na Mwl.Nyerere,sina budi kuwapongeza kwa hatua hii ya kijasiri.Naomba kila mmoja anayechukia ufisadi aungane na madiwani hawa walioamua kupambana ndani ya chama chao kwa kutumia platform sahihi bila kuvunja katiba.

Chama ambacho kinaona kwamba ni kosa la jinai kupinga ufisadi hakifai kuongoza serikali na wawakilishi wa wananchi wanatakiwa kuwa mfano bora kama walivyofanya madiwani hawa

1. Richard Gaspar (Miembeni )

2. Murungi Kichwabuta (viti maalum)

3. Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)

4. Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)

5. Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)

6. Robert Katunzi (Hamugembe)

7. Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na

8. Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).

Hatuwezi kuwa na taifa adilifu ikiwa hatutashinikiza uadilifu katika ngazi za halmashauri na ngazi nyingine.CHADEMA kiliwafukuza Madiwani wa Arusha kutokana na kukiuka misingi ya haki,matakwa ya wananchi na kwenda kinyume na msimamo wa Chama katika kuipigania haki ya wananchi.CCM wao wamefanya kinyume,wameamua kukaa upande wa kusaliti wananchi na kuwafukuza watetezi wa wananchi
 
Ndugu wanaCCM na wakereketwa wa chama chetu(dola) twawala,kama ilivyo ada katika mkakati wetu wa kuhakikisha kuwa tunaidhibiti CDM kwa kujibu mapigo.Kwaiyo ni furaha yangu mimi kama katibu wa chama tawala kuwatangazia rasmi kwamba siku ya leo tarehe 13/08/2013 chama chetu ngazi ya wilaya tumeamua kuwajibu CDM kwa kuwafukuza madiwani wetu wote nane wa wilaya ya Bukoba kama CDM walivyofanya jijini Arusha mwaka juzi.Ndugu wana CCM uamuzi huu umechukuliwa baada ya kutafakari kwa kina maslahi ya viongozi wetu wa ngazi za juu katika chama ambao wangeathirika kutokana na kusitishwa kwa mikataba hasa ule wa ujenzi wa soko kwani ulikuwa na maslahi manono,ivyo basi huu ni muendelezo wa kushughulikia wale wanachama wetu wote wenye viherehere kama tulivyomshughulikia Rais Jumbe alipochafua hali ya hewa visiwani mwaka 1984.Ndugu wanaCCM na wakereketwa ieleweke kwamba tunapofanya uamuzi huu mgumu hatumkomoi mtu bali tunatetea maslahi ya chama zaidi,rejea mijadala Bungeni ambapo mpaka sasa chama kimeweza kuliteka Bunge,sembuse madiwani??.Mwisho kabisa naomba wana-Bukoba watuelewe kwamba hakuna mtu aliye juu ya maslahi ya chama chetu twawala tukufu.KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZI,ZUDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI.Asanteni kwa kunisikiliza.
Ni mimi wenu mtiifu kwa maslahi ya chama na si taifa.
 
Waliofukuzwa ni wanafiki tu.Kwani kama pesa zinatoka manispaa kwa msaada wa meya kwenda kugharamia shughuli za chama ambacho hao madiwani ni sehemu yake,wanawezaje leo kujidai wanapinga eti ufisadi?Je hakuna collective responsibility?Je meya huwa ana saini voucher na cheque?Ni mtendaji gani aliwahi kuwajibishwa kwa ufisadi huo?Yapo maswali mengi ya kujiuliza na mwisho wa siku unaona ni unafiki tu hawana lolote!wangechukia ufisadi wasingekuwa CCM huo ndio ukweli

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Bw Avelin Mushi amemaliza Press Conf hivi punde na kufafanua kuwa kikao cha Halmasahuri Kuu ya mkoa wa Kagera imemaliza kikao chake hivi punde na kuamua madiwani 8 wa Manispaa ya Bukoba kufukuzwa katika chama na kufutiwa nyadhifa za udiwani kutoka na mgogoro uliokuwa ukiendelea.

NIMEONA ITV - LAKINI "SIAMINI"... INGAWA NAJUA MA-ccm NI WAONGO. NAPE NA WENZAKE WALISEMA NA KUAPA KUWA WAO HAWAFUKUZI MTU!.. BILA SHAKA VIKAO VYAO VILITAWALIWA NA CHADEMA.
 
wanafukuzwa kwa kukataa kwao ufisadi na rushwa ya million 20 kwa kila mmoja?
ama kweli CCM ni chama cha mafisadi,anaepingana na ufisaidi sio mmoja wao.
nawapongeza madiwani hao kwa ujasiri wao wa kukataa unafiki na uchama
wakaweka maslahi ya nchi mbele na sio ya chama.
uchaguzi lini nashauri hawa hawa waingie chadema kura zote zitawarudia.
shame on you CCM na kizazi chenu
hiyo rushwa ya million 20 nani awape!?,acha story bhana hakuna hata diwani mmoja hapo wa kukataa million 20, laki laki tu za Kagasheki zimewafanya wamsaliti mayor wao ije kua 20m!!! we unaijua bukoba au unaiskia!
 
Kawaponza Kagasheki hawa. Jamaa alikuwa anawatumia na kuwalipa kwa manufaa yake mwenyewe na wao wakingia mkenge. Haya ndio malipo kwao. Mwenzao ka save. Lakini nashangaa kile kikao kwa nini hakikumchukulia hatua na yeye huku wakijua dhahili kwamba yeye ndiye muasisi na mpigaji wa debe wa jambo hili?
Alafu kafukuzwa mwenyekiti wa wilaya uanachama kisha mnasema mnaviachia vyombo vya juu kuamua? Kuamua nini wakati yeye si mwanachama? Hivi anaweza kuitisha vikao vya wilaya kama kiongozi wa chama?
Too much contradictions?
Fukuza na Kagasheki bila hivyo shida itaendelea kuwepo manispaa ya Bukoba.
Shida itaendelea kwa ccm tu,wana bukoba wameipokea kauli hii kwa shangwe kuu,siyo kufukuzwa kwa madiwani,bali ni kufukuzwa ccm kagera.
 
Ndugu wanaCCM na wakereketwa wa chama chetu(dola) twawala,kama ilivyo ada katika mkakati wetu wa kuhakikisha kuwa tunaidhibiti CDM kwa kujibu mapigo.Kwaiyo ni furaha yangu mimi kama katibu wa chama tawala kuwatangazia rasmi kwamba siku ya leo tarehe 13/08/2013 chama chetu ngazi ya wilaya tumeamua kuwajibu CDM kwa kuwafukuza madiwani wetu wote nane wa wilaya ya Bukoba kama CDM walivyofanya jijini Arusha mwaka juzi.Ndugu wana CCM uamuzi huu umechukuliwa baada ya kutafakari kwa kina maslahi ya viongozi wetu wa ngazi za juu katika chama ambao wangeathirika kutokana na kusitishwa kwa mikataba hasa ule wa ujenzi wa soko kwani ulikuwa na maslahi manono,ivyo basi huu ni muendelezo wa kushughulikia wale wanachama wetu wote wenye viherehere kama tulivyomshughulikia Rais Jumbe alipochafua hali ya hewa visiwani mwaka 1984.Ndugu wanaCCM na wakereketwa ieleweke kwamba tunapofanya uamuzi huu mgumu hatumkomoi mtu bali tunatetea maslahi ya chama zaidi,rejea mijadala Bungeni ambapo mpaka sasa chama kimeweza kuliteka Bunge,sembuse madiwani??.Mwisho kabisa naomba wana-Bukoba watuelewe kwamba hakuna mtu aliye juu ya maslahi ya chama chetu twawala tukufu.KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZI,ZUDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI.Asanteni kwa kunisikiliza.
Ni mimi wenu mtiifu kwa maslahi ya chama na si taifa.

tehe tehe tehe mkuu umeniua kwa kicheko hapa daaa nimeipenda sana.
 
SANY0104.JPG

UFIPA PROJECT MANYANYA TEAM.

CC; HAMY-D, scramble, Lizaboni, chama,
 
Back
Top Bottom