CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

CCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8

Leo akili umeziweka kichwani make siku nyingine unaziwekaga miguuni, hongera sana assad
 
Kuna habari kwamba Ccm Lumumba wamesitisha uamuzi wa mkoa na sasa wanajiandaa kutoa tamko,
Machale yamewacheza, na pia siyo kawaida kwa Ccm kuwajibishana

Hao Madiwani wakirudishwa na CCM Taifa, nao wangeamua kujiuzulu ili kulinda heshima yao iliyo haribiwa mbele ya jamii.
 
Mkuu maamuzi gani?
Maamuzi yametolewa na ngazi ya Mkoa, wahusika wanafasi ya kukata rufaa ngazi za juu na Chama kikiona kuna namna nyingine ya kutatatua tatizo zaidi ya kuwafukuza kinaweza kubatilisha maamuzi....thats demekrasi

Mimi naongelea maamuzi iliyoyatoa,wasirudi nyuma hata kwa level ya mkoa!

Kinachonitia wasiwasi kwa udhaifu iliyonao sasa CCM haina ubavu wa kurinda hizo kata uchaguzi ukifanyika!
 
Chama cha mapinduzi kimewafukuza madiwani wake bukoba. Hili ni pigo kwani ninaamini hili litawagharimu utakapo itishwa uchaguzi mdogo lazima chadema watachukua baadhi ya kata na hivyo hasira ya mkizi nafuu ya mvuvi, kimsingi madiwani walikua wanasimamia haki je kuungana na chadema na cuf kudai haki ndio wamefanya kosa bila shaka yoyote chadema watachukua madiwani wengi uchaguzi mdogo utakapoandaliwa labda kipofu ndo hawezi kuliona hili. Mtu anatetea haki unamfukuza unataka atetee ufisadi hapa ccm mmechemka sana mtakuja kukumbuka maamuzi mabovu kama haya

Ninachoamini ni kwamba ccm mkoa wameamua kumtishia nyau mtu mzima. Siatarajii hata mara moja kama uongozi wa ccm lumumba wanaweza kubariki maamuzi ya kuwafukuza madiwani hao hata siku moja. Hakuna kitu wanchokiogopa ccm kama chaguzi ndogo kwakuwa wanatambua gharama kubwa na nguvu kubwa wanayotumia kukabiliana na Chadema.

Na kwa manispaa ya Bukuoba sina shaka kabisa kuwa tukienda kwenye uchaguzi mdogo lazima Chadema tutawaburuza ccm vibaya sana na kwa kulitambua hilo sitarajii hata mara moja mwenyekiti Kikwete akubali kuipoteza halmashauri ya manispaa ya Bukoba kirahisi kiasi hicho. Ninachosubiri kusikia ni tamko la lumumba la kusitisha uamuzi huo na kutafuta usuluhishi baina ya madiwani na meya wao kwakuwa huo ndio msimamo wa mwenyekiti wao wa Taifa.
 
Mimi naongelea maamuzi iliyoyatoa,wasirudi nyuma hata kwa level ya mkoa!

Kinachonitia wasiwasi kwa udhaifu iliyonao sasa CCM haina ubavu wa kurinda hizo kata uchaguzi ukifanyika!

Mkuu Lumumba kamwe hawawezi kukubali hili, wanajua muziki wa kutetea viti nane si wakitoto
Iko wazi uamuzi utabatilishwa na watarudishwa, CCM hawezi kukubali kwenda kwenye uchaguzi labda madiwani wenyewe waseme sasa cc basi
 
Makosa makubwa sana kwenye huu mgogoro yalifanywa na Mangula na Jk na walifanya hivyo ama kwa kutokujua ama walipewa taarifa zisizo sahihi

Sehemu yenye mgogoro haimalizwi na kauli za kutoa amri bali kuangalia chanzo na kukimaliza
Manguli aliamuru asiyetaka arudishe kadi mbele yake
Jk naye akaamuru madiwani wamalize mgomo mara moja
 
Mkuu Lumumba kamwe hawawezi kukubali hili, wanajua muziki wa kutetea viti nane si wakitoto
Iko wazi uamuzi utabatilishwa na watarudishwa, CCM hawezi kukubali kwenda kwenye uchaguzi labda madiwani wenyewe waseme sasa cc basi
Mimi nina hamu kubwa yakuona mchuano mkali kati ya CHADEMA na CCM katika kuzigombea kata hizo,maana vyama hivi sasa vimekuwa kama Simba na Yanga!Kama mungu akijalia mchuano huu ukatokea basi itakuwa burudani kubwa sana!
 
Yametimia, na yataendelea kutimia. Time will tel Us

  • A%20S%20kiss.gif






 
It is very very interesting kwamba kwa CCM wanaopinga ufisadi ndio hufukuzwa katika chama lakini yale mafisadi, majambazi, majangili, na mauza unga yaliyokubuhu ndio kwanza yanaachwa na hata kupewa nafasi za juu za uongozi katika chama, serikalini, na bungeni.

Hili linashangaza sana! Hivi CCM wanaweza kuwaeleza wananchi sababu ya msingi na inayoingia akili ya kuwafukuza hao madiwani zaidi ya bla bla za kisiasa za akina Nape?
Ni kweli kabisa nakuunga mkono kwa hilo,Chama Cha Maunga(CCM) kiko kwa ajili ya wanafiki,wanaojipendekeza,wazinzi na mafreemason,wale wote wenye kuonyesha msimamo wa kupinga hilo kwa maslahi ya wananchi hufukuzwa mara moja bali wale wenye kukandamiza wananchi ndio wanaopendwa na mafisadi ya chama,kumbuka Nyerere alishasema mwaka 95 wakati alipomkataa huyu mheshimiwa na kumpendekeza Mkapa kuwa amefanya hivyo kwa vile hayuko tayari kuona nchi ikitawaliwa na mbwa,watu hawakuelewa wakati ule kwani walijua anamaanisha vyama vya upinzani hasa Mrema wakati ule,sasa tunayaona aliyoyabashiri kutokea.hakika KIJANA YOYOTE MWENYE KUSHABIKIA MAGAMBA KWA SASA LAZIMA ATAKUWA MCHAWI UZEENI MWAKE,magamba hayakubaliki kuanzia sasa
 
Ndugu wanaJF;

Kutokana na uamuzi wa CCM kuwatimua Madiwani wake 8 Bukoba, je kutaijenga au kutaibomoa CCM na je, kuna uwezekano wa kurejesha kata zote au itakuwa ndio nafasi kubwa kwa upinzani kujitwalia kata hizo?
 
It is very very interesting kwamba kwa CCM wanaopinga ufisadi ndio hufukuzwa katika chama lakini yale mafisadi, majambazi, majangili, na mauza unga yaliyokubuhu ndio kwanza yanaachwa na hata kupewa nafasi za juu za uongozi katika chama, serikalini, na bungeni.

Hili linashangaza sana! Hivi CCM wanaweza kuwaeleza wananchi sababu ya msingi na inayoingia akili ya kuwafukuza hao madiwani zaidi ya bla bla za kisiasa za akina Nape?

HELLO DUDUS,

Hii inaingia akilini kabisa, la msingi kabisa ni bora uingie kiundani ujue nini hasa chanzo cha mgogoro. Masuala ya ujenzi wa soko na Standi ya mabasi yalipitishwa na Baraza la madiwani manispaa ya Bukoba, ambaye hakuwepo ni Mbunge Kagasheki tu jambo ambalo halizuii maamuzi kutekelezeka. Baada ya kuona mipango ikitekelezeka Meya atakuwa amenfunika(KAGASHEKI) akaanza kuzua zengwe huku akipata support ya vijana wa Seneti na wafanya biashara wa sokoni. Cha ajabu madiwani hao hao ambao ndiyo walipitisha wanakuwa kigeugeu kwa sababu ya vijisenti vya Kagasheki na kuanza kupinga maamuzi yao wenyewe. Hivi kama ni wewe utawaonaje watu kama hao? Mwenyekiti wa chama chao CCM ambaye ni rais alihacha ametoa maelekezo mazuri sana juu ya namna ya kuleta maelewano, lakini wao wakawa wakaidi. Hivi sasa soko lingekuwa katika hatua za kuelekea mwisho sasa hakuna kitu. Hivi utapenda kukaa na watu wanao pinga maendeleo badala ya kupambana ili tuone" Big results now".
Kwa taarifa Mhe. amani alishawauliza walete vielelezo vinavyoonyesha kuwa yeye ni fisadi, hawakufanikiwa.

Kilichofanyika ni sahihi kabisa na inaingia akilini kama utaihachia akili yako ifunguke na kufanya tafakuri yenye kuongozwa na hekima.
 
Mi nadhani itakuwa fursa kubwa kwa Upinzani kuchukua kata hizo maana moja kati ya sababu za kutimuliwa madiwani hao ni kupinga ufisadi kitu ambacho si utamaduni wa CCM.
 
Unaimanisha nini, kwani wewe ni chizi kiasi kwamba hujui kuwa meya wa Ilemela ni kibaraka wa magamba..
Mkuu mimi sio Chizi ila nilitaka kujua kama na hawa waliofukuzwa huko BK watatambuliwa kama huyu Meya wa Ilemela.
 
[h=4]Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera, leo kimewafukuza madiwani 8 wa Manispaa ya Bukoba kupitia chama hicho na kufutwa nyadhifa zao za udiwani kutokana na mgogoro uliokuwa ukiendelea[/h]
Waliofukuzwa ni:


  1. Richard Gaspar (Miembeni )
  2. Murungi Kichwabuta (Viti maalum)
  3. Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)
  4. Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)
  5. Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)
  6. Robert Katunzi (Hamugembe)
  7. Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na
  8. Dauda Kalumuna (Ijuganyondo)​
 
Back
Top Bottom