Elly B
JF-Expert Member
- Jan 11, 2011
- 1,194
- 906
Pamoja na kwamba Mwanzilishi wa thread hii ameforge na Kuchakachua ni dhahili kwamba Watanzania wamekomaa Kisiasa. Swala hapa Si CHADEMA wala CUF Kuwachukuwa Madiwani waliofukuzwa CCM , issue hapa ni kwamba Watu wamechoka , na hata ndani ya CCM kwa sasa wameamua kusema "Liwalo na Liwe" Maana "hamna Namna nyingine ya Kupambana na dhuruma ya CCM". Madiwani hao Wameonyesha Ujasiri Mkubwa na inabidi iwe mfano wa kuingwa kwa almashauri zingine zenye matendo ya Kifisadi. Kwa MaCCM ukizigatia upepo wa Kisiasa nchini naweza sema kwao hii ni Political Miscalculation kwani kwa kuiga CHADEMA's political strategy ya walivyowa fukuza Madiwani wao jijini Arusha, Itawagharimu Asilani. Swali ni Je CCM wakiingia Kwenye Uchaguzi leo hii Watavirudisha Viti hivyo???? na Je Madiwani waliotimuliwa wana support ya wapiga kura kwa kile walichokisimamia hadi wanafukuzwa Chamani???, Mwisho kabisa Uchaguzi Ukifanyika leo na ikatokea CCM Imeshindwa Kuvirudisha Viti hivyo vya Madiwani waliowatimua basi Watanzania Watakuwa Wamepata Somo zuri nalo ni "Ukiwapinga waziwazi na ukapambana na Mafisadi & Ufisadi ndani ya CCM ni dhambi Kubwa kama ugojwa wa Ukoma, baba wa taifa.
Ni kweli kwa sasa ni wananchi tu ndiyo wameshikilia power ya kutokomeza tabia za kifisadi kwa kuamua haki ndani ya masanduku ya kura.
Kuhusu hii ya CCM kufukuza madiwani, naona ni kosa baya sana. Na usishangae wakaamua kutoitisha uchaguzi tena. Vinginevyo kupoteza kuko wazi. Hata hivyo hiki wanachofanya mi hakijanistua. Kwa kawaida hata mchawi akiroga sana hufikia wakati akasahau mchana na usiku na akatoka kuwanga mchana kweupe. Ndilo lililowakuta CCM