kiwatengu
Platinum Member
- Apr 6, 2012
- 19,303
- 17,830
Habari!
Binafsi hili vuguvugu la kuiponda ccm na kuiona haifai linaniumiza sana,
Nimezoea kula bure (kula kwa kupitia deals).
Nasafiri bure (nadhani hapa ni kwa kodi za walala hoi).
Chochote nitakacho napata kwa sababu CCM ipo madarakani, rafiki zangu kibao wamepata ajira kubwa kubwa regardles ujuzi wao mdogo na elimu yakuunga unga walionayo,(wawili wapo bandari, wanne wapo maliasili) just because ccm ndiyo wameshikilia dola.
Nina magari zaidi ya mawili, i got them kwa sababu tu ccm iko madarakani.
Ninavyosikia juu ya kufa kwa CCM naweweseka sana jamani.
Ila ninaamini CCM wakishindwa 2015.
Tupo wengi sana tutakao kuwa maskini, si mimi peke yangu.
Machale yananicheza sana.
Akina riz washajiwekewa njia m'badala yakujinasua endapo chama hakitaingia madarakani 2015.
Tunapambana kwa kila njia kwa maslai yetu, umaskini si mzuri jamani!
Maisha yakupanda bodaboda na kugombania daladala ni magumu jamani.
Nitafurahi ccm isipokufa niendelee kuishi kwa ubwerere.
Hata wenzangu nao watafurahi..
Copy...
Sumu, Ritz, chama, hawa ni wanachama pia
Last edited by a moderator: