Uchaguzi 2020 Kwanini tuichague CCM na Magufuli kwa miaka mitano tena?

The Giantist

JF-Expert Member
Dec 12, 2018
214
86
Na: Giantist McWenceslaus
Dodoma


Ndugu wanabodi habari zenu.

Jioni ya Leo nimeona niwaletee kwenu uzi wenye faida kwenu kwa sasa na kwa vizazi vyenu vya baadaye. Napenda nitangulize utambulisho wangu mdogo kwenu. Jina langu nimeshaliandika hapo juu, mimi ni mwanachama kijana wa chama pendwa cha watanzania walio wengi wengi sana kwa idadi, chama changu ni CCM. Kabla sijaenda mbele zaidi, napenda niwakumbushe kuwa namba zangu sijaziandika kwa sababu tayari zimeshafika mahala husika. Sasa akija mtu hapa kuniambia eti weka namba zako za simu, nitamshangaa na kwa hakika ningeomba wanabodi wote msimwache bila kumpa neno lo lote mtu huyo. Ahsanteni.

Tangu uhuru hata sasa, Tanzania imeendelea kuwa salama, kwa sababu ya kuwepo kwa viongozi wazalendo na wenye kuwajali watanzania wenzao wote. Na usalama huo wa Tanzania, imesababishwa kwa kuwepo kwa haki na uhuru kwa watu wote waliopo ndani ya mipaka ya Tanzania. Na ndio maana kwa sababu hiyo, ukitembea maeneo mengi Tanzania, utapata kuwaona wageni wazungu kwa wachina kwa waarabu na watu wengine wengi, wakitembea kwa uhuru bila hofu na wakati mwingine wakiwa kwa miguu katika matembezi yao ya kawaida.

Na wengine wameamua kabisa kustakimu ndani ya Tanzania, ni kwa sababu wanaona amani na utulivu uliopo nchini, na hiyo haikuja kwa sababu tulistahili ila ni kwa sababu viongozi wetu wote wa serikali chini ya CCM wamekuwa wakitoa haki na uhuru kwa watu wake. CCM na wanaCCM wote wanafahamu kuwa uhuru na haki ni mbegu ya amani na utulivu kwa nchi.

Leo tunaona Tanzania imekuwa ni nchi ya Mfano wa kuigwa Barani Afrika na Duniani kwa Ujumla. Ni kwa sababu ya kuwepo kwa viongozi imara na misingi imara iliyowekwa na chama cha wananchi cha Mapinduzi CCM. Heshima hiyo kwa taifa ilikuwa hata kabla ya kuanzishwa kwa vyama vya ruzuku miaka ya 1992. Tanzania ni ya Watanzania, na watanzania ni wapenzi wa kweli kwa chama Chao CCM.

Rais Dkt. John P. Magufuli aliyelelewa katika imani ya CCM na viongozi wote wa serikali wa nchi ambao bila shaka ni wenye mapenzi mema na taifa lao na wananchi wenzao. Kwa miaka mitano tangu 2015-2020, Rais huyu wa nchi aliyetokana na CCM ameiongoza nchi katika misingi ile ile ya CCM ya kuheshimu watu, Uzalendo na kuchukia ubadhirifu na rushwa na kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zitawafaidisha watanzania wote na wala sio watanzania wachache.

Dkt. John P. Magufuli kwa miaka mitano amefanya mambo mengi katika sekta zote ikiwemo sekta ya Elimu, Afya, Maji, Umeme, Viwanda, kilimo, Mifugo na Uvuvi, Miondombinu, Usafiri, Ulinzi na usalama n.k. Na ukweli huo kwa sisi waungwana, tunafahamu kuwa watanzania wote wanaujua. Wameona katika Elimu, wameona katika Afya, wameona katika usafirishaji, wameona katika nishati, wameona katika ulinzi na usalama wa rasilimali za nchi, wameona katika utoaji na upatikanaji wa haki zao n.k ukweli huo, upo ndani ya watanzania na wataenda wenyewe kuuthibitisha kwa kumchagua tena DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI kuwa Rais wao wa nchi kwa miaka mitano mengine, kupitia sanduku la kura siku ya 28/10/2020.

Mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka mitano kuanzia mwaka 2015 mpaka sasa 2020 chini ya Rais Dkt. JPM ni mengi mno. Ila kwa uchache sana nitazungumzia mafanikio katika sekta ya ELIMU. Ni sekta ya Elimu kwa sababu ni miongoni mwa sekta ambazo zinagusa maisha ya watu moja kwa moja; ama awe wa kabila fulani au wa hali fulani au wa dini fulani, wote hao watahitaji elimu. Sekta ya maji ni muhimu lakini sitaisemea Leo kwa sababu, katika ilani ya uchaguzi ya mwaka huu inaenda kuondoa kabisa ajenda ya shida ya maji katika vijiji na vitongoji. Nikiwa nayaandika haya, kwa sasa upatikanaji wa maji mjini ni kwa 84% na upatikanaji wa maji Vijijini ni kwa 75%. Kwa hiyo unaweza kuona kwamba kwa miaka mitano ijayo hali ya upatikanaji wa maji nchini itakuwa katika hatua gani. Vivyo hivyo katika sekta ya Afya.

SEKTA YA ELIMU
Bunduki ni silaha ya ulinzi, hiyo ni kweli. Lakini Elimu ni silaha muhimu katika kuleta maendeleo ya mtu, jamii na taifa kwa jumla. Watu walioelimika ndio wanaoweza kutofautisha kati ya ujinga, upumbavu na uongo dhidi ya ukweli: watu walioelimika ndio wanaoweza kutofautisha baina ya vijarida vya uchaguzi na Ilani ya uchaguzi. Vita iliyotangazwa na serikali ya Tanzania baada ya uhuru ni vita dhidi ya Ujinga, umasikini na maradhi. Kwa miongo sita sasa Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana katika kufaulu vema vita hivyo. Katika kumkabili adui mjinga, serikali ya CCM imeendelea kuboresha huduma za elimu kwa kuweka mitaala ambayo inajibu shida za wananchi kisayansi, kwa kujenga miundombinu mizuri mashuleni, kwa kuweka mpango wa elimu bure bila malipo n.k.

Baada ya kusema hayo, yafuatayo ni baadhi ya mambo machache ambayo Rais Magufuli amefanikiwa kuyatekeleza kwa miaka mitano kwa mujibu wa ilani ya CCM. Nitayeleza kinaganaga

Mosi, Rais Dkt. John P. Magufuli alifuta Ada na michango yote kwa wanafunzi kuanzia Shule ya Msingi hadi Sekondari. Awali wanafunzi walilazimika kulipia ada ya SHULE kila mwezi shilingi 20,000/=. Pesa ya Taaluma ilikuwa kiasi cha shilingi 20,000/= hadi Shilingi 40,000/= ilitegemeana na Shule kwa kila mwezi.

Pesa ya Madawati kiasi cha Shilingi 15,000/= Pesa ya Ulinzi kiasi cha shilingi 5,000/= Pesa ya Maji na Umeme shilingi 5,000/= Pesa ya mitihani ya Moko na Taifa ambapo kwa kidato cha NNE alitakiwa alipie shilingi 50,000/= kwa ajili ya mtihani huu wa Taifa. Na alikuwa asipolipia basi matokeo yake yalikuwa yanafungiwa na wengine walikosa kufanya mitihani kwa vile hawajalipia Pesa ya mitihani ya Taifa.

Kwa kusema ukweli, utaratibu huo ulikuwa ukiumiza sana baadhi ya familia za kitanzania. Ni watanzania wengi sana ambao walikuwa na wakati mgumu katika kutafuta pesa hizo ili watoto wao waweze kupata elimu. Na hivyo kupelekea watoto wengi kuamua kuacha Shule ili waweze kukwepa kila siku kurudishwa nyumbani kwa kukosa kulipia mchango wowote hapo shuleni. Na kwa hakika wapo baadhi ya wazazi walithubutu hata kuzikimbia familia zao!

Lakini Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipoingia madarakani aliamua kuondoa malipo hayo yote na mzigo wote kubaki kuwa chini ya serikali. Tangu wakati huo hata sasa mwanafunzi halipi karo, halipi pesa ya Taaluma, pesa ya ulinzi,pesa ya madawati, pesa ya Ujenzi,pesa ya meme na maji. Na kwa sababu hiyo serikali ya CCM kupitia wizara yake ya Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi imekuwa na bajeti ya kiasi cha shilingi zaidi ya Bilioni 20 ili kuweza kugharamia ada za wanafunzi na malipo mengine, na ili kuwezesha mpango wa elimu bure bila malipo. Na hiyo ndiyo serikali ya CCM na huyo ndiye Rais DKT. JOHN POMBE MAGUFULI.

Pili, Serikali ya CCM chini ya Rais Dkt. John P. Magufuli imemsaidia mwanafunzi kuweza kusoma katika Mazingira yaliyo bora na rafiki ikiwemo kuhakikisha kuwepo kwa vitabu vya kutosha kwa kila shule; vitabu vya ziada na vitabu vya Kiada na hasa katika masomo ya Sayansi, masomo ya sanaa, masomo ya hesabu na masomo ya tehama, ili kuendana na mabadiliko katika kukua kwa Sayansi na teknolojia katika karne ya sasa ya 20.

Tatu, ujenzi wa Madarasa na vyoo katika Shule. Serikali ya CCM chini ya Rais Dkt. JPM imefanikiwa kukarabati Majengo ya shule kongwe za serikali. Ambayo kwa hakika yalikuwa hayafai na yalikuwa yakihatarisha usalama wa wanafunzi na walimu katika shule hizo. Shule hizo zimeboreshwa kwa kuwekewa mazingira mazuri na ya kisasa kwa kuwekewa malumalu, vigae, gipsam, miundombinu ya umeme pamoja na maji. Pia kumejengwa Vyoo vya kisasa na Matundu ambayo ambayo yanaendana na idadi ya wanafunzi. Ili kuhakikisha mazingira ya shule yanakuwa salama dhidi ya magonjwa ya mlipuko, kama kipindupindu; bila kusahau magonjwa ya UTI, Taifodi n.k

Nne, Ujenzi wa Maabara za kutosha. Ikiwa ni kuhamasisha kuongezeka kwa wanafunzi katika taaluma za sayansi. Shule zetu zilikuwa hazina maabara jambo lililopelekea wanafunzi kusoma kwa nadharia pekee lakini Leo hii maabara za kisasa zimejengwa ikiwemo vifaa vyake na kuwafanya wanafunzi kusoma kwa nadharia na kwa vitendo na kupelekea kuongezeka kwa ufaulu wa masomo ya sayansi. Serikali ya CCM imeendelea kuwa na utaratibu wa kupitia mitaala ili kuhakikisha vijana wa Tanzania wanajifunza sayanzi ya asili ambayo itaendana na mahitaji ya sasa.

Uhitaji wa maabara unaenda sambamba na maktaba. Ili kuhakikisha ubora wa elimu unapatikana kwa vijana wa kitanzania ambao inawapasa kuipata ikiwa ni sehemu muhimu ya haki yao, serikali ya CCM chini ya Dkt. JPM imehakikisha na kusimamia ujenzi wa maktaba za kutosha katika shule zote za umma na kwamba maktaba hizo zitatoshekezwa vitabu vya kuwatosha wanafunzi wote. Bila kusahau ujenzi wa mabweni, na hasa katika kuwaondolea adha watoto wa kike ambao mara nyingi wamejikuta wakishindwa kuendelea na masomo yao kutokana na mimba za utoto pamoja na ndoa za utotoni. Na hali imechangiwa kutokana umbali kuwa mrefu wakati wa kwenda kuitafuta shule, hivyo kuoelekea kukutana na vishawishi wakiwa njiani kuelekea shule. Serikali imeendelea na zoezi la ujenzi wa mabweni, ikiwa na lengo la kuwaweka karibu zaidi na masomo vijana wanafunzi na kwamba wanapata elimu bora.

Saba, inafahamika kuwa hali ya maisha ya waafrika asilimia kubwa ni masikini. Tanzania ni taifa la kiafrika hivyo, inaowajibu wa kuhakikisha kuwa haki ya kupata elimi ya Chuo kikuu ni haki ya kila mtanzania. Kwa muda mrefu CCM imekuwa ikiamini kuwa urithi pekee ambao kijana atapewa na utamfaa katika maisha yake leo na kwa siku zijazo ni elimu. Kwamba kijana akipata elimu atafahamu ni mahala gani au kazi gani afanye kwa ajili ya Taifa na ambayo ni kazi hiyo ndiyo itakayompatia pesa na kuweza kumudu kuishi. Inafahamika kuwa gharama za masomo kwa elimu ya juu ni kubwa mno, hivyo serikali ya CCM chini ya Dkt. JPM imekuwa ikiendeleza misingi ya CCM kwa kuongeza bajeti ya fedha kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wengi zaidi wa elimu ya juu. Ambapo kwa kipindi cha miaka mitano kwa wastani serikali imetoa mikopo kwa wanafunzi wa elimi ya juu zaidi ya shilingi Bilioni 400! Na katika hilo pia, serikali katika kipindi cha miaka mitano imefanikiwa kuondoa ile hali ya usumbufu na hasa ucheleweshaji wa fedha za mikopo kwa wanafunzi.

Ni ukweli usiokuwa na shaka kuwa serikali ya CCM na Rais Dkt. John P. Magufuli imefanya juhudi kubwa katika kuimarisha huduma ya elimu na katika kuifanya elimu kuwa ni haki ya watanzania wote kuweza kuipata. Na kwa hakika katika kipindi cha miaka mitano mengine katika utekelezaji wa ilani ya CCM ya uchaguzi ya 2020/2025, yenye zaidi ya kurasa 300!not Yapo mambo mengi na makubwa zaidi katika suala zima la sekta ya afya. Malengo ya serikali ya CCM ni kuhakikisha kabla ya mwaka 2025 wanafunzi wa vyuo vikuu wote waweze kupata mikopo. Na kwamba shule zetu zote ziwe katika ubora ambao utaenda sambamba na ubora wa elimu inayotolewa. Kwa miaka michache tumeweza kuona heshima za shule za umma katika matokeo ya kidato cha sita, ambapo shule nane baina ya shule kumi bora ni za serikali. Huo ni mwanzo tu.

Sasa KWANINI Tusimpe MAGUFULI awamu nyingine akaboreshe zaidi sekta hii nyeti na kuhakikisha Ujinga Tunautokomeza kabisa!

Sauti ya Mdodomia.

CHAGUA CCM
CHAGUA MAGUFULI
MITANO TENA

Screenshot_20200904-165923.png
 

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
52,639
49,909
JPM hauziki rafiki angu.

Hakuna hoja ya kumuuza JPM.

Hata huko vijijini wanaona huyu jamaa hafai hata kidogo.
 

Free-zy

Senior Member
Sep 30, 2015
122
76
JPM hauziki rafiki angu.

Hakuna hoja ya kumuuza JPM.

Hata huko vijijini wanaona huyu jamaa hafai hata kidogo.
HEBU TUMTOE DIAMOND JUKWAANI TUONE MEMBER WETU NI WANGAPI....MAANA NAONA MNAHISI SISIEM .....
 

The Giantist

JF-Expert Member
Dec 12, 2018
214
86
JPM hauziki rafiki angu.

Hakuna hoja ya kumuuza JPM.

Hata huko vijijini wanaona huyu jamaa hafai hata kidogo.
JPM ndiye Rais ajaye kwa miaka mitano mengine. Na kwa faida yako, JPM ni msimamizi na mtekelezaji wa ilani ya CCM ya uchaguzi mwaka huu. Kwa hiyo inayoenda kuuzwa ni ilani. CCM ni ya kipekee na kwa kiasi kikubwa imejitofautisha na vyama vya ruzuku ambavyo vinasimama kumuuza mtu binafsi badala ya chama na kijarida chao.
 

The Giantist

JF-Expert Member
Dec 12, 2018
214
86
Akituambia wasiojulikana ni akina nani nitamchagua maana naogopa akipewa mitano mingine wasiojulikana wataanza vitu vyao tena.
Zilikuwa ni ajenda za hamnazo. Watu wasiojulikana ni waharifu kama waharifu wengine ambao wamekuwa wakipepelezwa miaka na miaka na wakapatikana. Kwa hiyo wasiojulikana ni ajenda ya mtu anayeelekea kufa kisiasa. Kwa mfano unaweza kuniambia waliohusika na kifo cha Rais Kennedy wa Marekani mwaka 1963?
 

The Giantist

JF-Expert Member
Dec 12, 2018
214
86
Aisee mwaka huu mnahaha hata wake zenu mtashindwa kuwahudumia kwa stress! Hizi ni dalili kuwa mmeshikwa pabaya mnatia huruma!
Wanaohaha ni wale wanaouza sera kwa kurejelea masimulizi ya ubinafsi zilizopita badala ya kurejea kijarida chake cha uchaguzi, ama badala ya kueleza uwezo wake katika kuongoza. Hao ndio wanaohaha!
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
218,626
506,774

jaranono

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
2,012
1,599
JPM hauziki rafiki angu.

Hakuna hoja ya kumuuza JPM.

Hata huko vijijini wanaona huyu jamaa hafai hata kidogo.
Kwahiyo wale wanaojaa kwenye mikutano yake wanatokea wapi? na wanafata nini? ni kumwona kwa karibu tu au kupewa mil 5? Binafsi sielewi !! Kazi ni kubwa na ngumu kwa kweli,
 

ngaiwoye

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
1,304
1,581
JPM ndiye Rais ajaye kwa miaka mitano mengine. Na kwa faida yako, JPM ni msimamizi na mtekelezaji wa ilani ya CCM ya uchaguzi mwaka huu. Kwa hiyo inayoenda kuuzwa ni ilani. CCM ni ya kipekee na kwa kiasi kikubwa imejitofautisha na vyama vya ruzuku ambavyo vinasimama kumuuza mtu binafsi badala ya chama na kijarida chao.
Nakuunga mkono 100%
 

Valuhwanoswela

JF-Expert Member
Jun 27, 2019
1,229
1,124
Zilikuwa ni ajenda za hamnazo. Watu wasiojulikana ni waharifu kama waharifu wengine ambao wamekuwa wakipepelezwa miaka na miaka na wakapatikana. Kwa hiyo wasiojulikana ni ajenda ya mtu anayeelekea kufa kisiasa. Kwa mfano unaweza kuniambia waliohusika na kifo cha Rais Kennedy wa Marekani mwaka 1963?
Rais Kennedy aliuawa na Oswald na kukamatwa na Police siku hiyohiyo na kuuawa akiwa mikononi mwa Police na mtu aliyeitwa Rubby naye akauawa na Police waliokuwa wamemkamata Oswald. Mpaka leo inaaminika kuwa Rubby alikuwa mshirika wa Oswald na alimuua ili asimtaje na katika kurupushani hiyo nae akauawa ikawa end of the story. Haya yote yalitokea siku hiyohiyo na eneo hilohilo mjini Dallas alikouawa Rais John F. Kennedy,RIP.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom