- Thread starter
- #121
hongera mkuu umeweka wazi msimamo wako
ni wengi kama mimi wanaotaka kuweka misimamo yao wazi...
sema aibu tu,,
hongera mkuu umeweka wazi msimamo wako
Habari!
Binafsi hili vuguvugu la kuiponda ccm na kuiona haifai linaniumiza sana,
Nimezoea kula bure (kula kwa kupitia deals).
Nasafiri bure (nadhani hapa ni kwa kodi za walala hoi).
Chochote nitakacho napata kwa sababu CCM ipo madarakani, rafiki zangu kibao wamepata ajira kubwa kubwa regardles ujuzi wao mdogo na elimu yakuunga unga walionayo,(wawili wapo bandari, wanne wapo maliasili) just because ccm ndiyo wameshikilia dola.
Nina magari zaidi ya mawili, i got them kwa sababu tu ccm iko madarakani.
Ninavyosikia juu ya kufa kwa CCM naweweseka sana jamani.
Ila ninaamini CCM wakishindwa 2015.
Tupo wengi sana tutakao kuwa maskini, si mimi peke yangu.
Machale yananicheza sana.
Akina riz washajiwekewa njia m'badala yakujinasua endapo chama hakitaingia madarakani 2015.
Tunapambana kwa kila njia kwa maslai yetu, umaskini si mzuri jamani!
Maisha yakupanda bodaboda na kugombania daladala ni magumu jamani.
Nitafurahi ccm isipokufa niendelee kuishi kwa ubwerere.
Hata wenzangu nao watafurahi..
Kura yako unaipiga wapi 2015 au we ni banyamulenge haupigi kura?
Pouleh xana... Na hauna dauwa hiyo!!
Kwani chama kikishindwa uchaguzi ndio kinakufa?
CCM haina watu kama wewe, upo peke yako
lakini umeongea uhalisia wako,
Kifo cha CCM ni kifo cha wengi,msiba mkubwa sana
Chama cha Mapinduzi hakipo kingekuwepo madarakani hata CDM isingekubalika...kilichopo ni Dola iliyojivika nguo za Kijani na kujiita CCM na kuachukua yale yote ya CCM na kuyaita yakwake, ndio maana leo polisi wanaishi km miungu watu, uhamiaji wanaweza wakakuita wewe ni raia wa Chile na ikakubalika, Mahakama inaweza ikakuhukumu hata km jina la mtuhumiwa si lako, Waziri mkuu anaweza akaamrisha wananchi wake wauawe bila woga eti amechoka (sijui kwanini asijiuzulu wenye nguvu waendelee), rais anaweza akajenga hoja kuwa safari ndio msingi wa maendeleo ya nchi na ikakubalika, Mawaziri wana gawana wapi pa kuchukulia hela na kushindana na kajenga nini au kanunua gari gani, wanachama wa CCM ndio wananchi halali wa taifa hili wengine woote risasi ni halali yao....!