CCJ kuanza Charm offensive! - Ask your questions!

CCJ kuanza Charm offensive! - Ask your questions!

Yafuatayo ni maswali ya awali lakini nitauliza zaidi kadri muda utakavyoruhusu:-
  1. Naomba unieleze CCJ inaongozwa na falsafa ipi katika uongozi wa nchi? Siongelei blah blah za CCM kama kilimo kwanza, nguvu mpya ari mpya etc.
  2. CCJ wana mkakati gani wa kupigania mabadiliko ya kimsingi ya katiba na sheria yatakayotoa fursa sawa kwa vyama vya upinzani (ikiwemo CCJ) kuendesha siasa za haki nchini?
 
Binafsi ninaamini kabisa kuwa hakuna chama cha kupambana na chama cha kimafia katika anga za uchaguzi CCM. Kazi ya TISS na Police illiongezeka baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, kazi hiyo ni kuhakikisha vyama vya upinzani havipati nafasi ya kutangazwa washindi wa uchaguzi kwa vyovyote. Kwa mtazamo wangu yaliyoipata NCCR, CUF, CHADEMA yataipata pia CCJ unless CCJ iwe imeanzishwa strategically as a branch of CCM which ensures the same benefits to political tycoons regardless of who's in Power between the two parties.

1. Kitakachofanyika ni kuwa CCJ isitangazwe(kutangazwa ni tofauti na kushinda) imeshinda kiti chochote hata cha serikali ya mtaa, then people will forget it in five years time, will lead to its natural death

2. Kunyimwa usajili wa kudumu mwaka huu ili kukinyima nafasi ya kupimana nguvu na CCM

3. Kuwatisha viongozi wa CCJ na kuwashawishi kujiunga na CCM where they be given a place to seat infront of the plate.

4. Kukihusisha na Illegal activities ili kukipachika jina kama cha kidini, kikabila, kigaidi and the like.


Why I said that?, rejea uchaguzi wa 2005, CUF was a strongest opposition party. Kukinyima kiti hata kimoja cha ubunge Tanzania bara ilikuwa ni mbinu mahsusi ya kukimaliza nguvu, Haiingii akilini chama kishike nafasi ya pili kwa popular votes halafu kisipate mbunge hata mmoja. Wapinzani wangekuwa na umoja walitakiwa kuhitaji Tume huru ya uchaguzi kwanza kabla ya kuingiza timu uwanjani, malalamiko baada ya mechi huonekana kama kutoa machungu ya kubwagwa badala ya malalamiko yenye mantiki.

Tuchangie hii thread na kujiburudisha lakini CCM itaendelea kujitangaza mshindi na ikifanyika vurugu virungu vitapigwa, na ikibidi itakuwa kama walivyofanyiwa wafanyakazi wa wawili wa KILOMBERO SUGAR kupigwa risasi za moto na ikiwa bahati mbaya kwako utakufa na hakuna atakaye wajibishwa kwani green light imeshatolewa kuwa wanapofanya kazi yao sometimes inaweza tokea wakaua. pasipo malalamiko ya kuibiwa kura na maandamano hakuna atakaye pigwa virungu.
 
Hawa wapinzani ni feki tuu.. Wangekuwa na akili wangetengeneza chama kipya cha kuichallenge CCM. Hawaoni kuwa their efforts are futile. Fair enough serikali imeweka sheria yakijinga yakukataza coalitions which is unconstitutional anyway... below the standard of international practices and not to mention undemocratic, lakini in 5 years.. wanashindwa kuunda chama kimoja kikawa serious challenge wachukue ata 30% ya viti vya ubunge? Siasa should have the aim of influencing and changin policies, hweuzi tuu gombea urais miaka 20 unapata 2% of the vote and still you continue.. Watu wanamatope kichwani.
 
mimi sidhani kama mpinzani wa kweli wa CCM ameshapatikana, watanzania bado tuna chakura chakura kwenye pakacha, vyama viletwe tu tupate uwanja mpana zaidi wa kuchagua, upinzani wa kweli na nia ya kuongoza nchi hii utaonekana baada ya uchaguzi na sio wakati wa kuomba kura. chama bora cha upinzani kitakapopatikana wote wenye moyo wa kweli wa upinzani watajiunga nacho. watanzania wengi bado wana 'have a bite and spit out', nothing yet to swallow

Lazima watanzania tujue kuwa upinzani wa kweli utatokana na wananchi wenyewe. Upinzani hautatokana na vyama au viongozi fulani kama Dr. Slaa au Zito. Hawa wapinzani wanasaidia sana kutuelimisha wananchi ili tuelewe kuwatuna wajibu wa msingi wa kuleta mabadiliko ya kweli. Wengi wetu tunadhani kuwa tunaweza kukaa tu na kusubiri wapinzani waje watuondoe kwenye hii kadhia ya ufisadi wakati tunaendelea kuwachagua watu walewale, wenye sera zilezile, itikadi ileile.

Hii dhana imewaathiri hata viongozi wetu ambao wanadhani kuwa maendeleo yetu yataletwa na wafadhili na the so called wabia wa maendeleo.
 
Kwa sababu ndege ya usafiri wetu CCM imeanguka, vyama vya Upinzani walikuwa na wasiwasi nayo toka mwaka 1992, wakati hawa CCJ wakiwa wahudumu na waajiriwa wa shirika hili. Sasa baada ya kuanguka ndipo tunapata mawazo mengine toka kwao ya kutuchanganya akili zaidi..Kumbuka mkuu wangu wewe unazungumza kama mwanaCCJ sijui kama umesimama kama mpiga debe au mmoja wa viongozi hali mimi nazungumza kama mwananchi nayetaka kuokolewa..Imani yangu mwananchi kwako ndiyo muhimu kuliko maelezo yoyote yale na lazima ujali zaidi hofu ya mwananchi kuliko fikra zako wewe..

Nitarudia kusema hivi ile ndoto ya Ushindi haiwezi kuwepo kama hakuna muungano wa vyama. CCJ could be anything.. pengine ni watu wa Lowassa, Mkapa, Sumaye who knows..au hata JK mwenyewe anataka kujiengua CCM ya wazee na kuunda wagombea wapya through CCJ kama alivyofannya yule rais wa Malawi. Kifupi Ujio wa CCJ unatuchanganya zaidi sawa na hiyo misaada inayotolewa hivi karibu ya uchaguzi kama ni takrima au ndio ilikuwa Ilani ya mgombea. Mkuu mnatuvuruga tu akili zetu kuweni wazi. wakweli na kutazama ishara za wakati na ushindi, haya maswala ya kila kila mtu na usafiri wake ni maswala ya kutafuta orodha ya wanachama sio ushindi kwa Taifa zima.

Hapa uko right...Kwanini hao walio nyuma ya CCJ wasijitokeze sasa mpaka wapime upepo wa kupita ama kutokupita kwenye kura za maoni CCM? Au kwa nini wasubiri mpaka bunge livunjwe rasmi ili kuonyesha wao ni CCJ? Je haitii mashaka kwamba pamoja na Mpendazoe kuacha uanachama CCM bado anapata mafao kama vile alikuwa mgombea binafsi? Kwa nini wasimsimamishe ubunge haraka kwa visingizio dhaifu kwamba bunge halijapata taarifa reasmi? So it is very obvious kwamba CCJ ni zubaisha *****, yaani mahali watu wote watakaona mwelekeo wao kisiasa hauwaendei vizuri CCM , basi wajiunge CCJ. Ya Mkapa na Kikwete kucheka dakika hizi....yanatia mashaka. I remain vigilant
 
Kule Marekani mtu akisema yeye ni Republican tunajua anaegemea upande wa matajiri na akisema yeye ni Mdemocratic basi yeye anaegemea kundi la watu wa kawaida, Uingereza nako vile vile. Hapa kwetu pamoja na wingi wa Vyama, sidhani kama kweli kuna tofauti ya kiitikadi kati ya chama na chama tofauti na kutoa ajira kwa wale walio kwenye safu ya uongozi
 
Hapa uko right...Kwanini hao walio nyuma ya CCJ wasijitokeze sasa mpaka wapime upepo wa kupita ama kutokupita kwenye kura za maoni CCM? Au kwa nini wasubiri mpaka bunge livunjwe rasmi ili kuonyesha wao ni CCJ? Je haitii mashaka kwamba pamoja na Mpendazoe kuacha uanachama CCM bado anapata mafao kama vile alikuwa mgombea binafsi? Kwa nini wasimsimamishe ubunge haraka kwa visingizio dhaifu kwamba bunge halijapata taarifa reasmi? So it is very obvious kwamba CCJ ni zubaisha *****, yaani mahali watu wote watakaona mwelekeo wao kisiasa hauwaendei vizuri CCM , basi wajiunge CCJ. Ya Mkapa na Kikwete kucheka dakika hizi....yanatia mashaka. I remain vigilant

Sema weye kiazi,miye muhogo ntaambiwa nna mzizi...teh teh teh!
 
Mwanakijiji panga pangua kwenye mjadala huu,kwa namna ya uzoefu wa duru za siasa hapo bongo,kuna only 2 game changers ambazo each one has its consequences on the partys politics coming general election.....Sasa wewe uliposema mambo ya daraja,nikasema ala!kwa hiyo when you look over the horizon,you deal with just what you can see,aint that rgt?Hilo "daraja" naona hauli anticipate kabisa,based on yur statements...Kwamba mtadili nalo itakapofika huo wakati....Hata hivyo kwa upande mwingine,umeamua ku ignore upande wa pili wa sarafu,hata hivyo naona kuna kuliana timing kwa sana....Hata hivyo MKJJ,ikija kugundulika kuwa hao wapiganaji wanasusua kwa sababu ya "mafao" Basi wata loose sapoti kubwa sana....I mgt b wrong,we'll wait n c,time will tell!
 
Hapa uko right...Kwanini hao walio nyuma ya CCJ wasijitokeze sasa mpaka wapime upepo wa kupita ama kutokupita kwenye kura za maoni CCM?

Nani amekuambia kuna watu nyuma ya CCJ nje ya hawa waliojitokeza?

Au kwa nini wasubiri mpaka bunge livunjwe rasmi ili kuonyesha wao ni CCJ?

You guys you have to move from this mentality..

Je haitii mashaka kwamba pamoja na Mpendazoe kuacha uanachama CCM bado anapata mafao kama vile alikuwa mgombea binafsi? Kwa nini wasimsimamishe ubunge haraka kwa visingizio dhaifu kwamba bunge halijapata taarifa reasmi? So it is very obvious kwamba CCJ ni zubaisha *****, yaani mahali watu wote watakaona mwelekeo wao kisiasa hauwaendei vizuri CCM , basi wajiunge CCJ. Ya Mkapa na Kikwete kucheka dakika hizi....yanatia mashaka. I remain vigilant

I totally understand your sentiments.
 
Nani amekuambia kuna watu nyuma ya CCJ nje ya hawa waliojitokeza?



You guys you have to move from this mentality..



I totally understand your sentiments.

Mtaharibu otherwise,i c it....ccj imeanzishwa kuimega ccm,na si upinzai eti cjui cuf,ooh hii mentality ya upinzani,huwezi kuzaliwa kunywa uji na kutembea hapo hapo kama wewe mwanadamu!mnaogopa labda Lowassa naye ccj?Mficha maradhi kifo humuumbua,kinyume na hapo,mark ma words man!Hamwendi mahali bila credible endorsements,otherwise if ya'll dont care bout it then "mapandikizi theory" mgt den b viable....Bottom line "mtu mpya" asiyejulikana nani yuko "nyuma" yake,would certainly rais concerns
 
hadi uongee na wako kwanza,hapo vipi?Maana hiyo picha yako hapo kama kweli yako,basi mmnh!

Sina sista mimi bana....

Halafu wait a minute dawg....are u hitting on me or what? Nadhani umepotea njia.....mcheki Boflo
 
Mzee Mwakijiji,
Haya mathlan tukubali kwamba CCJ ni hao waliojitokeza ikiwa ni pamoja na wewe. Sawa kabisa, lakini mnashindwa kutuvuta kwa sababu moja kubwa. Nyie Kushindwa kuelewa TATIZO la wananchi hivi sasa ambalo ndilo linatangulia kabla ya hizo Itikadi zenu.
Nitakwambia tena na tena ili upate kunielewa vizuri natokea wapi.
Wengi wetu tunajiona kama wafungwa ndani ya gereza hili la chama CCM...Tunachokitaka ni kuondoka ktk hali hi ya ufungwa, na ndio maana nikatumia ule mfano wa ndege iloanguka kisiwani. Sasa unapokuja na idea ya kuroroka ni muhimu kwetu kusikia master Plan ya kutuwezesha ku escape toka kifungoni au kuondoka ktk adha za kisiwani hiki na kuwa HURU.

Sisi sote kwa ujumla wetu hapa JF tunataka kusikia mtaweza vipi kutuondoa ktk Utawala huu wa CCM na sio siasa za baadaye. Hata hao TANU chini ya na mwalimu Nyerere walitupa siasa za kujikomboa kwanza toka utawala wa mkoloni kabla ya itikadi za huo Ujamaa kuja miaka saba baadaye. Ndivyo wanavyofanya wana Mapinduzi wote duniani kutafuta support ya wananchi ili watoke ktk utawala unaowagandamiza.

Nachokiona mimi CCJ wanakuja na siasa za Itikadi kama vile nchi yetu haina matatizo, mkuu wangu sivyo wananchi wengi wanavyoitazama Tanzania ya leo..na kibaya zaidi viongozi na wanachama wa CCM wamekaa kama makaburu hawaoni shida hizi kwa sababu wao wako ktk hali nzuri ya kimaisha. Na kwa makosa ya wazi kabisa Utawala mzima unawanufaisha wale wanakubaliana nao kwa kuvaa magwanda ya Kijani kujionyesha wao ni watu tofauti kabisa na watawaliwa. Tofauti na makaburu, waliokuwa na Ubaguzi wa rangi sisi tunatumia ubaguzi wa mavazi na bendera za chama...na kwa bahati nzuri sii wananchi wengi wanakubali mfumo huu wa utengano.

Njia pekee ya CCJ kuweza kufanikiwa ni kuja na master Plan ya kuwakomboa wananchi toka gereza hili la CCM. Na ndio hapo tunapokuja na mchango wetu kwamba, hii great escape haiwezi kufanikiwa pasipo muungano wa makundi mengine yanayotaka pia kuondokana na kifungo hiki, pamoja na kwamba huko nje ya kifungo kila jumuiya inaweza kuwa na mipango yake. Walifanya Zimbabwe, South Africa nchi zote za Ulaya ya mashariki, Bosnia na majuzi tu Poland, Kenya, Zimbabwe tena na Liberia. Wote hawa walijenga mbinu za kukiondoa chama tawala pale wananchi hawakuwa na matumaini - Tumaini jipya kwa wananchi waliokosa Uhuru huanza na mbiu ya FREEDOM..na Uhuru hauwezi patikana pasipo wapinzani kuwa na nguvu moja japokuwa wana imani za kiitikadi tofauti..
 
Back
Top Bottom