Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,097
- 43,309
- Thread starter
- #201
Mzee Mwakijiji,
Haya mathlan tukubali kwamba CCJ ni hao waliojitokeza ikiwa ni pamoja na wewe. Sawa kabisa, lakini mnashindwa kutuvuta kwa sababu moja kubwa. Nyie Kushindwa kuelewa TATIZO la wananchi hivi sasa ambalo ndilo linatangulia kabla ya hizo Itikadi zenu.
Nitakwambia tena na tena ili upate kunielewa vizuri natokea wapi.
Wengi wetu tunajiona kama wafungwa ndani ya gereza hili la chama CCM...Tunachokitaka ni kuondoka ktk hali hi ya ufungwa, na ndio maana nikatumia ule mfano wa ndege iloanguka kisiwani. Sasa unapokuja na idea ya kuroroka ni muhimu kwetu kusikia master Plan ya kutuwezesha ku escape toka kifungoni au kuondoka ktk adha za kisiwani hiki na kuwa HURU.
Sisi sote kwa ujumla wetu hapa JF tunataka kusikia mtaweza vipi kutuondoa ktk Utawala huu wa CCM na sio siasa za baadaye. Hata hao TANU chini ya na mwalimu Nyerere walitupa siasa za kujikomboa kwanza toka utawala wa mkoloni kabla ya itikadi za huo Ujamaa kuja miaka saba baadaye. Ndivyo wanavyofanya wana Mapinduzi wote duniani kutafuta support ya wananchi ili watoke ktk utawala unaowagandamiza.
Nachokiona mimi CCJ wanakuja na siasa za Itikadi kama vile nchi yetu haina matatizo, mkuu wangu sivyo wananchi wengi wanavyoitazama Tanzania ya leo..na kibaya zaidi viongozi na wanachama wa CCM wamekaa kama makaburu hawaoni shida hizi kwa sababu wao wako ktk hali nzuri ya kimaisha. Na kwa makosa ya wazi kabisa Utawala mzima unawanufaisha wale wanakubaliana nao kwa kuvaa magwanda ya Kijani kujionyesha wao ni watu tofauti kabisa na watawaliwa. Tofauti na makaburu, waliokuwa na Ubaguzi wa rangi sisi tunatumia ubaguzi wa mavazi na bendera za chama...na kwa bahati nzuri sii wananchi wengi wanakubali mfumo huu wa utengano.
Njia pekee ya CCJ kuweza kufanikiwa ni kuja na master Plan ya kuwakomboa wananchi toka gereza hili la CCM. Na ndio hapo tunapokuja na mchango wetu kwamba, hii great escape haiwezi kufanikiwa pasipo muungano wa makundi mengine yanayotaka pia kuondokana na kifungo hiki, pamoja na kwamba huko nje ya kifungo kila jumuiya inaweza kuwa na mipango yake. Walifanya Zimbabwe, South Africa nchi zote za Ulaya ya mashariki, Bosnia na majuzi tu Poland, Kenya, Zimbabwe tena na Liberia. Wote hawa walijenga mbinu za kukiondoa chama tawala pale wananchi hawakuwa na matumaini - Tumaini jipya kwa wananchi waliokosa Uhuru huanza na mbiu ya FREEDOM..na Uhuru hauwezi patikana pasipo wapinzani kuwa na nguvu moja japokuwa wana imani za kiitikadi tofauti..
Mkandara,
a. kwanini muungano wa kuiondoa CCM umeshindikana sasa hivi miaka 15 tangu kurudi kwa mfumo wa vyama vingi?
b. Kwanini muungano huo utamanike na uonekane unawezekana kwa ujio wa CCJ?
c. Kwanini vyama vilivyopo sasa (ukiondoa CCJ ambacho hakina itikadi, hakielewi matatizo ya wananchi na hakina mpango unaoeleweka wa ukombozi wa Mtanzania kutoka katika utumwa wa CCM) visiungane mara moja kwani tayari vina usajili wa kudumu na vina sera na mipango kamambe ya kuiondoa CCM?