ninafurahi kwamba mgawanyo tunaoutaka ndio unaendelea kuwepo. Wale wanaoamini chadema, cuf au vyama vya upinzani vilivyopo ndiyo vinawakilisha matamanio yao na njozi zao wana haki kabisa ya kuendelea kuwemo humo na kuviimarisha; wale wanaoamini kuwa ccm ndiyo suluhisho la matatizo ya watanzania na kuwa ndio chama pekee chenye uwezo wa kutuletea maendeleo nao wana haki ya kuendelea kuunga mkono na kujiunga nacho. Lakini si haki kujaribu kuwataka watu wote wajiunge na upinzani wa zamani au chama tawala ati kwa sababu chama kipya hakieleweki, hakijulikani n.k n.k hakuna ratiba ya kuundwa chama ili kikubalike; hakuna masharti ya chama kiwe kimeundwa kwa muda gani ili kiwe kinavutia watu; chama ni itikadi na muundo. Hadi hivi sasa hakuna chama kwenye upinzani huu zamani chenye itikadi ya ccj, period. Sasa kutaka watu wa ccj au mashabiki wake kujiunga na vyama vya upinzani wa zamani ili mradi tu wasiwe na chama chao ni kujaribu kuweka mawazo huru ya watu kwenye chupa moja ya upinzani.
Naomba nipendekeze; wale mnaoamini chadema, cuf au vyama vya upinzani vya zamani kuwa ndio uchaguzi wenu endeleeni tu kwani ni sehemu ya demokrasia. Kama watu hamkubaliani kiitikadi, mtazamo au mapendekezo yenu ya kitaifa hamuwezi kuungana. Sielewi kwanini ccj wanatakiwa kujiunga na vyama vingine wakati hawakubaliani navyo kiitikadi, mtazamo au malengo! Hatuwezi kujiunga na vyama vingine ili "kuiondoa ccm madarakani"; muungano wa namna hiyo ni muungano dhaifu kwani unaundwa katika lengo la udhaifu. Huweji kuwa na lengo la kuondoa ccm madarakani kama msingi wa muungano!
Wale walioridhika na ccm waendelee hivyo hivyo na wale ambao tunataka kuleta pendekezo jipya kwa wapiga kura na watanzania, pendekezo lenye misingi ya historia yetu kama taifa basi tutafanya hivyo. Yawezekana tusifanye vizuri kama tunavyotaka kwenye uchaguzi huu lakini tunachotaka ni kuwa na sisi wenye mawazo tofauti na yale ya ccm au upinzani uliopo sasa tuwe na nafasi katika siasa za nchi yetu? je hili linawatisha sana hadi mtushauri tujiunga na watu ambao hatukubaliani nao kiitikadi, mfumo, mtazamo au usuluhishi wa matatizo ya kitaifa? Tuungane nao ili nani afurahi?
mzee mwanakijiji,
mkuu wangu mawazo yako ni ya kibinafsi.. Yaani unaonyesha wazi kwamba unachoamini wewe hata kama ni kinyume basi sawa tu hali wakati huo huo unatumainia ushindi pasipo kuunganisha nguvu... Hii haiingii akilini hata kidogo. Maelezo yako kwa ujumla hayana tofauti na ile hotuba ya jk alipowaambia wafanyakazi kwamba - haitaji kura zao.. Jambo ambalo limetupa picha kwamba jk anafikiri anaweza kushinda pasipo kura za wafanyakazi. Fikra hizi tu zinaweza kumgharimu sana kinyume na matajario yake.
Mkuu mara zote kauli ya mtu ndio humfunga ktk matendo yake, hivyo unaposema ccj hawana sababu ya kuungana na vyama vingine kwa sababu za kiitikadi, malengo na kadhalika inanipa wasiwasi mkubwa zaidi kwa sababu nimeisoma katiba ya ccj na hakuna jipya.. Ccj imeundwa kutokana na matokeo ya uongozi mbovu aambao wote hawa wameutumikia kwa zaidi ya miaka 26 muda mrefu zaidi ya utawala mzima wa nyerere. Hawa watu walikuwa viongozi ngazi za juu kwa miaka yote 26 wasione sababu ama umuhimu wa upinzani kwamiaka yote 26 ila tu baada ya kuingia jk ndipo tunawaona wakisimama.
Kifupi hawa naweza kuwaita ni wana mapinduzi, ccj ni chama kinachotaka kupindua ccm kwa amani lakini ni kizazi kile kile kilichotufikisha hapa tulipo leo. Mabaya yote wanayoyaona leo ccm ni mabaya ambayo vyamavingine vimeyaona miaka zaidi ya 15 iliyopita wakati wao hawaoni makosa haya. Leo ujio wao uyaone makosa yote ya upinzani kisha basi badala ya wao kuyarekeebisha ili ushindi upatikane wanachukua jukumu hilo wao wenyewe kwa matumaini kwamba sisi wananchi tutawaamini kwa sababu tu wanatumia jina la mwalimu nyerere.
Hapana mkuu wangu... Ccj wakiwa viongozi ndani ya ccm wamepiga kura nyingi sana dhidi ya miradi ambayo imetuingiza ktk hasara. Walikuwa moja ya sababu kubwa ya bunge letu kupitisha sheria ambazo zimetufikisha hapa. Walikuwa wajumbe wa mkutano ulopitisha azimio la zanzibar na kuliua azimio la arusha hali wakidai azimio hilo halikufa. Na wakayapokea mafisadi ndani ya chama wakijua fika kwamba chama kinapoteza mrengol lakini hawakutoka. Sasa iweje leo hawa watu waje hapa kutuhakikishia ushindi hali wakijitenga na kutohitaji nguvu ya wanamapinduzi wengine waliowatangulia.
Mkuu wangu nimekwambia wazi kabisa kwamba hata zimbabwe ambao walikuwa na uhasama mkubwa wa kikabila na chuki ya jadi. Iliwachukua kuungana kwa nguvu zao kuweza kumshinda kaburu ian smith. Huko south pamojana upinzani mkubwa wa kiitikadi baina ya anc na pac walikuja unganisha nguvu zao kumlazimisha kaburu kuachana na apartheid. Uhuru wa msumbiji na kadhalika, hizi zote ndizo hekima za mwalimu nyerere alizotuonyesha ama kutuachia kwamba ni lazima tuondoe tofauti zetu tunapomkabiri adui mmoja. Maswala mengine ya kiitikadi yatafuata baada ya ushindi na kubomoa nguzo au kuta za berlin (katiba, sheria na taratibu za kiutawala).
Kinyume cha kufanya hivyo ni kukataa wazi hekima za mwalimu lakini bado mkitumia jina lake kwa faida yenu..ikiwa ushindi ni lazima basi shurti mkubali ukweli kwamba umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.. Mkikataa haya binafsi sioni sababu kabisa ya chama hiki ccj kutumia jina la mwalimu hali msingi mkubwa wa itikadi yoyote ni kuwaunganisha watu dhidi ya utawala dhalimu.
Felister,
Mkuu wangu hata sijakufahamu kabisa unachozungumza. Kwanza hakuna mtu aliyedharau mtu isipokuwa tunazungumzia chombo hiki cha CCj.. Ni swala jingine kabisa kusema Mwanakijiji hawezi kitu pasipo kujua mapana ya Mwanakijiji, tofauti na kuznugmzia chombo cha usafiri ambacho lengo lake ni kuwachukua Watanzania wote na sio wanachama wake kufika ktk promise land. Na hata huo mfano unazungumzia huyo Mtume alisema yeye peke yake akiwa na maana kuwa ndiye pekee Muumini wa Mwenyezi Mungu na haikuwa na maana hapakuwepo na watu wengine wenye uwezo. Ni swala la kiimani zaidi ya uwezo na nguvu zake.
Ni muhimu sana swala hili tusilichukulie Unazi au ushabiki kwa sababu tunazungumzia Mustakabali wa nchi nzima na raia wake. Hili sio swala la wanaCCJ na waumini wake against the rest.. hatupiganii nani ataingia peponi kabla ya mwenzake ila swala zima linatuhusu sote inapofikia nani awe kiongozi wetu na chombo gani tukitumie. Sasa mkianza kufikiria kuna akina HAO against SISI wenye elimu na uwezo, ndipo mnapoweza kupoteza kabisa maana ya usajili wenu. CCJ ni chama kinachotakiwa kuwa wazi hakuna sababu kabisa ya kujificha ficha viongozi kisha mnatwambia kama hatuwezi tuwaachie wanaoweza hao wamejificha..
Mzee Mwanakijiji,
Unaposema CCJ sio chama kilichanzishwa na wana CCM hapa mkuu utakuwa unatufunga kamba tu ama kujilaghai mwenyewe. Huwezi kutumia majina ya watu waliopo leo hii kushindana na CCM ktk nchi hii. Ukweli huu lazima mmuukubali. Hayo majina ya kina Mpendazoe mtashindwa vibaya sana kwa sababu Nitarudia tena Watanzania tu Wajinga na Malimbukeni. Itachukua zaidi ya majina haya kuwapeni hata nafasi ya kushinda majimbo na laukama nia yenu ni nzuri basi bila shaka mtakubaliana nami kwamba ipo kila haja ya kukusanya nguvu zetu wote wanaopenda mabadiliko kupambana na utawala wa CCM..To me tatizo sio Kikwete, na fact zipo kwamba kafanya mengi mazuri (policies) kuliko mabaya isipokuwa kashindwa kusimamia utawala wake...Kosa moja kubwa la JK - he is a WEAK president.. Hili kosa moja tu linaondoshaa kabisa sifa zake zote za kushika ajira yake...
Nafuatilia sana ndugu yangu ndio maana nikamuuliza kinaganaga kama ni mwanachama kwa kuwa analikimbia kiaina hilo swali - nioneshe alipolijibu kwa uwazi kabisa!
Thank You!Mkandara, kwanini CCJ iungane na vyama vingine? Na ni chama gani ambacho kinafaa CCJ kuungana nacho na kwanini?
Rudi ukurasa wa kwanza na wa pili...............
Naona wewe na jmushi hamuoni umuhimu wa cross-checking na triangulation. Rejea posti #33 ya Mwanakijiji. Jibu lake linadhihirisha kuwa sio mwanachama mwanzilishi 'absolutely'! Pia tembelea posti zake za zamani kuhusu CJJ. Kisha angalia falsafa zake na uzilinganishe na falsafa mchanyato anazodai kuwa ni za CJJ - tangu lini chama kikawa na mirengo miwili. How can you talk left and walk right or talk right and walk left?
...hadi hivi sasa wameweza kujiunga kuanzia Japan, South Africa, Uingereza na US yenyewe...
Kwa nini umesema na US yenyewe? Kwa nini isingekuwa na Tanzania yenyewe? What does this tell?
2. Pili inawezekana kabisa Mzee Mwanakijiji ukawa uko Kazini, na hii piga debe yote ikawa ni sehemu tuu ya majukumu tuu ya kazi
Its just thinking aloud!,
Kama wewe MM ni among founders! !! inabidi nikitupie macho - wacha tuvute subira inawezekana neema ikawa imefunuliwa kwa watanzania - Chama Mbadala kuzaliwa - kilichosubiriwa kwa miongo mingi kitakacholeta tumaini jipya la ukombozi wa kweli.absolutely!
usipoangalia utamiss mengi kweli;.. nenda nyuma kidogo ya "zamani"..
I will not dare to speculate what this means..
Mzee Mwanakijiji, let me be frank and open,
1. Kwanza: CCJ is for real, and its more that what we see and hear mpaka mtu wa calibre ya Mzee Mwanakijiji kujiunga. Ili nijiridhishe, its for real, natamani kuijua 'the motive behind Mzee Mwanakijiji ndani ya CCJ'.
2. Pili inawezekana kabisa Mzee Mwanakijiji ukawa uko Kazini[/B], na hii piga debe yote ikawa ni sehemu tuu ya majukumu tuu ya kazi
Its just thinking aloud!,
Companero, nadhani haya ni mambo ya ndani sana kuyaweka hadharani, hata kama ningekuwa ni mimi, nisingejibu, ila kuwa mshabiki/mwanachama muanzilishi, sio lazima uwe ulipata kadi ya uanachama, namba ngapi, lini na wapi. Inavyosikika wale makamanda ndio wanachama waanzilishi huku bado kadi zao za CCM wamezishikilia wakisikilizia hatima ya usajili wa CCJ.Mkuu acha mazingaombwe. Mimi ni msomaji mzuri wa posti zako, kuanzia mashairi mpaka uchambuzi. Mtazamo wako wa kisiasa naweza hata kuuandikia wasifu - hili la CCJ ni bango tu la kutimiza uliyoshindwa kuyatimiza kupitia vyama vingine. Hebu jibu maswali haya kama u mwana-CCJ:
1. Wanachama waanzilishi wa CCJ wapo wangapi?
2. Ulipata kadi ya CCJ lini, wapi na ni namba ngapi?