CCJ kuanza Charm offensive! - Ask your questions!

Mzee, kuna watu wako kwenye sidelines wanasubiri CCJ kipate usajili wa kudumu wajiunge kwa fujo. Naambiwa CCM watabaki wakubwa na wale wanaonufaika!
 
Dada najua tena sana!! Na ndio hofu yangu kwa sababu hata CCM wenyewe wanaombea (wanaweza kusababisha) CCJ isipate usajili wa kudumu on technicality. Mojawapo ya mambo ambayo yamefanyika badala ya kuacha msajili aende tu kufanya uhakika CCJ imepita kila mkoa na kuhakikisha wanachama wake wapo.. Msajili akiwa na nia itamchukua siku kumi tu atatoa usajili wa kudumu.
 
Una cheo chochote ndani ya chama?

Kwa sasa nibakie kuwa ni mwanachama tu sina cheo chochote na sitamani cheo chochote zaidi ya kuwa mpiga prapaganda mkuu (in the tradition of Caville na Rush).

Na itikadi yenu ni ipi?
Kwa sasa nibakie kuwa ni mwanachama tu sina cheo chochote na sitamani cheo chochote zaidi ya kuwa mpiga prapaganda mkuu (in the tradition of Caville na Rush).

Itikadi ni ya mlengo wa kulia, nitafafanua zaidi wiki ijayo: Kwa ufupi:

- Limited but responsible government
- Minimal gvt spending
- promotion of free enterprise
- Self - Reliance
- African Socialism as corrected by the new understanding in economics, social justice
- Rule of law
- Restoration and promotion of founding principles of our nation(among them equality of status, accessibility to wealth and of opportunity, african unity - we are not afraid of Kenyas or Ugandans!, etc)
- Defense of the traditional family
- Absolutely and categorical opposition of all forms of exploitation of man by man!
- Fighting for the rights of workers and peasants of our country to give them opportunity to prosper in the globalized economy.
.. na mengine mengi..

kama uko 99% in tandem na hayo hapo juu consider urself an ideological member!

Samahani kama maswali yamezidi lakini yote haya ni ktk jitihada za kuwajua/ kuwafahamu zaidi. Huwezi jua...mnaweza mkaongeza mwanachama leo....
kama uko 99% in tandem na hayo hapo juu consider urself an ideological member!
 
Itikadi ni ya mlengo wa kulia, nitafafanua zaidi wiki ijayo: Kwa ufupi:

Mpaka hapo swaafi kabisa!

- Limited but responsible government
- Minimal gvt spending
- promotion of free enterprise
That sounds like fiscal conservatism to me...

- Self - Reliance
- African Socialism as corrected by the new understanding in economics, social justice
- Rule of law
- Restoration and promotion of founding principles of our nation(among them equality of status, accessibility to wealth and of opportunity, african unity - we are not afraid of Kenyas or Ugandans!, etc)
This is in line with my social responsibility ideology....

- Defense of the traditional family
- Absolutely and categorical opposition of all forms of exploitation of man by man!
- Fighting for the rights of workers and peasants of our country to give them opportunity to prosper in the globalized economy.
.. na mengine mengi..
I'm sure personal accountability can fit in there somehow....

I am fiscally conservative, socially responsible, and personally accountable.....therefore I'm in (ideologically)...
 
tunataka kuwa a clear alternative to CCM's ideology. Tunataka watanzania wagawanyike si kwa misingi ya "sera" bali kwa misingi itikadi. Itikadi ndio huongoza sera ndio maana utaona leo kina Clegg na Cameron kule UK wamekaa chini kushirikiana huku wakijua tofauti zao za kiitikadi ni kubwa. Kwa hiyo kushirikiana kwao kuna msingi wa sera tu fulani fulani bila kucompromise itikadi zakila chama.
 
Kumbe mkubwa Mwanakijiji ni mwanachama mwanzililshi wa CCj.

Sasa nimepata miwani ya kukusoma vema. Kila la kheri.
 
Kwa sasa nibakie kuwa ni mwanachama tu sina cheo chochote na sitamani cheo chochote zaidi ya kuwa mpiga prapaganda mkuu (in the tradition of Caville na Rush).

Kwa sasa nibakie kuwa ni mwanachama tu sina cheo chochote na sitamani cheo chochote zaidi ya kuwa mpiga prapaganda mkuu (in the tradition of Caville na Rush).

Itikadi ni ya mlengo wa kulia, nitafafanua zaidi wiki ijayo: Kwa ufupi:

- Limited but responsible government
- Minimal gvt spending
- promotion of free enterprise
- Self - Reliance
- African Socialism as corrected by the new understanding in economics, social justice
- Rule of law
- Restoration and promotion of founding principles of our nation(among them equality of status, accessibility to wealth and of opportunity, african unity - we are not afraid of Kenyas or Ugandans!, etc)
- Defense of the traditional family
- Absolutely and categorical opposition of all forms of exploitation of man by man!
- Fighting for the rights of workers and peasants of our country to give them opportunity to prosper in the globalized economy.
.. na mengine mengi..

kama uko 99% in tandem na hayo hapo juu consider urself an ideological member!

kama uko 99% in tandem na hayo hapo juu consider urself an ideological member!

Nadhani itikadi hizi ni nzuri,ni kama za ccm ila mabadiliko kidogo sana,tatizo tulilo nalo si itikadi,bali ni viongozi!
Tukirudi kwenye maswali,nina maswali kadhaa yenye vifungu kadhaa;

1)Nini msimamo wenu CCJ kuhusu mwenendo wa upinzani kwenye siasa zetu Tanzania?kama kuna matatizo,

a)je ni yapi na yanarekebishika?(do you believe in "umoja ni nguvu?")

2) nini msimamo wenu kuhusu baadhi ya viongozi wa upinzani tunao waaminia ie Dr Slaa?

a)Siombei mkose usajili,binafsi kama nikijiunga na chama hicho basi itakuwa ni influence kutoka kwako kwasababu naamini maamuzi yako mara nyingi huwa sahihi ama yenye busara licha ya kwamba wewe bado si mzee kama unavyodhani ama kujiita(Lol!)

However.......Mkikosa usajili,halafu msimamo wenu kuhusu upinzani kama nilivyouliza hapo juu

b)je mtakubali wanachama na wafuasi wenu wakipe chama kingine sapoti,and if so which one?

I hope maswali hayo yanajibika,naomba nianze na haya kwasasa.....Natanguliza shukran!
 
Nimeipenda hii....Kutoka kwa Gender sensitive kuhusiana na mfumo wa vyama vingi and what we're actually practicing...Tafadhali (msisitizo kwenye highlights)mna mpango wa kufanya anything differently? Ama na nyie mnataka kuzitumia sheria hizo hizo kwa manufaa ya CCJ endapo itapewa nchi?Pia kumbuka bado kuna kadhaa hapo juu!

Tangu tupate uhuru hadi leo hatujawahi kuwa na Demokrasia katika maana yake na upana wake, tulikuwa na uongozi au utawala wa chama kimoja. Rais alikuwa na mamlaka yote, chama kilikuwa kinaongoza Serikali kwa mwongozo wa Rais. Huu ulikuwa ni Udikteta namba moja. Bahati tuliyokuwa nayo ni kwamba tulikuwa na Udikteta Mtakatifu. Udikteta huu ulitufaa kiasi chake kwa vile dikteta mwenyewe alitenda kwa manufaa ya wananchi. Huyu alikuwa Baba wa Taifa, hayati mwalimu J.K Nyerere (Mungu amweke mahali pema mbinguni, ampe Heri na Utakatifu).

Mwalimu aliamua na kuelekeza siyo kwa manufaa yake au familia yake au kabila lake, bali kwa manufaa ya watanzania wote. Binadamu wote tunakasoro. Kinachoangaliwa ni makusudio mema japo watekelezaji waweza kupindisha makusudio hayo.Nyerere aliteua Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya, Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu, Gavana wa BoT na viongozi wengine kama hao. Hawa walioteuliwa nao waliteua waliokuwa chini yao hadi ngazi ya tarafa. Huo ndio uliokuwa udikteta mzuri wenye nia njema kadiri ya dikteta.

Utawala wa kiimla ndani ya chama kimoja waweza kuwa mzuri kwani hata Bunge linakuwa moja lenye msimamo mmoja kwa maslahi ya wananchi kwa sababu nalo linapata maelekezo kutoka kwa Waziri Mkuu aliyeteuliwa na dikteta mwema, mwenye kulenga maendeleo na maisha bora ya wananchi wake. Hiyo nayo ni Demokrasia ndani ya chama kimoja.

Kasheshe, songombingo inaanzia pale unapokuwa na Demokrasia ya Vyama Vingi ambako kuna kutokukubaliana na kutofautiana kwa Mtazamo,Malengo na Itikadi lakini mfumo mzima unabakia kama ule ule wa chama kimoja hapo ndipo neno Demokrasia linapokosa maana yake na maendeleo ya nchi yanaanza kurudi mwendo hasi (Development of Underdevelopment).

Rais anachaguliwa kidemokrasia kwa kupigiwa kura na wananchi,baada ya kuingia madarakani Rais huyu anaunda Baraza lake la Mawaziri na kuanza kufanya teuzi mbalimbali kama ifuatavyo;

Rais anateua Msajili wa Vyama Vya Siasa
Rais anateua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.
Rais anateua Wajumbe wa Tume hiyo
Rais anateua Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Rais anateua Jaji Mkuu(Kada wa Siri)
Rais anateua Waziri Mkuu-Mwanachama-Kada
Raisa anateua Majaji-Wanachama
Rais anateua Wakuu wa Mikoa
Rais anateua Wakuu wa Wilaya
Halmashauri za Wilaya zinaajiri Maafisa Watendaji wa Kata-ambao ni wawakilishi wa Mkuu wa Wilaya.

Na Mauteuzi mengine kibao.

Hapo ndipo Udikteta ndani ya Mfumo wa Vyama Vingi unakamilika.Hakuna kushirikisha wananchi.Wananchi wakimchagua kiongozi wao kuwa Mbunge,Rais anamchomoa anakuwa Waziri ,au Naibu Waziri au Mkuu wa Mkoa,Kiongozi huyu anakuwa upande wa Serikali,msemaji wa Serikali na sio mtetezi wa wapiga kura wake kwenye jimbo lake.Timu ya Udikteta inaimarika.

Je tunayo Demokrasia Tanzania kwa muundo huo,Mabalozi wanatusifia nini?Au ndio kwa mgongo wa chupa wanatupaka mafuta waendelee kutupora?

Source: Gender Sensitive "Udikteta kwenye mfumo wa vyama vingi"
 
I guessed this, sitashangaa kusikia wakuuu wengi wa JF wakawa wanachama waanzilishi, maneno yetu hapa si ya bure. For sure naenda kujiunga CCJ.

labda niseme CCJ haihusiani kwa namna yoyote na JF; kila mtu anaingia kwa namna na dhamira yake..
 
Mwanakijiji mtajibu maswali yangu ama no?Naomba unijulishe ili nisiendelee kui flood thread yako......Pia nina swali la nyongeza,vyama vingine vya upinzani huwa havina utaratibu wa kuwataja wafadhili ama wachangiaji wakuu wa chama,nyie msimamo wenu upi?

Ni kweli viongozi wa CCJ wengi wao hawana majina bongo,but who is behind them?kwasababu mafanikio mliyoyapata kwa muda mfupi,pamoja na sera na itikadi za chama,pia gharama za hali ya juu lazima zilihitajika ili muweze kufikia hapo mlipo,kama sera yenu ni kutokutaja waliochangia,basi tuishie hapo,hata hivyo naamini lazima kuna watu ambao ni pro mwalimu wako nyuma yenu, maybe i am wrong, lakini watu kama kina Butiku etc walikuwa wakihusishwa na chama hicho.....If its a right party,then theres also right answers for honest questions,tuwekeane wazi,hatutaki mambo ya fuata upepo tena.
 
Nadhani itikadi hizi ni nzuri,ni kama za ccm ila mabadiliko kidogo sana,tatizo tulilo nalo si itikadi,bali ni viongozi!
Tukirudi kwenye maswali,nina maswali kadhaa yenye vifungu kadhaa;

1)Nini msimamo wenu CCJ kuhusu mwenendo wa upinzani kwenye siasa zetu Tanzania?kama kuna matatizo,

Mwenendo wa upinzani uliopo sasa ni kitu kimojawapo tu kilichochangia kuanzishwa kwa CCJ; Hata hivyo CCJ haikuja ili kutoa nguvu kwa upinzani au kuongeza idadi wapinzani. CCJ imekuja ili iwe mbadala wa kiuongozi kwa taifa.

a)je ni yapi na yanarekebishika?(do you believe in "umoja ni nguvu?")

Umoja ni nguvu kama ni umoja wa msingi; kuna umoja usio na msingi ambao si umoja. Huwezi kuwa na umoja usio na msingi ukawa na nguvu.

2) nini msimamo wenu kuhusu baadhi ya viongozi wa upinzani tunao waaminia ie Dr Slaa?

Naona unaweka msisitizo mkubwa sana kwenye suala la "upinzani". Watanzania wenye uwezo wa kuongoza wapo wengi na haitakuwa haki kuanza kumchagua mmoja na kusema juu yake. Tunatambua mchango wa pekee wa Dr. Slaa na viongozi wengine walio nje ya chama tawala na ndani ya chama tawala ambao wametoa mchango mkubwa katika kuamsha taifa.

a)Siombei mkose usajili,binafsi kama nikijiunga na chama hicho basi itakuwa ni influence kutoka kwako kwasababu naamini maamuzi yako mara nyingi huwa sahihi ama yenye busara licha ya kwamba wewe bado si mzee kama unavyodhani ama kujiita(Lol!)

Kujiunga kusinitegemee mimi au mtu mwingine; kuwe ni kwa sababu ya ushawishi wa uzuri wa itikadi, mantiki ya hoja zetu na mvuto wa mipango yetu ya ujenzi wa taifa. HIvyo, kuwe ni kujiunga kwa sababu umeshawishika CCJ ni chaguo lako kwa sababu inakubaliana na wewe au wewe unakubaliana nayo.

However.......Mkikosa usajili,halafu msimamo wenu kuhusu upinzani kama nilivyouliza hapo juu

Hatutakosa usajili kwa sababu hakuna sababu ya kutunyima.
b)je mtakubali wanachama na wafuasi wenu wakipe chama kingine sapoti,and if so which one?

Sasa hivi tunafikiria CCJ nausajili wa kudumu. Hatufikirii CCM, au chama kingine chochote. Ila kama tutakutana na daraja mbele ya safari tutaamua kama tulivuke au tutafute njia nyingine ya kufika huko tunakotaka kwenda.
 
Mwenendo wa upinzani uliopo sasa ni kitu kimojawapo tu kilichochangia kuanzishwa kwa CCJ; Hata hivyo CCJ haikuja ili kutoa nguvu kwa upinzani au kuongeza idadi wapinzani. CCJ imekuja ili iwe mbadala wa kiuongozi kwa taifa.

Umoja ni nguvu kama ni umoja wa msingi; kuna umoja usio na msingi ambao si umoja. Huwezi kuwa na umoja usio na msingi ukawa na nguvu.

Naona unaweka msisitizo mkubwa sana kwenye suala la "upinzani". Watanzania wenye uwezo wa kuongoza wapo wengi na haitakuwa haki kuanza kumchagua mmoja na kusema juu yake. Tunatambua mchango wa pekee wa Dr. Slaa na viongozi wengine walio nje ya chama tawala na ndani ya chama tawala ambao wametoa mchango mkubwa katika kuamsha taifa.

Kujiunga kusinitegemee mimi au mtu mwingine; kuwe ni kwa sababu ya ushawishi wa uzuri wa itikadi, mantiki ya hoja zetu na mvuto wa mipango yetu ya ujenzi wa taifa. HIvyo, kuwe ni kujiunga kwa sababu umeshawishika CCJ ni chaguo lako kwa sababu inakubaliana na wewe au wewe unakubaliana nayo.

Hatutakosa usajili kwa sababu hakuna sababu ya kutunyima.

Sasa hivi tunafikiria CCJ nausajili wa kudumu. Hatufikirii CCM, au chama kingine chochote. Ila kama tutakutana na daraja mbele ya safari tutaamua kama tulivuke au tutafute njia nyingine ya kufika huko tunakotaka kwenda.

Duh! eee eh!Ama kweli wewe mwanasiasa,nimechoka,nashukuru hata hivyo,ila naomba urejee usemi wako kuwa mna kila sababu ya kupewa usajili,lakini nadhani kuna pahala ulimention something about an order not to register the party.....Na wewe umeignore swali kwenye mojawapo ya postings zangu hapo juu kuhusiana na Raisi kumteua msajili wa vyama,hivi unadhani msajili anaamini kuwa yeye ni mwajiriwa wa wananchi,binafsi naamini ni mwajiriwa wa wananchi lakini indirectly kwa sababu asingeajiriwa na wananchi bila kupata baraka za Rais,na hivyo ni wazi atamsikiliza Rais,kuna wanaodai kuwa chama hiki ni "famba" yani pandikizi la chama tawala,isije ikawa ni gia tu.....

Pia kuhusu Dr Slaa,naomba uelewe kuwa bila mchango wake msingepata wanachama wote hao mlio nao hadi sasa kwasababu wamesaidia sana kuyaweka madudu ya ccm wazi kwa wananchi,hivyo kama mtawasideline mnaweza kugawana kura,naamini mna confidence,jambo ambalo ni muhimu,hata hivyo kutafakari ni vyema pia,na ndilo hasa lengo la swali langu kuhusu "Umoja ni nguvu" jambo ambalo umejibu kwa kusema ni lazima kuwe na misingi ya umoja huo,na umeshasema wazi kuwa "Hamjali kuhusu vyama vingine....Kama kuna misingi inayoweza kuwaunganisha,misingi hiyo ni ipi?
Pia kuhusu "Daraja" unamaanisha daraja kama mtanyimwa usajili?
 
kama uko 99% in tandem na hayo hapo juu consider urself an ideological member!

Je kwa wale wanao kubaliana na hizo itikadi let's say kwa asilimia 70-80....nao vipi? Should they consider themselves ideological members as well? Is the CCJ tent big enough to accomodate a diverse bunch?
 
absolutely.. kuna mambo ya msingi yanayofanya CCJ kuwa CCJ; ukiyakubali yale ya msingi basi yale mengine kuna leeways. Ni sawa sawa na dini fulani hivi kuna mambo ya msingi ya kuyaamini na kutoka hapo mnaweza kuamua kama kupiga magoti au kutopiga magoti, kuvaa hijabu wakati wote au la.. so kuna mambo ya msingi ambayo yataifanya CCJ kuwa tofauti na vyama vingine vyote. Sasa ukiyakubali hayo (core principles) basi mengine we will definitely work with you.. there is enough room for everyone, but for everyone who agrees on the fundamentals of the party.
 
Duh! eee eh!Ama kweli wewe mwanasiasa,nimechoka,nashukuru hata hivyo,ila naomba urejee usemi wako kuwa mna kila sababu ya kupewa usajili,lakini nadhani kuna pahala ulimention something about an order not to register the party.....Na wewe umeignore swali kwenye mojawapo ya postings zangu hapo juu kuhusiana na Raisi kumteua msajili wa vyama,hivi unadhani msajili anaamini kuwa yeye ni mwajiriwa wa wananchi,binafsi naamini ni mwajiriwa wa wananchi lakini indirectly kwa sababu asingeajiriwa na wananchi bila kupata baraka za Rais,na hivyo ni wazi atamsikiliza Rais,kuna wanaodai kuwa chama hiki ni "famba" yani pandikizi la chama tawala,isije ikawa ni gia tu.....

kwa kweli siwezi kuzungumzia hisia za mtu mwingine.. sijui yeye Tendwa anajichukuliaje.

Pia kuhusu Dr Slaa,naomba uelewe kuwa bila mchango wake msingepata wanachama wote hao mlio nao hadi sasa kwasababu wamesaidia sana kuyaweka madudu ya ccm wazi kwa wananchi,

I will not claim that with such an absolute certainty.

hivyo kama mtawasideline mnaweza kugawana kura,naamini mna confidence,jambo ambalo ni muhimu,hata hivyo kutafakari ni vyema pia,na ndilo hasa lengo la swali langu kuhusu "Umoja ni nguvu" jambo ambalo umejibu kwa kusema ni lazima kuwe na misingi ya umoja huo,na umeshasema wazi kuwa "Hamjali kuhusu vyama vingine....Kama kuna misingi inayoweza kuwaunganisha,misingi hiyo ni ipi?

Well.. ipo misingi na ni misingi ya kiitikadi.

Pia kuhusu "Daraja" unamaanisha daraja kama mtanyimwa usajili?

yep
 
Back
Top Bottom