CCJ kuanza Charm offensive! - Ask your questions!

Miaka 18 baada ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa bado watu wako busy kujisajili na CCM na sio vyama vingine vya upinzani, kwanini?je kuna dalili za vyama vya upinzani kujirekebisha ili kuondokana na hali hiyo? na je tukate tamaa kwa kuwa hakuna muelekeo wa kuiangusha CCM kwa sasa?...la hasha.

Tusiwasingizie wananchi katika hili, wananchi wapo tayari na wana hamu ya mabadiliko lakini vyama vya upinzani havijafanya vya kutosha kuweza kuchukua matarajio ya wananchi hawa na kuwajengea imani kuwa nchi itakuwa bora zaidi na salama mikononi mwao.

jamani hadi sasa CCJ imeshakusanya wanachama elfu 20! Hii ni kabla ya usajili wa kudumu na kabla ya uhamasishaji mwingine. Baadhi ya hawa wanatoka kwenye vyama vingine na wengine kwa mamia wanakuja wakiwa hawana chama bali sasa hatimaye wamepata chama ambacho kinaendana na hisia na matamanio yako kama Watanzania. Wapo wanaojiunga CCM, wapo wanaojiunga CHadema na CUF na wapo wanaojiunga na watakaojiunga na CCJ. Ndio uzuri wa demokrasia.
 
Chama cha mwamko mpya wa ujenzi wa taifa CCJ kinaanza harakati za kukutana na kuzungumza na wananchi katika kujitambulisha zaidi kwa wananchi wakati kinaendelea kusubiri usajili wa kudumu. Hadi hivi sasa maelfu ya Watanzania wameamua kujiunga na chama hiki ambacho hakina "jina kubwa" na ambacho viongozi wake "hawana majina makubwa" katika medani za siasa nchini.

Katika siku chache zijazo CCJ itapita kusalimiana na kukutana (meet and greet tour) wananchi katika sehemu mbalimbali za Tanzania Bara na Visiwani.

Yawezekana una maswali mengi kuhusu CCJ ni yapi hasa na ungependa hasa kujua nini?

Kawaida hatuzungumzii mimba isipokuwa mtoto,hivyo hao Chukua Chako Jikate(Jiondoe) hawana mvuto hadi watapopata usajili wa kudumu!
 
jamani hadi sasa CCJ imeshakusanya wanachama elfu 20! Hii ni kabla ya usajili wa kudumu na kabla ya uhamasishaji mwingine. Baadhi ya hawa wanatoka kwenye vyama vingine na wengine kwa mamia wanakuja wakiwa hawana chama bali sasa hatimaye wamepata chama ambacho kinaendana na hisia na matamanio yako kama Watanzania. Wapo wanaojiunga CCM, wapo wanaojiunga CHadema na CUF na wapo wanaojiunga na watakaojiunga na CCJ. Ndio uzuri wa demokrasia.

I agree.

Lakini Itikadi peke yake haitoshi, ili CCJ iweze kuishi kwenye matarajio ya wafuasi wake na kisha kupenya katika mioyo ya Watanzania inapaswa pia kujifunza katika makosa ya NCCR-MAGEUZI, CUF na CHADEMA ili kuweza kuleta upinzani wa maana katika nchi hii ambao umeshindikana ata baada ya miaka 18 ya vyama vingi.
 
mimi sidhani kama mpinzani wa kweli wa CCM ameshapatikana, watanzania bado tuna chakura chakura kwenye pakacha, vyama viletwe tu tupate uwanja mpana zaidi wa kuchagua, upinzani wa kweli na nia ya kuongoza nchi hii utaonekana baada ya uchaguzi na sio wakati wa kuomba kura. chama bora cha upinzani kitakapopatikana wote wenye moyo wa kweli wa upinzani watajiunga nacho. watanzania wengi bado wana 'have a bite and spit out', nothing yet to swallow
 
HAYA WALE WA 2010 jitayarisheni kwenye majukwaa ya siasa , kwani wakati huo ndio pekee waheshimiwa wanakuwa na adabu uchaguzi ukipita tuu wote mnageuzwa mizigo na kutukanwa kwenye kila hotuba za walioshinda sijui nchi yetu na wananchi wetu nini wamepungukiwa?

wanasiasa wanatakiwa wajue kwamba hakuna ukombozi wa kweli pasipo jamii moja kujuta kati ya watawala na watawaliwa
 
Kawaida hatuzungumzii mimba isipokuwa mtoto,hivyo hao Chukua Chako Jikate(Jiondoe) hawana mvuto hadi watapopata usajili wa kudumu!

tatizo wengine wameshahukumu hiyo mimba kuwa si mimba bali matambara tu! si wasubiri mama ajifungue kwanza. Watu wanakaa kusubiria wakafyeke katoto ketu kwa sababu kanakuja kutimiza unabii!
 
I agree.

Lakini Itikadi peke yake haitoshi, ili CCJ iweze kuishi kwenye matarajio ya wafuasi wake na kisha kupenya katika mioyo ya Watanzania inapaswa pia kujifunza katika makosa ya NCCR-MAGEUZI, CUF na CHADEMA ili kuweza kuleta upinzani wa maana katika nchi hii ambao umeshindikana ata baada ya miaka 18 ya vyama vingi.

bado mnafikiria in terms of upinzani wa zamani; we don't. Siku mpya, fikra mpya!
 
mimi sidhani kama mpinzani wa kweli wa CCM ameshapatikana, watanzania bado tuna chakura chakura kwenye pakacha, vyama viletwe tu tupate uwanja mpana zaidi wa kuchagua, upinzani wa kweli na nia ya kuongoza nchi hii utaonekana baada ya uchaguzi na sio wakati wa kuomba kura. chama bora cha upinzani kitakapopatikana wote wenye moyo wa kweli wa upinzani watajiunga nacho. watanzania wengi bado wana 'have a bite and spit out', nothing yet to swallow

bado mnafikiria mambo ya upinzani.. get over this mentality.. please do.
 
Swali:

Chama hiki kuanzishwa au kuota kama uyoga kipindi hiki cha Uchaguzi, je ni coincidence au ndio yale yale...? Pili nawasifia sana kwa kuchagua jina zuri lakini zaidi ya hapo... aaah... labda tutaona ilani ya uchaguzi!

Nawatakia kila la kheri maana kwa sasa hakuna kimbilio,,, kimbilio lilikuwa CHADEMA lakini ubinafsi umewafanya wote wanataka kuwa wabunge... kwa maana kila mmoja atakuwa busy na wapiga kura wake... Chama kitakuwepo tu kama mbeleko.
 
Natamani watanzania waelewe kuwa hakuna wakuwaletea mabadiliko ila kwakila mmoja anaetaka mabadiliko kubadilika yeye kwanza.

Kwasababu hiyo CCJ inatoa opportunity kwa wale wote wapenda mabadiliko kabla haijawa jinsi tusivyopenda iwe; hivyo ni jukumu la kila mmoja mwenye mapenzi mema kusimama kwa zamu yake kuhakikisha CCJ inakuwa jinsi tunavyotaka iwe...Dont wait for others, join now make the lead and others will follow!

Mi ni mwanachama wa CCJ kwa itikadi na si kwa kadi and soon will lead for others to follow! I will stand at my watch to make sure CCJ becomes the party I dream to lead my country for the best of myself and of others!
 
Yaani, CCM wametupa kweli wajinga sisi watanzania!! Ili kuiondoa CCM lazima kuwe na chama kimoja tu cha upinzani ambacho itikadi yake ni ANTI_CCM, that is it. Huu mlongolo kila mtu kuanzisha chama chake ni ujinga wa hali ya juu, sasa utaishinda vipi ccm?? ooh mimi sipendi bia, chama cha wasiopenda bia, mimi sili nyama :: chama cha wasiokula nyama, blah blah. Kwenye hizi nchi zenye democracy ya ukweli at most kuna vyama vya siasa 3, lakini sisi Tanzania tuna zaidi ya 10.

Yaani kazi kweli kweli
 
Natamani watanzania waelewe kuwa hakuna wakuwaletea mabadiliko ila kwakila mmoja anaetaka mabadiliko kubadilika yeye kwanza.

Kwasababu hiyo CCJ inatoa opportunity kwa wale wote wapenda mabadiliko kabla haijawa jinsi tusivyopenda iwe; hivyo ni jukumu la kila mmoja mwenye mapenzi mema kusimama kwa zamu yake kuhakikisha CCJ inakuwa jinsi tunavyotaka iwe...Dont wait for others, join now make the lead and others will follow!

Mi ni mwanachama wa CCJ kwa itikadi na si kwa kadi and soon will lead for others to follow! I will stand at my watch to make sure CCJ becomes the party I dream to lead my country for the best of myself and of others!
ms Felister,kwangu mimi ni mfuasi wa itikadi zao,na nilishaweka hapo nyuma kuwa itikadi zao zinaelekea kuturudisha excactly at the point we were supossed to better ourselves from from poverty and so forth,and what failed us was and still are the leaders!
Its good that you drem to lead your country,hizo ni lugha nzuri tu za kimwamko,lakini hakuna jipya,ukishamchagua kiongozi you dont lead enimore and the dream is dead if not becoming a nightmare!

Tunapokuja sasa hapo kwenye leading,tunaambiwa kuwa viongozi wao hao ni wapya,sawa hilo liko wazi,lakini amin nakwambia kama wale wazalendo wengine wa kweli ambao wananchi wanawakubali hawaingii humo,sidhani kama wengi wetu wako tayari kugamble,Hata Obama mwenyewe kama si democratic party asingeshinda no matter what kind of a party he wouldve formulated! Na pia wengi waliweka imani baada ya watu kama marehem Kennedy na wengi wenye influence kubwa kwenye majority ya wanajamii wa kawaida (ambao kwa kweli they wanted something new or changes no matter what)endorsements matters no matter what ya'll say,Obama alikuwa endorsed na watu ambao walikuwa wakipewa heshma ya kuwa "watu wa watu" wenye kupigania maslahi ya jamii in a vast scope!

Mi bado nasuburia,kama ni kweli chama kinafuta "Misingi" ya kweli ikiwa ni pamoja na kuanzia kwa kurekebisha pale tulipokwama ndo solution,itikadi za chama hiki zenye kufanana na za TANU,zinzonyesha ni zile za kuturudisha kwenye msitari,hivyo ni lazima tuanze na wale waliokuwa wakipinga ufisadi toka enzi na enzi,ambao bado wapo,na wanaheshimika na watu wa kawaida kwa ujumla,yani masikini walio wengi,na kuchanganya na wale wa kizazi kipya kama wapo ie kina Renatus Muhabi na wenzake,inavyoonekana ndio hao viongozi wa ccj,ni lazima tuwaone hao watakaojitoa zaidi ya Mpendazoe,then we'll go from there,i dont really believe there's such a thing as "Brandnewey" in dis game.
 
Nyani Ngabu usijidai eti ulikuwa hujui kirefu cha CJJ,all the details ulizonazo ambazo mwananchama mwanzilishi anakubaliana na wewe mnaonyesha biasness hapa,ndivyo mlivyo,Huwezi kuleta propaganda hapa JF,JF ni kipimo cha the highest level of all kinds and ways of thinking!Sikuchagulii cha kuuliza dont get mi wrong!Lakini based on your previous postings,kama ni kweli ulikuwa hujui maana ama kirefu cha ccj,basi lingekuwa swali lako la kwanza....Yale yale tu!Ndivyo mlivyo!

CHADEMA wa JF naona wamechukia kweli kweli, CCJ inawanyima nafasi ya kupata ulaji.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu mawazo yako ni ya KIBINAFSI.. yaani unaonyesha wazi kwamba unachoamini wewe hata kama ni kinyume basi sawa tu hali wakati huo huo unatumainia ushindi pasipo kuunganisha nguvu... Hii haiingii akilini hata kidogo. Maelezo yako kwa ujumla hayana tofauti na ile hotuba ya JK alipowaambia wafanyakazi kwamba - Haitaji kura zao.. jambo ambalo limetupa picha kwamba JK anafikiri anaweza kushinda pasipo kura za wafanyakazi. Fikra hizi tu zinaweza kumgharimu sana kinyume na matajario yake.

Mkuu mara zote kauli ya mtu ndio humfunga ktk matendo yake, hivyo unaposema CCJ hawana sababu ya kuungana na vyama vingine kwa sababu za Kiitikadi, malengo na kadhalika inanipa wasiwasi mkubwa zaidi kwa sababu nimeisoma katiba ya CCJ na hakuna jipya.. CCJ imeundwa kutokana na matokeo ya Uongozi mbovu aambao wote hawa wameutumikia kwa zaidi ya miaka 26 muda mrefu zaidi ya Utawala mzima wa Nyerere. Hawa watu walikuwa viongozi ngazi za juu kwa miaka yote 26 wasione sababu ama umuhimu wa Upinzani kwamiaka yote 26 ila tu baada ya kuingia JK ndipo tunawaona wakisimama.
Kifupi hawa naweza kuwaita ni wana MAPINDUZI, CCJ ni chama kinachotaka kupindua CCM kwa amani lakini ni kizazi kile kile kilichotufikisha hapa tulipo leo. Mabaya yote wanayoyaona leo CCM ni mabaya ambayo vyamavingine vimeyaona miaka zaidi ya 15 iliyopita wakati wao hawaoni makosa haya. Leo ujio wao uyaone makosa yote ya Upinzani kisha basi badala ya wao kuyarekeebisha ili ushindi upatikane wanachukua jukumu hilo wao wenyewe kwa matumaini kwamba sisi wananchi tutawaamini kwa sababu tu wanatumia jina la Mwalimu Nyerere.

Hapana mkuu wangu... CCJ wakiwa viongozi ndani ya CCM wamepiga kura nyingi sana dhidi ya miradi ambayo imetuingiza ktk hasara. Walikuwa moja ya sababu kubwa ya bunge letu kupitisha sheria ambazo zimetufikisha hapa. walikuwa wajumbe wa mkutano ulopitisha Azimio la Zanzibar na kuliua Azimio la Arusha hali wakidai Azimio hilo halikufa. Na wakayapokea MAFISADI ndani ya chama wakijua fika kwamba chama kinapoteza mrengol lakini hawakutoka. Sasa iweje leo hawa watu waje hapa kutuhakikishia ushindi hali wakijitenga na kutohitaji nguvu ya wanamapinduzi wengine waliowatangulia.

Mkuu wangu nimekwambia wazi kabisa kwamba Hata Zimbabwe ambao walikuwa na uhasama mkubwa wa kikabila na chuki ya jadi. Iliwachukua Kuungana kwa nguvu zao kuweza kumshinda Kaburu Ian Smith. Huko South pamojana upinzani mkubwa wa kiitikadi baina ya ANC na PAC walikuja unganisha nguvu zao kumlazimisha Kaburu kuachana na Apartheid. Uhuru wa Msumbiji na kadhalika, hizi zote ndizo hekima za Mwalimu Nyerere alizotuonyesha ama kutuachia kwamba ni lazima tuondoe tofauti zetu tunapomkabiri adui mmoja. Maswala mengine ya kiitikadi yatafuata baada ya ushindi na kubomoa nguzo au kuta za Berlin (katiba, sheria na taratibu za Kiutawala).

Kinyume cha kufanya hivyo ni kukataa wazi hekima za mwalimu lakini bado mkitumia jina lake kwa faida yenu..Ikiwa ushindi ni LAZIMA basi shurti mkubali ukweli kwamba Umoja ni nguvu na utengano ni Udhaifu.. mkikataa haya binafsi sioni sababu kabisa ya chama hiki CCJ kutumia jina la Mwalimu hali msingi mkubwa wa itikadi yoyote ni kuwaunganisha watu dhidi ya utawala dhalimu.
 
CHADEMA wa JF naona wamechukia kweli kweli, CCJ inawanyima nafasi ya kupata ulaji.

Subiri muda si mrefu utaniita ccj wa jf,kuhusiana na hisia hapa sasa ndo tafsiri halisi!Sina chama na sijawahi kuwa na chama,wewe ni mswazi tu nawajua,chadema nao wapuuzi wameshindwa kujua adui yao mkubwa ni waswahilii!wangefanya marekeisho na kuondokana na hizo tuhuma za ukabila ambazo kwangu zina amount to matusi,wengi hapa JF "Hamnazo" pengine kizazi kipya wasipenda kujisomea ama kufanya utafiti na kujua tulikotoka,hakuna vita dhidi ya ukabila tena,waswazi bana,washatuharibia nchi!
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu mawazo yako ni ya KIBINAFSI.. yaani unaonyesha wazi kwamba unachoamini wewe hata kama ni kinyume basi sawa tu hali wakati huo huo unatumainia ushindi pasipo kuunganisha nguvu... Hii haiingii akilini hata kidogo. Maelezo yako kwa ujumla hayana tofauti na ile hotuba ya JK alipowaambia wafanyakazi kwamba - Haitaji kura zao.. jambo ambalo limetupa picha kwamba anaweza kushinda pasipo kura za wafanyakazi.

Mkuu mara zote kauli ya mtu ndio humfunga ktk matendo yake, hivyo unaposema CCJ hawana sababu ya kuungana na vyama vingine kwa sababu za Kiitikadi, malengo na kadhalika inanipa wasiwasi mkubwa zaidi kwa sababu nimeisoma katiba ya CCJ na hakuna jipya.. CCJ imeundwa kutokana na matokeo ya Uongozi mbovu aambao wote hawa wameutumikia kwa zaidi ya miaka 26 muda mrefu zaidi ya Utawala mzima wa Nyerere. Hawa watu walikuwa viongozi ngazi za juu kwa miaka yote 26 wasione sababu ama umuhimu wa Upinzani kwamiaka yote 26 ila tu baada ya kuingia JK ndipo tunawaona wakisimama.
Kifupi hawa naweza kuwaita ni wana MAPINDUZI, CCJ ni chama kinachotaka kupindua CCM kwa amani lakini ni kizazi kile kile kilichotufikisha hapa tulipo leo. Mabaya yote wanayoyaona leo CCM ni mabaya ambayo vyamavingine vimeyaona miaka zaidi ya 15 iliyopita wakati wao hawaoni makosa haya. Leo ujio wao uyaone makosa yote ya Upinzani kisha basi badala ya wao kuyarekeebisha ili ushindi upatikane wanachukua jukumu hilo wao wenyewe kwa matumaini kwamba sisi wananchi tutawaamini kwa sababu tu wanatumia jina la Mwalimu Nyerere.

Hapana mkuu wangu... CCJ wakiwa viongozi ndani ya CCM wamepiga kura nyingi sana dhidi ya miradi ambayo imetuingiza ktk hasara. Walikuwa moja ya sababu kubwa ya bunge letu kupitisha sheria ambazo zimetufikisha hapa. walikuwa wajumbe wa mkutano ulopitisha Azimio la Zanzibar na kuliua Azimio la Arusha hali wakidai Azimio hilo halikufa. Na wakayapokea MAFISADI ndani ya chama wakijua fika kwamba chama kinapoteza mrengol lakini hawakutoka. Sasa iweje leo hawa watu waje hapa kutuhakikishia ushindi hali wakijitenga na kutohitaji nguvu ya wanamapinduzi wengine waliowatangulia.

Mkuu wangu nimekwambia wazi kabisa kwamba Hata Zimbabwe ambao walikuwa na uhasama mkubwa wa kikabila na chuki ya jadi. Iliwachukua Kuungana kwa nguvu zao kuweza kumshinda Kaburu Ian Smith. Huko South pamojana upinzani mkubwa wa kiitikadi baina ya ANC na PAC walikuja unganisha nguvu zao kumlazimisha Kaburu kuachana na Apartheid. Uhuru wa Msumbiji na kadhalika, hizi zote ndizo hekima za Mwalimu Nyerere alizotuonyesha ama kutuachia kwamba ni lazima tuondoe tofauti zetu tunapomkabiri adui mmoja. Maswala mengine ya kiitikadi yatafuata baada ya ushindi na kubomoa nguzo au kuta za Berlin (katiba, sheria na taratibu za Kiutawala).

Kinyume cha kufanya hivyo ni kukataa wazi hekima za mwalimu lakini bado mkitumia jina lake kwa faida yenu..Ikiwa ushindi ni LAZIMA basi shurti mkubali ukweli kwamba Umoja ni nguvu na utengano ni Udhaifu.. mkikataa haya binafsi sioni sababu kabisa ya chama hiki CCJ kutumia jina la Mwalimu hali msingi mkubwa wa itikadi yoyote ni kuwaunganisha watu dhidi ya utawala dhalimu.

Umesema,they sometimes call dat arrongancy,i hope it aint "false pretence of a sense of well being" kinda "euphoria and or illusionism?"
 
Back
Top Bottom