Mzee Mwanakijiji,
Kwa kuongezea tu nitakupa ukweli ambao wengi hatupendi kuuweka maanani leo hii. Waislaam waliutaka Uhuru wa Tanzania mapema lakini wasingeweza kufanikiwa pasipo support ya Wakristu. Ndipo walipokuja na plan ya kuwavuta Wakristu na mwalimu akapewa Uenyekiti.
Pamoja na tofauti za kiimani, itikadi na malezi yao mwalimu alipokea kitu kicho akiwa pia na nia moja tu - kumwondoa mkoloni kwanza. Mwalimu aliweza kuwatumia waislaam na Wakristu kwa pamoja (umoja wao) kuleta Uhuru na kisha kuleta itikadi zake za Ujamaa na Kujitegemea, jambo ambalo kina Marealle na Mtenvu walishindwa kuliona - We should learn from Him..
.
Mkandara, nimekusoma muda mrefu unavyojaribu ku-inject sense ya 'umoja ni nguvu' into Mwanakijiji's head and it doesn't sink. Naomba usikate tamaa, ila hili la vyama kutoshirikiana ni tatizo ambalo hata mimi nimekuwa nikiliona kwa muda mrefu na kulinyamazia.
Kwa vile hawa viongozi wa upinzani ni wenzeni, tunakutana nao kila siku kwenye social interactions za hapa na pale, naomba try as much as you can to sink this into their hard heads kuwa yoyote kati yao, hawezi bila ya kuwashirikisha wengine.
Kati ya majimbo 9 ya uchaguzi mkoani Kilimanjaro, CCM ina walk over majimbo matatu tuu mawili kati yake ni ya Upareni. Majimbo sita yaliyobakia, CCM imeshinda 5 na Chadema 1. Majimbo yote hayo matano, CCM imeshinda less than 50% wapinzani wamezigawa kura za upinzani hali iliyopelekea CCM kuibuka kidedea. Mfano Moshi Vijijini, CCM imeshinda kwa only 27% na Chadema, NCCR na TLP wakagawana 73%. Hawa wasipokubaliana tena, CCM itashinda hivyo hivyo, only Jimbo la Ndesa, CCM haiwezi kushinda hata kwa dawa, labda kama wata dhikr ...bila nguo.
Kwenye pita pita zangu na kutana kutana na hawa wanasiasa, nimekuwa siku zote nikiwauliza hili viongozi wa vyama, Lipumba analielewa, ila kwenye CUF, Lipumba hana kitu zaidi ya Baraghashia yake, realy powes lies with Seif, ambao muungano wa wapinzani kwake hauna maslahi yoyote.
Dr. Slaa anasema hatuwezi kushirikiana na vyama mamluki, wao wanaushahidi kuna viongozi wakuu wa vyama wako kwenye payroll ya CCM.
Watu pekee wenye matumaini ni viongozi vijana kama Zitto na Jussa, hili wameliona na wamelikubali, tatizo ni wakuu wa vyama vyao sijui kamma watalielewa.
Kwa vile mimi binafsi sio mwanachama wa chama chochote ila ni mshabiki wa demokrasia ya kweli, nadhani umefikia wakati to play more active role. If there is anything anybody can do to inject the sense of 'united we stand', or 'together we can' kwa spirit ya 'umoja ni nguvu', uchaguzi wa mwaka huu, hata kama hawatachukua nchi, ila CCM wataitikisa na bungeni kwa wingi watatinga.