CAG: Mradi wa Umeme wa Bwawa la Nyerere unatumia upembuzi wa mwaka 1970

Kila mwenye akili timamu na uwezo wa kufikiria alikuwa anajua kabisa hii Nchi ilikuwa inapigwa sana kipindi cha JPM, na kwa vile alikuwa anajiona yeye bora hakuwa radhi watu waseme madhaifu ya watu wake, hapo ndipo tatizo lilipokolea, angeshika hii Nchi kwa miaka 10 tungekuwa na hali mbaya sana.
 
CAG : Mradi wa umeme bwawa la Nyerere unatumia upembuzi wa mwaka 1970​

Thursday April 08 2021​

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limeshindwa kuhuisha vipengele vyote vya upembuzi yakinifu uliofanyika awali katika ujenzi wa mradi wa umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP), imeeleza ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali.

By Elias Msuya
More by this Author

IN SUMMARY​

Advertisement
Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limeshindwa kuhuisha vipengele vyote vya upembuzi yakinifu uliofanyika awali katika ujenzi wa mradi wa umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP), imeeleza ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG).
Badala yake ripoti hiyo ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 2020 imesema Tanesco lilitegemea upembuzi yakinifu ambao ulifanywa katika miaka ya 1970 na 1972 na kampuni ya M/S Norconsult ya Norway.
Pia shirika hilo linatumia mpango mtambuka wa mradi na ripoti ya uchunguzi wa kiufundi uliofanywa na kampuni ya M/S Hafslund na M/s Norplan pia kutoka Norway ambayo ilihuisha vipengele vya taarifa ya upembuzi yakinifu miaka ya 1980.
“Vipengele ambavyo havikufanyiwa mapitio na kuhuishwa ni pamoja na utafiti wa kiuchumi na kifedha wa mradi, tafiti za kuwepo kwa maji na uendeshaji endelevu wa mradi,” imesema ripoti hiyo.
Ripoti hiyo imesema maofisa waandamizi wa Tanesco waliozungumza na CAG walieleza kwamba, upembuzi yakinifu uliofanyika katika miaka ya 1970 ulionesha kwamba mradi unawezekana kitaalamu, kiuchumi na kifedha.
“Maofisa waliongeza kuwa kutokana na uharaka wa kuanza utekelezaji wa mradi, taarifa za upembuzi za awali hazikuweza kupitiwa upya zote ili kuzihuisha,” inaeleza.
Ripoti hiyo imesema kuhuishwa huko kwa upembuzi kunatakiwa kwa mujibu wa Sheria ya Umeme ya mwaka 2008, Sheria ya Umwagiliaji ya Kitaifa ya mwaka 2013, Sheria za Usimamizi ya Vyanzo vya Maji ya mwaka 2009 na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya 2004.
Wapi imeonekana kuna wizi au ufisadi kwenye huu mradi?
 
Sasa wewe ulitaka uendelee kufanya kazi serikalini na cheti cha kufoji? Punguza jazba brother kaka ndio imeshakula kwako hvyo!

Nimeanza sasa PhD yangu hivyo kama Cbuo Kikuu huwa wanapokea Vyeti Feki ( vya Kufoji ) wakati Vyeti vyangu vya Vyuo Vikuu vyote Viwili ( vinavyotambuliwa na Serikali ) nilivyosoma Kihalali vipo na Kumaliza vyema kabisa basi sawa.
 
ufisadi sio kuiba pesa za umma tu. hata kutumia vibaya Kodi na rasilimali za umma ni ufisadi, kwa akili ndogo tu unaweza kujenga ikulu nyingine ya bilioni 500 na ushehe huku wanafunzi wanakosa vyoo na madarasa?
 
Hii inaonesha kuwa upembuzi yakinifu Wa mwaka 1972 bado haujapitwa na wakati!! Si mnaona mradi unaendelea vizuri! Si kila kitu huwa kinapitwa na wakati!! Hata Newton laws of motion hazijapitwa na wakati hadi leo!! Inaonekana wazi Kabisa kuwa upembuzi yakinifu ulikuwa projected kwa miaka mingi ya mbele!
Wapigaji walitaka upembuzi yakinifu mwingine ufanyike ili wapige pesa tena!! Upembuzi yakinifu wa mradi kama ule ungechukua muda usiopungua miaka miwili!! Mafisadi wana hasira walikoseshwa ulaji!! "We are watching".
Elewa kuwa nilikuwa na budget ya upembuzi mpya, ilitumikaje? Au unawaza maandishi tu kuwa ni ya mwaka 40 au current?
 
Nchi ilikuwa inaendeshwa kwa utashi was MTU sheria zooote ziliwekwa pending!!
Kwa taratibu za kifedha karibu miradi yooote ya stoni itakuwa nje ya utaratibu!!
Kunahaja serikali yooote ijiuzulu tufanye uchaguzi upyaaa!! Stone hakushauriwa vyema na makamu wake,waziri mkuu,spika,bunge,chama nk.
Kama walijua hashauriki kwanini walituletea kama mgombea na wakawa wanamsifu kila dakika??
Kistaarabu serikali yooote ijiuzulu tuchague upya asisingiziwe MTU mmoja asiyeweza kurudi kuitetea!!!
  • bandari hovyo
  • atcl hovyo
  • utalii hovyo
  • mawasiliano hovyo
  • elimu hovyo
  • afya hovyo
  • demokrasia hovyo
Embu serikali istep down kidogo turudie uchaguzi maana Samoa alisema stone alikuwa mwalimu wake sasa kama mwalimu kaharibu hivi mwanafunzi wake je??
Tena ukileta independent auditing firm ndiyo kutakuwa na hatari zaidi
 
Thursday April 08 2021​

By Elias Msuya

IN SUMMARY​

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limeshindwa kuhuisha vipengele vyote vya upembuzi yakinifu uliofanyika awali katika ujenzi wa
Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limeshindwa kuhuisha vipengele vyote vya upembuzi yakinifu uliofanyika awali katika ujenzi wa mradi wa umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP), imeeleza ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG).

Badala yake ripoti hiyo ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 2020 imesema Tanesco lilitegemea upembuzi yakinifu ambao ulifanywa katika miaka ya 1970 na 1972 na kampuni ya M/S Norconsult ya Norway.

Pia shirika hilo linatumia mpango mtambuka wa mradi na ripoti ya uchunguzi wa kiufundi uliofanywa na kampuni ya M/S Hafslund na M/s Norplan pia kutoka Norway ambayo ilihuisha vipengele vya taarifa ya upembuzi yakinifu miaka ya 1980.

“Vipengele ambavyo havikufanyiwa mapitio na kuhuishwa ni pamoja na utafiti wa kiuchumi na kifedha wa mradi, tafiti za kuwepo kwa maji na uendeshaji endelevu wa mradi,” imesema ripoti hiyo.

Ripoti hiyo imesema maofisa waandamizi wa Tanesco waliozungumza na CAG walieleza kwamba, upembuzi yakinifu uliofanyika katika miaka ya 1970 ulionesha kwamba mradi unawezekana kitaalamu, kiuchumi na kifedha.

“Maofisa waliongeza kuwa kutokana na uharaka wa kuanza utekelezaji wa mradi, taarifa za upembuzi za awali hazikuweza kupitiwa upya zote ili kuzihuisha,” inaeleza.

Ripoti hiyo imesema kuhuishwa huko kwa upembuzi kunatakiwa kwa mujibu wa Sheria ya Umeme ya mwaka 2008, Sheria ya Umwagiliaji ya Kitaifa ya mwaka 2013, Sheria za Usimamizi ya Vyanzo vya Maji ya mwaka 2009 na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya 2004.

Mwananchi
Huu mradi utatulipukia. Tofauti na walivyosema hao maofisa waandamizi, washauri waliona huu mradi hautalipa kutokana na uharibifu wa mazingira ( kukata miti, athari katika Rufiji Delta). Aidha, bwawa litajaa matope mapema sana. Ndio maana miaka yote hii hakujitokeza mtu kuufadhili au kuwekeza. Ni tembo mweupe.

Amandla...
 
Ilani ya ccm 2020 - 2025 inasema tutaendelea kupambana na rushwa na ufisadi kwa nguvu zote.

Haisemi ufisadi umeisha.

Hata Ulaya kina Morinyo, Messi, Ronaldo mara kwa mara tunasikia aamepelekwa mahakamani kwa kukwepa kodi.

Hata Chadema wabunge wengi walihama mwaka jana sababu ya ufisadi michango yao. Kinachotakiwa ni kuendelea kupambana na ufisadi
Hiyo ya Chadema unawasingizia. CAG kapitia na kupitisha mahesabu yao. Baada ya wale wakina mama na Lijualikali kumwaga sumu bungeni, Takukuru nae akasema atapitia na mpaka leo yuko kimya. Hao wabunge walihama kwa maslahi yao binafsi na sio ufisadi wa michango yao.

Amandla...
 
Back
Top Bottom