Business Partner Anahitajika Katika Upanuzi wa uzalishaji Sabuni za ngozi na Mafuta Ya Nywele

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
1,195
1,661
1686125698492.png

NATURAL SKIN SOLUTION
IMANI YETU
Tunaamini kazi kubwa ya msimamizi wa biashara (CEO) ni kuunganisha sera, mipango , rasilimali pamoja na miundombinu kuhakikisha biashara inapata faida kubwa kwa kadri inavyowezekana
Katika kufikia lengo hili , CEO atajikita kufanya maamuzi ya aina mbili;
Moja: Kupanga ,yaani kutumia nguvu kulivuta kila lenye maslahi na biashara
Mbili: Kupangua,yaani kuliweka mbali na biashara kila linalotishia faida

MTINDO WA UONGOZI
Tunaamini kadri biashara inavyokua, tunahitaji kuchuja kazi za kipaumbele za kuzalisha kipato (IGA) na kazi za kutoingiza kipato moja kwa moja. Na uzoefu unaonesha ni 20% ya shughuli za kipaumbele ikiwemo kutoa ushauri kwa wateja na 80% ya shughuli za kutoingiza kipato ikiwemo kukusanya malighafi n.k , mtindo hujulikanao kama (80/20).
Na sasa ...

Tunamshukuru Mola tumeweza kwa muda wa miaka 5 kuzalisha na kusambaza mikoani bidhaa 5 za ngozi na nywele. Sasa wingi wa oda kwa mawakala wa mikoani, unafanya tushindwe kuwahudumia kwa wakati kwa upungufu wa mtaji.
Tumeweza zalisha bidhaa 5 ambazo ni
1.Udongo tiba
2. Sabuni za udongo
3.Lotion
4. Mafuta ya Nywele
5. Shampoo
Hivyo nahitaji Partner mpya aangalie ramani ya biashara , vipi atawekeza,vipi atapata faida za kifedha na za uwezo wa kibiashara. Partners wasizidi 2 kwa kuanzia ili uendeshaji uwe rahisi na kiasi cha uwekezaji kwa partner mmoja kianzie milioni mbili na kisizidi milioni tano kwa kipindi hiki kilichobaki cha mwaka hii kulingana na plan.

kwa maelezo ya mkataba na mgawanyo wa faida. Tuko Kibaha mjini.

Whatsapp au Piga 0713-039 875
 
Nimesoma Tangazo lako lote sijaona bidhaa unazozalisha ili nipime kama nazifahamu,nishakutana nazo au kujielemisha kama kweli ni bidhaa nzuri. Sababu umeweka jina la kurasa yako ya Instagram kwenye picha uliyoweka jukwaani,nimetembelea Ukurasa huo nikaone bidha unazozalisha badala yake nimekuta picha za watu mbalimbali wenye changamoto za Ngozi. Naomba nikuulize,ni bidhaa zipi unatengeneza? brand yako sokoni ni ipi? ufanisi wa bidhaa zako upoje?
 
Akikujibu naomba unitagi please
 
Back
Top Bottom