Tajirika na sabuni za Kigoma

Jemima Mrembo

JF-Expert Member
Jul 19, 2021
2,791
8,005
Caustic Soda kilo 3, Mafuta ya mawese lita 20, Sodium Silket, Maji lita 10, Rangi ya bluu 100gram.

Jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua

1)-Chukuwa caustic soda changanya na maji na uanze kukoroga kuelekea upande mmoja endelea kufanya hivyo hadi vichanganyikane vizuri baada ya hapo iache kwa saa 24

2)-Chukuwa kindoo kidogo na upunguze mafuta lita 3 kwa ajili ya kuweka rangi pembeni, weka rangi vijiko 3 ,changanya na mafuta uliyopunguza lita 3 kisha koroga mpaka yachanganyikane vizuri kabisa.

3)-Chukuwa caustic soda uliyoloweka kwenye ndoo kubwa, kisha tia mafuta na uendelee kukoroga kuekekea upande mmoja kwa nguvu na kwa haraka, tia sodium silgett kwa kunyunyuzia kidogo kidogo, endelea kukoroga hadi vichanganyikane viwe kitu kimoja.

4)-Baada ya hapo andaa ndoo nyingine ndogo, chukuwa uji uliokoroga au mkorogo wako kiasi kwa ajili ya kuchanganya na rangi mwanzo na mafuta kisha koroga kwa pamoja vichanganyikane vizuri.

5)-Kishaa andaa box la kukaushia sabuni na mimina mkorogo wako kwenye box, kisha chukuwa mkorogo wenye rangi na umimine juu kwa stail ya zigzaga kisha pitisha mwiko ili rangi iingie mpaka chini

Baada ya hapo iache kwa saa 24 ili ikauke vizur, kisha itoe na uikate kate sabuni yako

Kama unataka sabuni nyingi vipimo vinaongezeka, au kama ni kidogo vipimo vinapungua inategemea na wewe mwenyewe unatakaje.
Chukua laki 5 wekeza mwenye mradi wa 'sabuni za Kigoma' itakulipa sana. Tafuta mtu mwaminifu ambaye atakusimamia Utapata sana faida kwasababu ni biashara isiyo doda na inaingiza mapesa mengi kwa mkupuo.
 
Caustic Soda kilo 3, Mafuta ya mawese lita 20, Sodium Silket, Maji lita 10, Rangi ya bluu 100gram.

Jinsi ya kutengeneza hatua kwa hatua


Chukua laki 5 wekeza mwenye mradi wa 'sabuni za Kigoma' itakulipa sana. Tafuta mtu mwaminifu ambaye atakusimamia Utapata sana faida kwasababu ni biashara isiyo doda na inaingiza mapesa mengi kwa mkupuo.
Asante sana mrembo
 
Elaborate please

Unaona sasa unaandika vitu usivyovijua, you don’t know how it is dangerous to impose false knowledge. Hakuna sabuni za Kigoma zinazotengenezwa kwa kutumia mafuta ya mawese unless unataka kuanza wewe mama.
Sabuni za Kigoma zinatengenezwa kwa kutumia mafuta ya mise yaani yale mafuta meupe mfano wa Korie au OK yatokanayo na mbegu za mise.

Wakati mwingine andika vitu unavyovijua uache ku mislead watu kwa taarifa zisizo sahihi.
 
Hapana mkuu, nimeipenda lakini nilitamani atoe neno  tajirika. Na badayake aweke neno fanikiwa
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kufanikiwa na kutajirika. Kutajirika ni kupata mali. Kufanikiwa ni kutimiza ndoto zako. Mfano ndoto yako ni kupata mtoto, ukishapata mtoto utakuwa umefanikiwa. Unaweza kuwa tajiri lakini hujatimiza ndoto zako, hivyo basi huna mafanikio
 
Back
Top Bottom