Bomu Arusha - Vatican yawasilisha taarifa UN

Status
Not open for further replies.

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,899
bomu.jpg

Askofu Mkuu Frances Chullikatt

Tukio la bomu latua UN
Tukio la kutupwa bomu katika Kanisa Katoliki la Joseph Mfanyakazi, Arusha limetua katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) baada ya kuwasilishwa na Balozi wa Vatican UN, Askofu Mkuu Frances Chullikatt. Askofu Chullikatt anakuwa kiongozi wa kwanza wa Vatican kutoa tamko kuhusiana na shambulizi hilo ambalo mmoja wa viongozi wake alikuwapo.

Bomu hilo lilirushwa katika kanisa hilo wakati likizinduliwa na Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Francisco Padilla Mei 5, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi zaidi ya 50. Wakati wa shambulizi hilo, Askofu Padilla na Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha, Josephat Lebulu walionusurika.

Akihutubia Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York, Marekani juzi, Askofu Chullikatt alisema tukio lililotokea Arusha linadhihirisha kuwa kuna umuhimu ya kupambana na ugaidi katika Afrika ili kuimarisha amani na usalama wa kimataifa. “Unahitajika mshikamano na ushirikiano wa pamoja wa mataifa mbalimbali katika kuchukua hatua za maisha na kulinda haki za binadamu,” alisema Askofu Chullikatt, ambaye amekuwa mwakilishi wa Vatican kwenye Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2010.

Askofu Chullikatt, ambaye ni mzaliwa wa India, alisema suala la ugaidi linahitaji kuzuiwa duniani kote na hasa Afrika kutokana na matukio hayo kuharibu maisha ya binadamu na kutokea katika maeneo wanayofanyia ibada. Askofu Chullikatt alisema pale ugaidi unapofanyika kwa kutumia dini, waumini na viongozi wao ni lazima wahakikishe wanapambana nao ili kuutokomeza.

Alisema suala la ugaidi linahitaji viongozi wa kisiasa, kijamii na kidini kulilaani kwani ni la kikatili katika maisha ya binadamu hivyo si vyema kukaa kimya suala hilo linapotokea. Askofu Chullikatt alisema ugaidi unaotokea Afrika unatakiwa kuangaliwa kimataifa ili kuzipa uwezo nchi hizo kupambana na kuzuia matukio hayo.

Shambulio la bomu dhidi ya kanisa la Arusha lilikuwa tukio la pili la ugaidi uliolenga kushambulia wageni nchini. Mara ya kwanza ilitokea mwaka 1998, wakati Ubalozi wa Marekani nchini ulipolipuliwa kwa bomu na kusababisha vifo vya watu kumi na moja huku 85 wakijeruhiwa.
 
Siyo maamuzi ya mabaya kama hatuchukui hatua madhubuti katika mambo ya msingi ngoja watu saidie katika kupambana na hili janga inaoratibiwa na wahuni wachache kwa minajili ya dini.

"IT IS DIFFICULT TO FIGHT AGAINST FAITH THAN KNOWLEDGE" .ADOLPH HITLER.
 
KIJANA AMBROSE KATIKISA MPAKA UMOJA WA MATAIFA!! DAH MAKUBWA?

WAWEZA KUTA WAZAZI WAKE NA HATA YEYE WOTE WALIKUWA WAKISALIA KT KANISA ILO, DAH PASUA KICHWA SANA UYU DOGo
 
Mwakilishi wa Vatikan UN amechemsha! kwanza bomu la Arusha halina uhusiano na Ugaidi kwasababu waliokamatwa mpaka sasa hivi ni Vijana wa Kikristo na hata Kardinali Pengo kathibitisha hilo! pili huyu Mwakilishi wa Vatikan UN ni Mhindi, na huko kwao India milipuko ya mabomu na ulipuaji wa Majumba ya ibada nikitu cha Kawaida! hasa tukio kubwa la kulipua na kuchoma Msikiti mkubwa wa kihistoria huko Ayodha India mwaka 1992 na kuuliwa mamia ya Waislamu na Baniani lakini Muhindi huyu haoni huko kwao bali macho yake yako Arusha na Afrika!

Huu ni ubaguzi wa rangi unaoonyeshiwa na Mwakilishi huyu wa Papa UN! Milipuko ya mabomu India na Asia hayajafikishwa UN kwanini iwe ni Afrika tu? unaweza kulinganisha mabomu yanayolipuka Afrika na yale ya Asia?
 
Kwa hii serikali yetu tusitegemee jibu la mana. Kama watuhumiwa wanaachiwa huku serikali haijui mhusika wewe unategemea nini cha zaidi? Nchi hii tuna wasomi lakini wakisha pewa ulaji wanapoteza maana.
 
HII NDO GHARAMA INAYOTUPATA KWA KUMCHAGUA BWANA DHAIFU AKITOKEO CHAMA DHAIFU, MATOKEO YAKE NDIO HAYA DHAIFUUU.,..

SIJUI NI LINI TANZANIA TUTAACHA KUFANYA MAAMUZi YASOKUWA NA TIJA KWETU, CCM NI JANGA KWA JAMII, JANGA KWA UCHUMI, JANGA KWA ULINZI, JANGA KWA ELIMU, JANGA KA KATIBA MPYA, JANGA KWA DINI, JANGA KWA AFYA, JANGA KWA MIUNDO MBINU...
JAMANI ACHENI KUICHAGUA CCM NI JANGA LA TAIFA
 
Mwakilishi wa Vatikan UN amechemsha! kwanza bomu la Arusha halina uhusiano na Ugaidi kwasababu waliokamatwa mpaka sasa hivi ni Vijana wa Kikristo na hata Kardinali Pengo kathibitisha hilo! pili huyu Mwakilishi wa Vatikan UN ni Mhindi, na huko kwao India milipuko ya mabomu na ulipuaji wa Majumba ya ibada nikitu cha Kawaida! hasa tukio kubwa la kulipua na kuchoma Msikiti mkubwa wa kihistoria huko Ayodha India mwaka 1992 na kuuliwa mamia ya Waislamu na Baniani lakini Muhindi huyu haoni huko kwao bali macho yake yako Arusha na Afrika!

Huu ni ubaguzi wa rangi unaoonyeshiwa na Mwakilishi huyu wa Papa UN! Milipuko ya mabomu India na Asia hayajafikishwa UN kwanini iwe ni Afrika tu? unaweza kulinganisha mabomu yanayolipuka Afrika na yale ya Asia?

Penye red,

Gaidi anaweza kuwa mkristo, muislam hata mpagani. Ugaidi hauna ubaguzi wa rangi, gaidi anaweza kuwa mzungu, mmatumbwi, muarabu hata mjapani.

Kwa msaada tu definition ya terrorism: Systematic use of violence to create a general climate of fear in a population and thereby to bring about a particular political objective.

Angalia kwa makini hii definition, haitaji mmakonde, mweusi, mzungu, mwaarabu, mkristo, muislam wala mpagani.

Kamanda, unapo jadili haya mambo jitahidi kuwa sensitive na udini na race. Wewe mwenyewe unaweza kuwa mbaguzi wa rangi (Penye blue) kama ulivyo sema.
 
Pumbafu kabisa...kaa kimya kama huna kitu cha kuongea...
 
  • Thanks
Reactions: mja

Kwa hiyo unataka kusema kuwa bomu la Arusha ni Ugaidi? na ni ugaidi wa ndani au ugaidi wa Kimataifa? vipi kuhusu Vatikan kutaja Afrika tu na sio Asia? huo ndio ubaguzi naouzungumzia! lakini kumbuka Tanzania tuna sheria ya Ugaidi na sheria hii inawahusu Waislamu tu! ndio maana Wanasheria wa Lwakatare waliishangaa Serikali kumshitaki kwa ugaidi na baadae Mahakama kumfutia kosa la ugaidi!
 
Mwakilishi wa Vatikan UN
amechemsha! kwanza bomu la Arusha halina uhusiano na Ugaidi kwasababu
waliokamatwa mpaka sasa hivi ni Vijana wa Kikristo na hata Kardinali
Pengo kathibitisha hilo! pili huyu Mwakilishi wa Vatikan UN ni Mhindi,
na huko kwao India milipuko ya mabomu na ulipuaji wa Majumba ya ibada
nikitu cha Kawaida! hasa tukio kubwa la kulipua na kuchoma Msikiti
mkubwa wa kihistoria huko Ayodha India mwaka 1992 na kuuliwa mamia ya
Waislamu na Baniani lakini Muhindi huyu haoni huko kwao bali macho yake
yako Arusha na Afrika!

Huu ni ubaguzi wa rangi unaoonyeshiwa na Mwakilishi huyu wa Papa UN!
Milipuko ya mabomu India na Asia hayajafikishwa UN kwanini iwe ni Afrika
tu? unaweza kulinganisha mabomu yanayolipuka Afrika na yale ya
Asia?
Balozi kachemsha vipi wakati Rais Kikwete, waziri wa mambo ya ndani tz, waziri wa mambo ya nje tz, Rc Arusha, wanasema ni tukio la kigaidi? au una tatizo binafsi ya balozi?
 
Pumbafu kabisa...kaa kimya kama huna kitu cha kuongea...

Wewe umeongea nini hapa zaidi ya matusi? jibu hoja kwa hoja matusi hayana nafasi JF! sana sana ukiendelea na matusi kila mwenye akili atakudharau! jiheshimu ndugu!
 
Mwakilishi wa Vatikan UN amechemsha! kwanza bomu la Arusha halina uhusiano na Ugaidi kwasababu waliokamatwa mpaka sasa hivi ni Vijana wa Kikristo na ....!

Huu ni ubaguzi wa rangi unaoonyeshiwa na Mwakilishi huyu wa Papa UN! Milipuko ya mabomu India na Asia hayajafikishwa UN kwanini iwe ni Afrika tu? unaweza kulinganisha mabomu yanayolipuka Afrika na yale ya Asia?

Huyu anatuthibitishia kwamba wakristu hawafanyi ugaidi.
 
Kwa hiyo unataka kusema kuwa bomu la Arusha ni Ugaidi? na ni ugaidi wa ndani au ugaidi wa Kimataifa? vipi kuhusu Vatikan kutaja Afrika tu na sio Asia? huo ndio ubaguzi naouzungumzia! lakini kumbuka Tanzania tuna sheria ya Ugaidi na sheria hii inawahusu Waislamu tu! ndio maana Wanasheria wa Lwakatare waliishangaa Serikali kumshitaki kwa ugaidi na baadae Mahakama kumfutia kosa la ugaidi!

Mkuu, upo misinformed. Nitapoteza muda hapa. Endelea kuamini unavyo amini. Good luck.
 
Acheni kutokwa na povu.....tayari kuna report mbili, moja ni ya FBI na nyengine ni ya SMZ kwa mashirikiano na SMT. Wakiamua kuzitoa hizo ndipo sasa tutajua tatizo ni nini na wapi pakuanzia!
 
Mwakilishi wa Vatikan UN amechemsha! kwanza bomu la Arusha halina uhusiano na Ugaidi kwasababu waliokamatwa mpaka sasa hivi ni Vijana wa Kikristo na hata Kardinali Pengo kathibitisha hilo! pili huyu Mwakilishi wa Vatikan UN ni Mhindi, na huko kwao India milipuko ya mabomu na ulipuaji wa Majumba ya ibada nikitu cha Kawaida! hasa tukio kubwa la kulipua na kuchoma Msikiti mkubwa wa kihistoria huko Ayodha India mwaka 1992 na kuuliwa mamia ya Waislamu na Baniani lakini Muhindi huyu haoni huko kwao bali macho yake yako Arusha na Afrika!

Huu ni ubaguzi wa rangi unaoonyeshiwa na Mwakilishi huyu wa Papa UN! Milipuko ya mabomu India na Asia hayajafikishwa UN kwanini iwe ni Afrika tu? unaweza kulinganisha mabomu yanayolipuka Afrika na yale ya Asia?

kwahyo kaka ulifuraia hilo tukio. Hata wakristo wanapotumiwa vibaya waweza kua magaidi. Ila wewe ni fara 2
 
Kwanini wamewaachia wale Waarab wa Saudi Arabia lakini Wanaendelea kuwashikilia Watanzania Wakristu.Chuki ya Serikali hii ya CCM kwa Wakristu inanistaajabisha.
 
KIJANA AMBROSE KATIKISA MPAKA UMOJA WA MATAIFA!! DAH MAKUBWA?

WAWEZA KUTA WAZAZI WAKE NA HATA YEYE WOTE WALIKUWA WAKISALIA KT KANISA ILO, DAH PASUA KICHWA SANA UYU DOGo

Ama kweli! Haikosi ndio sababu umembeba mbuzi mgongoni. pic.PNG
 
Mwakilishi wa Vatikan UN amechemsha! kwanza bomu la Arusha halina uhusiano na Ugaidi kwasababu waliokamatwa mpaka sasa hivi ni Vijana wa Kikristo na hata Kardinali Pengo kathibitisha hilo! pili huyu Mwakilishi wa Vatikan UN ni Mhindi, na huko kwao India milipuko ya mabomu na ulipuaji wa Majumba ya ibada nikitu cha Kawaida! hasa tukio kubwa la kulipua na kuchoma Msikiti mkubwa wa kihistoria huko Ayodha India mwaka 1992 na kuuliwa mamia ya Waislamu na Baniani lakini Muhindi huyu haoni huko kwao bali macho yake yako Arusha na Afrika!

Huu ni ubaguzi wa rangi unaoonyeshiwa na Mwakilishi huyu wa Papa UN! Milipuko ya mabomu India na Asia hayajafikishwa UN kwanini iwe ni Afrika tu? unaweza kulinganisha mabomu yanayolipuka Afrika na yale ya Asia?
Aisee wengine mkoje!? Kipi kibaya alichosema balozi huyo? Hapo penye nyekundu inaonyesha una kichwa kidogo mno! Hivi wewe unataka kutuaminisha kuwa ugaidi unatendwa na wale wasio wakristo tu? Shame on UUU!!!!!!!dude!
 
Kwanini wamewaachia wale Waarab wa Saudi Arabia lakini Wanaendelea kuwashikilia Watanzania Wakristu.Chuki ya Serikali hii ya CCM kwa Wakristu inanistaajabisha.

Sina-ajira
Mtuhumiwa wa tukio ni lazima awe mwarabu?

Wanashikiliwa watanzania? Au wakristo?

Ulipendelea nani akamatwe? Mkenya? wapagani? waislamu? wahindi? watalii au wawekezaji?

Kuna mdau ametoa maana ya ugaidi hapo juu. Kama utakubaliana na maana hiyo ya ugaidi basi yeyote anaefanya/atakaefanya vitendo hivyo, awe, mwarabu,mchaga, mmanyema, mngoni, mzanaki, mzungu, muhindi, mwarabu, mwafrika,pagani,mkiristo,muislamu basi atakuwa gaidi.

Nitakachokubaliana na wewe katika kulalamika ni kuona matokeo mengi yameshatokea Tanzania lakini serikali haiweki hadharani matokeo ya uchunguzi, upelelezi wanaoufanya. Na pale kesi zinapofikishwa mahakamani tunaona ni usanii tu. Hali hii inapelekea wananchi kuona kuwa wanapigwa changa la macho tu.

Tutakaponasa katika mtengo wa udini ndio tunakaribisha maangamizi.Wapo wanaopendelea kuona Tanzania inakuwa kama Congo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom