Tujikumbushe: Yule Askofu mwenye kiburi amepewa Ukuu wa Kanisa

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
8,098
9,994
Mwaka 2018 Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) lilitoa waraka wa Pasaka ambao ulikua unakosoa, kuonya na kushauri mambo mbalimbali yaliyokua yakiliathiri taifa kwa wakati huo. Waraka huo ulikua moto kwa serikali ya Magufuli kwa sababu ulikosoa mambo mbalimbali ikiwemo matumizi ya nguvu kufunga biashara pamoja na vitendo vya watu kutekwa, kupotea na miili ya watu kuokotwa baharini kwenye mifuko ya sandarusi.

Kanisa liliitaka serikali ichukue hatua kukomesha vitendo hivyo na kuagiza waraka huo usomwe katika Dayosisi zote nchini. Kati ya Maaskofu 27 wa KKKT, Maaskofu 24 walitii na kuusoma waraka huo kwenye Dayosisi zao, lakini Maaskofu watatu walizuia usisomwe. Maaskofu hao ni Solomon Massangwa wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati (Arusha), Askofu Lucas Judah Mbedule wa Dayosisi ya Kusini Mashariki (Mtwara) na Askofu Alex Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Kufuatia Maaskofu hao watatu kwenda kinyume na agizo la Kanisa, waliagizwa kuomba radhi na Halmashauri kuu ya Kanisa. Askofu Lucas Judah Mbedule wa Dayosisi ya Kusini Mashariki aliomba radhi kwa kulala kifudifudi akiwa kwenye vazi lake rasmi la Uaskofu, kama ishara ya unyenyekevu.

Askofu Massangwa wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati (Arusha) aliomba radhi kwa maandishi, na taarifa yake ya kuomba msamaha ilichapwa kwenye gazeti la Mtanzania la April 30, mwaka 2018.

Askofu Malasusa hakuomba radhi na hivyo, kikao cha Baraza la Maaskofu wa KKKT kikalazimika kuketi April 29 mwaka 2018 ili kujadili suala lake. Kikao hicho kiliazimia kumtenga Askofu Malasusa na kumzuia kuwakilisha Kanisa hilo nje ya Dayosisi yake kama hataomba radhi. Baada ya shinikizo hilo Askofu Malasusa alilazimika kuomba radhi kwa maandishi.

images.jpeg

Askofu mbedule aliomba radhi kwa kuanguka kifudi fudi kwa unyenyekevu mkubwa

Pia soma
- Baada ya Malasusa kutengwa, askofu KKKT aomba radhi waraka kutosomwa kanisani

- Baadhi ya waumini wa KKKT wataka Askofu Malasusa aombe radhi na Kustaafu
 
Utulivu wa taasisi zetu za dini ni utulivu wa watanzania ...

Mwenyezi Mungu azidi kutupa busara na hekima ya utulivu na heshima kwa wengine ,aaaamin aaaamin

#Tanzania Kwanza

#JMT Daima
 
Ni muda sasa wakugeukia kanisa la kirutheli africa mashariki KKAM
Serikali inamtaka malasusa lakini kanisa halimtaki Malasusa, Yeye Malasusa anautaka ukuu wa kanisa la KKKT lakini waumini hawataki awe mkuu wa kanisa.
 
Nitegemee dominica yenye mpasuko KKKT natabiri tatizo litaaanzia Njombe na karagwe
 
Shoo alitawaliwa na malasusa miaka yote ya utawala wake hakuwahi kuwa askofu huru labda kidogo mwanzoni mwa utawala wake.

Huko Serikali itamchagua Askofu Shoo. Maana kama aliwasikiliza waka muweka malasusa, basi huyo ndiye chaguo lao kwa sasa.
 
Serikali inamtaka malasusa lakini kanisa halimtaki Malasusa, Yeye Malasusa anautaka ukuu wa kanisa la KKKT lakini waumini hawataki awe mkuu wa kanisa.
Malasusa atawasaidia sana Mbeleni. Atasaidia kampeni za kijana wenu kujaribu kupenya kwenye Urais, japo pana Ugumu. RC itamleta Nchimbi.
 
Mwaka 2018 Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) lilitoa waraka wa Pasaka ambao ulikua unakosoa, kuonya na kushauri mambo mbalimbali yaliyokua yakiliathiri taifa kwa wakati huo. Waraka huo ulikua moto kwa serikali ya Magufuli kwa sababu ulikosoa mambo mbalimbali ikiwemo matumizi ya nguvu kufunga biashara pamoja na vitendo vya watu kutekwa, kupotea na miili ya watu kuokotwa baharini kwenye mifuko ya sandarusi.

Kanisa liliitaka serikali ichukue hatua kukomesha vitendo hivyo na kuagiza waraka huo usomwe katika Dayosisi zote nchini. Kati ya Maaskofu 27 wa KKKT, Maaskofu 24 walitii na kuusoma waraka huo kwenye Dayosisi zao, lakini Maaskofu watatu walizuia usisomwe. Maaskofu hao ni Solomon Massangwa wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati (Arusha), Askofu Lucas Judah Mbedule wa Dayosisi ya Kusini Mashariki (Mtwara) na Askofu Alex Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Kufuatia Maaskofu hao watatu kwenda kinyume na agizo la Kanisa, waliagizwa kuomba radhi na Halmashauri kuu ya Kanisa. Askofu Lucas Judah Mbedule wa Dayosisi ya Kusini Mashariki aliomba radhi kwa kulala kifudifudi akiwa kwenye vazi lake rasmi la Uaskofu, kama ishara ya unyenyekevu.

Askofu Massangwa wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati (Arusha) aliomba radhi kwa maandishi, na taarifa yake ya kuomba msamaha ilichapwa kwenye gazeti la Mtanzania la April 30, mwaka 2018.

Askofu Malasusa hakuomba radhi na hivyo, kikao cha Baraza la Maaskofu wa KKKT kikalazimika kuketi April 29 mwaka 2018 ili kujadili suala lake. Kikao hicho kiliazimia kumtenga Askofu Malasusa na kumzuia kuwakilisha Kanisa hilo nje ya Dayosisi yake kama hataomba radhi. Baada ya shinikizo hilo Askofu Malasusa alilazimika kuomba radhi kwa maandishi.

View attachment 2729837
Askofu mbedule aliomba radhi kwa kuanguka kifudi fudi kwa unyenyekevu mkubwa

Pia soma
- Baada ya Malasusa kutengwa, askofu KKKT aomba radhi waraka kutosomwa kanisani

- Baadhi ya waumini wa KKKT wataka Askofu Malasusa aombe radhi na Kustaafu
Ameiba uchaguzi, kama CCM! eti nalo ni kanisa, pumbavu
 
Serikali inamtaka malasusa lakini kanisa halimtaki Malasusa, Yeye Malasusa anautaka ukuu wa kanisa la KKKT lakini waumini hawataki awe mkuu wa kanisa.
Huo ukuu kaupata kwa kura nyingi, wajumbe waliompigia kura hawakuwa wajumbe halali?
 
Back
Top Bottom