SI KWELI Bibi na Bwana wameondolewa katika nembo ya taifa inayotumika kwenye Podium ya Rais Samia

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Salaaam Wakuu,

Nimeona katika sehemu mbalimbali picha zikisambaa zikionesha nembo inayotumika kwenye Podium ya Rais Samia haina bibi na bwana kama ambayo alikuwa anaitumia Rais Magufuli.

Hili limekaaje Wakuu tunaomba ufafanuzi.

1692078839081.png

Nembo anayotumia Rais Samia ikiwa haina Bibi na Bwana

1692078914132.png

Nembo aliyokuwa akiitumia Hayati Magufuli ikiwa na Bibi na Bwana
 
Tunachokijua
Kumeibuka hoja katika mitandao ya kijamii ikihoji utata uliopo katika matumizi ya nembo ya Taifa katika Podium inayotumiwa na Rais Samia. Wadau hao wanahoji ikiwa nembo ya Taifa imebadilishwa kwa kuondolewa kwa Bibi na bwana kama ambavyo imeletwa na mleta mada hapo juu.

Mathalani, mtumiaji wa mtandao wa X aitwaye @kumbushodawson aliweka andiko fupi likihoji kuhusu nembo hiyo ya inayotumiwa na Rais Samia imetolewa wapi. @kumbushodawson akiambitisha picha ya Rais Samia na Hayati Magufuli ameandika:

Hii nembo anayotumia Rais Samia ni ya nchi Gani? Imeokotwa wapi?Sheria ya Nembo ya Taifa ya Mwaka 1971 imeweka Wazi kwamba Nembo ya Taifa itakuwa na Picha za bibi na Bwana walioshika pembe za Ndovu .

Hata hivyo, katika andiko hilo la @kumbushodawson wamejitokeza wadau waliopinga hoja yake na kujaribu kufafanua kuhusu nembo hiyo:

Kilumbi82 anapinga madai ya nembo hiyo kubadilishwa na kudokeza kuwa hiyo ni nembo ya Rais na Rais Samia amekuwa akitumia zote mbili. Katika ufafanuzi wake Kilumbi82 anaandika:

Tatizo lako hutaki hata kuumiza Fuvu lako kidogo, umebeba caption na picha kutoka kwa Yericko na kuweka kwako. Nenda Google, utakuta Rais Samia Suluhu Hassa huwa anatumia nembo zote mbili. Lakini hata Magufuli alitumia sana nembo ya RaisAngalia Meza ya Magu hapo Chini:

1692080401836-png.2717787

Naye Mwanachama wa JamiiForums anayeitwa Stuxnet anapinga hoja ya nembo ya taifa kubadilishwa kuwa kufafanua kuwa hilo ni suala la kiitifaki. Katika hoja hiyo Stuxnet anasema:

Hiyo ni nembo ya Rais mara nyingi hutumika kwenye mikutano ambayo Rais pekee ndio ataongea kwenye hiyo Podium ya kwake. Endapo podium itatumiwa na watu tofauti tofauti huwa inawekwa nembo ya Bibi na Bwana, kwa ujumla ni mambo ya Protocol

Je, ni kweli Bibi na bwana wameondolewa katika nembo inayotumiwa na Rais Samia?
Baada ya kusambaa kwa hoja hii JamiiForums imefanya uchunguzi na kubaini yafuatayo:-

Nembo hiyo yenye pembe pembeni ni Nembo ya Rais (Presidential Seal) ambayo Rais huitumia na huonesha uwepo wake, nembo hii pia ipo kwenye bendera ya Rais. Nembo ya Rais yaweza kuwekwa kwenye vitu mbalimbali anavyovitumia vikiwemo podium, kiti anachokalia na ndio huwekwa kwenye gari analotumia katika sehemu ya plate number sambamba na Bendera ya Rais ambayo hupeperushwa kulia kwa gari anayotumia.
Rais pia anaweza kukutana na mazingira ambayo anatumia nembo ya Serikali (Court of Arms), ni kwa sababu mbalimbali ikiwemo kwamba yeye ndiye Mkuu wa Serikali. Na pia kuna mazingira ambayo Rais anaweza kuwa anatumia podium hiyo hiyo na watumiaji wengine wasiopaswa kutumia Nembo ya Rais.
Aidha, kuwepo ama kutokuwepo kwa nembo hizi katika mazingira ambayo Rais yupo hakuondoi Urais wake. Yapo mazingira ambayo Rais anaweza kukutana nayo na kusiwepo Nembo ya Rais na ikawepo Nembo ya Serikali, haimzuii Rais kutekeleza majukumu yake. Yapo mazingira ambayo Rais anaweza asikutane na nembo zote mbili, pia hamzuii kutekeleza majukumu yake. Mfano ni mikutano ya njiani ama mikutano/ziara za kushtukiza ambazo Mkuu wa Itifaki hakupata muda wa kufanya maandalizi.
Hakuna sheria yoyote inayoelekeza bali Rais hutumia kanuni ya kufaa kwa mazingira (The Rule of Convinience). Mazingira haya ni pamoja na anapohudhuria mikutano ya Kimataifa nje ya nchi ambapo anaweza kukutana na podium yenye nembo ya taasisi inayowakusanya washiriki mfano mikutano ya Umoja wa Mataifa, ama Rais anapokwenda kwenye nchi nyingine na kukutana na Rais wa nchi husika ambapo podium hutumika zenye nembo ya Rais wa nchi hiyo ama nembo ya Serikali ya nchi hiyo nakadhalika.
Kwa ujumla wake matumizi ya Nembo ya Rais na Nembo ya Serikali sawa na ilivyo kwa matumizi ya bendera huratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Itifaki kulingana na mazingira na kufaa kwake. Wakati mwingine katika mazingira ambayo kuna interest zaidi ya moja mipangilio hii hutegemea makubaliano ya pande zinazohusika kulingana na miongozo ya kiitifaki na vigezo vyake.

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom