ni wazo zuri mkuu songa mbele. ila jitahidi ujue ni samaki ya aina gani utakuwa unapeleka kutoka mwanza. kwa sababu samaki aina ya sangala ni bei kubwa sana mwanza kwa sababu ya kuwepo kwa viwanda. so wasi wasi wangu usije ukawanunua then ukienda kuuza wananchi wako wakaona ni bei kubwa. jaribu kuangalia samak aina ya sato na wengine ila sangala fikiria mala mbili kabla ya kuuza.
Kama utakuwa unanunua mwanza tafuta ofisi weke frige na kuwa unakusanyia mzigo hapo hata kwa muda mfupi. jambo lingine jitahidi kujiridhisha na usafiri wa kudumu. haya malori hayafai kabisa yameisha tia watu hasara. hata samaki wakiwa wamekaushwa gari ikiharibika usababisha hasara sana. ila hizo ni changa moto ambazo ukizijua mapema ni vyema kuzitafutia ufumbuzi haraka.
Kama utapata soko zuri za sangala uko arusha, kumbuka sangala mwanza anakuwa na thamani kwa na vitu vikuu viwili.
kwanza mnofu kwenye viwanda na pili ndani ya sangala tumboni kuna kitu wanaita bondo sijajua kama ni kiswahili au la ila nimezoea kusikia wanaita hivyo, hii kitu ni hela sana kwa sangala alie mkubwa. watu wa arusha usiwauzie na hilo bondo litoe na ukaliuze mwanza kwa wachina hela nzuri.
nahisi usingize ngoja nilale nitakupa data kesho tena
Wakuu, nashukuru kwa michango yenu ila samaki ninaotaka kupeleka ni sangara wakuu maana hao sato ni ghali sana
Wakuu, natamani na tayari nimepata mtaji wa kusafirisha samaki toka Mwanza kwenda Arusha ila nahitaji msaada wa jinsi ya kuanza na masoko ya huko Arusha, tafadhali naombeni msaada
Bei ya sato ni kiasi gani arusha?
Habari mkuu, ulishaanza Biashara yako?Pamoja na maelezo mhimu ya King, na kwakuwa nipo kwenye mchakato wa kuanzisha hii biashara naomba niongezee kidogo. Mimi nategemea kuifanya katika kwa kiwango cha kati na hivyo wateja wangu wakuu nitategemea mahotel na watu wa kipato cha kati na siyo mama lishe. Mambo makuu ninayoyafikiria ni haya
- Jina la kampuni linalofanana fanana na chakula-nitakuwa na matawi mikoa mitatu (Dodoma, Arusha, Dar)
- Location ya biashara-nafikiria iwe kwenye junction kama mwenge kwa Dar
- Means of Transportation-Nitakuwa na gari kubwa ya freezer kwaajiri ya kusafirishia kutoka Lake zone na kupeleka Arusha, Dar then Dodoma kabla haijageuza kurudi Lake Zone.
- Nitakuwa na Gari ndogo kila centre kwaajili ya kusambaza kwa wateja wa kudumu kama wenye hotel na mashule.n.k
- Nitakuwa na Deep freezer kwa kila kituo.
- Nitakuwa na standby Generator kukabiliana na changamoto za TANESCO kwa kila kituo
- Nitatengeneza machinjio ya kisasa-hii ni plan ya baadae baada ya kupata shamba la kutunzia mifugo
- Nitakuwa na shamba la mifugo ambayo ndiyo malighafi yangu
- Nitakuwa na kituo cha kukusanyia samaki hapo Mwanza-Natafuta mtaalam wa kutengeneza Coldroom
- Bidhaa nitakazoanza nazo ni-Nyama ya Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo. Kuku wa kisasa na kienyeji, Samaki aina ya Sato na Sangara, Lakini pia nitakuja na mchele kwa Arusha na Dodoma......tayari nina 100bags za kuanzia na nipo nafunga mshine ya kisasa ya kukoboa na kubangua mchele na kufunga 5, 10. 15, 20kg
- Project to start in June 2014.
Tafadhali mawazo yenu. Nipo tayari kulipa gharama za Busness Plan ila kwa mtu mwenye input ya maana.
Haya watu wanaspea kuleta mrejesho.
Hembu mliopo Mwanza.
Niambieni kunasifisha SATO na SANGARA kwa ufupi samaki kuja huku Zanzibar kwa Ndege,ita cost kiasi gani.
Yaani nipeni mchanganuo wa gharama kwa kilo,na pia gharama za usafiri kwa ujumla wake.
Nafikiria kuanzisha hii biashara ila bado nasita kwanza,maana Direct flight kutoka Mwanza Kuja Zanzibar ni issue.Ila wazoefu mnajua hizi connections na gharama zake.
Haya tujuzane
Samahani hivi wewe unajishughulisha na nini?maana kila kitu wakitaka weye..
Samahani nahisi kama weye janjajanja tu kupoga stori humu