Nahisi sina bahati na biashara

Yohimbe bark

JF-Expert Member
Sep 1, 2019
1,050
2,576
Habari wakuu, nipo kwenye kisiwa cha maisome kilichopo Sengerema, nina mwezi sasa nafanya biashara ya uchuuzi wa samaki aina ya sato natoa huku napeleka Mwanza ila faida sipati kwasababu nilikuwa nachukua kwa walanguzi sio direct kutoka kwa wavuvi so faida ilikuwa inaishia kwenye malazi na usafiri, ndio nikashauriwa nitafute wavuvi niwadhamini nyavu, pumba na kuwakodishia mitumbwi ili waniuzie samaki kwa bei rahisi kidogo.

Aisee nina week zaidi ya mbili hapa wavuvi kuwapata imekuwa mziki, wote wako chini ya watu nazidi kula mtaji tuu nishaanza kukata na tamaa, kuna wavuvi nilifanyiwa connection kutoka kisiwa kingine nikaongea nao vizuri tuu waje nikawapa na offer nzuri but toka juzi wananiambia wameshakuja wapo ila nikiwaambia tuonane tuongee wananiambia wanakuja, muda unazidi kwenda hakuna ninachofanya yaani basi tuu haya maisha hayana maana, mtanisamehe kwa uandishi m'bovu, nipo confused.
 
GoldDhahabu njoo uchukue notice huku

Mleta mada ingia hapa
 
Habari wakuu, nipo kwenye kisiwa cha maisome kilichopo sengerema nina mwezi sasa nafanya biashara ya uchuuzi wa samaki aina ya sato natoa huku napeleka mwanza ila faida sipati kwasababu nilikua nachukua kwa walanguzi sio direct kutoka kwa wavuvi so faida ilikua inaishia kwenye malazi na usafiri, ndio nikashauliwa nitafute wavuvi niwadhamini nyavu, pumba na kuwakodishia mitumbwi ili waniuzie samaki kwa bei rahisi kidogo aisee nina week zaidi ya mbili hapa wavuvi kuwapata imekua mziki wote wako chini ya watu nazidi kula mtaji tuu nishaanza kukata na tamaa, kuna wavuvi nilifanyiwa connection kutoka kisiwa kingine nikaongea nao vizuri tuu waje nikawapa na offer nzuri but toka juzi wananiambia wameshakuja wapo ila nikiwaambia tuonane tuongee wananiambia wanakuja, mda unazidi kwenda hakuna ninachofanya yani basi tuu haya maisha hayana maana, mtanisamehe kwa uandishi m'bovu nipo confused.
Kutengeneza connection nzuri ya biashara nayo ni sehemu ya mtaji.
Ukiishiwa mtaji, lakini ukawa na wazo la biashara lililonyooka plus connection nzuri, mtaji utapatikana tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom