Madear
Member
- Feb 13, 2020
- 45
- 107
Ni kawaida sana kuona watu wakifuga kuku, ng'ombe, mbuzi, nguruwe, n.k. Lakini ni nadra sana kuona watu wakifuga samaki licha ya kuwa mazingira yetu yanafaa sana kwa shughuli za ufugaji samaki kutokana na kuwepo kwa maeneo yenye maji ya kutosha na hali nzuri ya hewa. Baadhi ya mataifa kama China na Misri kufuga samaki imekuwa utamaduni wao na hadi leo wamefanikiwa sana kwenye hii sector.
Kadri miaka inavyozidi kwenda samaki wanazidi kupungua kwenye vyanzo vya asili (ziwani, baharini na mitoni) Hii ni kutokana na ongezeko la watu hali inayopelekea samaki kuvuliwa kupita kiasi ili kukidhi mahitaji ya watu bila kutoa muda wa kutosha wa samaki kuzaliana.
Matokeo yake ni upungunguvu mkubwa wa samaki kwenye vyanzo vya asili na ufugaji wa samaki ndio unaonekana kama njia mbadala ya kuzalisha samaki wengi ili kukidhi mahitaji ya watu.
Haya mazingira yanafanya tuone ufugaji wa samaki ni fursa nzuri sana ya kujiinua kiuchumi, rafiki kwa mazingira na ianaweza kumaliza/kutatua tatizo la uhaba wa samaki hususani samaki wa maji baridi, hapa naongelea samaki pendwa Sato.
Huu ni wakati sahihi kwa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla kujifunza utamaduni huu mpya wa kufuga samaki kwenye mazingira yetu kama njia ya kujiongezea kipato, kutunza mazingira, kutumia resources zetu vizuri na pia ufugaji wa samaki ni njia nzuri ya kupunguza msongo wa mawazo kuona tu samaki wanavyofanya manuvering ni burudani tosha
Kunanjia nyingi rahisi za kufanya ufugaji samaki kama vile kwa kutumia mabwawa, matanki au vizimba. Sio raziama ufanye uwekezaji mkubwa unaweza kujenga kibwawa kidogo tu au ukafugia kwenye tanki hapo kwako na ukawa unajipatia kitoweo (Sato fresh kabisa) au unaweza kufuga samaki na kulima bustani kwa wakati mmoja, badala ya kumwaga maji yaliyochafuka wakati wa kufuga samaki wewe unaweza kuyatumia maji hayo yenye mbolea kumwagilia bustani, ukaboresha kilimo chakona kikawa chenye tija