Biashara ni ubunifu. Mafundi wa kazi kama hii wanapatikana Dar es salaam?

M Priska

Member
May 10, 2020
17
11
Habari zenu ndugu zangu. NATAFUTA FUNDI !

Nimepata bahati ya kusafiri Asia na nikakutana na ubunifu huu (picha hapo chini). Wenzetu bajaji zao sio za kusafirishia abiria tu, ila wana zi design kitofauti na kufanya nazo biashara zingine.

Mtu anachukua bajaji ya kawaida, anaondoa siti za nyuma, (inakua sehemu yakuweka bidhaa zako), anaweka paa juu, then paka rangi vizuri na mchezo umeisha. Kama unataka maurembo mengine ni pesa yako tu.

Nimekua very inspired na ningependa kujaribu kitu kama hiki home.

Swali: Je, kwetu Dar es Salaam kazi kama hii inawezekana? Kama mafundi wapo, karibuni tuongee.

IMG_1875.jpeg
IMG_1874.jpeg
 
Ina maana ni abiria mmoja na mzigo wake? Au ni dereva na vitu vyake Yaan kamefanywa ni gari ya kutembelea🤔
 
Nimewahi kukutana na dogo amedesign Bajaj yake Kama kiosk kinachotembea. Ameikata kata Kama hii ya kwenye picha.

Ameweka vitu vidogo vidogo Kama makava ya simu,vitu vya kuchezea watoto,urembo wa wanawake nk. Pia nikabahatika kumuona akihojiwa kwenye moja ya tv channel maarufu akidai anapiga hella na ubunifu wake watu wengi wameupenda hasa wadada.

Kama mtu unaishi Kati ya ubungo,na mbezi ya Kimara,unaweza kukutana na huyo dogo.
 
Shukran sana kaka !!

Kama kunajinsi yeyote mtu ataweza ni link nae au fundi yeyote mzoefu anaeweza ku design bajaji iwe hivi, itakua poa sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom