Natafuta kazi, nipo Dar es Salaam

P Accountant

JF-Expert Member
Sep 26, 2020
369
169
Natumaini nyote ni wazima wa afya njema.

Natafuta kazi ya aina yoyote, ambayo itaweza nipatia kipato ambacho kitanisaidia kupata walau chakula na malazi. Ndani na nje ya Dar es Salaam.

Taarifa zangu binafsi kwa ufupi:
Kijana mchapakazi, mwenye nidhamu na mwepesi kuzoea mazingira ya kazi.
Jinsia: Kiume
Mahali nilipo: Dar es salaam.
Elimu: Chuo Kikuu.
Shahada: Uhasibu.
Uzoefu: Mafunzo kwa vitendo (Uhasibu) katika Ofisi ya wilaya.

Nipo tayari kufanya kazi aina yoyote ndani na nje ya elimu yangu, au kama kunaeneo/Ofisi inahitaji muhasibu wa kujitolea nipo tayari walau kwa malipo kidogo niweze kuendesha maisha.

Naweza kufanya kazi kama:
√ Kuuza duka la bidhaa za aina yoyote.
√ Kutoa huduma za miamala ya simu kama M Pesa, Halopesa, Airtel Money, n.k
√ Na nyinginezo nyingi

Naombeni kazi Wakuu wangu. Muwe na wakati mwema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom