mmbangifingi
JF-Expert Member
- Mar 9, 2011
- 2,839
- 559
Mkapa was clever!!! firm/stable! alicontrol inflation, uchumi uliimarika, hata kama kutakuwa na ya hapa na pale mapungufu, Ben remains to be a capable Presidaaa baada ya the late Mwl
Kwa watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri wakiona wenzao wanafanya kazi wanachukulia kirahisi na kuona wao wanaweza kufanya vizuri zaidi. Mkapa alikuwa mchapakazi sana na ana uwezo mkubwa sana wa kufanya maamuzi. Kilichotokea wanamtandao wakadhani wao wanauwezo zaidi na wakabeza aliyofanya Ben. leo wako wapi? Angalia deni la taifa, Ben alilipunguza sana na nchi ikawa inakopesheka. leo deni linatisha. Tunarudi kule kwa mwinyi ambapo Tz hatutakopesheka tena.
Pamoja ma mapungufu yake mzee Mkapa lakini inchi ilikuwa pazuri kuliko ilivyo sasa,he is much better kwani inchi ilikuwa na displine ya hali ya juu,leo bei ya sembe na sukari bado iko juu mbali ya mkuu wa kaya kutoa tamko vishuke,then what is this?,sasa hivi kila mtu anatoa matamko na haya fanyiki yanayoogizwa!!
Baada ya vyombo vya habari vilivyokuwa vimenunuliwa na genge la mtandao kumsakama sana kwa habari nyingi za kumponda. Mkapa aliwahi sema maneno machache sana kuwa Watanzania tutamkumbuka. Kwa kweli hali ya nchi iliyopo saizi hakika jamaa tutamkumbuka tu, tutake tusitake. Nchi kila kitu kinaenda hovyo, na wanaonufaika ni wachache waliokuwa vinara wa hilo genge. Hakika sipati picha itakapofika 2014 hali itakuwaje. Saizi hela haina thamani kabisa, naamini soon BOT itaprint note zingine za elfu 20 na elfu 50. Ki ukweli buku 10 haina thamani tena. Ukishachenji imeisha.
Nchi huwa haiongozwi kwa blabla bali inahitaji commitment ya hali ya juu sana.
Kila la kheri.....
Du ni kweli kabisa UKAPA ulikuwepo sana hata uhuru haukuonekana ni mtu mwenye jazba, mngewauliza waandishi kama walikuwa wanaweza andika lolote baya kumhusu.Mkuu SWK, Nchi ilikuwa pazuri kivipi wakati Watanzania walikuwa wanalalamika na UKAPA. Alilazimisha ununuzi wa rada pamoja na Watanzania wengi kupinga ununuzi ule, kumbe kulikuwa na ufisadi ndani yake wa $12 millioni. Aliuza nyumba za serikali kwa bei poa na hadi sasa maamuzi yake yameigharimu Serikali shilingi 200 bilioni and counting. Aliwaingiza wale makaburu wa NET GROUP solutions kwa mtutu wa bunduki pamoja na kuwa walikuwa hawajui chochote kuhusu umeme. Alifanya ufisadi katika manununuzi ya ndege ya Rais ambayo ilinunuliwa akiwa amebakisha miezi mitatu tu katika awamu yake, ununuzi wa helicopters na magari ya jeshi. Aliiba Kiwira na kujimilikisha kisha kuwashinikiza wale Net Group solutions wasaini mkataba na kampuni yane wa shilingi bilioni 26. Aliuza mashirika ya umma kwa bei poa katika kile kilichoitwa privatisation na hadi sasa Watanzania hatujaona manufaa makubwa ya sera ile. Mwaka 2000 alisaini mikataba ya uchimbaji wa dhahabu kwa bei ya kutupa inayotupa mrahaba wa 3% tu na hadi hii leo mikataba hiyo haijabadilishwa. Alikuwa akisifiwa sana na WB na IMF kwamba amefanya vizuri kiuchumi lakini wakati huo huo kulikuwa hakuna ajira zilizoongezeka na pia Watanzania wengi walikuwa wanalalamikia UKAPA. EPA, Meremeta na Kagoda vyote vimetokea ndani ya utawala wake. Jamani tutapojadili hizi awamu mbali mbali lazima tuwe wachambuzi makini ili kuhakikisha hatumsifii mtu bila kuangalia mabaya aliyoyafanya akiwa madarakani. Kwa upande wangu mabaya ya Mkapa ni mengi mno kuliko mazuri aliyoyafanya na kama nchi yetu ingekuwa na utawala bora wa sheria alitakiwa awe jela huyu.