Benjamin Mkapa: Watanzania mtanikumbuka

Mkapa was clever!!! firm/stable! alicontrol inflation, uchumi uliimarika, hata kama kutakuwa na ya hapa na pale mapungufu, Ben remains to be a capable Presidaaa baada ya the late Mwl
 
despite of the scandals he is accused, Mkapa still deserve accolades in many aspects of his government. One among them is sound fiscal, and monetary policies which saw the country regain confidence in international arena. Inflation never reached two digit percentage, and opening our country with road networks.
 
Kwa watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri wakiona wenzao wanafanya kazi wanachukulia kirahisi na kuona wao wanaweza kufanya vizuri zaidi. Mkapa alikuwa mchapakazi sana na ana uwezo mkubwa sana wa kufanya maamuzi. Kilichotokea wanamtandao wakadhani wao wanauwezo zaidi na wakabeza aliyofanya Ben. leo wako wapi? Angalia deni la taifa, Ben alilipunguza sana na nchi ikawa inakopesheka. leo deni linatisha. Tunarudi kule kwa mwinyi ambapo Tz hatutakopesheka tena.

Yaani katika hili la kutupunguzua madeni, natamani Ben angebaki miaka kumi zaidi, yaani angechukua na hii ya kikwete, leo hii tungekuwa tuna deni dogo sana. Kikwete hajui kupangilia, udhaifu mkubwa wa huyu rais wetu ni kwamba he is not visionary, ukuanzia tu katika maisha yake binafsi sasa hadi na nchi nzima!

I miss you Ben!
 
Mimi namkumbuka nyerere tu, maana baada ya nyerere mambo yote ya nchi hii yalianza kuharibika, japo kadri siku zinavyokwenda ndivyo mambo yanavyozidi kuharibika, yaani leo ni afadhari ya jana. Kwa kanuni ya leo afadhari ya jana ok mkapa anakumbukwa, na kikwete atakumbukwa jana yake ikifika.
 
Tusogeze miaka tu tuone hao wanaosema udini kama wataendelea na msimamo huu. Angalia data hizi ni self explanatory, then mtajua kwanini watu wengi wenye uelewa mkubwa wanamkubali Benjamin Mkapa. Alichukua nchi 1995 ikiwa na inflation ya 23.969% na kuiacha 2005 ikiwa na inflation ya 4.359%. Mapungufu mengine ni lazima awe nayo kama binadamu yoyote, ila angalia pia alivyorudisha heshima kubwa kwa mfanyakazi na pia kwa elimu. Enzi za mzee wa ruksa wafanyakazi walikuwa wanadharauliwa sana, na pia shule ilikuwa ni kama kupoteza muda. Angalia Mkapa alivyoongeza idadi ya ajira, fanya tathmini ya watu waliomaliza vyuoni miaka ya tisini mwishoni na elfu mbili mwanzoni kama walisota mtaani kama wanaomaliza miaka hii. Kuna vigezo vingi vya kufanya comparison sio kung'ang'ania udini. Kama ni dini mwenyewe hapa ni Mwislamu.

Equivalent Data From the International Monetary Fund


Variable: Inflation, average consumer prices
Note: Data for inflation are averages for the year, not end-of-period data.
Units: Percent change
Source: International Monetary Fund - 2010 World Economic Outlook


YearInflation, average consumer pricesPercent Change198030.205 198130.30.31 %198225.7-15.18 %198328.912.45 %198427.1-6.23 %198536.133.21 %198633.3-7.76 %198732.4-2.70 %198847.70247.23 %198920.602-56.81 %199022.5629.51 %199128.03724.27 %199221.935-21.76 %199323.6197.68 %199437.14657.27 %199523.969-35.47 %199620.496-14.49 %199715.443-24.65 %199813.161-14.78 %19998.996-31.65 %20004.589-48.99 %20015.14712.16 %20024.555-11.50 %20034.429-2.77 %20044.138-6.57 %20054.3595.34 %20067.25166.35 %20077.028-3.08 %200810.27646.22 %200912.14418.18 %20107.22-40.55 %
 
Mi namkumbuka siku ile aliyokuwa anamwachia madaraka playboy JK alishuka kutoka upstairs za uwanja wa taifa kuelekea chini huku akikimbia!!!! kwa pale sikumuelewa ila sasa naelewa kwa nini na ndo maana namkumbuka.
 
All in all,he was deserve to be respect,kwa uwezo wake kafanya kazi sana hata jamaa alipoenda fungua daraja la umoja kamsifia,maji kanda ya ziwa kamsifia,kama alifanya makosa ni ya kiubinadamu tu cos he is not an angel,alichagua watu compentent kila post,wakafanya kazi walizotumwa,why jk asimuite amuelekeze watu wa kufanyanao kazi,much love,much respect to ben
 
Pamoja ma mapungufu yake mzee Mkapa lakini inchi ilikuwa pazuri kuliko ilivyo sasa,he is much better kwani inchi ilikuwa na displine ya hali ya juu,leo bei ya sembe na sukari bado iko juu mbali ya mkuu wa kaya kutoa tamko vishuke,then what is this?,sasa hivi kila mtu anatoa matamko na haya fanyiki yanayoogizwa!!

Mkuu SWK, Nchi ilikuwa pazuri kivipi wakati Watanzania walikuwa wanalalamika na UKAPA. Alilazimisha ununuzi wa rada pamoja na Watanzania wengi kupinga ununuzi ule, kumbe kulikuwa na ufisadi ndani yake wa $12 millioni. Aliuza nyumba za serikali kwa bei poa na hadi sasa maamuzi yake yameigharimu Serikali shilingi 200 bilioni and counting. Aliwaingiza wale makaburu wa NET GROUP solutions kwa mtutu wa bunduki pamoja na kuwa walikuwa hawajui chochote kuhusu umeme. Alifanya ufisadi katika manununuzi ya ndege ya Rais ambayo ilinunuliwa akiwa amebakisha miezi mitatu tu katika awamu yake, ununuzi wa helicopters na magari ya jeshi. Aliiba Kiwira na kujimilikisha kisha kuwashinikiza wale Net Group solutions wasaini mkataba na kampuni yane wa shilingi bilioni 26. Aliuza mashirika ya umma kwa bei poa katika kile kilichoitwa privatisation na hadi sasa Watanzania hatujaona manufaa makubwa ya sera ile. Mwaka 2000 alisaini mikataba ya uchimbaji wa dhahabu kwa bei ya kutupa inayotupa mrahaba wa 3% tu na hadi hii leo mikataba hiyo haijabadilishwa. Alikuwa akisifiwa sana na WB na IMF kwamba amefanya vizuri kiuchumi lakini wakati huo huo kulikuwa hakuna ajira zilizoongezeka na pia Watanzania wengi walikuwa wanalalamikia UKAPA. EPA, Meremeta na Kagoda vyote vimetokea ndani ya utawala wake. Jamani tutapojadili hizi awamu mbali mbali lazima tuwe wachambuzi makini ili kuhakikisha hatumsifii mtu bila kuangalia mabaya aliyoyafanya akiwa madarakani. Kwa upande wangu mabaya ya Mkapa ni mengi mno kuliko mazuri aliyoyafanya na kama nchi yetu ingekuwa na utawala bora wa sheria alitakiwa awe jela huyu.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya Economic development na Growth

Tanzania kipindi cha Mkapa ili grow sana interms of GDP lakini la kusikitisha It did not trickle down to Tanzanian Majority ambao wapo Kijijini wanaishia kula ugali na nyanya chungu za kuchemsha.

Kama ni maendeleo interms of numbers Mkapa way better (GDP, Inflation, etc )

Lakini hawezi kukwepa tuhuma za EPA na mambo mengineo
 
at least ben alikua anauma anapuliza,huyu wa sasa anachota tu wala hana habari na chochote zaidi ya safari yaani anaponda raha na familia yake mpaka hiyo miaka 10 iishe siijui tutakuwa wapi:disapointed:
 
Baada ya vyombo vya habari vilivyokuwa vimenunuliwa na genge la mtandao kumsakama sana kwa habari nyingi za kumponda. Mkapa aliwahi sema maneno machache sana kuwa Watanzania tutamkumbuka. Kwa kweli hali ya nchi iliyopo saizi hakika jamaa tutamkumbuka tu, tutake tusitake. Nchi kila kitu kinaenda hovyo, na wanaonufaika ni wachache waliokuwa vinara wa hilo genge. Hakika sipati picha itakapofika 2014 hali itakuwaje. Saizi hela haina thamani kabisa, naamini soon BOT itaprint note zingine za elfu 20 na elfu 50. Ki ukweli buku 10 haina thamani tena. Ukishachenji imeisha.

Nchi huwa haiongozwi kwa blabla bali inahitaji commitment ya hali ya juu sana.

Kila la kheri.....

Tunamkumbuka kwa wizi wa EPA, Kiwira, Meremeta na TanGold. Tutamkumbuka pia kwa kumlea na kumsimika rasmi Rostam Aziz kuwa raisi wa Tanzania. Hatuwezi kumsahau kwa wizi wa kwenye Rada na ndege ya rais. Tutamsahuje mtu aliyeuza nyumba za serikari akagawana na rafiki zake? Hatuwezi kumsau mtu aliyetuponda kwamba tuna wivu wa kijinga na hatuwezi kufikiri. Tutamkumbuka sana, tena sana. Tutamsahauje mtu aliye tuletea NET group solutions ili iipeleke TANESCO kuzimu? Tutamsahauje mtu aliye uza NBC kwa marafiki zake Makaburu, mtu aliyeua ATCL? Tumsahauje mtu aliyeua kiwanda cha milingoti cha Iyunga Mbeya, na sasa milingoti ya umeme tunaagiza toka nje ya nchi? Mkapa? Si rahisi tumsahau bwana. Tutamsahauje mtu aliye buni mradi wa kukabidhi migodi ya madini kwa wageni akawaruhusau wachukue asilimia 97 na sisi akatuachia asilimia 3% tu ya mauzo? Huwezi kumsahau mwizi bana , labda uwe hujaibiwa!
 
Mkapa aliweza kuongeza kwa kiwango kikubwa makusanyo ya kodi lakini asilimia kubwa ya makusanyo hayo aliyatumia katika kulipa madeni yetu ya nje hivyo Watanzania hatukuona manufaa makubwa katika ongezeko hili kubwa la ukusanyaji wa kodi. Na hata Baba wa Taifa alianza kulipigia kelele kwamba Kiongozi wa nchi huwezi tu ukawa unatumia sehemu kubwa ya mapato yako kulipia madeni ya nchi maana hata nchi za magharibi zina madeni makubwa tu lakini hazitumii mapato yao makubwa kulipia madeni yao.

Pamoja na ongezeko hilo kubwa la ukusanyaji wa kodi, bado madarasa mengi ya shule zetu yalikuwa hayana hadhi ya kuitwa madarasa, bado wagonjwa/wajawazito wengi katika hospitali zetu walishare kitanda kimoja kuanzia wagonjwa wawili hadi saba na wengine walilala chini, bado wanafunzi wengi wa Kitanzania walikaa chini katika mashule yetu mbali mbali bado mahospitali yetu yalikuwa hayana madawa na pia mishahara ya Wafanyakazi wengi ilikuwa ni midogo mno ukilinganisha na gharama halisi za maisha ila aliweza kupandisha mishahara ya Mawaziri, Wabunge na Rais.
 
Hili si swala la kujadili chema chajiuza kibaya chajitembeza. Wote wanaombeza huyu Chingaboy wanatumia jeuri ya uchumi imara alioujenga katika kipindi chake. Jamaa alikuwa focused, alijua kuchagua priorities na hakujihusisha na trivial issues. Big up BWM
 
Kwa kweli Mzee Mkapa alitoa kauli nzito mnoooo bila ya ufafanuzi wa kina kwa sisi Watanzania wenzake. Ni kweli tunajuta mno kwa kukijua CCM ya baada yake yeye kuondoka madarakani. Je, aliona nini huku mbele ya safari na kwa nini hakulitaja wazi wazi???????????
 
Mkuu SWK, Nchi ilikuwa pazuri kivipi wakati Watanzania walikuwa wanalalamika na UKAPA. Alilazimisha ununuzi wa rada pamoja na Watanzania wengi kupinga ununuzi ule, kumbe kulikuwa na ufisadi ndani yake wa $12 millioni. Aliuza nyumba za serikali kwa bei poa na hadi sasa maamuzi yake yameigharimu Serikali shilingi 200 bilioni and counting. Aliwaingiza wale makaburu wa NET GROUP solutions kwa mtutu wa bunduki pamoja na kuwa walikuwa hawajui chochote kuhusu umeme. Alifanya ufisadi katika manununuzi ya ndege ya Rais ambayo ilinunuliwa akiwa amebakisha miezi mitatu tu katika awamu yake, ununuzi wa helicopters na magari ya jeshi. Aliiba Kiwira na kujimilikisha kisha kuwashinikiza wale Net Group solutions wasaini mkataba na kampuni yane wa shilingi bilioni 26. Aliuza mashirika ya umma kwa bei poa katika kile kilichoitwa privatisation na hadi sasa Watanzania hatujaona manufaa makubwa ya sera ile. Mwaka 2000 alisaini mikataba ya uchimbaji wa dhahabu kwa bei ya kutupa inayotupa mrahaba wa 3% tu na hadi hii leo mikataba hiyo haijabadilishwa. Alikuwa akisifiwa sana na WB na IMF kwamba amefanya vizuri kiuchumi lakini wakati huo huo kulikuwa hakuna ajira zilizoongezeka na pia Watanzania wengi walikuwa wanalalamikia UKAPA. EPA, Meremeta na Kagoda vyote vimetokea ndani ya utawala wake. Jamani tutapojadili hizi awamu mbali mbali lazima tuwe wachambuzi makini ili kuhakikisha hatumsifii mtu bila kuangalia mabaya aliyoyafanya akiwa madarakani. Kwa upande wangu mabaya ya Mkapa ni mengi mno kuliko mazuri aliyoyafanya na kama nchi yetu ingekuwa na utawala bora wa sheria alitakiwa awe jela huyu.
Du ni kweli kabisa UKAPA ulikuwepo sana hata uhuru haukuonekana ni mtu mwenye jazba, mngewauliza waandishi kama walikuwa wanaweza andika lolote baya kumhusu.
Naongezea tu kuwa Wabunge wote walikuwa hawaruhusiwi kuikosoa Serikali wnaitwa Chamwino Ikulu, Sumaye anaambiwa awadhibiti, hadi tukasikia mfanyabiashara akitaka kutajirika ahamie !!!! ccm,
Jamani kwa miaka ya sasa huwezi kuwabana wananchi na waandishi angalieni MISRI, LIBYA, BAHRAIN, YEMEN mbona angekuwepo angetumaliza?
km aliweza kumweka rostam mwekahazina wa Chama na zikachotwa bilioni EPA basi hakufanya kitu
Bana mm nanyamasa
 
Sintamkumbuka Mkapa kwa lolote jema zaidi ya kumkumbuka kwa wizi na unafiki wake dhidi ya Mwalimu..Hata hizi figure za Inflation hazimsaidii mwananchi hata kidogo kwa sababu mimi nakumbuka vizuri nilikuwa Bongo mwaka 1995 alipoingia madarakani nyumba Kariakoo zilikuwa zikiuzwa kwa Tsh millioni 20 kwa exchange rate ya 500, na niliporudi mwaka 2005 zilifikia dollar 800,000 kwa exchange rate ya 1100. Kila kitu kilipanda bei asilimia 100 ya bei niliyoiacha mwaka 1995 isipokuwa usafiri wa daladala. Umeme wa mgao na maji hakuna, reli ya kati imesimama ktk utawala wake, ATC inakufa na kutemwa na South, mvua zimegoma hadi watu wamekufa njaa kwa mara ya kwanza ktk historia ya Tanzania..

Maisha magumu kwa Mtanzania yalianza wakati wa Mkapa, na hata hizo sifa za ukusanyaji wa kodi haziwezi kusifika kiasi hicho ikiwa kabla ya hapo, nchi nzima ilikuwa ya Kijamaa na serikali ndio ina control njia zote za uchumi, sasa mlitegemea kodi ikusanywe vipi tofauti na serikali ya Mkapa iliyokusanya fedha toka soko huru ambalo halikuwepo awali?..

Definitely, kutakuwepo na tofauti ya makusanyo hata kama njia alizotumia ni mbaya sawa na nyumba za kariakoo zilizokuwa wakiishi familia bure mara wakaanza kupangisha na kukusanya kodi kisha unahesabu tofauti ya fedha toka kuishi wenyewe bure na ile ya kupangisha bila kutazama ubora wa pangisho kulingana na market rate ya kupangisha kama wanavyopangisha wengine..

sasa kwa msomi yeyote anaejua Ukusanyaji kodi na taratibu zake atakubaliana nami kwamba kilichofanyika ni kuwabana tu wananchi walipe kodi ya pango badala ya kuishi bure lakini utaratibu wenyewe haukuzingatia thamani ya vitu hivyo wala njia bora za kudhibiti urasimu na ukiritimba ndani ya vyombo vya ukusanyaji.. Matokeo yake wafanyakazi wa TRA wametajirika tokana na wizi wa kodi pia mafisadi wameiba matrillioni ya kodi, uuzaji wa mashirika na nyumba za nyumba za serikali ktk bei ya kutupa ili mradi mfuko wa serikali uonekane umetuna..

Guyz, huwezi kusifia mtu wa Kariakoo aliyeuza nyumba ya urithi kwa dollar millioni akaenda kuishi Mabibo, asiwekeze ila kaoa wake wanne kuwa ni wazo zuri zaidi kwa sababu kauza nyumba ambayo mzee wake hakuona thamani ya nyumba hiyo alipokuwa akiishi yeye. Kwa nini asisifiwe mzee alojenga Kariakoo kuwa ndio kiini cha utajiri wa huyu bwana kama mnavyomponda mwalimu kila siku bila kujua kwamba pasipo ujenzi wa mwalimu, Mkapa had nothing to sale..Na pasipo utandawazi na soko huria Mkapa had nothing to correct from...Kwa hiyo kama kuna sifa mnayotaka kumpa Mpaka ni kuthaminisha alichokifanya baada ya kukusanya fedha hizo za urithi - Kiuchumi Mkapa kenda kuoa wake wanne!
 
Huenda mimi siyo mtanzania kwa vile sintamkumbuka Mkapa kwa lolote jema kama anavyotaka, ila labda kwa mabaya tu. Baya zaidi ya yote lilikuwa lile la kumruruhusu huyu Bulicheka kuwa rais wetu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom